CCM kujivua ‘gamba’ Dodoma

CCM kujivua ‘gamba’ Dodoma

kiukweli swala la udini linazungumzwa sana hata mimi kunawakati linaniumiza na hata sijui hawa ndugu zangu waislamu wamelishwa vipi hii zana inafikia hata wakikujua na wewe ni chadema inakuwa ishu...labda jamaa ana point viongozi waliangalie hili ili na sisi tukae na amani tuikomboe nchi yetu toka kwa hawa mafisadi
 
Hii nchi inaendeshwa kisanii sana.

Mpaka leo hatujui tunafuata mfumo gani wa uchumi, kijamii, kisiasa nk.

Katiba yetu mpaka leo inaongelea ujamaa nakujitegemea wala hakuna anayesumbuka kuona kuna tatizo.

Waziri wa Sheria na Mwanasheria Mkuu wana mtazamo tofauti kuhusu Katiba mpya wala hakuna anayewachukulia hatua badala yake wanaandaa muswada wa kipuuzi tunaanza kupiga kelele usipitishwe! Sasa aliyeshinda ni nani kwa kutokupelekwa Bungeni? Si Waziri wa Sheria na Mwanasheria Mkuu ambao hawaoni umuhimu wa Katiba Mpya? Hata kama ni ushindi wa muda mfupi lakini wameshinda!

Hayo ni ya baadae, hili la kujivua gamba. Shangwe na vifijo vimetawala baadhi ya maeneo kwamba sasa CCM ni safi. Imejivua gamba. Ni mwaka jana tu mwezi wa Oktoba walikuwa wanatafuta Bil. 50 wachaguliwe na kujinadi kwamba wao ni safi.

Raisi aliwanyanyua hao wanaopewa siku 90 wajiuzulu mikono na kusema ni wasafi. Leo anasema wamevua gamba! CCM sasa hivi ni safi.

Kwa maneno yao wanasahau kwamba nyoka huzaliwa na gamba, anakua nalo halafu analivua linaota lingine! Kuvua kwake gamba hakumbadilishi kuwa samaki!

Hizi ndio fikra za CCM. Kwa kuangalia mfano wao wa gamba unaweza kuona ni viongozi wa aina gani.

Lakini kushindwa kwetu kubadili hali iliyopo ndicho kinasumbua zaidi. Wanavua gamba tunawaangalia tu, hatuwapondi kichwa! Tunaamini aaahg! amevua gamba, hana sumu!! Dawa ni kumuua nyoka sio kufukia gamba alilovua.
 
