CCM kujivua ‘gamba’ Dodoma

CCM kujivua ‘gamba’ Dodoma

Jk akipiga picha na Wanaume huwa ananuna kweli, lakini akipiga na hao kina dada supastaa meno yote nje.
 
Mpaka hivi sasa wasomi wanachama weeengi sana ndani ya CCM kama akina Prof Palamagamba Kabudi na wengine wengi tu husemekana kana kwamba waonekana kujiweka kando kidogo katika masuala mengi tu ya chama chao hicho baada ya kuonekana mawazo yao ya kitaala kupuuzwa kila mara kukiboresha CCM kuendana na kizazi cha Doti Komu wanavyotaka na badala yake mawazo ya akina Mzee Makamba kuzingatiwa zaidi na mwisho wa yote Chama kuota magamba sugu yasiyovulika kila kona nchini!!!
 
Nakuambia UVCCM wa mikoa mbali mbali nchini pamoja na wale wana-CCM wanaofikiria kugombea urais 2015 na hata ndugu zetu Watanzania Visiwani pindi watakapong'amua siri nzima chini ya hii ngonjera yoooote inayoendelea ndani ya CCM basi nadhani kutakua hakukaliki teeeeeeeeeena mle ndani.

Hebu watu tusubiri kidogo kuona zahama na gharika la moto mkubwa utakavyolipuka CCM Chimwaga - a point of no retur heree machaliii wangu!!!

wait for the new episode...
 
WATANZANIA TUJIHADHARI SANA NA HIZI MBINU ZA RAIS KIKWETE NA UVCCM-PWANI KUMUANDALIA NJIA HUSSEIN MWINYI NA KULIBATIZA HILO ZENGWE JINA LA 'CCM-KIKWETE KUJIVUA GAMBA'

Watanzania napenda niwatahadharishe ya kwamba Zengwe Jipya ndani ya CCM kuwakata miguu mapema mapema wale wanaodhaniwa kuwa ni wagombea shupavu wa urais ndani ya jahazi la CCM, na kubatizwa jina la kuvua gamba, yoote ni ghiliba za mkoa wa Pwani kupitisha mgombea dhaifu ili kubakisha urais huko.

Wenye kung'amua na mng'amue toka hapa hivi sasa. Mara baada ya vikao kibado za usiku sirini katika jiji la Dar es Salaam, Tanga na Zanzibar na baadaye UVCCM-Pwani kusakiziwa ujumbe wa ghubi ghubi (kama pre-emptive tactics) iliyoleta zogo kubwa ndani ya chama tawala hivi karibuni si lolote wala nini.

Leo hii Edward Lowassa et al wanadondoshwa kwa lengo hilo hilo kama ilivyowahi kuropokwa na UVCCM-Pwani na vile vile kupata nayo KURA ZA HURUMA kutoka kwetu kama jamii ya Tanzania. Pindi watakapomalizana na MV Lowassa kwa ugombeaji Urais ndani ya CCM, wanajua vile vile kwamba wale watu waliopangwa na EL, AC na RA mikoa yote pamoja na ndani ya vyombo vyote vya maamuzi ya CCM kamwe hawatompitisha SIX sawa sawa na jinsi ambavyo hawatompitisha MWANDOSYA et al huko nyanda za juu kusini huku Dr Magufuli wakiwa wameshamtia mchanga kitumbua katika ndoto zake hadi hivi sasa hivyo UVCCM-Tabora kuchinjwa katika dakika za majeruhi huko mbele ya safari.

Kwa mujibu wa habari za ndani mwao CCM, hizi zote ni mbinu ya katika kutafuta kule kuwadhibiti tu wagombea wenye nguvu mle ndani mwao na kuwaangusha chini na baadaye kuja kutumia kanuni yao mpya ya uteuzi wa wagombea ndani ya chama chao kumpitisha mgombea dhaifu KAMA COMPROMISE CANDIDATE atakayeungwa na makundi makubwa kadhaa yenye nguvu ndani ya CCM kwa imani tu kwamba wakifanya hivyo basi watakua wameweza kulikomoa vilivyo kundi lingine adui mle ndani; hivyo, napenda niwataarifu kwamba GHILIBA ZA HIVI SASA CCM-KIKWETE kujivua magamba kukiwa kumekucha yoote ni vita vya kumpigania Hussein Mwinyi urais kubaki Pwani.

