CCM kujivua ‘gamba’ Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kujivua ‘gamba’ Dodoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 2, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  CHAMA cha Mapinduzi kinakabiliwa na shinikizo kubwa la mabadiliko ya uongozi, taarifa zikibainisha kuwa msukumo huo unatoka miongoni mwa wana-CCM na hata nje na hasa upepo mbaya wa kisiasa unaovuma ukichochewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Raia Mwema, imeelezwa.

  Taarifa zinasema ya kuwa kuna uwezekano mkubwa wa mabadiliko ya uongozi wa juu wa chama hicho kikongwe nchini yakatangazwa katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM inayokutana Dodoma wiki ijayo.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo, mabadiliko hayo yanagusa uongozi wa juu wa chama hicho ikiwamo sekretariati nzima inayoongozwa na Katibu Mkuu, Yusuf Makamba, ambaye anatajwa kuwa chanzo cha chama hicho kufaya vibaya katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana.

  Wajumbe wengine wa Sekretariati inayotarajiwa kusafishwa katika mabadiliko hayo, yanayoweza kuwasilishwa NEC na Rais Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho, ni pamoja na Mweka Hazina wa chama hicho, Amos Makala, John Chiligati, Bernard Membe, George Mkuchika, Saleh Feruzi, Sophia Simba, Balozi Athman Mhina na Benno Malisa (anayekaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM-UVCCM).

  Wakati wa sherehe za miaka 34 ya CCM, Rais Kikwete alisema CCM inalazimika kuachana na wanachama na viongozi wanaokua mzigo kwa chama hicho na kujifananisha na nyoka ambaye huwa anajivua gamba linapochakaa.

  Taarifa zaidi zinaeleza kuwa vikao kadhaa rasmi vya chama hicho, vikiwamo vilivyohusisha baadhi ya makatibu makini wa mikoa na wilaya vimebainisha kuwa uongozi wa chama hicho ni mzigo katika kukikwamua chama na bila kusita, vimependekeza Makamba ang'oke.

  Vikao hivyo vya shinikizo vinatajwa kufanyika kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam na Bagamoyo mkoani Pwani, ikitajwa kuwa ni utangulizi wa kuibua matokeo yanayokubalika na umma, wakati wa mkutano wa NEC unaotarajiwa kufanyika mjini Dodoma.

  Taarifa zinasema katika hali ya Makamba kuondoka, baadhi ya majina yamekuwa yakitajwa kuchukua nafasi yake ambayo ni ya Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Jaka Mwambi na Abdulrahaman Kinana ambaye amekuwa Mwenyekiti wa kampeni za Rais Jakaya Kikwete tangu mwaka 2005.

  Majina mengine yanayotajwa ni ya Steven Wassira, sasa Mbunge wa Bunda; na kwa mbali anatajwa pia Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Philip Mangula kuwa anaweza kurejea; japo inaaminika kwamba hakubaliani na mambo kadhaa katika uendeshaji wa CCM ya sasa, aliyomwachia Makamba. Katika orodha hiyo anatajwa pia Chiligati, ambaye kwa wadhifa wake wa sasa ni Katibu wa Uenezi.

  Sababu kadhaa zinatajwa kuhusu haja ya mabadiliko hayo, miongoni mwake ni kukidunga sindano ya uhai mpya chama hicho, ikizingatiwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita, kwa kuwa baadhi ya viongozi hawakutoa mchango wowote katika kusaidia ushindi wa chama hicho na badala yake walikuwa kwa matamshi yao na matendo wakisaidia kuporomosha umaarufu wa chama hicho.

  Inaelezwa kuwa wakati wa mchakato wa kampeni, palikuwa na hujuma ikitokea makao makuu ya chama na mara kadhaa uratibu wa kampeni ilibidi ufanyike chini ya uangalizi maalumu.

  "Uongozi uliopo sasa, hasa Katibu Mkuu wa chama ndio tatizo kubwa la chama. Huyu ndiye aliyeteua makatibu wa mikoa na wilaya, wengi wao wakiwa hawana uwezo wa kumudu changamoto za kisiasa.