CCM, chama tawala, chama makini kulinda ufisadi na kutetea uovu, chama kilichoshindwa kuleta maendeleo miaka 50 madarakani, chama kinachorithishana madaraka na mengine mengi. ETI kimejivua gamba! Eti na wanaotuhumiwa kwa ufisadi wamepewa siku 90 wajiuzulu ili kukinusuru chama! Magizo ya kutosha, asanteni kwa maigizo yenu. Najiuliza, "kujivua gamba ni kumwondoa huyu Makamba ambaye kimsingi amezeeka au ni kuwafukuza wanaokichafua chama kwa ufisadi wao na kisha kuwafikisha mahakamani." upuuzi mtupu! Nape Nnauye, kaanza kuropoka kama vile hana elimu kichwani. "Wapinzani wacheze ngoma ya CCM, na sio wao CCM wacheze ngoma ya wapinzani". Hakuna utafiti wa kina kuangalia wapi pakuanzia, anaropoka tu. Strategies na targets efective hakuna. . Eti wamejivua gamba, tunashuhudia maigizo na tunaendelea kupata burudani. Nawashauri, wafanye utafiti wa kina wajue ni Watanzania wangapi waliobaki na imani na CCM, ushauri huu ni wa bure tu!kamwe haiwezekani kuendelea kudanganya umma wa Watanzania kwa kauli zilezile toka uhuru hadi leo! Anyway, Nchi nyingi Africa zimeanzisha democracy yao ya ajabu kwamba ukishindwa uchaguzi, mbane aliekushinda na mgawane madaraka ili kumridhisha. Mfano Kenya na Zimbabwe. Haipo mbali tena hapa kwetu Tz kabla ya hili. Baadhi ya chaguzi hapa kwetu zilionyesha CCM hawakushinda ila waliwachezea rafu wapinzani wao na kuwatupilia mbali. Mfano 1995, tukumbushane uovu unaofanywa na CCM, leo wanajivua gamba, lipi na kwa faida ya nani. Watupe mchanganuo wa kina, nini maana ya kuvua gamba.. Msekwa nae anawajia juu Jf kuwa ni tishio kwa CCM, igizo tamu kweli. Wanamtafuta mchawi nje ya CCM wakati mchawi yupo ndani ya yao. Kwani hawajui! Si maigizo haya? Eti wamejivua gamba. Wanadai magwanda sio ujemedari, mropokaji mwingine, kweli mtoto wa nyoka ni nyoka. Hapa gamba limevuliwa au umerithisha madaraka.. Kama vile haitoshi, eti CHADEMA ndo wavaa magwanda na sio ujemedari. Badala yakujipanga na kujua waanze na mkakati gani, wanaanza na CDM!. Sielewi sana, mtachangia wadau na tutapata mawazo chanya yakujenga. Ukweli ni kwamba CCM ni mgando wa bongo. Mindset zimelala. Mwisho wao unakuja. Nawashauri wapinzani wajipange kimikakati kuliko kupigana vijembe na CCM. Wajenge hoja za msingi na kuwaelimisha watu pasipokudanganya lolote. Ukweli utatuweka uhuru na kutupatia mafanikio. CCM waendelee na maigizo yao, tutaendelea kufuatilia movie zao na Watanzania wataendelea kufanya tathmini ili kuweza kuchagua "right party". Ni jukumu la kila Mtanzania kuwapima watu hasa wanasiasa. usiri unaondelea na kuficha uovu ndani ya CCM ni maigizo tosha. Swali, ni nani wa kumvalisha paka kengele. Kuna wakati fulani panya alijitoa muhanga akamvalisha paka kengele ili panya wote watakaposikia kengele wajifiche na kuwa mbali. Paka kwa kujua uwezo mkubwa aliokuwa nao yule panya, walika kimya na mpaka leo hakuna kesi. Yule panya alidai kuna paka anawadhulumu panya maisha kwa kuwaibia mali na rasilimali zao. Panya aliwataja paka kwa majina kuwa ni "mafisadi papa". Panya wengi waliwatambua wazi, panya aliejitolea kumvisha paka kengele alikosa support akaamua kukaa kimya. . Wale paka wezi waliendelea kuiba bila hofu huku panya wanateseka na ktda.
 
Wakati taifa likishuhudia CCM wakikubali kuwa wao wanazalisha mafisadi serikali kwa kuwaruhusu wanachama wake kupata fedha za wizi bila ya kufanya kazi na kulipa kodi, huku wakiwaacha bila kuwafikisha mahamani. Ina leta maswali mengi ya ktaka kujua kwamba ndani ya chama hicho ni nani asiye fisadi.

Hawa wenzetu wameamua kubadili mahakama kuwa ni chama cha siasa, wametambua kuwa wanatuibia na wanaendeleza kile tunachokipigia kelele kila siku, mwizi apelekwe mahakamani halafu segedance. Kutuambia kwamba wao ni mafisadi wanatuibia halafu kusema watawatoa tu wale walitajwa bila kuwa na uthubutu wa makusudi kuwafilisi na kuwaburuza mahamani unakuwa uhuni .

Ufisadi wanaotufanyia ni pamaoja na kuulinda ufisadi kwenye mwavuli wa siasa. Mwenyekiti wa CCM ndiye Raisi wa Jamhuri, anateua idadi kubwa ya watendaje serikali na hao nusu yao ni mafisadi papa na dagaa. Ana usalama wa taifa unaomletea taarifa kila siku nani kaiba nini, wapi na saa ngapi. Nani kakwepa kodi wapi na kwa vipi. Nani kaiba kura wapi na kwa vipi. Malori yalitoka vipi bot nani alipeleka fedha bank nani alichukua fedha bank za epa, meremeta, tangold, nk. Sasa huu usanii wa kutupiga mchanga eti kujivua gamba wakati wezi wana kuwa huru kimazingaombwe mimi sita kubali hata kidogo.

Kwa uchungu huu nitazunguka nchi nzima kuwaeleza wananchi kuwa wanaibiwa na CCM na wanadharauliwa kwa kiwango cha juu sana. Tuandamane nchi nzima kutaka fedha zote zilizoibwa na mafisadi wa CCM zirudishwe kuanzia zile zilizomwingiza mkuu wa kaya ikulu.

Mode ukifuta hii naomba sababu ya msingi. Umenifutia tatu so far. Ila mimi sita kaa kimya mpaka nifutwe na mimi. Nikiacha kuwatetea watanzania kakaa kaa langu liungane na ulimi.
 
