Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 45,886
- 101,877
Wanabodi,
Kutokana na majukumu yangu kama Mshauri wa Siasa wa Ubalozi fulani, moja ya kazi zangu ni kufanya kitu kinaitwa "stakeholders mapping", hii hufanyika kwa kitu kinachoitwa "interactions" hivyo from time to time, huwa nawajibika kuwapo Dodoma kwa interactions na waheshimiwa wabunge.
Sasa nikiwa hapa Dodoma kwenye hili Bunge jipya, nimebahatika kukutana baadhi ya wabunge wapya wa CCM na wa kambi ya upinzani, kujaribu kufahamiana nao, sio siri, baadhi yao. kwa kuwaangalia tuu na kuzungumza nao, hawana kabisa any substance ya ni nini kilichowafanya washinde, na kwa wabunge wa viti maalum ndio kabisa usiseme!, kwa baadhi ya wabunge hawa wa viti maalum, sikuona ni kipi kilichowafanya wateuliwe na vyama vyao kuwa wabunge wa viti maalum!, wengi wao japo wameteuliwa kutimiza hitaji la usawa wa kijinsia, sababu za uteuzi wa baadhi yao ni ile jinsia yao kwa matumizi ya kutoa zile huduma muhimu za kibinaadamu kama vidumu vya waheshimiwa sana na sio kwa ajili ya kuchangia mijadala na hoja nzito za bungeni, na hili litathibitishwa na michango yao bungeni katika mijadala mbalimbali, kuna baadhi mtawashuhudia kazi yao itakuwa ni kuonyesha umaridadi wa mavazi, kuonyeshea shapes na kuuza tuu sura kule mjengoni! na mwisho wa siku hivi 'vidumu' vitakuja kuwaponza wamiliki wa 'vidumu' hivi kwa kupata mapigo ya karma ya wake wa ndoa wa waheshimiwa hao.
Nilipoongea na baadhi ya wale makamanda waliokata magogo kule Kanda ya Ziwa, kiukweli nimewaona baadhi yao ni watu wa kawaida sana tuu with nothing special kilichowafanya wachaguliwe na kuibwaga CCM na vigogo wake wenye nguvu, influence na pesa, iliyoota mizizi kwenye kanda hivyo , hivyo nimefikia jibu moja tuu la uhakika, kuwa CCM katika baadhi ya maeneo, imechokwa mpaka basi!, upinzani hata ungesimamisha jiwe, jiwe lingechaguliwa!, nadhani hii ni moja ya sababu kuu iliyopelekea wengi wa waliojiandikisha kupiga kura, hawakujitokeza kupiga kura, waliona kujitokeza kupiga kura ni wastage of their valuable time, ni kujisumbua tuu!.
Nasisitiza CCM imechokwa, na ule ushindi wa kishindo wa Kikwete toka asilimia Zaidi ya 80% mwaka 2005 hadi asilimia 60% 2010, ni uthibitisho tosha, Watanzania sasa wameichoka CCM ila pia hawakuwachagua wapinzani kwa wingi zaidi, kwa sababu wapinzani bado hawajaonyesha kukomaa vya kutosha kuweza kukabidhiwa nchi kwa kushindwa kuonyesha utayari kukamata dola na kutawala.
Najua kwa dhati, japo CCM na JK wanafurahia ushindi huu kiduchu kwa furaha, ni furaha ya machoni tuu, lakini moyoni ni maumivu na vilio kwa huzuni ya kukataliwa toka ushindi wa kishindo wa asilimia 80% ya 2005 hadi ushindi kiduchu wa asilimia 60 za 2010, na hiyo asilimia 20% ya kukataliwa, kukataliwa ni kukataliwa tuu kunauma!.
Hivyo chama makini chochote lazima kikae chini na kujiuliza, hivyo CCM lazima watakaa chini na kujiuliza kulikoni, ni katika kujiuliza huko, huenda wakajipanga upya na kuja kwa mbinu mpya, kwa nguvu zaidi na kasi zaidi, ila kwa vile CCM imechokwa, hata ijipange upya vipi, kama Chadema itajipanga, then kwa CCM, safari ya kwaheri ndio imeanza, there is nothing to stop it from failing down unless ibadilike kwa revamping.
Dawa pekee ya kuitibu CCM chovu iliyochokwa, ni kuirevamp CCM completely, task nambari moja ni Makamba and his old guards pale Lumumba, should go, kupisha new blood. Tena CCM msisubiri mpaka uchaguzi mkuu wa chama chenu, miaka miwili ijayo (2012), itakuwa too little too late. If you are to do anything, just do it now and fast!. Leteni fresh blood kina January type, Kippi, Nape type and the like ambao wanaziweza siasa za kisasa za .dot com type.
Hakuna ubishi, Chadema imenyanyuka, toka wabunge 5 mpaka 22 wa kuchaguliwa tena majimbo ya haja yenye impact ikiwemo kuyashika majiji makubwa katika mikoa the big five!, huku sio kukua bali ni kupaa, tatizo kubwa la Chadema, bado hawajipanga mkao wa kichama tawala, ili kikabidhiwe nchi, kitawale, Chadema bado kimekaa kichama harakati, hivyo kuna wengi wanakiona kama bado hakijakomaa kiasi cha kukabidhiwa ikulu yetu!.