Ndio, narudia hapa ili wenye kuyaelewa na wayaelewe mapema zaidi kwamba chini ya mizizi ya haya madai ya CCM kujivua magamba wala hakuna lolote na hivyo napenda niwathibitishieni hapa jukwani kwamba kinachoendelea hivi sasa ni Kikwete kujaribu kusembua njia kwa ajili ya UVCCM-Pwani ili waibuke washindi dhidi ya UVCCM-Arusha na UVCCM-Tabora kuja kudondoshwa huko mbele ya safari katika dakika za majeruhi ili Hussein Mwinyi apitishwe kupitia mlango wa nyuma kuja kuwa rais wa nchi hii.

Ni ukweli usiopingika ya kwamba wagombea maarufu sana, kwa viwango wa ndani ya CCM huko, ni hatari zaidi kwa umoja wake hivyo mara baada ya CCM kumaliza hizi SINEMA za Wilisoni NdiaMukama (application of a silent Elimination Method Tactics to Tream down otherwise Powerful Presidential Candidates within CCM and keep the Rising Star of the Opposition parties at bay) kwisha na wagombea wenyewe kudhoofishwa ipasavyo.

Hapo ndipo NdiaMukama anapanga kuja kutumia janja za 'Divide and Rule' (Mbinu za CCM hivi sasa ni sawa na zile za Mnyama Sungura kujificha katika kichaka huku akimfunga tembo kamba mguuni na upande wa pili kamfunga kamba ya mguu mnyama kiboko kisha anadanganya kila mmoja wao kwamba ni yeye sungura mwenye nguvu za ajabu ndiye atakaye mmvuta kila mmoja wao hao wanyama milima wawili hao) to manupulate them against each other's neck na mwisho wake kumpitisha mgombea dhaifu.

Ndio, katika zengwe hili ni kwamba itakua ni katika kutekeleza kule AGENDA YA SIRI YA MKOA WA PWANI na vile vile kujifanya kwamba Zanzibar safari hii wametengewa awamu yao kutoa rais - wakati rais mwenyewe ni TX kutoka Kisarawe aliyepandikzwa huko Visiwani kwa dharura kama hizi tu ili Watanzania Visiwani waendelee kunyimwa zamu ya na CCM bila ya wao kuelewa chochote kitu.

Nguvu ya Umma, tuendeleeni kuzitazama hizi mbio za sakafuni ambazo ukingo wake safari hii ni kupiga kura chini ya Tume Huru ya Uchaguzi kote Bara na visiwani.

Nimejaribu sana kufikiria jina la Profesa Palamagamba (Kabudi?) umelitumia la nini ktk title ya hizi porojo zako. Mwache professor nje ya siasa zenu za maji taka.
 
Wameanza kutoa siri zao za ndani ya ndoa... tunasubiri next episode baada ya siku 90 tuone wakipeana talaka!!!
 
Wajumbe hii issue nilisha izungumzia like 2 months a go. but ilichomwa kwa kuwa nilikua sina ushaidi wa kutosha kuusu, kikundi fulani ndani ya CCM kinamwandaa mgombea Urais kutoka zanzibar, but naona sasa kunawatu wanakuja na more details. sasa nikweli Uyo kijana anaandaliwa na CCM kugombea Urais. 1. Alikuwa Mbunge wa (jina tunaifadhi) uku bara akaamishiwa ubunge Zanzibar(jina tunaifadhi).
2. Ndiye mbuge pekee asiye na kashfa ya Ufisadi mpaka sasahivi.
3. Ndiye mbuge pekee asiye zungumziwa na vyombo vya habari mara kwa mara
4. Amepewa wizara nyeti sana, pamoja na misukosuko aliyo pata akuweza kujiuzulu kwani alikuwa analidwa mkuu.
5. Amekua akikwepa sana kutoa matamko na kuonekana mara kwa mara kwy media.

kifupi mpaka sasa ndiye mtu pekee anaoneka kua na uwezekano wa Kugombea Urais kwa Tanzania kunusuru muungano na pia mpasuko uliopo.

