CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!

CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!

Wapenda kula rushwa hawawezi kuiacha ccm. Ndiyo inayowaweka mjini.
 
gamba.jpg
 
Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wasipokuwa makini wataendelea kukalia kiti cha upinzani maisha, wanatakiwa kuwa makini katika maamuzi juu ya watu wanaokifanya chama kusikika kwa watu, wawe na utulivu na kukaa meza moja na watu wanaowaona wanaenda kinyume na matakwa yao, wasikurupuke kwa kuangalia washabiki wasio na upeo na mambo ya siasa. Kuna watu ni mashabiki tu, tena akigombea hata ujumbe wa serikari ya kijiji hapati hata kura moja ila yuko mbele kusema kiongozi fulani afukuzwe kwenye chama, inafaa kutulia wachukue nchi kwanza kisha kuanza kuwamaliza mmoja baada ya mwingine. Kwasasa ni hatari sana hawa watu wana washabiki wao wakiondoka wanaondoka na idadi fulani ya watu, na pengo hilo kuliziba itachukua muda kuliziba. Naomba viongozi wawe makini na maamuzi, tumeliona hilo kwa NCCR-MAGEUZI, tumeliona kwa CUF, siasa ni kama mchezo wa mpira kosa lako anaweza kutumia adui kujiimarisha au kushinda! UMAKINI WA MAAMUZI NI KITU MUHIMU KULIKO KUTUMIA USHABIKI!
 
Zitto kubali kutokubali kuwa ulikosea then omba usamaha basi kwa maandishi na kama una kesi futa zote.Wewe ni nyota ndani ya ukawa muda mchache ujao.
 
Nini wpinzani, hawa itafikia wakati watakuwa wasindikizaji tu kama vile NLD, CCJ n.k
 
Zitto kubali kutokubali kuwa ulikosea then omba usamaha basi kwa maandishi na kama una kesi futa zote.Wewe ni nyota ndani ya ukawa muda mchache ujao.
Kwa mwenye akili timamu, wa kuomba msamaha ni CHADEMA kumuomba ZITTO na siyo ZITTO kuomba msamaha.
 
Chadema ni wachumia tumbo si wapinzani wa ukweli. Wale vingozi kila mmoja yupo pale kwa maslahi yake binafsi na si vinginevyo.
 
Kwa mwenye akili timamu, wa kuomba msamaha ni CHADEMA kumuomba ZITTO na siyo ZITTO kuomba msamaha.
Ninachowashangaa CHADEMA ni hili la kila siku kuomba ZITTO aombe msamaha, ili iweje kama siyo kuogopa kuondoka kwake kutakuwa na madhara makubwa kwa CHAMA. Zitto naye alivyosmart anawasikilizia tu wanabwabwaja.
 
Kwa mwenye akili timamu, wa kuomba msamaha ni CHADEMA kumuomba ZITTO na siyo ZITTO kuomba msamaha.

zito atoke aende kwenye chama chake cha ACT , kwani yeye ni wa kwanza kutoka wametoka wengi lakini bado chadema watanzania wanakiamini , uchaguzi wa serikali za mitaa umedhihirisha hilo kwamba chadema imesambaa hadi vijijini kwenye mikoa mingi . Chadema imemjenga amepata umaarufu akajiona yeye ni zaidi ya wenzake akataka kumpanda mwenyekiti mabegani hana tofauti na lusifeli aliyetaka kumpanda Mungu kichwan.
 
Chadema ni wachumia tumbo si wapinzani wa ukweli. Wale vingozi kila mmoja yupo pale kwa maslahi yake binafsi na si vinginevyo.

wapinzani wameungana wakaunda UKAWA.
CCM ni vipande-vipande, sasa wachumia tumbo wameunda
Team Lowasa
Team Membe
Team Pinda
Team Wassira
Team Makamba
Team Nyalandu
Team Ngeleja
N.K
Je, viongozi wa chama kipi kati ya CCM au CDM ndiyo wachumia tumbo??
 
Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wasipokuwa makini wataendelea kukalia kiti cha upinzani maisha, wanatakiwa kuwa makini katika maamuzi juu ya watu wanaokifanya chama kusikika kwa watu, wawe na utulivu na kukaa meza moja na watu wanaowaona wanaenda kinyume na matakwa yao, wasikurupuke kwa kuangalia washabiki wasio na upeo na mambo ya siasa. Kuna watu ni mashabiki tu, tena akigombea hata ujumbe wa serikari ya kijiji hapati hata kura moja ila yuko mbele kusema kiongozi fulani afukuzwe kwenye chama, inafaa kutulia wachukue nchi kwanza kisha kuanza kuwamaliza mmoja baada ya mwingine. Kwasasa ni hatari sana hawa watu wana washabiki wao wakiondoka wanaondoka na idadi fulani ya watu, na pengo hilo kuliziba itachukua muda kuliziba. Naomba viongozi wawe makini na maamuzi, tumeliona hilo kwa NCCR-MAGEUZI, tumeliona kwa CUF, siasa ni kama mchezo wa mpira kosa lako anaweza kutumia adui kujiimarisha au kushinda! UMAKINI WA MAAMUZI NI KITU MUHIMU KULIKO KUTUMIA USHABIKI!

Mleta mada una angalizo la msingi. Ila naona walakini wa angalizo lako. Ni nani kwa mfano ambaye ana wafuasi wengi akifukuzwa ataondoka nao? Hao wanachama walifuata mtu ama chama? Kwa maneno mengine huyo kiongozi akifariki, uanachama wao utakoma? kwa hiyo wasipochukua nchi wataendelea kuwa naye hata kama hafuati taratibu za chama mpaka hapo watakapochukua nchi? Halafu unasema wakiondoka wataondoka na watu, hilo sina ubishi nalo, je hiyo cdm haiwezi kupata wanachama wapya bali hao ilionao tu sasa? Hizi mada zinafanya watu wawe na shaka hasa inapotekea watu kutoa ushauri hapa jukwaani na sio kwenye vikao. Huoni kwamba hiyo hofu yako itachangia kupata viongozi dhaifu kama tunaowaona sasa kwa watu kushindwa kuchukuliana hatua kisa tu ni mwenzo hata kwa makosa yaliyo dhahiri. Kumbuka kila uamuzi una faida na hasara zake. Inawezekana cdm wamepima faida na hasara wameona watapata faida zaidi kuliko hasara.
 
Acheni kushupalia upuuzi...

Chama cha siasa kinaongozwa kwa katiba,sheria,kanuni na taratibu

Na sio personality za watu.

Full stop
 
Kwa mwenye akili timamu, wa kuomba msamaha ni CHADEMA kumuomba ZITTO na siyo ZITTO kuomba msamaha.
yaani mimi niende kumuomba yule kibiritingoma msamaha! you mast be joking mnene! CHEDEMA NI IMANI kuelekea ukombozi wa kweli
 
Back
Top Bottom