Kwa falsafa na uelewa wa ccm, jibu ni ndio. Kisayansi jibu ni hapana.
Kujivua gamba ni msemo mpya (nionavyo) ambao una lengo la kuwasilisha hoja fulani za ccm kwa manufaa ya kisiasa. Ni ujinga kwao kutumia paronamasia by merely playing with empty words.
Kazi yao kwisha.
Mambo ya kuwakumbuka wenyeviti wa CCM:
Falsafa ya Mwenyekiti wa TANU: Ujamaa na Kujitegemea
Falsafa ya Mwenyekiti wa I wa CCM: Mapinduzi (Kilimo, Elimu, siasa ya Ujamaa na Kujitegemea)
Falsafa ya Mwenyekiti wa II wa CCM: Ruksa, utandawazi
Falsafa ya Mwenyekiti wa III wa CCM: Uwazi na Ukweli?, utandawazi?
Falsafa ya Mwenyekiti wa IV CCM: Ari mpya, Nguvu mpya, Kasi mpya -> ya nini?
Falsafa ya Mwenyekiti wa IV CCM: Ari zaidi, Nguvu zaidi, Kasi zaidi -> ya nini?
Falsafa ya Mwenyekiti wa IV wa CCM: Chama kujivua Magamba => CCM ni joka? kama viongozi wake ni magamba, CCM mwenyewe anayebaki ni nani? Sera na imani za chama sio! Na wanachama ni nini kwenye hii model ya nyoka? Na wananchi ni nani!