CCM Kagera yawafukuza madiwani wake 8

CCM Kagera yawafukuza madiwani wake 8

Waitu congratulation wote aambao mumeona kuwa inchi inaenda kubaya mwakora muno kasinge waitu.wacha nikapete karubisi kangu kure kikomera!nasubiri taarifa baaadaye!
 
tayari hizo kata ni zetu kilainiiiii,M4C piga kambi huko mapema,ila hao madiwani ni wazalendo nashauri wajigeuze waje wavalishwe magwanda wagombee kwa tiketi ya chama chetu cdm,mnaonaje wadau?

Wale waliogombea 2010 wakashindwa mtawapeleka wapi?
 
Kwa hali hii CCM wata warudisha madiwa wote kisingizio wame wasamee.
 
Pamoja na kwamba Mwanzilishi wa thread hii ameforge na Kuchakachua ni dhahili kwamba Watanzania wamekomaa Kisiasa. Swala hapa Si CHADEMA wala CUF Kuwachukuwa Madiwani waliofukuzwa CCM , issue hapa ni kwamba Watu wamechoka , na hata ndani ya CCM kwa sasa wameamua kusema "Liwalo na Liwe" Maana "hamna Namna nyingine ya Kupambana na dhuruma ya CCM". Madiwani hao Wameonyesha Ujasiri Mkubwa na inabidi iwe mfano wa kuingwa kwa almashauri zingine zenye matendo ya Kifisadi. Kwa MaCCM ukizigatia upepo wa Kisiasa nchini naweza sema kwao hii ni Political Miscalculation kwani kwa kuiga CHADEMA's political strategy ya walivyowa fukuza Madiwani wao jijini Arusha, Itawagharimu Asilani. Swali ni Je CCM wakiingia Kwenye Uchaguzi leo hii Watavirudisha Viti hivyo???? na Je Madiwani waliotimuliwa wana support ya wapiga kura kwa kile walichokisimamia hadi wanafukuzwa Chamani???, Mwisho kabisa Uchaguzi Ukifanyika leo na ikatokea CCM Imeshindwa Kuvirudisha Viti hivyo vya Madiwani waliowatimua basi Watanzania Watakuwa Wamepata Somo zuri nalo ni "Ukiwapinga waziwazi na ukapambana na Mafisadi & Ufisadi ndani ya CCM ni dhambi Kubwa kama ugojwa wa Ukoma, baba wa taifa.
 
ni baada ya vikao na majadiliano ya muda mrefu yaliyofanywa kwa usiri mkubwa na viongozi wa chadema taifa kwa kushirikana na viongozi wa chadema mkoa wa kagera kwa lengo la kuwashawishi madiwani wa ccm kuendelea na mgomo wao dhidi ya vitisho wa wakuu wa ccm huku lumumba kwa kuwaahidi kuwapokea na kuwapa nafasi ya kugombea kata husika ikiwa watafukukuzwa ndani ya ccm.kwa mujibu wa nyaraka zilizopatikana madiwani hao wameagizwa kutoyakatia rufaa maamuzi ya ccm mkoa ya kuwavua uanachama mahakamani au ngazi za juu za ccm kwa luwa watapewa nafasi za kugombea kata husika bila kipingamizi.
hili linakuja baada ya vuta nikuvute ya muda mrefu kati ya madiwani 8 wa ccm walioamua kuuasi uongozi wa ccm huko kagera na kuamua kuungana wa wapinzani yaani cuf na chadema kupinga mipango ya ufisadi inayoratibiwa na meya wa manispaa ya bukoba akishirikianna na baadhi ya viongozi wa ccm mkoa na taifa wenye masilahi katika ufisadi huo kwa kutumia kampuni nyingi zilizoibuliwa kama uyoga kwa ajli ya kula fedha za manispaa.
kinachoendela kwa sasa ni kuwa kuna mkurugenzi mmoja wa chadema aliyetumwa kagera kwa ajili ya kukamilisha mpango huo mapema usije ukatekwa nyara na cuf.
mpango huu umelenga kuiangamiza ccm ndani ya kanda ya ziwa kuelekea uhaguzi mkuu 2015.tusubiri tuone

Hapo kwenye red; sidhani kama kile chama mfu cha Sheikh Ponda kina jeuri hiyo.
 