Kwa sisi wapiganaji huu ni wakati muafaka wa kujipanga kuangalia jinsi ya kuwamaliza jamaa waondoke kabisa kwy Uongozi
 
JF MOVEMENT POPOTE TULIPO TUENDELEZENI WAJIBU WA KUHABARISHA WANANCHI 'KWA WAKATI', KULINDA MAKAMANDA WETU NDANI NA NJE YA CCM VILIVYO, NA KUTAMBUA YA KWAMBA VITA DHIDI YA UFISADI BADO NI MBICHI NCHINI

Mpango dhidi ya Kamanda wa Machalii wa kweli nchini wa kupigana na UFISADI uliokithiri kila pembe ya taifa letu, Mheshimiwa wa kweli Godbless Lema, ni jambo la muda mrefu sana ndani ya hemaya hizo. Aonekana mwiba zaidi sawa tu na JF inavyosomeka kwa CCM-Kikwete.

Lakini kwa jinsi anavyopendwa na Vijana kote nchini hasa ndio imekua kikwazo kikubwa sana kumfanyizia kwa hofu ya YALE YATAKAYOFUMUKA KOTE NCHINI VALANGATI KUSHUKA NA ZAHAMA ZAKE zote kwa wahusika na serikali yao.

JF ikulu na JF Chimwaga tafadhali fanyeni kazi ya kuwalinda makamanda wa kweli wanolinda maslahi ya wananchi walioko ndani na nje ya CCM. Vita bado mbichi, Vijana tukaze mwenzo na zaidi huku tukiwa tunasubiri Muswada wa Katiba kwenye Bunge letu miezi miwili ijayo (June).
 
Palamagamba Kabudi, kama Profesa mwingine yeyote yule huo uprofesa wake peke yake unamfanya awe ni TAASISI katika jamii yetu. Kwa mantiki hiyo wewe chagua kutete Palamagamba Kabudi na wala si Profesa Palamagamba Kabudi niliyekua nikimzungumza humu.

Pili, mtu yeyote atawazwaye uprofesa katika jamii yetu ama kwa kusomesha watu darasani au kujikita katika kufanya utafiti (wafikirie makada hao wa elim kama vile Prof Baregu, Prof Bangu, Prof Shivji, Prof Mbilinyi, Prof Nyagawa, Prof Masenge, Prof Tibaijuka ...) moja kwa moja wooote hawa ni mali na miliki ya umma ambayo mtu yeyote kama wewe huna hati miliki nayo kiasi cha kutamani kuzuia maoni yoyote juu yao.

Hali halisi ni kwamba pindi tunapochagua kuwatawaza ukada huo wa kisomi katika jamii yetu ni kwamba tayari Watanzania wooooote nje ya mipaka zetu za KIITIKADI tayari tumewapembua kama mchele wetu wa kutusaidia KUJIBU MASWALI MAGUMU NA KUTOA MAWAZO YENYE USHAHIDI hasa bila uegemeo mwingi kwa upande fulani pale hoja nzito inapoibuliwa katika jamii yetu.

Kwa lugha nyepesi, nasema hivi; pindi unionapo nikimtaja Prof Palamagamba Kabudi ni kwamba namzungumzia yeye mmoja akiwa kama SURA YA JOPO KUBWA ZAIDI ya wasomi walioko ndani ya chama tawala ambao hata humo wanao jukumu kubwa la kuibua, kuongoza na kutekeleza FIKRA MPYA na yenye faida zaidi kwa jamii nzima ya Tanzania katika ujumla wetu.

Lakini kwa bahati mbaya sana, wasomi wengi sana kama huyu Prof Palamagamba WAMEKUA WAKIPUUZWA NA AU KUZINGATIWA MAWAZO YAO kutekelezwa ki-roborobo au kutupwa kabisa kapuni bila ya kuheshimu na kujiuliza kwamba wazo lenyewe lilitokana na mtu mwenye ukada gani wa uelewa wa mambo katika jamii. Badala yake mawazo ya akina yakhe ambao wengi wao ndio wamesoma lakini bado ni mbumbumbu tu vile vile ndio siku zote hupata baraka ya kutekelezwa kwa haraka na matokeo yake chama kufikwa mithili ya CCM kilivyofikwa hivi leo.