Katika mwonekano wa kawaida unaona kwamba mwendesha Bunge analiendesha kibabe!Na wabunge wa chama tawala wanafata mkumbo na wanaendeshwa kwa ushabiki tu hakuna kingine!
Hivyo unakuta hakuna tija katika uwakilishi wa wananchi kwenye Bunge!!!
 
Najua bado kuna wadanganyika wengi tu Tanzania, wanaofurahia kujivua gamba, lakini CCm ikijivua gamba kweli, ili ibaki safi, itakuwa chama kama chama cha upinzani kidogo kuliko chochote.
 
Lissu na wabunge wote wa CDM wako straight forward na wako kwa ajili ya taifa letu. Hata kina CHEYO, LYATONGA, HAMAD RASHID na wengineo ni wazuri ila njaa inawaondolea confidency na hivyo kuwa pale kama hawapo. Tamaa mbaya. Unaambiwa ukitaka kukosa haki na kuuza uhuru upende offer na ku solicit vi msaada vya hapa na pale. Unajimaliza chap. Wale wa magamba kati ya 300 hawazidi kumi wenye uelewa. Wengine wote ni wapo kama hawapo. Itafikia wakati kizazi kitakuwa kipya na hakutakuwa na nafasi zao tena. Msiangalie Cv tu ndugu zanguni. Elimu ni kwa upana wake. Waweza kuwa hata prof but ukaendelea kuwa upo kama haupo. Ni knowledge na understanding vinapaswa kuwa pamoja ndo uweze kupata kazi ya kuwakilisha sheria. Ni ngumu kumsimamia hakimu wakati hujui chochote kuhusu sheria. Na wabunge wa magamba wamepuuza hoja hiyo. Hebu fikiria hili la madiwani kumsaili daktari au nesi au hata mhasibu. Kituko my bros and sis. Poleni sana.
 
Unaushahidi ya kuwa cdm wanapewa fedha toka mataifa ya nje? au umekurupuka ukaona usitoke JF bila kuandika ki2 leo?.. Rafiki ulionao wote ni wa dini moja? Mbona Vyuo,Shule, wafanyakaz wanaendelea na shughuli zao kila siku sijasikia watu wakipigana kwa sababu ya udini?. Au wewe unamaanisha nini unaposema udini? Tafakari kwanza kabla ya kupost thread yako uone kama ina logic au la!
 
Wewe ndugu yangu naona U ccm unakuumiza ongelea maendeleo ya nchi acha UTWANA...

sio siri chadema ndio chama kikuu cha upinzani kwasasa lakini kimekuwa kina kashfa nyingi sana kama vile swala la udini,ingawa walijaribu kumuita kundini prof safari ili kufuta dhana ya udini lakini bado swala la udini halijafutika mioyoni mwa watu,pia liko swala la kupewa fedha na mataifa ya nje,liko swala la ukabila,pia liko swala la vurugu,mfano hai ni pale mbunge machachari Godbless Lema alipotamka live bungeni kuwa milango ifungwe watu wapigane!(mwananchi ya leo) hivi kweli mtu aliyepewa dhamana na wananchi anaweza kutamka maneno kama hayo katika chombo kikuu cha maamuzi nchini?? sasa je chadema kuvua gamba na kuwa na sura mpya katika macho ya watu?
 
Hayati Mwalimu nyerere aliwahi kusema kazi mojawapo ya bunge ni kuipa 'misukosuko' serikali(rejea hotuba za mwalimu) hivyo wabunge wawapo bungeni wanategemewa kuihoji,kuisimamia na kuishauri serikali juu ya mambo ya msingi yanayohusu taifa.sijui ni nini kilichomfanya mwalimu kutoa angalizo hili lakini naamini alikuwa sahihi.
Kitendo kilichofanywa na wabunge 'majority'ambao naamini ni wa ccm ni cha kusikitisha sana!hivi ni kweli wananchi hawataki uhuru kamili wa mahakama?ni kweli hawataki mahakama ziwezeshwe kiuchumi ili kuengeza tija na ufanisi?je wabunge mliopinga hoja ya mh.TUNDU LISSU mlifanya consultation kwa waajiriwa wenu(wananchi) na mkaona ni vyema kuipinga hoja hii?

Waheshimiwa wabunge(ccm) nyinyi ndio majority hivyo uzembe wote utakaotokea kipindi cha 2011-2015 kupitia bunge mtawajibika.