Hawa ndio wapinga ufisadi ndani ya CCM. wengine jifunzeni kutoka Kagera. Urafi na unafiki wa Wabunge na Madiwani wa CCM mikoa ndo inaimaliza nchi. Shikilia hapo waungwana. Hakuna kukata rufaa CCM, Rufaa ikatwe kwa wananchi waliowachagua.
 
unajua CCM wanacheza ngoma wasiyoijua na waache kuiga maana unawafukuza madiwani wazarendo na kuukumbatia usaliti na ufisadi, kweli hizi akili ndogo katu haziwezi kutawala akili kubwa! Hizo kata zote zitaenda kwa CHADEMA.
 
katika jambo lakushangaza nikuona viongozi wa CCM kagera wakiogopa kumfukuza mbunge wa Bukoba mjini ambaye pia niwaziri ndugu Kagasheki wakati wakijuwa kuwa yeye ndiyo chanzo na alitamka kwenye mkutano wakati Rais akiwa ziarani mkoani Kagera kuwa hawezi kufanya kazi na meya nakumchongea meya mbele ya Rais na wananchi leo wanaofukuzwa ni madiwani pekee hili nijambo la ajabu. Kama kiongozi wakwanza kutokuwa naimani na meya nimbunge Kagasheki.
Ushauri wabure kama mnaubavu mfukuzeni na Mbunge Kagashe
 
It is very very interesting kwamba kwa CCM wanaopinga ufisadi ndio hufukuzwa katika chama lakini yale mafisadi, majambazi, majangili, na mauza unga yaliyokubuhu ndio kwanza yanaachwa na hata kupewa nafasi za juu za uongozi katika chama, serikalini, na bungeni.

Hili linashangaza sana! Hivi CCM wanaweza kuwaeleza wananchi sababu ya msingi na inayoingia akili ya kuwafukuza hao madiwani zaidi ya bla bla za kisiasa za akina Nape?

wale madiwani walikuwa na roho za cdm ningeshauli uongozi uwape chaka haraka.
 
Nimeamini kweli ukipinga ufisadi,ujangiri,u drug dealer,uonevu,ukandamizwaji ,rushwa etc CDM is the right place to stand with-karibuni wana wapotevu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Bw Avelin Mushi amemaliza Press Conf hivi punde na kufafanua kuwa kikao cha Halmasahuri Kuu ya mkoa wa Kagera imemaliza kikao chake hivi punde na kuamua madiwani 8 wa Manispaa ya Bukoba kufukuzwa katika chama na kufutiwa nyadhifa za udiwani kutoka na mgogoro uliokuwa ukiendelea.

Waliofukuzwa ni:

1. Richard Gaspar (Miembeni )

2. Murungi Kichwabuta (viti maalum)

3. Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe)

4. Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai)

5. Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga)

6. Robert Katunzi (Hamugembe)

7. Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na

8. Dauda Kalumuna (Ijuganyondo).

Katibu huyo ameongeza kuwa madiwani hao wanaweza kukata rufaa kwa ngazi za juu za chama wakiona hawakutendea haki na kuwa ngazi ya mkoa ina mamlaka ya kufanya hivyo kwa madiwani wa ngazi hizo.

Aidha amesema kwa Bw Yusuph ngaiza amabye ni mwenyekiti wa CCM bukoba,nafasi yake hiyo inasubiriwa ngazi za juu amabazo ndizo zenye mamlaka juu yake(kwa cheo hicho)

