CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!

CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!

Huu ni mwanzo wa historia mpya lakini Chadema wanatakiwa nao wajifunze kitu kimoja hapo "wanasiasa" hawatakiwi kuwa watendaji wa serikali na hii ndio siri ya wao kuonekana wakifanya kazi nzuri sababu waliikosoa serikali mchana kweupe sababu hakuna mgongano wa kimaslahi sasa na wao kama wanamaanisha hii kazi kwa maana ya kumaanisha basi kujipanga kwao ni lazima wakubali watendaji wa kweli hawana muda sana na siasa za kivyama na wakubali kufanya kazi na watu ambao politically wako neutral ingawa objectively wako tight na committed kwenye kazi!!!!

Wako tayari kwa hilo, au watataka watendaji wakuu wa serikali wapatikane kwa mfumo wa wabunge wa viti maalumu???!!!
Mkuu Olesa, kuna kitu cha muhimu sana umekizungumza hapa!, they must, andif they are ready!.

Pasco
 
Sio siri CCM ni legelege kupindukia haijawahi tokea . Kama kungalikuwa na upinzania wa nguvu kidogo ni wazi tungalipata rais mpya kutoka chama cha upinzani. Udhaifu wa wapinzani ni ule wa miaka nenda rudi, hawataki kujichafua matope hawaendi vijijini. Hawana kampeni za nguvu zinazotikisa ,hawana watu wanaomudu majukwaa, hawana mipango endelevu, wamejiweka katika nafasi ya kuifuatilia CCM kinyume cha mika ile ambapo CCM ilikuwa infuatilia NCCR mageuzi. Wamebaki kukosoa teuzi na kauli za viongozi wa CCM badala ya kueneza sera zake, wamebaki kulumbana na viongozi wa CCM kwenye television badala ya kuanzisha media yao kama magazeti na TV. Hawajindai mapema wanasubiri last days hadi kuruhusu mapingamizi,Sasa hawajiandai tena katiba itapita CCM wanatambaa kama nyoka wakijiandaa na wanaandaa shambulizi kubwa la knock-out
 
Nikiiangalia Chadema naona kama ni chama cha wachaga kwa sehemu kubwa na ndio maana kama sijakosea mara zote mwenyekiti wake huwa anatoka kaskazini tangu kianzishwe, Ukikiangalia CUF nacho naona kama ni chama cha waislamu, NCCR Mageuzi wale waliokimbia kutoka Chadema ndio wako pale.Vyama vya Upinzani Tanzania vinaendeshwa kama kampuni ya mtu binafsi.Tunataka chama ambacho kitatuunganisha watanzania bila kujali kabila wala dini, hicho ndio chama kinachoweza kuiondoa CCM madarakani vinginevyo CCM itaendelea kutawala, mkiendelea kubisha hata hicho chadema nacho huenda kikafa kama NCCR Mageuzi.

Watanzania wengi hatuipendi CCM kutokana na mapungufu yake makubwa sana lakini tunalazimika kukipa kura mara baada ya kuona wapinzani wengi ni wababaishaji.Watanzania wengine wanaamua kuacha kupiga kura kabisa na kwa tathimini ya haraka wasomi wengi ndio hawapigi kura.Fanya research ofisini kwako kama uko ofisini utapata majibu.

Wapinzani jipangeni vyema.
 
Acha unafiki, kama unawanyima upinzani kura kwa kuwa wana mapungufu unawezaje kuwapa ccm kura wakati wanamapungufu pia. Siasa za kizamani kwa sasa hazina nafasi. Kiambie chama chako wajinga wameshaerevuka, werevu mko mashakani. Unaonekana utakuwa ni mzee na kama ni kijana ni mtoto wa fisadi ambaye huna uwezo wa kufanya kazi bali unapenda maisha mazuri. Unaoogopa kikija chama kingine hapo mjini utakuwa house boy. Nilitarajia uonyeshe nini hivi vyama vinatakiwa kufanya ili kuikomboa tanzania na hivyo vyama vifaidike na ushauri wako hatimaye iwe faida kwa taifa. Huu utoto unaoufanya hapa kutuona wote ni watoto sijui kutuambia wachaga, sijui waislam huu ni upuuzi.

