Kinachoendelea ndani ya CCM ni vita ya makundi, yaani kundi la Lowassa na kundi la kina Sitta. Kwa nje CCM inaonekana imejivua gamba yaani imevaa uupya kitu ambacho hakipo.
Ukitaka kuja hali hiyo wasikilize wakiwa majukwani, ni vijembe, kupayuka, propaganda sana. Kujisifu sana kwamba wana serikali sikivu kitu ambacho hakipo. Wanalumbana na wapinga ufisadi nje ya CCM.
Naona kinachoendelea ni furaha ya kundi moja ndani ya CCM kupewa nafasi kupiga vita kundi lingine.
Ni vita kati ya mafisadi wakubwa na wadogo.