  "Yeye na timu yake ya makatibu wamekuwa mzigo karibu wakati wote wa kampeni. Baadhi yao ndio wamevuruga uchaguzi wa kupata wagombea ndani ya chama, wapo waliopewa au kuomba rushwa....wanajulikana. Ni vigumu kuacha watu hawa waongoze chama.

  "Sisi tunaona ni kama Mwenyekiti anachelewa kufanya mabadiliko na kwa maana hiyo chama kinazidi kuchelewa kujinusuru mbele ya wananchi," anasema kiongozi mwandamizi wa chama hicho kwa masharti ya kutotajwa jina lake gazetini.

  Vyanzo kadhaa vya habari vinasema kuna wakati palikuwa na msigano wa wazi kati ya Katibu Mkuu Makamba na mwenyekiti wa kampeni Kinana, huku Makamba akilalamikia kile kinachoelezwa kuwa ni kunyimwa fursa ya kusimamia moja kwa moja mfuko wa kampeni.

  Ukiacha haya ya ndani ya chama, shinikizo jingine linatokea nje ambako nguvu za uchumi, kwa mfano, zimekifanya chama hicho kinachoendesha Serikali kuonekana kuwa kisichoyafanyia kazi matatizo halisi ya Watanzania wengi wa hali ya chini ambao ndio wapiga kura.

  " Watu wanalinganisha, katika miaka 10 ya Serikali ya awamu ya tatu sukari, unga, mafuta ya taa, mchere na maharage, vitu ambavyo ni mahitaji ya msingi ya mtu wa kawaida, havikupanda bei.

  " Leo mahitaji hayo yamepanda, mengine kwa asilimia 200. Mfumuko wa bei uko juu, shilingi imedorora. Na sasa mbaya zaidi, hata zile ajira za mitaani zinazotegemea umeme zimekufa kutokana na kwamba umeme haupo.

  " Katika hali hii usitarajie watu wa kawaida waendelee kuishangilia CCM; wanaona ile tofauti ya walionacho na wao ikikua siku hadi siku, wanaona kwamba hali ngumu ya maisha wameandikiwa wao. Mkapa (Benjamin, Rais wa awamu ya tatu) hakufanya mazuri kila siku, lakini walau wakati wake na serikali yake bidhaa muhimu zilipatikana kwa bei ambayo wengi waliimudu,"anasema mwanasiasa mwingine.

  Anaongeza: " Usishangae kusikia kwamba wapo wazee ambao wamekuwa wakikutana na baadhi ya waliokuwa katika serikali ya awamu ya tatu kuwashawishi wajiandae kumpokea Rais Kikwete mwaka 2015. Sijui itakuwaje ukichukulia ushindani wa makundi mbalimbali kuhusu uchaguzi ujao ulivyo ndani ya CCM, lakini dhahiri wale wa wakati wa Mkapa wana rekodi wanayoweza kuonyesha."

  Mtikisiko huu wa CCM, wachunguzi wanasema, umekuja katika kipindi kibaya na unachochewa pia na hali ya kutokuaminiana kati ya taasisi za baadhi ya madhehebu ya dini na Serikali.

  " Watu na hasa baadhi ya viongozi wa CCM, wanasema eti sasa kuna udini wakitaja baadhi ya madhehebu ya Wakristo, lakini wanasahau kwamba aliwahi kutawala Ali Hassan Mwinyi hapa na lugha hii haikusikika. Ukiona madhehebu ya Waluteri, Waanglikana na Wakatoliki, kwa maana ya Askofu Malasusa, Dk. Mokiwa na Kardinali Pengo wote wanazungumzia jambo moja, ujue huko serikali kuna mambo yasiyofurahisha yanafanyika.