Kichama, wanachadema mkubali msikubali, chama chenu kwa sasa japo kipo juu, lakini bado hamjakomaa kufikia kiwango cha kukabidhiwa nchi, bado mko kiuana harakati zaidi kuliko ki chama tawala, na hamjajipanga kwa sura ya kitaifa na utayari wa kutawala nchi.
Kwa vile CCM imechokwa na imekaa mkao wa kifo, hii ndio opportunity yenu Chadema kuongeza offensive ili kuisindikiza CCM kaburini, kwa kujipanga kimkakati ili muwe na sura ya kitaifa, kwa kuonyesha Watanzania kuwa mmekomaa na mko tayari kutawala, hivyo Watanzania watawamini watawakabidhi nchi mwaka 2015.
Sehemu muhimu kabisa kwa Chadema to keep watch kuhakikisha hamuiachii ni hiyo Kanda ya Ziwa ambayo imeipokonya CCM na kuishika, hii ndio Kanda determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii. Aliyeishika Kanda ya Ziwa ndio rais wa Tanzania. Hivyo CCM imeumia sana kupoteza Kanda ya Ziwa na wataelekeza all it might powers to reclaim what it has lost, hivyo Chadema itumie uwezo wake wote kulinda what it has!.
Kwa upande wa Chadema, lazima kibadilike, first and foremost, anzeni na Mwenyekiti wenu Freeman Mbowe, he should go!. Ajiuzulu uenyekiti, ampishe more able person kama Dr. Slaa kwenye usukani wa chama, Katibu Mkuu mpeni Zitto strategically, hii itaifuta ile dhana ya nepotisim kwenye chama chenu, na kulivua lile koti la ukanda na ukabila ili walioichoka CCM wawafungulie mikono kwa kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura 2015 kwa kujionyesha Chadema ni chama cha wote, dini zote na kanda zote.
Kupumzishwa kwa Freeman Mbowe sio kuwa hafai no, anafaa sana lakini kwa background yake na nature ya kazi zake, as a businessman, hapo alipoifikisha Chadema amaishafanya kazi kubwa na kufikia mwisho wa uwezo wake. Kwa background yake ya a former DJ na sasa ni mfanyabiashara, focus ya wafanyabiashara kote dunia nzima ni maximisation of profits, hivyo Mbowe atahitaji ruzuku ya Chadema itumike kuivest kwenye assets, kwenye vitu vya kuonekanika yaani assets kama magari, mavazi, etc
Ili Chadema kiweze kushika nchi 2015, it has to invest on people na sio ku invest kwenye vitu. Chadema must invest kwenye mass mobilisation na sio kutegemea mikutano ya hadhara na maandamano. Chadema needs to have able people kuiwezesha kushika dola five years to come kwa kutumia reaching out mechanism kuwafikia the mases kwa kumiliki media yake yenyewe. Chadema lazima ifanye recruitment ya loyal able people, watakaokuja kuendesha serikali ya Chadema. Mbowe hawezi kukubali ruzuku ya Chadema itumike to invest on people, kwasabu it's a loss making venture kwa mfanyabiashara na kuivest kwenye mass media sio profitable investment kwa business man ambaye ni in for profits making!. Dr.Slaa na Zitto sio wafanyabiashara hawa ni ma technocrats. Chama kishikwe na wanasiasa watendaji ma technocrats na sio wanasiasa wafanyabiashara!. Chadema iwekeze kwenye watu na kupanua mtandao wake hadi vijijini, ili kwenda kuiongoa CCM kuanzia kule chini kabisa kwenye mizizi yake ambako ni kule kwenye mashina. Chadema imiliki media yake yenyeshe for mass mobilization na sio kutegemea mikutano na maandamano, huko ni kuendeleza uanaharakati, Chadema inatakiwa kukaa mkao wa kutawala, ikitangaza kitu, kinafika Tanzania nzima!
Chadema ina tatizo la umimi. Kitendo cha Chadema kuihodhi kambi rasmi ya upinzani Bungeni, huu ni udhaifu mkubwa ambao hautawafikisha mbali. Pamoja na kanuni za Bunge kuruhusu Chadema kuunda kambi rasmi ya upinzani peke yake, Chadema peke yenu hamuwezi!. Lazima muwashirikishe wapinzani wengine wote hata kama hawastahili. You have to unite and work as one against a common enemy. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.
Kama CCM ndio hii iko ICU na Chadema haijajipanga, spika ndio huyo mama ma over confidence na over reaction, 2015 tutegemee nini?. Kama Chadema haitabadilika, then 2015, japo imechokwa, japo chovu, ni CCM tena!.
Angalizo: Paskali wa Jamii Forums ni political commentator ambaye yuko objective, bila kuegemea chama chochote, upande wowote na hufanya kazi kwa wote, ila ni muumini wa demokrasia ya kweli ndani ya bunge for the balance of power, hivyo nashangilia sana kambi ya upinzani kuingiza vichwa 100 bungeni, ni matumaini yangu, 2015 kazi itakamilishwa!.
Paskali