Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,010
- 132,723
- Thread starter
- #161
Niliipandisha hii thread, 2010, sasa tuko 2014, tukielekea 2015, jee Chadema imejipanga, inajipanga, unaendelea kujipanga?!.
Pasco
Pasco
Hii thread kipindi kile niliichukulia ni ya kawaidaa. leo nimeisoma tena nimeiona kama ni mpya aisee!
Uzalendo ni pale unapoipigania nchi yako na ikibidi kuifia!.Sema nini watanzania 99% hatuna uzalendo kabisa
hili pia ni Tatizo. Nyie wachambuzi kina Pasco mnaliona je hili.?
ccm imechokwa nikweli tupu ila chadema kutojipanga apo nadhani iko ivi, watanzania wamechoshwa na siasa za ulaghai na ndoo maana vilipovuma vyama vingi kama TLP,NCCR,CUF, watanzania walivisuport but at the end wakakosa direction coz watanzania wanaexpect mambo makubwa toka upinzani, more than the power wanayoipa upinzani katika kutetea haki zao.i belive chadema for now watanzania wengi wanaikubali coz ina mikakati iliyo wazi, na tumaini jipya kwa waliowengi ila je, ni wangapi waliotayari kuyapokea mabadiliko?i mean chadema ina nguvu na nguvu ni ya wananchi ila wananchi bado wanaitaji kuelimishwa na kuandaliwa katika kuyapokea mabadiliko.with new constitution i belive tutafika kuliko sahihi
Wanabodi,
Hakuna ubishi, Chadema imenyanyuka, toka wabunge 5 mpaka 22 wa kuchaguliwa tena majimbo ya haja, huku sio kukua bali ni kupaa, tatizo kubwa la Chadema, bado hawajipanga.
Kichama, wanachadema mkubali msikubali, chama chenu japo kipo juu, lakini bado hamjajipanga kwa sura ya kitaifa.
Kwa vile CCM imekaa mkao wa kifo, hii ndio opportunity yenu kujipanga muwe na sura ya kitaifa, Watanzania wawamini wawakabidhi nchi mwaka 2015.
Kitendo cha kuihodhi kambi ya upinzani Bungeni, huu ni udhaifu mkubwa ambao hautawafikisha mbali. Pamoja na kanuni za bunge kuruhusu Chadema kuunda kambi rasmi ya upinzani, Chadema peke yenu hamuwezi!.
Angalizo: Pasco wa Jamii Forums ni political commentator ambaye yuko objective, bila kuegemea chama chochote, upande wowote na hufanya kazi kwa wote, ila ni muumini wa demokrasia ya kweli ndani ya bunge for the balance of power, hivyo nashangilia sana kambi ya upinzani kuingiza vichwa 100 bungeni, ni matumaini yangu, 2015 kazi itakamilishwa!
Wanabodi,
Nikiwa hapa Dom, nimebahatika kukutana baadhi ya wabunge wapya wa CCM na wa kambi ya upinzani, kujaribu kufahamiana, sio siri, baadhi yao hawana hata substance ya ni nini kilichowafanya washinde, na kwa viti maalum ndio usiseme kabisa!, wengi wao kama si makapi tuu, basi ni vidumu, basi ni kwa ajili ya kutoa huduma na kibinaadamu!, na hili litathibitishwa na michango yao kikao cha Januari.
Nilipoongea na baadhi ya wale makamanda waliokata magogo kanda ya ziwa, nimewaona ni wa kawaida tuu, hivyo nimefikia jibu moja la uhakika, kuwa CCM katika baadhi ya maeneo, imechokwa mpaka basi!, upinzani hata ungesimamisha jiwe, lingechaguliwa!, nadhani ni moja ya sababu kuu iliyopelekea wengi hawakujitokeza waliona kujitokeza kupiga kura ni kujisumbua tuu!.
Nasisitiza CCM imechokwa, na ule ushindi wa kishindo wa toka Asilimia 80% niliyohakikishiwa na mwana CCM mwandamizi mpaka asilimia 60% ni uthibitisho tosha, Watanzania wameichoka CCM ila pia hawakuwachagua wapinzania kwa wingi zaidi, kwa sababu wapinzani hawajaonyesha wako tayari kukamata dola.
