Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayeshughulikia Oganaizesheni, Paulo Chacha, amesema CCM imejijengea msingi imara wa kisiasa unaoiwezesha kuendelea kushinda uchaguzi katika ngazi mbalimbali za uongozi nchini, huku ikijiwekea lengo la kuendelea kuongoza dola kwa miaka 100 ijayo.
Chacha ametoa kauli hiyo mkoani Tabora wakati wa hafla ya kumuaga na kumpongeza kwa kuanza majukumu yake mapya ya uongozi, ambapo amesema hadi sasa hakuna Chama cha siasa chenye uwezo wa kuiondoa CCM madarakani."Bado chama cha kuitoa CCM madarakani hakijazaliwa. Hivi vilivyopo tayari vimeshindwa, vingine vinaendelea kuanzishwa," amesema Chacha.
Aidha, amesema hata baada ya CCM kutimiza miaka 100 ya uongozi, chama hicho kitaendelea kujiwekea malengo ya kuongoza kwa kipindi kingine cha miaka 100, akieleza kuwa mafanikio hayo yanatokana na misingi imara ya chama, ikiwemo kuwa na wanachama wengi na wenye ushiriki hai katika shughuli za kisiasa.