Bado mna magamba mnayohitaji kujivua,style mnayoitumia ya 'kwaya' ya ndioooooo au siooooo kwa manufaa ya chama na kuiacha serikali ipitishe mambo bila kupingwa itawagharimu!
Achaneni na mambo ya "NAUNGA MKONO HOJA KWA asilimia 100 LAKINI..."
mambo ya chama yatengane na mambo ya serikali ili tuhuma za chama zisiwe za serikali.leo chama chenu(ccm) kimejibebesha lawama za serikali na watazamaji watawahukumu kwa hilo.


Jiulizeni ni wakati gani wabunge kama Sitta,mwakyembe,selelii,kilango na ole sendeka walipata au wanapata sifa nzuri mbele ya wananchi?jibu mnalo kama hamuelewi mni-pm.

Poleni kwa majukumu na tukutane mnadani,M.k na kwenye ile tafrija yetu ya TDL.
 
Kiukweli,sizani kama wabunge ccm wa ccm wanajua wanachotengeneza. Kwangu naona wanasaidia kukiua chama chao, kukiongezea maadui, na kukionyesha ujuha kilionao.
Kukataa hoja kwa vile tu imeanzishwa au kutolewa na mtu wa upinzani ni jambo la hatari na la kiwendawazimu.
Sizani kama yupo mwananchi anayeathiriwa na mfumo wa maisha sasa atakayeshabikia utumbo huo.
People's power ndio itaamua.
 
Mmekuwa na tabia ya kupuuzia mambo na kukumbuka shuka wakati kumekucha! Badilikeni mapema.
 
Samaki akikwanguliwa gamba tunamla lakini nyoka akijivua gamba sumu yake iko palepale ukifanya mchezo anakuuma na unakufa hivo haleti tofauti yeyote zaidi ya yeye kujifuhia ngozi yake tu kubadilika.
 
Wote wanaoimba kwaya ya ndiyoooooo ....... kwa mambo yasiyo ya msingi na kinyume chake majina tunayo na tutawashughulikia sisi waajiri wenu,tunategemea baadhi yenu mtakuja kuomba kura tena 2015
 
Siri ya ‘gamba’ CCM yaanikwa

Imeandikwa na Na OSCAR MBUZA; Tarehe: 16th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 250; Jumla ya maoni: 0








CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), hatimaye kimetoa siri hadharani ya sababu zilizokifanya kujivua gamba ili kuzaliwa upya kwa lengo la kurejesha imani na umaarufu wake machoni
mwa wanachama wake na wananchi.

Akihutubia maelfu ya wanachama wa chama hicho na wananchi waliojitokeza ili kuilaki
Sekretarieti mpya ya chama hicho katika viwanja vya Bakhresa, Manzese, Dar es Salaam Jumapili, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa alisema zipo sababu sita zilizokifanya chama hicho kujivua gamba.

Alisema matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini kote mwaka 2010 yalitoa ishara
kwamba chama hicho kimeanza kupoteza umaarufu wake na wananchi kukosa hatua iliyomfanya Rais Kikwete kuunda Kamati Maalumu ya watu sita, iliyowajumuisha wataalamu
wasio wanaCCM ili kuchunguza kiini cha chama hicho kuanza kupoteza umaarufu na imani
kwa wananchi kwa kasi, Kamati iliyokuwa chini ya Wilson Mukama.

Alisema tathimini ya Kamati ya Mukama, ilieleza sababu kuu sita zilizosababisha wananchi
kuikataa CCM na kuwapigia kura chache mgombea wa urais kupitia chama hicho, Rais Kikwete,
wabunge na madiwani na kukifanya chama hicho kupoteza viti vingi vya ubunge wa majimbo
na wa viti maalumu, hatua iliyofanya ruzuku kupungua.

Alisema Kamati hiyo ilieleza kwamba CCM ilikuwa imebebeshwa mzigo mzito wa kuwa na wanachama wanaoshutumiwa na wananchi kuhusika katika vitendo vya ufisadi na rushwa
na hivyo wananchi kuwaona viongozi wote wa CCM kama ni mafisadi na wala rushwa.

“Hili lilikuwa ni tatizo la kwanza na Mwenyekiti (Rais Kikwete), alichukua hatua kuonesha kuwa sisi si mafisadi wala hatuukumbatii ufisadi na hivyo tumeamua kwa dhati kwamba tutaachana na wanachama wote wenye sifa hizo.”

