CCM kujivua ‘gamba’ Dodoma

CCM kujivua ‘gamba’ Dodoma

Kama anabusara anatakiwa hadi uo ubunge ajiuzuru ili kulinda chama chake,
Pia Jk anapaswa kutueleza ni wapi alipoutoa ujasiri wa kumnadi jukwaani ilhali alifahamu kuwa ana kashfa ya ufisadi,akishindwa kufanya hivyo naye awajibishwe!
 
Kwa nini kila wakati Lowassa ndiye anayekuwa kondoo wa wa kafara!! Kama kuna mwanaJF ambaye yupo karibu na Lowassa amshauri akubali kujiuzulu lakini aweke wazi siri zote ili hao wanaojifanya wao ndiyo wenye 'moral authority' ya kunyoshea vidole wenzao nao waaibike.
 
Kila kukicha hapa Arusha vijana kwa wazee ni meya atoke ila yeye kwa undani wake hapendi kuona watu wakimkataa kila kona ya Arusha lakini kwa kuwa alishnikizwa na chama hana ujanja inabidi atii, kwa habari za toka jamaa wa karibu baada tu ya uchaguzi Mkuu 2010 kwa ushindani ulivyokuwa hapa Arusha alitaka kujiuzuru naona aliahidiwa umeya ndo maana hakujiuzuru inasemekana aliandika barua ya kujiuzuru baadae akaacha kupeleka hiyo barua mda mfupi tu ndo tukasikia kuwa kapewa umeya sio kuchaguliwa bali alipewa na chama hivo hili gamba sio rahisi kuvulika labda kwa nguvu ya umma.
 
Suala la Lowasa litafuata mtiririko ufuatao:-
1. Kupokea barua ya Katibu Mkuu wa CCM;
2. Kujiuzulu nyadhifa zote ndani ya CCM
3. Kupoteza ubunge
4. Kutokuwa mwenyekiti wa kamati
5. Kurudi Monduli

Hivyo Mr. Mamvi amekaa pabaya! hesabu zake tofauti na matarajio yake LABDA CDM mumpe hifadhi
Je aliyemsifu kwamba ni mchapa kazi wa ajabu hajawahi kuona achukuliweje? Ni gamba au gome?
 
Haujaainisha vizuri uchambuzi wako hasa ukihusisha Marekani na Tanzania. Hayo yote hayatatokea kama Tanzania haitapata KATIBA. Angalia muda uliotumika kuwavua viongozi waandamizi wa CCM uligongana na mchakato wa Mpango wa Katiba feki. Watanzania wachache wameliona hilo. Kama kawaida wanahabari hawakulihusisha wala kuwahoji CCM kwanini wanawahadaa watanzania kwa maslahi yao. Istoshe kutimuana madarakani na kwenye CCM kulikuwepo toka enzi za 'fikra safi za mwenyekiti Nyerere'. Kwa ufupi CCM waliuhadaa wananchi ili kujilinda nampango wao wakulazimisha katiba feki ambao umekwenda mrama. Haya tusubiri sabasaba.
 
Hata mafisadi wakijitoa wote still tatizo litabaki pale palee!!!!!!!!!
Labda wakibomoe na kubadili jna kabsa,, CCM inanuka;
:redfaces:
 
Pia Jk anapaswa kutueleza ni wapi alipoutoa ujasiri wa kumnadi jukwaani ilhali alifahamu kuwa ana kashfa ya ufisadi,akishindwa kufanya hivyo naye awajibishwe!

Mkuu angalia usije ukaambiwa uchochezi.
 
Na jana nimemsikia yule katibu wa UVCCM akisema eti uchaguzi wa meya Arusha haurudiwi kamwe..
 
Ni kweli mafisadi wana haki ya kuanzisha chama chao, lakini sasa CCM yote ni mafisadi kwahiyo unamaana kwamba wabadili tu jina linaloendana na falsafa yao ya sasa ya ufisadi? Tatizo la CCM kwa sasa ni mfumo mzima unaopelekea ku-deviate kutoka kweli malengo yao ya mwanzo ya kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi na kuwa chama cha mafisadi. Hakuna namna unayoweza kumtenganisha Kikwete serikali yake, na kamati zake zote na ufisadi. Wapo watu watasema sio wote ni wachafu ndani ya CCM, ni kweli inaweza kuwa hivyo lakini kwa vile wapo kwenye mfumo mbovu nao ni wachafu pia! Tumeona kwa mfano Pinda akijinadi kuwa mtoto wa mkulima na mtetezi wa wanyonge lakini pengine kutokana na mfumo naye amekuwa fisadi na mwongo pengine kuliko Waziri Mkuu yoyote aliyetangulia. Hivi unapomtoa Makamba mkubwa na kumuingizia Makamba mdogo au kufanya recycling ya watoto wa mafisadi (e.g Nape Mnauye) kwenye nafasi kubwa katika chama unategemea umevua gamba au ndio unali-coat vizuri gamba? Mimi nadhani ni kuongeza speed ya ufisadi na kufanya chama kuwa cha kisultani.
 
