WATANZANIA TUJIHADHARI SANA NA HIZI MBINU ZA RAIS KIKWETE NA UVCCM-PWANI KUMUANDALIA NJIA HUSSEIN MWINYI NA KULIBATIZA HILO ZENGWE JINA LA 'CCM-KIKWETE KUJIVUA GAMBA'
Watanzania napenda niwatahadharishe ya kwamba Zengwe Jipya ndani ya CCM kuwakata miguu mapema mapema wale wanaodhaniwa kuwa ni wagombea shupavu wa urais ndani ya jahazi la CCM, na kubatizwa jina la kuvua gamba, yoote ni ghiliba za mkoa wa Pwani kupitisha mgombea dhaifu ili kubakisha urais huko.
Wenye kung'amua na mng'amue toka hapa hivi sasa. Mara baada ya vikao kibado za usiku sirini katika jiji la Dar es Salaam, Tanga na Zanzibar na baadaye UVCCM-Pwani kusakiziwa ujumbe wa ghubi ghubi (kama pre-emptive tactics) iliyoleta zogo kubwa ndani ya chama tawala hivi karibuni si lolote wala nini.
Leo hii Edward Lowassa et al wanadondoshwa kwa lengo hilo hilo kama ilivyowahi kuropokwa na UVCCM-Pwani na vile vile kupata nayo KURA ZA HURUMA kutoka kwetu kama jamii ya Tanzania. Pindi watakapomalizana na MV Lowassa kwa ugombeaji Urais ndani ya CCM, wanajua vile vile kwamba wale watu waliopangwa na EL, AC na RA mikoa yote pamoja na ndani ya vyombo vyote vya maamuzi ya CCM kamwe hawatompitisha SIX sawa sawa na jinsi ambavyo hawatompitisha MWANDOSYA et al huko nyanda za juu kusini huku Dr Magufuli wakiwa wameshamtia mchanga kitumbua katika ndoto zake hadi hivi sasa hivyo UVCCM-Tabora kuchinjwa katika dakika za majeruhi huko mbele ya safari.
Kwa mujibu wa habari za ndani mwao CCM, hizi zote ni mbinu ya katika kutafuta kule kuwadhibiti tu wagombea wenye nguvu mle ndani mwao na kuwaangusha chini na baadaye kuja kutumia kanuni yao mpya ya uteuzi wa wagombea ndani ya chama chao kumpitisha mgombea dhaifu KAMA COMPROMISE CANDIDATE atakayeungwa na makundi makubwa kadhaa yenye nguvu ndani ya CCM kwa imani tu kwamba wakifanya hivyo basi watakua wameweza kulikomoa vilivyo kundi lingine adui mle ndani; hivyo, napenda niwataarifu kwamba GHILIBA ZA HIVI SASA CCM-KIKWETE kujivua magamba kukiwa kumekucha yoote ni vita vya kumpigania Hussein Mwinyi urais kubaki Pwani.
Ndio, narudia hapa ili wenye kuyaelewa na wayaelewe mapema zaidi kwamba chini ya mizizi ya haya madai ya CCM kujivua magamba wala hakuna lolote na hivyo napenda niwathibitishieni hapa jukwani kwamba kinachoendelea hivi sasa ni Kikwete kujaribu kusembua njia kwa ajili ya UVCCM-Pwani ili waibuke washindi dhidi ya UVCCM-Arusha na UVCCM-Tabora kuja kudondoshwa huko mbele ya safari katika dakika za majeruhi ili Hussein Mwinyi apitishwe kupitia mlango wa nyuma kuja kuwa rais wa nchi hii.
Ni ukweli usiopingika ya kwamba wagombea maarufu sana, kwa viwango wa ndani ya CCM huko, ni hatari zaidi kwa umoja wake hivyo mara baada ya CCM kumaliza hizi SINEMA za Wilisoni NdiaMukama (application of a silent Elimination Method Tactics to Tream down otherwise Powerful Presidential Candidates within CCM and keep the Rising Star of the Opposition parties at bay) kwisha na wagombea wenyewe kudhoofishwa ipasavyo.
Hapo ndipo NdiaMukama anapanga kuja kutumia janja za 'Divide and Rule' (Mbinu za CCM hivi sasa ni sawa na zile za Mnyama Sungura kujificha katika kichaka huku akimfunga tembo kamba mguuni na upande wa pili kamfunga kamba ya mguu mnyama kiboko kisha anadanganya kila mmoja wao kwamba ni yeye sungura mwenye nguvu za ajabu ndiye atakaye mmvuta kila mmoja wao hao wanyama milima wawili hao) to manupulate them against each other's neck na mwisho wake kumpitisha mgombea dhaifu.
Ndio, katika zengwe hili ni kwamba itakua ni katika kutekeleza kule AGENDA YA SIRI YA MKOA WA PWANI na vile vile kujifanya kwamba Zanzibar safari hii wametengewa awamu yao kutoa rais - wakati rais mwenyewe ni TX kutoka Kisarawe aliyepandikzwa huko Visiwani kwa dharura kama hizi tu ili Watanzania Visiwani waendelee kunyimwa zamu ya na CCM bila ya wao kuelewa chochote kitu.
Nguvu ya Umma, tuendeleeni kuzitazama hizi mbio za sakafuni ambazo ukingo wake safari hii ni kupiga kura chini ya Tume Huru ya Uchaguzi kote Bara na visiwani.