Hata hivyo hebu ngoja kwanza Senior Bachelor ndio utakua unaelekea kusema nini katika hili fungu la maneno la 'SIASA ZENU ZA MAJI TAKA???' Hivi unayo habari kwamba kati ya watu ambao wanayo DENI KUBWA NA JAMII YETU ya Tanzania na Prof Palamagamba Kabudi naye yumo kwa maana ya KULIPIWA MASOMO YAKE kwa kiasi kikubwa na walipakodi wa nchi hii hivyo hana pa kuanzia kutuwekea uzio wa kutokuguswa Mabadiliko ya kweli yanapoonekana kushindikana with and under his watch???

Think about and posible come over with unreseved appologies to earlier innuandoes that may have accidentally slipped off your cheeks and a demonstration of above board critical thinking readiness.

amoja
Nimejaribu sana kufikiria jina la Profesa Palamagamba (Kabudi?) umelitumia la nini ktk title ya hizi porojo zako. Mwache professor nje ya siasa zenu za maji taka.
 
Ndio zake Rais mzima HOVYO.. Hawa madada / mama pia wasije kupata shot ya umeme tuu.
 
Watabamba tu kuwa na magamba ni ukomavu kutokuwa na magamba ni uchanga nchi lazima iongozwe na wenye magamba
 
JANUARY MAKAMBA NJIA PANDA KATI YA UPWANI NA KUSALITI KULE MKONO UNAOMLEA NA HATA KUMFIKISHA BUNGENI BILA KUTARAJIA

Ni miezi michache tu iliopita tangu huyu kijana mwenzetu wa Mombuli aulize swali ambalo wengi hadi leo hii hudhania ya kwamba aliliuliza akiwa kwenye ndoto usingizini lakini hasa kumbe ndio sura halisi ya mambo: alisika akiuliza ndani ya sebule la Bunge letu tukufu kule Dodoma; Je, mimi January Makamba nimefikaje hadi nami nikawa mmojawapo watu wanaopachishwa neno lenye upekee la MHESHIMIWA hapa Mjengoni?????

Endapo mtu atakua akidhani kwamba nyuma ya hilo swali kulikua na mzaha wowote basi nakwambia utakua umeliwa hela yako kwenye kuzungumzia hili!! Kwa wale wanaomjua Mheshimiwa huyu ukweli ni kwamba hakua hata na ubavu wa kuwa namba tatu nyuma ya Mhe Selukindo kwenye kinyang'anyiro cha kiti cha ubunge wa pale Mumbuli.

Hivyo hayo maneno yake January Makamba ya kuonyesha kule kama vile kuduwazwa vile mambo yalivyokwenda kwa kasi ajabu mpaka hata na yeye kujikuta KALE KAMUUJIZA KALIKOTOKEA KWENYE UCHAGUZI WETU WA 2010 kakimzoa na kumpaisha ndotoni hadi anajikuta tu kaketi kwenye kiti kimojawapo (Kiti Cha Ubunge wa Mumbuli) ndani ya mjengo kwa jina la uwakilishi wa wale wale watu ambao hawakupata kumfahamu tangu utotoni hadi kupelekwa kwake kijijini kukichukua kiti cha ubunge mara baada ya kurudi masomoni huko Ughaibuni (Marekani).

Ukweli ni kwamba kunakadiriwa kwamba wapo wabunge zaidi ya nusu hivi kwa upande wa CCM ambao si tu kwamba nao walijikuta mjengoni kutokana na hicho hicho kimbunga (Tsunami ya Unyakuzi kura zetu kusema tusivyopenda) cha ajabu kuwahi kutokea katika chaguzi zetu tangu uhuru nchini bali pia husemekana kukinga mkono kwa malipo toka kwa akina EL, AC na RA kila mwezi iendayo kwa Mungu.