Suala la Lowasa litafuata mtiririko ufuatao:-
1. Kupokea barua ya Katibu Mkuu wa CCM;
2. Kujiuzulu nyadhifa zote ndani ya CCM
3. Kupoteza ubunge
4. Kutokuwa mwenyekiti wa kamati
5. Kurudi Monduli
Hivyo Mr. Mamvi amekaa pabaya! hesabu zake tofauti na matarajio yake LABDA CDM mumpe hifadhi

Kwani CHADEMA ndio wanahitaji fisadi afterall ni CDM ndio waliibua hoja ya ufisadi
 
Nionacho uvumilivu sasa umemfika ukomo mh.mamvi, lazima mara hii AUMBUE YOTE NA KUMWAGA MCHELE.
 
Suala la uchaguzi wa Meya wa Arusha lilishahitimishwa na Waziri wa Tamisemi kuwa UCHAGUZI wa Meya Hautarudiwa hivyo CDM wasubiri 2015 na si vinginevyo! :nerd:
 
Hata wakianzisha chama haitasaidia kama jamii bado inawaona ni mafisadi, watapata wapi wanachama? Kama wale ambao jamii inawaamini kwamba sio mafisadi wakitoka na kuanzisha chama chao at least wanaweza kupata wanachama na wakawa na nguvu, hata hivyo haina haja ya wao kutoka either mafisadi au sio mafisadi na kuanzisha chama, kwa kuwa vyama vilivyopo vinatosha waende huko labda kama wanauroho wa madaraka.Huu utitiri wa vyama nao haufai kwa kuwa unawachanganya na kuwagawa wananchi mno, hivyo vinakosa nguvu, vyama vilivyopo vinatosha.
 
kati ya mameya vilaza huyu anaongoza,hana upeo kabisa,lazima watu wa arusha wamwondoe vinginevyo arusha itaendelea kuwa shamba la bibi.
 
Kwa muda wa wiki moja sasa CCM na Makada wake wamejaribu kuilazimisha hii Nadharia ya "Kujivua Gamba"kuingia katika Vichwa vya Watanzania. Wanajaribu kuuhadaa uma wa Watanzania kwamba sasa CCM imeongoka na iko Tayari Kusimamia Agenda za Wananchi. Binafsi nimekaa na Kutafakari sana ni nini Maana ya Gamba linalozungumzwa na Makada hao Vijana Wakiongozwa na Wazee wao. Nimejiuliza Je Gamba wanalolizungumzia CCM ni "WATU"au Gamba ni "MFUMO". Nimekuja kugundua kwamba CCM wenyewe hawajui Aina ya Gamba Walilolivua na Aina ya Gamaba waliloamua Kulivaa sasa.

Kitu kimoja napenda kuwaambia Makada hao wa CCM ni kwamba Kwa Kweli GAMBA walilolivaa sasa hivi aidha kwa kujua ama hata Kutojua LINAWAPENDEZA na LINAWATAMBULISHA vizuri kwa Watanzaia.

Nasema Hivyo kwa sababu

1. Tangia Vita Kali Dhidi ya Mafasadi izinduliwe Pale Mwembe yanga na Dr. W. Slaa Makada wote wa CCM wamekuwa Wakikana Futi Mia na kumwita Dr. Slaa kwamba ni Mwongo na wengine wengi wakatishia kwenda Mahakamani lakini wote walitoweka.

2. Yamekuja Mambo ya Buzwagi, Richmond na Mengine Mengi tukaona namna CCM kutumia wingi wa Wabunge wake kuwatetea wale wote waliokuwa wanatuhumia na hata kuwapoza wale waliojeruhiwa na Vita Hii Takatifu na Kuwaambia eti ni ''Äjali ya Kisiasa"

3. Wengine katika kuwatetea waliwaambia wale wote walio kuwa Upande wa Wananchi kwamba '' Kelele za Mpangaji .......''

Leo CCM inasimama hadharani na Kuwataka wale wote walioodheshwa kwenye List of Shame wawe wamejitoa Ndani ya siku 90, leo CCM inakiri ( Kwa kujua ama kutojua) kwamba Dr. Slaa alikuwa sahihi na sasa iko Tayari kuwatosa wale wote wanaotuhumiwa kwa Ufisadi ( Sijui JK ataponaje hapa).

Ndugu wanajamvi maadam CCM Imekubali Kulivaa "Gamba la Ufisadi" ni Jukumu letu sasa Kulivua Hilo Gamba namaanisha CCM sasa kimekuwa Chama Cha Magamba

Hongera CCM maana sasa Watanzania wanatambua kwamba Mmekubali ninyi ni Chaka la Mafisadi na Kokote mtakakokwenda Mtakataliwa tu
 
Back
Top Bottom