- Habari yako mkuu haiko sawa, CCM Mkoa wa Bukoba kwa katiba ya CCM Taifa haina Mamlaka ya Kumfukuza Diwani ni Kamati Kuu ya CCM tu ndiyo yenye huo uwezo, Mkoa unaweza kuwasimamisha tu na kusubiri maamuzi ya Kamati Kuu ya CCM kama kusimamisha huko ni kwa halali su sio halali, lakini kufukuza ni Kamati Kuu tu ndio yenye huo uwezo, so hii habari haiko sawa.
- Madiwani hao 8 tayari wameshaandika kwa CCM Taifa kuiomba itengue uamuzi huo ambao umefanywa na Viongozi walio upande mmoja wa Vita kubwa ya kisiasa ambayo imekuwa ikiendelea katika Manispaa na jimbo la Ubunge la Bukoba Mjini.
- My Take ni CCM Mkoa wamekurupuka na kujidhalilisha sana na this ishu, kwa sababu bado Madiwani wanaweza kwenda Mahakamani na kubaki na Udiwani wao, uwezekano wa Madiwani hao kufukuzwa na Kamati Kuuu sidhani hata kama upo, kwa kuzingatia sababu za msingi zilizowapeleka CCM Mkoa kuwasimamisha, ni aibu sana kwa Viongozi wa Mkoa wa CCM, tena mmoja Katibu Mkuu wa Mkoa akiwa ni rafiki yangu wa karibu sana, ameniskitisha sana na this!!
Le Mutuz