Hakika mtu huhitaji kuwa na elimu hata ya sekondari ndio upate kuelewa ya kwamba January Makamba alijiruhusu nafsi yake kutafuta kukiri si na maneno yake kupata kuingizwa katika kumbukumbu zetu rasmi ya Bunge (Parliamentary Hansard) akidai kwa lugha ya mwili wake kwamba yeye ni ZAO HALISI LINALOISHI YA GAMBA LA UFISADI NA UCHAKACHUAJI linaloishi na kuonekana kwa macho. Kijana Makamba anatuthibitishia ya kwamba kweli yeye ni miongoni mwa Watanzania waliobahatika kuota wakiwa ni mbegu na matunda ya UFISADI NA UCHAKACHAUJI ndani ya bunge letu.

Jambo tu ambalo huenda Makamba Junior huenda anatafuta muda muafaka kuja Press Conference kutangazia Umma hadi sasa hivi huenda ni kule kuendelea kubahatika kwake kunawirishwa zaidi na vyeo zaidi na chama chake CCM kukiwemo kukabidhiwa jukumu kubwa na zito ajabu la kupiga vita na hata kubandua kabisa KATI YA MAGAMBA SUGU YA CCM AMBAYO NDIO HASA YALIYOMFANYA AFIKIE HADI HAPO ALIKOFIKIA (akiweza kweli kuyapiga vita mambo haya basi nitavaa mabango na kumpongeza peke yangu barbara zima Dar-Mpaka-Tanga kwa ujasiri wa kuweza kung'ata mkono unaomlisha).

Ndio, ndugu huyu huenda pia anatafuta kututhibitishia kwamba kamwe CCM hakina ubavu wa kujivua hata tone la gamba wakati maambukizi ya magamba zaidi ndio hivyo yameshafikia mbali kiasi hicho!!! Ukweli huu unajikita katika ukimya wake wenye kishindo kikuu tangu atwishwe cheo kikubwa ajabu ndani ya CCM Secretariate mbali na kile cheo cha UKIRANJA Wa Wizara kibao kule Bunge.

Surely, who is all that crazy to ever let off a mousel (tonge mdomoni) that fortune places his mouth just like this happy-go-lucky young Makamba!!!!!!!!!!! With a war on Mega-Graft case with Makamba Junior at the forefront, I may still need to re-think that the more right from now - ndio maana waka Ndiamukama na Mnauye wanapoendelea kuchakaza Edward Lowassa et al platoon, yeye January Makamba wala hayuko jirani kusema lolote juu ya hilo!! Na tangu azawadiwe Ubunge wa Mumbuli na ule Uwenyekiti wa kamati ya kudumu kimojawapo huko bungeni, jambo pekee ambalo jamii ya Tanzania inakumbuka kwake bila kigugumizi ni UDALALI WAKE kuhakikisha ya kwamba makambuni hewa ya EL et al inapewa ulaji zaidi ndio Watanzania tubahatike umeme majumbani na kibaruani.

Nasema kama makanda wapya wa CCM katika vita dhidi ya UFISADI NA UCHAKACHUAJI uliokithiri nchini ni lazima kuhesabiwa January Makamba kwenye safu nzima yenyewe hiyo katika chama hiki kujibandua kule magamba basi ni vema Watanzania tujihesabilie kushindwa kwa vita hivi nchini hata kabla ya kuanza kwa mapambano yenyewe.

Kwa kumaizilia, hakika kama kuna mtu ambaye hivi sasa anajikuta kati ya miamba na nchi kavu katika vile vita vinavyoendelea hivi sasa ndani ya CCM na kikundi fulani kati ya malengo ya KUHAKIKISHA USHINDI WA AGENDA YA URAIS KUBAKI PWANI kwa upande mmoja na vile vya kuhakikisha ya kwamba njia inakua nyeupe kwa kudakia vita dhidi ya UFISADI NA UCHAKACHUAJI chini ya ubatizo wa CCM KUJIVUA MAGAMBA nchini, mtu huyo anaitwa Mishimiwa January Makamba wa jimbo la Mumbuli.
 