  "Haya ndiyo madhehebu makubwa ya Wakristo, hata kama kuna nyakati Serikali inawajibu kupitia katika makanisa madogomadogo ya uamsho. Ukichanganya hayo na migomo ya wahadhiri na wanafunzi vyuoni, ni dhahiri kwamba CCM inahitaji kufanya mabadiliko," anasema mchambuzi mwingine wa siasa za Tanzania.

  Mkutano ujao wa NEC-CCM unakuwa mkutano wa pili unaozongwa na shinikizo la mabadiliko ya uongozi wa juu, ukitanguliwa na mkutano kama huo uliofanyika Butiama, mkoani Mara, Machi, mwaka 2008.

  Mkutano wa wakati huo wa Butiama ulizongwa na shinikizo la kutaka kufukuzwa baadhi ya viongozi wa CCM hasa waliokuwa wakizongwa na kashfa mbalimbali za kitaifa.

  Hata hivyo, katika mkutano huo ambao haukuhudhuriwa na marais na wenyeviti wastaafu wa CCM, Mwinyi na Mkapa, vigogo waliolengwa kufukuzwa walibaki tena wakisifiwa kwa umahiri wao katika uongozi hali iliyowakatisha tamaa waliokuwa na kiu ya kuona mabadiliko ya uongozi.

  Inaelezwa pia ya kuwa kati ya mambo yaliyozidi kuwapa nguvu upinzani na hasa CHADEMA ni CCM kushindwa kuwajibishana katika makosa yaliyo wazi mbele ya jamii.

  Kwa kadiri siku zinavyozidi kusogea, makada mbalimbali wa CCM wamekuwa wakitoa kauli za kutoridhishwa na mwenendo wa chama hicho na kuanza kubainisha kasoro hizo hadharani.

  Tofauti na utamaduni uliozoeleka wa kuzungumzia masuala au kasoro za chama hicho kwa ujumla wake bila kushambulia viongozi, hali sasa imebadilika.

  Makada kadhaa wanaeleza kuwa tatizo la chama hicho ni uongozi na hivi karibuni mmoja wa makada hao aliyesema hadharani alikuwa Joseph Butiku, mtendaji mkuu wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere.

  Butiku alizungumza na waandishi wa habari mkoani Mwanza akisema CCM imepoteza dira na kwamba tatizo lake kubwa ni viongozi wa sasa wanaoshindwas kusimamia misingi ya uadilifu ya chama hicho.

  Hata hivyo, katika hali inayoonyesha kushindwa kuvumilia ukosoaji huo, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa, alimjibu akisema chama hicho hakijapoteza dira na ndiyo maana kimekuwa kikishinda Uchaguzi Mkuu, ngazi ya urais na viti vingi vya u ubunge na udiwani.
   
 2. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2011
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Too let to catch a fast moving train
   
 3. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tatizo kuu la viongozi wa CCM ni mentality kwamba watatawala milele! Wamesahau kwamba hakuna dola idumuyo milele isipokuwa dola ya ki-Mungu pekee!
   
 4. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  watahangaika sana
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ni vigumu kuvua gamba hilo!
   
 6. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,030
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 180
  :usa2:
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  RIP CCM!
  Hakuna mbeleko yoyote duniani inayofaa kukibebea chama hiki...mfupa uliomshinda fisi huu!
  Kubadilisha watu hakutakuwa na effect yoyote, maana kila atayekuja kazi yake kuu ni kutetea ufisadi na kulindana,,,mambo ya "huyu ni mwenzetu"
   
 8. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Kinana na hao waliotajwa wana magamba magumu kama kobe hayavuliki aslani. Hilo ni pamoja na uelwe finyu kama ninihiiiiiii,. Wapi anayeweza hata chembe ya haradani mbele ya Dk PHD ya ukweli?
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni mwenyekiti wao!
   
 10. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,967
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Mazungumzo kati ya mwanafamilia na mganga kuhusu hali ya mgonjwa;

  Mwanafamilia: Mganga, hali ya mgonjwa wetu kweli si nzuri, amekuwa mahututi kwa muda mrefu na afya yake inazidi kudidimia. Unadhani atapona kweli? Tuambie tu ukweli!