Manispaa ya Bukoba ina kata 14 na kati ya hizo kata 4 zinaongozwa na CDM(2) na CUF(2) hivyo kwa Bukoba mjini CCM imebakiza madiwani 3 TU wa kuchaguliwa .kama ifuatavyo
1.Kashai-Amefukuzwa
2. Miembeni-Amefukuzwa
3.Miembe-Amefukuzwa
4.Nyanga-Amefukuzwa
5.Hamugembe-Amefukuzwa
6.Kitendaguro-Amefukuzwa
7.Ijuganyondo-Amefukuzwa
8.(1)Kagondo-Amebaki (CCM) (Meya Amani)
9.(2)Nshambya-Amebaki(CCM)
10.(3)Kahororo-Amebaki(CCM)
11.Bilele-Amebaki(CUF)
12.Kibeta-Amebaki(CHADEMA)
13.Bakoba-Amebaki(CUF)
14.Rwamishenye-Amebaki(CHADEMA)
XXXXXXXXXXXXX

Kujua historia ya chanzo cha yote hapa fungua hapa chini.
Historia ya mgogoro wa kisiasa Bukoba manispaa


Baadaye nitaingiza video.

Kagasheki yeye amenusurika kwa kuwa ni diwani kwa mujibu ya sheria ambapo mbunge automatically ni diwani kwenye halmashauri yake (nilirejea uzi aliouleta KAUDO kuhusu madiwani 9 akiwemo Kagasheki kugomea kuhudhuria baraza la madiwani na ndio maana 8 wamepigwa chini)
 
Last edited by a moderator:
- Habari yako mkuu haiko sawa, CCM Mkoa wa Bukoba kwa katiba ya CCM Taifa haina Mamlaka ya Kumfukuza Diwani ni Kamati Kuu ya CCM tu ndiyo yenye huo uwezo, Mkoa unaweza kuwasimamisha tu na kusubiri maamuzi ya Kamati Kuu ya CCM kama kusimamisha huko ni kwa halali su sio halali, lakini kufukuza ni Kamati Kuu tu ndio yenye huo uwezo, so hii habari haiko sawa.

- Madiwani hao 8 tayari wameshaandika kwa CCM Taifa kuiomba itengue uamuzi huo ambao umefanywa na Viongozi walio upande mmoja wa Vita kubwa ya kisiasa ambayo imekuwa ikiendelea katika Manispaa na jimbo la Ubunge la Bukoba Mjini.

- My Take ni CCM Mkoa wamekurupuka na kujidhalilisha sana na this ishu, kwa sababu bado Madiwani wanaweza kwenda Mahakamani na kubaki na Udiwani wao, uwezekano wa Madiwani hao kufukuzwa na Kamati Kuuu sidhani hata kama upo, kwa kuzingatia sababu za msingi zilizowapeleka CCM Mkoa kuwasimamisha, ni aibu sana kwa Viongozi wa Mkoa wa CCM, tena mmoja Katibu Mkuu wa Mkoa akiwa ni rafiki yangu wa karibu sana, ameniskitisha sana na this!!

Le Mutuz
Minor Correction, ni CCM Mkoa wa Kagera kwani Bukoba ni makao makuu ya Mkoa wa Kagera
 
safi sana karibuni chadema na kata zenu ziko wazi

Sidhani Hata mmoja wao taingia CDM, Hao wote ni watu wa kagasheki. La kushangaza ni kuwa hao hamutawaita masalia wa cm, bali mtawaita Makamanda. Ili hali wameingia CDM.

Pia hebu jamani kuweni na siasa makini, mukiwachukua hawa kihorera na kuwapa fursa kusimama uchaguzi hapo bkk, jee waliokufa na cdm, ambao kwa miaka sasa wamefanya kazi kubwa mpaka cdm imetambulikana BKK, Au fukira zenu ni kuwa hizo ziara za kina slaa, mbowe na zitto, ndizo zinazoleta votes mikoani, Apana ile kuna wale wanaoitwa FOOT Soldiers ndio wanaofanya kazi halisi haswa. CDM hapa imepoteza haki na ndio mwanzo wa mwish wao BKK
 
kwa mara nyingine tena naona wazee wa anga wametengenezewa barabara swafiiiiiiiii kuichukua halmashauri! ama kweli magamba yameiga kunya kwa tembo!!!!!!! Long live CHADEMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA!!
 
Back
Top Bottom