MWANANGU NAONA HAPA VINA VIMEKUBALI KAREKODI MIKANDA JUU YA MAGAMBA KABLA YA KUTIWA KAMBA

Aise, hivi vina vimekubali mzee japo vimebeba tu maana ya kishetani kwa walalahoi Tanzania.

Lakini nakuhakikishia ukupeleka hivi vina pale Sound Crafters lazima upatikanaji wa KEY haitosumbua sana na wengi tu ndani ya Chama Cha Magamba watapenda sana kujinunulia japo ka-kanda juu ya magamba ya akina makamba na kule kwao kutafuta kujinyonga makamba na hii dhana sumu kwao.

Hebu tafuta kutoka mwanangu japo maganda kutoka kwao hawa akina Magamba Family mapema kabla Nguvu ya Umma hatujawatia kamba hapo baadaye kidogo.

Watabamba tu kuwa na magamba ni ukomavu kutokuwa na magamba ni uchanga nchi lazima iongozwe na wenye magamba
 
Hivi gamba la CCM kweli limevuka?

Written by Ally Saleh - Zanzibar

mzalendo_balozi-564x272.jpg


Tumesikia mengi wiki iliyopita kuhusiana na Chama cha Mapinduzi ambacho ndicho kinachotutawala hapa nchini, Zanzibar na Tanzania kwa jumla bda ya ushindi wake wa mwaka jana tu.
Chama hiki wiki hiyo iliyopita kilifanya mabadiliko makubwa ya ndani ambayo yamepelekea kujiuzulu taasisi mbili kubwa za ndani na kusaidia kuuna upya tasisis hizo ambazo zilikuwa na majukumu makubwa ndani ya chama hicho kikongwe kabisa nchini.
Tumeona kuwa katika taasisi hizo za ndani sura nyingi mpya zimeingia lakini wengi wakiwa ni wanachama ambao ni vijana kidogo na waliokuwa mstari wa mbele na maarufu toka mwanzo kwa kiasi fulani.
Kwa maneno mengine uundaji mpya wa taasisi hizo za ndani umewasogeza watu ambao tokea hapo baadhi yetu tulikuwa tukiwafikiria wangekuwapo hapo mbele lakini ukiritimba na ukongwe wa chama ulishindwa kutoa nafasi kwao.
Na hili ndilo ambalo limekuwa tatizo la chama hiki ambacho kina mitizamo hadi leo kuwa ni chama kilicholeta ukombozi, japo sicho moja kwa moja, na kwa hivyo fikra ya kukaa katika chama mpaka mtu afie humo inakitawal.
Kila mtu anjua kuwa kelele za kufanya mabadiliko ndani ya chama hicho si za leo wala jana na aliyekuwa akiliengwa wazi wazi alikuwa ni Katibu Mkuu Yussuf Makamba na timu yake ya Serkretarieti, ambayo kawaida hutakiwa iwe ni moyo au mashine ya chama chochote kile.
Tunajua majibu ya Makamba kuhusu kuondoka kwake ili chama kijipange upya, kije na fikra mpya, kije na mikakati ya kisasa yalivyokuwa nab ado chama kilikaaa kimya na kikaingia katika uchaguzi katika hali hiyo ya kuwa kinakosa nguvu, lakini kina fedha na uzoefu na kinashika dola na kwa hivyo nguvu.
Ilionekana wazi kuwa mtindo wa mtu kujiona mkubwa kuliko chama ulikuwa umesaki ndani ya mfumo wa CCM kwa kuwa hakuwa Makamba tu aliyepungukiwa na dira ya kuwa kiongozi, lakini wengine mbali mbali, ila kila mmoja alishikilia alipoweza kubaki uongozini.
Tulishuhduida CCM ikiteua tume kufuatilia mambo kadhaa ndani ya chama hicho kuhusiana na muundano, shutuma za kupoteza itikadi na pia kupungua mvuto wake jambo ambalo kila mtu anajua kuwa lilikuwa katika manada na chama hicho kuwa hatarini kupoteza sifa yake na uwezo wake na kwa hivyo hatarini kukosa utawala.
CCM ilijichukulia kwa ujumla tu kuwa bado ni chama imara, kinachopendwa na ambacho hata ndoto ya kuwa kitapata upinzani haikuwepo kabisa na imekuwa na kauli za kuashiria kuwa itatawala nchi hii milele.
CCM pia kwa sababu za kihistoria iliwahi hata kuwa na kauli kuwa ni chama peke yake ambacho kinaweza kuongoza nchi hii na kwa njia ya amani ingawa huko nyuma Mwenyekiti wake wa kwanza Julius Nyerere, aliye wahi pia kuwa Rais wa Tanzania alishaonyesha dalili ya kuchakaa kwa CCM na kubashiri kuwa inaweza kukosa nguvu za kutawala kama haijabadilika.
Lakini kulikuwa kuna vitu vinavyoipa jeuri CCM mojawapo ni ukubwa wa chama hicho, pili kule kutangulia kuwa madarakani na kwa hivyo kuumiliki mfumo wa utawala, tatu ni kule kuwa na rasilmali na uwezo mkubwa wa kifedha unaotokana na vyanzo mbali mbali.
