Source: Magazeti ya Rai, Alhamisi Aprili 14-20,2011;na Mtanzania Jumatano APRILI 13,2011;
kATIKA Rai nimevutiwa mno na nukuu za viongozi wapya hawa wawili, Nape Nnauye, Katibu wa Itikadi na Uenezi; na Katibu wake Mkuu Wilson Mukama:-
Nape: Uk wa 2 "Kuna mapinduzi makubwa yanakuja. Maadili kwa wengi wao yamepotea. Kwa hiyo basi nawaomba wajipange upya kama kuna mtu anajiona ni mchafu na hataki kubadiklika basi ajiondoe kabla ya kuondolewa,"
Wilson: "Ni lazima tukijenge upya chama chetu, watu wenye kashfa watalazimika kujiondoa wenyewe kabla hatujawafukuza."
Katika Mtanzania nimevutiwa na taarifa hii ya kipekee:-
Kichwa cha habari iliyopewa uzito wa kwanza kwamba "CHILIGATI, NAPE WAMCHIMBA JK" Kichwa hiki kiliambatana na habari iliyosheni utamu kwamba Chiligati na Nape saa chache baada ya kushika nyadhifa hizo wameanza kumchimba Mwenyekiti wao, Rais Jakaya Kikwete; , ambaye kwa mujibu wa habari hizo ni kwamba ni mtuhumiwa wa 11 kwenye orodha ya watu wanaotuhumiwa kuwa mafisadi kwa mujibu wa orodha ya LIST OF SHAME ya iliyosomwa na CDM DSM Mwembeyanga miaka kadhaa iliyopita nakurudiwa katika viwanja vya Jangwani mwaka jana 2011; na mpaka leo ushahidi wa dhahiri umethibitisha kulingana na kashfa za EPA, KAGODA, RICHMOND, DOWANS, IPTL, nk.
Bila shaka matamko ya aina hii yanazidi tu kujenga maswali mengi zaidi ndani ya waTz wanaofuatilia utekelezaji wa dhana ya Kujivua Gamba yenye Kaulimbiu "Towards New CCM"
Wakati nikitafakari kama kweli kuvua gamba kwa staili hii kutazaa CCM Mpya, nilikumbuka maneno ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CDM kwamba CCM inaumwa kansa kwenye damu, na siyo kwenye gamba; tena nikajuiliza kwamba hawa jamaa Nape na Chiligati ni wazao wa hawa wazee wanaotuhumiwa??? Je wana ubavu wa kutikisa hili dude CCM bila support ya waasis wa ufisadi walioenguliwa katika CC ya CCM na kupewa eti siku 90 kujitoa wenyewe!!!!!!!!!! WanaJF hivi JK naye yumo kwenye hizo siku 90????? YETU MACHO NA MASIKIO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!