Kamati ya Mukama pia ilitueleza kwamba kulikuwa na mfumo mbaya wa uendeshaji wa chama hicho, ambapo madaraka kutoka ngazi ya Taifa yalikuwa yakiruka ngazi husika kwa viongozi wa kitaifa kwenda ngazi za chini kutoa maelekezo badala ya kufuata muundo wa Taifa, Mikoa, Wilaya, Kata na Mashina.

“Hili liliwafanya viongozi wetu wa chama kushindwa kuwa karibu na wananchi na hivyo kupoteza ushawishi wa chama chetu machoni mwa wanachama na wananchi kwa ujumla.

Kamati ilitushauri na sasa tutaanza mara moja kufuata muundo unaokubalika.” Aliitaja sababu ya tatu kuwa ni hali ngumu ya maisha ya Watanzania, ambapo wataalamu walisema chama hicho kimeshindwa kusimamia na kurahisisha maisha ya wananchi na hivyo kushindwa kusimamia kwa vitendo kaulimbiu yake ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania.

“Hali ya maisha ipo juu, kuna mfumuko mkubwa wa bei na matatizo makubwa ya kiuchumi.
Wataalamu walisema wananchi sasa wanauliza maisha bora kwa wananchi yapo wapi. Hili
tumelichukua kama changamoto na tunapaswa kulifanyia kazi mara moja.”

Sababu ya nne kwa mujibu wa Msekwa ni kukosekana kwa nguvu za vijana katika ushawishi
na badala yake chama hicho kuwakumbatia zaidi viongozi wazee; ”Walituambia mnayo
hazina kubwa ya vijana lakini hamuwatumii vizuri na tulilichukua hilo na kuanza kulifanyia
utekelezaji mara moja.”

Msekwa aliitaja sababu ya tano kuwa ni kuwepo kwa makundi miongoni mwa wanaCCM, ishara iliyojionesha wazi katika Bunge lililomaliza muda wake mwaka jana, hatua iliyomfanya Rais Kikwete kuunda Kamati chini ya Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, Msekwa na Abdulrahman Kinana ili kubaini kiini cha makundi hayo.

Sababu ya sita ni CCM kuwapelekea wananchi wagombea wasiokubalika kila uchaguzi unapowadia, hatua aliyosema itafanyiwa kazi ili kutafuta muundo mzuri wa kuwapata wagombea wa CCM wanaokubalika na wananchi. Kwa mujibu wa Msekwa, mbio za urais mwaka 2015, ilikuwa sababu nyingine iliyokuwa inakitia kitanzi chama hicho kutokana na kuibuka kwa watu walioanza kujipanga kwa nafasi hiyo na kukwamisha utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa mwaka 2010/2015.

Alisema sasa CCM inatafuta mfumo mzuri na muafaka wa kumpata mgombea. Alisema kujiuzulu kwa Sekretarieti na Kamati Kuu ya chama hicho ngazi ya taifa ilikuwa ni hatua ya kwanza ya mageuzi ndani ya CCM na kwamba mageuzi hayo yatafuata katika ngazi za mikoa, wilaya, kata na mashina.

“CCM baada ya kupokea mapendekezo yale ndio maana ikamteua kiongozi wa kamati ile
(Mukama) kuwa Katibu Mkuu wa chama ili kusimamia mabadiliko hayo na kujenga CCM mpya.

Njia kama hii aliwahi kuitumia Mwalimu Nyerere (Julius-Baba wa Taifa), pale tulipokuwa tunaunganisha TANU na ASP ambapo mimi niliteuliwa kusimamia kamati ya kuangalia namna ya kuwa na muundo mzuri wa chama na nilipomaliza akanikabidhi kazi ya Kuwa Katibu Mkuu Mtendaji wa CCM,” alisema Msekwa.

Naye Halima Mlacha anaripoti kutoka Chalinze kwamba CCM haijakosea ‘kujivua gamba’ na kuchagua viongozi wake wapya wa Kamati Kuu na Sekretarieti na kwamba kazi iliyopo mbele yake sasa ni kubadili taswira ya chama hicho iliyochafuka.

Pia viongozi wa chama hicho wapya walioteuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa NEC ya chama hicho hivi karibuni, wameendelea kusisitiza kuwa, hawatavumilia wanaokiharibia chama hicho na kutaka suala la ‘kuvua gamba’ lifike ngazi za chini.

Akizungumza katika hafla ya kuwapongeza viongozi hao wa Kamati Kuu na Sekretarieti ya
CCM, iliyofanyika Chalinze na Kibaha mkoani Pwani, Makamu Mwenyekiti, Bara, Pius Msekwa,
alisema kilichofanyika ndani ya chama hicho ni kubadili taswira mbaya na kuijenga CCM mpya.
 