Kwa hivyo katika hali hiyo CCM ikajiachia. Ikaanza kuwa ni chama kinachokimbia kidogo kidogo wanachama wake, chama ambacho kidogo kidogo kikkaanza kuwa ni cha matajiri, chama ambacho kidogo kidogo kikaanza kuwa cha makundi na chama ambacho kidogo kidogo kikaanza kuwa kinachopoteza itikadi lakini hata baadhi ya misingi yake mikuu.
Serikali ambazo CCM imekuwa ikizinogoza zikaanza kuwa regerege, zenye madai makubwa ya rushwa, zenye madai kibao ya ufisadi, zenye kupoteza uzalendo wan chi hii na zenye kujenga matabaka ambapo wenye nachona wasio nacho wakazalishwa kwa wingi na umasikini ukatamalaki kinyume na neema ambayo wana nchi waliitarajia seuze kuwepo kwa maisha boara kwa kila Mtanzania.
Kwa hivyo kwa fikra zangu ni kwamba CCM ilikuwa na gamba kwa muda mrefu lakini haikutaka kujivua kwa kuwa haikupata msukosuko wowote ule wa kuitisha kuiondosha madarakani.
Gamba ambalo linasifiwa kwa mbwembwe leo kuwa limevuliwa, kwa kweli ni moja tu ya magamba mengi ambayo CCM imejivua lakini bdo ina magamba mengine kadhaa ya kujivua hadi irudi katika hali ambayo tungeitarajia kwa chama kikubwa, makini na chenye uzoefu kama hicho.
Pengine wengine wanasema gamba linalovuliwa leo lilikuwa livuliwe tokea mfumo wa vyama vingi ulipokuja ambapo CCM ilitiwa kishindo cha kuondoshwa madarakani. Lakini tunajua jinsi NCCR ilivyosambaratishwa wakati ilipojitokeza kuwa tishio mwaka 1995.
Tunajua jinsi ambavyo CUF ilivyopigwa vita ilipoanza kwua tishio Bara lakini pia kuwa mbadala halisi wa CCM kwa upande wa uongozi wa kiserikali hapa Zanzibar. Uchakachuaji wa matokeo ya Zanzibar hautaki kuhadithiwa upya.
Kwa mawazo yangu uvuaji wa gamba unaodaiwa CCM kuufanya unatokana na kupata mshtuko mkubwa katika uUchaguzi Mkuu wa mwaka jana ambapo kulikuwa na nafasi kubwa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuchukua madaraka.
Kwa madhumuni ya makala hii sina haja ya kwenda kwenye mdai ya uchakachuaji au idadi ya kura ya chama hiki au kile au kukosekana uwazi au kubanwa chama hiki au kile, lakini nataka niamini kuwa kama kulikwua na wakati CCM ilioona tonge inawatoka Tanzania Bara ilikuwa ni mwaka jana.
Naamini hilo gamba kuvuliwa linatokana na mshtuko huo. Leo tunasikia CCM wakisema kuwa kimepoteza kura za Urais na kupokonywa majimbo kwa kuwa wananchi wanaawaadabisha kwa kutokuwa wasikivu wa vilio vyao. Lakini kweli hwakuwa wakivisikia, kitu ganikiliwafanya wawe na jeuri ya kutovisikiliza?
Kwa hivyo dhana inayojengwa ni kuwa gamba likishavuliwa basi chama kitarudi katika hali yake halisi na kwa hivyo kitaanza kujipanga kiitikadi, kimsingi, kimiundo na hata kiutekleezaji na hivyo kitarudisha mvuto na mapenzi yake kwa umma na wapiga kura.
Hiyo inaweza kuwakweli na pia isiwe kweli. Sio watu wote wnaoweza kuridsha mioyo yao iwapo wamesalitiwa, wameongopewa na wamefanywa ni takwimu tu ndani ya nchi yao na sio wanachama u rais wenye haki, usawa na kueza kuishi maisha yanayo wastahili.
Itategmeea mambo mengi CCM kuweza kurudisha wanachama iliowapoteza huko Bara kwa CHADEMA kama ambavyo tumeona CCM kushindwa kurusisha wanachama wake iliyokuwa imewapoteza hapa Zanzibar na mifano kama hiyo ikiwa nchi zilizopita mchakato kama wa CCM Barani Afrika.
Itategemea sana wanachama na wananchikuamini kwamba nikweli gamba limevuliw? Na jee kwa muda ambao CCM ilikuwa katika “kujisahau” kulikuwa kumeota gamba moja tu? Na jee baada ya gamba hilo ni rahisi kiasi gani kurudi katika uhalisi wa kichama?
Ninavyoamini kuna kazi kubwa sana ya kufanywa na CCM na ikijua kwamba huku yenyewe ikijinadi kuwa imevua gamba, chama pinzani cha CHADEMA kilicho shndikiza CCM kufikia hapa nacho kinajenga hoja kuwa gamba liko pale pale na kwa kweli hasa linazidi kuwa gumu na la hasara zaidi kwa Watanzania.
Maana kwa hakika kujivua gamba ni dhana tu, ukweli ni matendo. Jee CCM itakuwa na ukweli wa matendo? Na umma utaamini maana Waswahili husema Ukitafunwa na Nyoka Unaogopa Ungo’go. Kama muda wote CCM ilipigiwa kelele ikajitia haisikii, jee kwa nini iaminiwe tena haitafnya gamba jengine?
 