Najua kwa dhati, japo JK anafurahia ushindi kwa furaha ya machoni, lazima atakuwa na huzuni moyoni kwa kukataliwa na hiyo asilimia 20% kukataliwa ni kukataliwa tuu, kunauma. Hivyo CCM lazima watakaa na kujiuliza kulikoni, huenda wakajipanga upya na kuja kwa mbinu mpya, ila kwa vile CCM imechokwa, hata ijipange upya vipi, safari ya kwaheri ndio imeanza, there is nothing to stop it from failing down!.
Dawa pekee ya kuitibu CCM, ni kuirevamp CCM completely, task nambari moja ni Makamba should go first with his old guards team. Msisubiri mpaka uchaguzi mkuu wa chama chenu, miaka miwili ijayo (2012), itakuwa too late. If you are to du anything, doi it now and fast!. Leteni fresh blood kina January type, Kippi, Nape type and the like ambao wanaweza siasa za kisasa za dot com type.
Hakuna ubishi, Chadema imenyanyuka, toka wabunge 5 mpaka 22 wa kuchaguliwa tena majimbo ya haja, huku sio kukua bali ni kupaa, tatizo kubwa la Chadema, bado hawajipanga.
Kichama, wanachadema mkubali msikubali, chama chenu japo kipo juu, lakini bado hamjajipanga kwa sura ya kitaifa.
Kwa vile CCM imekaa mkao wa kifo, hii ndio opportunity yenu kujipanga muwe na sura ya kitaifa, Watanzania wawamini wawakabidhi nchi mwaka 2015.
Kwanza Freeman Mbowe, ajiuzulu uenyekiti, ampishe Dr. Slaa kwenye Usukani, Katibu Mkuu mpeni Zitto, hii itaifuta ile dhana ya nepotisim kwenye chama chenu, ili Walioichoka CCM wawafungulie mikono kwa kujitokeza kuwapigia kura 2015.
Kitendo cha kuihodhi kambi ya upinzani Bungeni, huu ni udhaifu mkubwa ambao hautawafikisha mbali. Pamoja na kanuni za bunge kuruhusu Chadema kuunda kambi rasmi ya upinzani, Chadema peke yenu hamuwezi!.
Kama CCM iko ICU na Chadema haijajipanga, spika ndio huyo mama ma over confidence na over reaction, 2015 tutegemee nini?.
Angalizo: Pasco wa Jamii Forums ni political commentator ambaye yuko objective, bila kuegemea chama chochote, upande wowote na hufanya kazi kwa wote, ila ni muumini wa demokrasia ya kweli ndani ya bunge for the balance of power, hivyo nashangilia sana kambi ya upinzani kuingiza vichwa 100 bungeni, ni matumaini yangu, 2015 kazi itakamilishwa!
Naendelea kuifuatilia hii thread kwa mwaka wa nne sasa!, huku nikiupima msingi wa hoja kuu mbili za uzi huu, kwanza ni CCM imechokwa!, hivi sasa tunapoichungulia 2015, jee CCM bado imechokwa?, CCM ni dholfu bin taaban, au CCM imepunguza uchovu?. Nilisema Chadema haijajipanga, jee sasa imejipanga, inajipanga na itajipanga?!.Wanabodi,
Kwa vile CCM imekaa mkao wa kifo, hii ndio opportunity yenu kujipanga muwe na sura ya kitaifa, Watanzania wawaamini wawakabidhi nchi mwaka 2015.
Pasco
Naendelea kuifuatilia hii thread kwa mwaka wa nne sasa!, huku nikiupima msingi wa hoja kuu mbili za uzi huu, kwanza ni CCM imechokwa!, hivi sasa tunapoichungulia 2015, jee CCM bado imechokwa?, CCM ni dholfu bin taaban, au CCM imepunguza uchovu?. Nilisema Chadema haijajipanga, jee sasa imejipanga, inajipanga na itajipanga?!.
Pasco
Matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa ni uthibitisho wa kuchokwa kwa CCM, jee pia ndio uthibitisho wa kujipanga kwa Chadema?!.
Pasco