PHP:
Alisema matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini kote mwaka 2010 yalitoa ishara 
kwamba chama hicho kimeanza kupoteza umaarufu wake na wananchi  kukosa  hatua iliyomfanya Rais Kikwete kuunda Kamati Maalumu ya watu  sita,  iliyowajumuisha wataalamu 
wasio wanaCCM ili kuchunguza kiini cha chama hicho kuanza kupoteza umaarufu na imani 
kwa wananchi kwa kasi, Kamati iliyokuwa chini ya Wilson Mukama. 
 
Alisema tathimini ya Kamati ya Mukama, ilieleza sababu kuu sita zilizosababisha wananchi 
kuikataa CCM na kuwapigia kura chache mgombea wa urais kupitia chama hicho, Rais Kikwete, 
wabunge na madiwani na kukifanya chama hicho kupoteza viti vingi vya ubunge wa majimbo 
na wa viti maalumu, hatua iliyofanya ruzuku kupungua.

Kumbe Mukama ndiye yule "consultant" wa CCM ambaye aliitupia madongo JF.........................................kumbe hajui mchawi wa CCM yumo ndani ya CCM na kwa hiyo ushauri wake wa kulaumu walioko nje ya CCM ni kuipotosha CCM.....................
 
PHP:
"CCM baada ya kupokea mapendekezo yale ndio maana ikamteua kiongozi wa kamati ile 
(Mukama) kuwa Katibu Mkuu wa chama ili kusimamia mabadiliko hayo na kujenga CCM mpya.

Tatizo kwa CCM ni..........can Mukama be a judge of his own cause?????????????????????????????????
 
Hakuna cha gamba wala ngozi mpya,wizi mtu.wananchi wanaumia tangu zamani na wakapata nguvu ya kulalamika dhahiri tangu 2007 wao kazi yao ikawa ni kujibu vibaya tu eti wao wasafi sana,tena huku mwenyekiti wao akitabasamu na kufurahia majib yao na yake pia.sasa leo 2011 kimewasibu nini?hatudanganyiki!wamesahau kama huyo mkapa wao aliwaita wananchi makokoto kwnye kuhitimisha kampen zao za mwaka jana!ccm inakisukari kikali na tiba yake kwa sasa ni kukata shingoni.obvious lazima ife.waache kutapata kwa kukata kidole na sukari ishafika shingon.shame on them
 
1: matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini kote mwaka 2010 yalitoa ishara
kwamba chama hicho kimeanza kupoteza umaarufu wake na wananchi kukosa hatua iliyomfanya Rais Kikwete kuunda Kamati Maalumu ya watu sita, iliyowajumuisha wataalamu
wasio wanaCCM ili kuchunguza kiini cha chama hicho kuanza kupoteza umaarufu na imani
kwa wananchi kwa kasi, Kamati iliyokuwa chini ya Wilson Mukama.
2:Mfumo mbaya wa uendeshaji wa chama,ambapo madaraka kutoka ngazi ya taifa yaliruka ngazi husika ya viongozi wa kitaifa kwenda ngazi za chini kutoa maelezo bila kufuata mfumo wa kitaifa,mkoa,wilaya,kata na mashina.
3:“Hali ya maisha ipo juu, kuna mfumuko mkubwa wa bei na matatizo makubwa ya kiuchumi.
Wataalamu walisema wananchi sasa wanauliza maisha bora kwa wananchi yapo wapi. Hili
tumelichukua kama changamoto na tunapaswa kulifanyia kazi mara moja.”
4:Kukosekana kwa nguvu ya vijana katika ushawishi na badala yake kuwakumbatia wazee.
5:Kuwepo makundi miongoni mwa wanaCCM.
6:CCM kuwapelekea wananchi wagombea wasio kubalika kila uchaguzu unapowadia epecially mafisadi.
 
poll.png
Hapana huu ni ubabaishaji wa siasa za maji taka, wanazunguka mbuyu 290 54%

Ni bora wakifutilie mbali na kuanzisha chama kingine, gamba huwa linakomaa tena
105 19.6%

Ndiyo kutaimarisha chama, na kuja na mikakati mipya ya kujenga nchi
77 14.3%

Wataleta mabadiliko ya nukta baadaye watarudi katika hali yao ya ufisadi
65 12.1%
 
Back
Top Bottom