CCM kujivua ‘gamba’ Dodoma

JK namfagilia kiasi fulani, kwani CCM kipindi hiki kinataka kiongozwe na watu wa kutumia mabavu kama Mukama, muda wa longo longo haupo tena. CDM wakimwaga mboga CCM imwage ugali hapo KITAELEWEKA! Suala la kuajiri watu wa kwao si tatizo ili mradi wawe na uwezo, asiwe kama Makamba kujaza wasambaa akiwemo Tambwe Hiza bila ya kujali uwezo wake. Sifa ya ziada ya Mukama ni kujenga hoja na mzungumzaji mzuri katika mdahalo! Hivyo Dr. Slaa ajiandae kwa mdahalo CCM sasa hivi ina katibu mkuu msomi sio Makamba mkimbia midahalo

Mbano hukutupa jibu kuhusu Ufisadi wa Kutoa Ukusanyaji wa Ushuru katika Kituo cha Ubungo kwa kampuni yenye uhusiano na familia ya Kingunge alipokuwa kuwa Mkurugenzi wa Jiji?
 
Wana JF,

Mimi binafsi nimefurahishwa na maamuzi ya Jk ya kuvua gamba (la nyoka?) wengi wanasema sumu itavuliwa lini?

Ukiwa unaangalia mambo kwa mapana bila kuelemea upande wowote, na kama ulifuatilia kwenye TV vikao vya Dodoma, utagundua kuwa kwa uwazi kabisa wanaoitwa mafisadi (to me not yet proved beyond reasonable doubt) kuwa waangalie tuhuma wapime na wachukue hatua wenyewe.

Hii ni ya kupongeza jamani, tulizoea kulaumu lakini CCM imeonyesha nia ya mabadiliko. Rome haikujengwa siku moja, tuwape muda. Kilichofanyika Dodoma kwa kweli haijawahi kufanyika katika historia ya CCM- kuambiana ukweli wazi wazi.

Big up CCM sasa kilichobaki ni KUTEMA SUMU!!

Wasalaam

FP
 
Katika kile kinachoonekana kama kutaka kurejesha thamani yake mbele ya macho ya wananchi CCM imetoa single iitwayo "Kujivua Gamba" ambapo baadhi ya viongozi wake Mafisadi wametolewa kafara katika staili ile ile iliyozoeleka ya kuwapatia tiketi ya kwenda kufaidi raslimali walizofuja walipokuwa watumishi wa umma; bali ya hatua zozote za kisheria kuchukuliwa dhidi ya wahusika ikiwemo kuwataka kurejesha walichoiba.

Kama Mazumbu Kuku watanzania walio wengi wanaonekana kufurahia kauli mbiu hiyo na kitendo cha kuwaruhusu Mafisadi wakatumbue raslimali walihujumu wakiwa watumishi wa umma kwa amani na utulivu. Tunashindwa kujiuliza ni watanzania wangapi wamepoteza maisha kwa kukosa huduma za afya, maji safi n.k kwa Serikali kukosa fedha za kuwapatia huduma hizo ilihali Mafisadi hawa wakijichotea mabilioni ya fedha kupitia EPA. KAGODA, MEREMETA n.k

Uzumbukuku wetu watanzania unajidhihirisha zaidi hata pale Halmashauri Kuu ya CCM inapokubali kuwa baadahi ya wajumbe wa vikao vyake vya juu ni Mafisadi wa kutisha na wamekuwa wakihusika katika kulifilisi taifa hili kiasi cha wananchi kuwachukia.

Kwa kuwa CCM ndio yenye kuongoza Dola, ikiwemo Polisi, Takukuru, Mahakama n.k imeshindwa kuwachukulia hatua watu hao na badaka yake kuwataka wakapumzike vyema huku wakiondoka na mabilioni ya watanzania ambao watoto wao wanakaa chini hawana madawati, zahanati hazina dawa wala vitendea kazi n.k. Wakati CCM ikishindwa kuchukua hatua dhidi ya watu inaokiri ni Mafisadi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ametangaza kuwepo kwa Uifisadi Mkubwa sana katika Ukaguzi aliofanya katika Serikali Kuu na za Mitaa kwa kipindi cha 2009/10. Hivi tunangoja nini kutojitokeza kwa mamilioni kuandamana hadi chama hiki kingoke madarakani kama ilivyotokea huho Misri
 
Sio siri kumuamini mtu yeyote ndani ya ccm kama mtu msafi kwangu mimi ni ngumu!
 