  Mganga: Kwa kweli hali yake si nzuri. Labda Mungu akifanya muujiza, lakini nadhani mgonjwa wenu hatapona.

  R.I.P CCM.
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Kumbuka UKIMWI hauna tiba.

  Moja wapo ya mabango ya watanzania huko mkoani Kagera
   
 12. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hilo gamba halivuki kwa sababu hilo JOKA 'CCM' lilishajizeekea siku nyingi.... RIP CCM
   
 13. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  CCM = shetani
   
 14. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Walijisadikisha kuwa tanzania hakuna chama cha kuking'oa madarakani CCM, Kumbe walipaswa kujitambua kuwa si wao tu ila kuna NGUVU YA UMMA ndiyo mhimili wa chama kuwa madarakani .Walijisahau kuwa NGUVU YA UMMA ikikukataa hata uwe na ma-trioni ya fedha haitasaidia.Leo hii fedha za RA na EL wanaanza kuzihisi zinawaka moto.

  PEOPLESSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSS POWER
   
 15. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #15
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wakati tunafurahia ccm "kujivua gamba" pengine tujiulize ina maana gani hasa.

  Kama tunatumia mfano wa nyoka kujivua gamba basi naona tunakosea kuamini kwamba ccm imebdalika. Kwa sababu nyoka anapojivua magamba hubaki kuwa ni nyoka yule yule kwa tabia, aina na sifa zake zote. Tena kama ni nyoka wa hatari au wa sumu hubaki kuwa hivyo hivyo.

  Walichofanya ccm ni kama mtu kubadili gari tu. Gari jipya (au kuukuu kama Mukama) halibadili chochote katika tabia na sifa za mwenye gari. Lakini walichofanya hakileti mabadiliko yoyote kwa sababu viongozi wakuu wamebaki kuwa wale wale wa tangu enzi za TANU na Afro Shirazi. Mawazo na uwezo wao pia ni wa karne hiyo.

  Wazee wanang'ang'ania madaraka hata pale wanapoona wameshindwa kabisa!
   
 16. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #16
  Apr 11, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Nyoka anabaki kuwa nyoka kwa sifa zake zoote.
  Na aliyekwisha kuumwa na nyoka kila akiona jani ushituka.
   
 17. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #17
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Falsafa ya nyoka kubadili gamba ni kuwa kila napofanya hivyo hukua zaidi. Hii ndiyo maana nyoka huendelea kukua tu hata kama ataishi miaka milioni. Sasa walichofanya hawa mafisadi ni kubuni njia nyingine za kuzidisha na kutamalaki zaidi. Nawaambia kweli watazidi na kuongezeka. They will become numerous like stars or they will be as many as stars. Everyone is going to be a fisadi in the near future.
  Hukuna chema kitakachotoka thithiem period!
   
 18. A

  Awo JF-Expert Member

  #18
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Ndio falsafa za Kikwete hizo. Shallow sana. Kujivua gamba ndio cosmetic changes - hamna kitu.
   
 19. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #19
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Wastage of resources, and plundering once again...vikao wanavyofanya sasa hv n upotevu wa muda, rather wangebakia tu dar na kufanya shughuli zingine...
  Ccm watuambie ni kwa vp kumwondoa Makamba na kumweka Mukama kutabadilisha chochote..unless km watasema chama kinaendeshwa kwa intuition ya mtu binafsi, na si sera...
  Amkeni jamani, hz ni ngonjera na ufundi wa kutamka maneno yanayovutia kuskiliza, but actions=ZERO..
   
 20. N

  Nyota Njema Senior Member

  #20
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii maana ya kubadili gamba inabidi ifanyiwe uchunguzi wa kina, si ajabu Kikwete na rafiki zake walio-chance kupata madaraka ndani ya chama hicho wana maana nyingi ya neno hilo, lakini msingi mmoja tu....chama kama kampuni ambayo wawekezaji ni familia zao!
   
Loading...