Gamba la CCM kuvulika baado ni safari ndefu sana.

Na katika Thread hii hapa kila mara tutakua tukishirikishana kiundani zaidi, juu ya afisa mmoja mmoja ndani ya CCM na kisha CCM chenyewe, ili watu tupate kuelewa kwa nini gamba la CCM halivuliki hata kwa tindikali.

Magamba hapo nje kaeni mkao wa kuvuliwa na Nguvu ya Umma tu na wala si CCM kwa kuwa hakina ubavu wa kufanya hivyo.
 
Katibu mkuu mstaafu wa ccm mh. Philip mangu'la amesema mpango wa kujivua gamba unaofanywa na ccm hautakisaidia chama hicho,badala yake amekitaka kirudi katika misingi na kuwaenzi mabalozi wa nyumba kumikumi.

Source:habari magazetini.
 
huyo PHILIP MANGULA hapo hajanena, ikiisha waenzi ndio ufisadi kwisha.........? dawa ni kurudi katika AZIMIO LA ARUSHA. tena kwa dhati kabisa kabisa.
 
Mzee Philip Mangula siyo mnafiki ndiyo maana amekuwa kimya siku zote. Kweli chema chajiuza na kibaya chajitembeza. Huwezi kulinganisha utendaji wa huyu mzee Mangula na Katibu Mkuu wa CCM aliyejivua gamba bwana Makamba. Kwakweli Makamba alikuwa ni uchuro kabisa na ndiye aliyekifikisha chama hapo pabaya kilipofika
 
makamba ni kiongozi bora anayestahili tuzo ya nobel kwa kurahisisha kifo cha chama chake.kwa hili tutamkumbuka sana
 
Back
Top Bottom