Naomba kuwasilisha huku nikichelea kupongeza yaliyotokea huko makao makuu . Napata tabu kusifu au kusema dawa imepatika kwa kuwa fikra za hofu kuwa ramani ni ile ile bali mwongoza njia amebadilika. Tulitaka kufika Mwanza kwa njia ya kati lakini tumebadilishiwa "ya mizigo" tukapewa "ya abiria" . Historia nadhani itupe funzo tukifanya rejea tatizo lilikuwa ni nini ili tuweze kuona mwanga. Nauliza, je wao walikuwa wakigombania tunda? Je waliogombania wametoka suluhu au kuna upande umepata na sasa wananawa mikono waanzae kula. Walikula kwa uma sasa wanatuonesha tofauti kwa kula kwa vijiti. Msamiati wameubadili wanataka tuelewe maana mpya. Siamini kama waweza tangaza ufufuko halafu michango ya hitma hujaisimamisha.​
 
Pamoja na mashaka yaliyopo kuhusu dhamira ya kufanya mabadiliko ya kweli na nia ya kuboresha uwezo wake kiutendaji, ni wazi kwamba chama kimeonyesha maturity ya hali juu kwa kukiri udhaifu wake na kutambua changamoto zinazokikabili - this is a good sign in the right direction.
 
Kinachotokea ccm kwa sasa ni ujinga mtupu.

Ufisadi hauanzia yanakoaazia magamba..bali ni mioyoni mwa wa tuhumiwa wote.

Wamevua magamba lakini wote waliovuliwa na waliobaki MOYONI WANA UFSADI WA KUANGAMIZA TAIFA!!

KiKwete hana moyo wa dhati ... wa kuumaliza ufisadi...hata yeye anajua haya..Kama asingetishiwa nafasi yake..asingefanya alichofanya...

HAPAKUWA NA DHAMIRA YA KWELI NA YA DHATI YA KUVUA GAMBA KAMA ILIKUWEPO ...USHAHIDI ULETWE HAPA.

..Mwalimu nyerere: alisema Mapinduzi ni moyoni kabla ya silaha... hata vita ikiwa ngumu namna gani lakini kama imepiganwa moyoni na kushinda nje inakuwa NI LAZIMA LAKINI NI MOYONI KWANZA..

Hali sivyo ilivyo na mtindo wa kitoto wa kuvuana magamba ...hapo ccm..

HAKUNA MWENYE MOYO NA UJASIRI WA DHATI WA KUUMALIZA UFISADI !!!!!!
 
nyoka ni nyoka hataakivua gamba hawezi kuwa kinyonga ccm ni wezi hawawezi kuacha kuiba kubadilisha uongozi hayo ni maigizo tumewashtukia hawana lolote
 
1)Mwanakijiji. Mwandishi anaejificha ficha aliongoza hapa jf na kwenye magazeti kufichua uozo wa ccm kupitia makala zake. Hongera mwanakijiji.
2)Kubenea. tusisahau alimwagiwa acid baada ya kumdondosha EL juu kutoka uwaziri Mkuu hadi NEC na sasa EMPTY SPACE kwa kuchapisha ufisadi wa RICHMOND na DOWNS. na sasa ccm imejivua gamba.

3)INVISIBLE. kuruhusu uchafu wa ccm kuanikwa na hatimae kujivua gamba.
ENDELEZA
 
Wakuu,nyoka anapozeeka hujivua gamba lakini haimaanishi sumu hutoweka.Ili sumu itoweke ni lazima umng'oe meno,lakini pia meno yataota hapo baadae.Kwa hiyo ili sumu itoweke kabisa,inakupasa kumgonga kichwa.Hili la CCM kujivua gamba bado halitoshi kwani sumu iko pale pale,ki msingi ni wananchi kupiga kichwa kwa kuing'oa kabisa madarakani ndipo italeta nidhamu ya utawala bora Tanzania.Kujifua gamba wakati sumu,meno,na maumbile mengine yako pale pale hakusaidii kabisa,sana san kujivua gamba kunarudisha nguvu mpya ya kushambulia kuliko mwanzo.Kwa hiyo watu wasitegemee mapya kwa kujivua gamba.
 
Tuendelee kuwatia moyo hawa wazalendo maana safari bado ni ndefu.

Ujasiri wao ni sawa na kujitoa muhanga.
Mola awajalie wapiganaji wote kuona matunda ya jasho lenu!
 
Back
Top Bottom