Sasa nakusaidia, watanzania waliojitambua tunafahamu matatizo yetu ni maji, elimu, afya, miundo mbinu ya barabara, umeme nk. Huo upuuzi mwingine wa uislamu, uchaga nk ni wako wewe na chama chako kilichokosa sera bali kuibia wananchi kwa uelewa wao finyu. Jitambue na shika adabu.
 
tanzania ni miongoni mwa nchi zenye kufuata mfumo wa vyama vingi. katika nchi yetu kuna zaidi ya vyama 10 vya siasa na miongoni mwao mwao vipi vilivyomaarufu na vipo ambavyo si maarufu.

ni jambo la kusikitisha kama si kustaajabisha kuwa vyama vyote vinagombania kuongoza nchi hii bila kutoa picha/taswira halisi kuhusu tanzania wananchi waitakayo.

mimi ni mpinzani wa ccm ila sijawahi kuona au kusikia mchumi yoyote kutoka vyama upinzania ambaye ameonyesha kuwa ni mchumi ambaye chama chake kikishika hatamu watasaidia nchi.

je! ni wachumi kutoka chama gani waliofanikisha angalau vyama vyao kujikwamua kiuchumi au jamii zao? kuna vyama vinavyopokea ruzuku. je! hao wachumi wameonyesha uchumi wao katika nini ikiwa hata ndani ya vyama vyao wanashindwa kuonyesha uchumi wao. kama vyama vinavyotaka kutuongoza havina wachumi ni ukweli usiopingika kuwa maendeleo ya taifa hili bado sana. Sifa ya mwanauchumi siyo kwenye media na makaratasi bali ni katika matendo ya kila siku ya kawaida
 
Hujaona chama mbadala kwakuwa una mtazamo wa kiccm. Na unalazimisha kwamba hujaona mchumi kutoka kwenye hivyo vyama. Hebu tutajie wachumi toka ccm ambao unaona wamepandisha uchumi wetu mpaka leo. Halafu kitu kingine nikusaidie, uchumi lazima ufanywe na wanasiasa. uchumi utafanywa na wachumi, chama cha siasa kitaunganisha tu sera za uchumi lakini utendaji halisi utabiki kwa wachumi wenyewe. Una lingine la maana?
 
mie siyo ccm na sijawahi kuwa ccm. kampeni tokea mwanzo mwisho napigia chama tofauti na ccm na daima nitaendelea kuwa mpinzani wa ccm
 
You have a point
Though sio kila kitu lazima wewe uone.
Kama hujaona basi kula bati
 
You have a point
Though sio kila kitu lazima wewe uone.
Kama hujaona basi kula bati

ebu nionyeshe wewe uliona aidha chama chenye mchumi wa kweli na siyo wa kwenye vitabu na makaratasi
 
Hujaona chama mbadala kwakuwa una mtazamo wa kiccm. Na unalazimisha kwamba hujaona mchumi kutoka kwenye hivyo vyama. Hebu tutajie wachumi toka ccm ambao unaona wamepandisha uchumi wetu mpaka leo. Halafu kitu kingine nikusaidie, uchumi lazima ufanywe na wanasiasa. uchumi utafanywa na wachumi, chama cha siasa kitaunganisha tu sera za uchumi lakini utendaji halisi utabiki kwa wachumi wenyewe. Una lingine la maana?

mchumi yupi ambaye wewe unamzungumzia? ebu weka jina na tokeo la uchumi wake ulivyonufaisha aidha chama chake au jamii kwa ujumla
 
mchumi yupi ambaye wewe unamzungumzia? ebu weka jina na tokeo la uchumi wake ulivyonufaisha aidha chama chake au jamii kwa ujumla

Ungenisaidia sana kama ungenitajia wachumi wa ccm na walichokifanya kwenye taifa hili kisha uniuilze hao wa upinzani.
 
Tanzania ya sasa imebakiwa na watu wachache sana wanayoipenda CCM,na weng wao wanaipenda kinafiki kwa kuwa wanamaslah binafsi kutokana na serikali iliyopo madarakani ya CCM.Jumatatu ya wiki inayoishia leo nilikuwa Bahi Dodoma kila mwanabahi anakwambia nimeichoka CCM,pia mwishon mwa mwezi uliopita nilifika iringa na mbeya na weng ukijaribu kuwaelezea kuhusu CCM wanakwambia hawaitaki hata kuisikia.kama Tanzania tungekuwa na chama imara cha upinzani nadhani kuanzia mwaka 1995 tusingekuwa na CCM. Watanzania tufanyeje tuiondoe CCM?
 
Hakuna chama kinachoweza kuwa IMARA kwa harakati za Serikali na CCM yenyewe kuuzima upinzani sababu ya MASLAHI ya viongozi na waandamizi wao,bila kusahau FAMILIA na MARAFIKI wao wa karibu.Hata hivi vilivyopo vimejitahidi sana na inabidi tufike mahali tuvipongeze............
 
Mazoea hujenfga tabia.
Kwanamna CCM ilivyoishiwa uhalali wa kuendelea kutawala Tanzania, ni dhahili kuwa wanachama wa chama hicho wanaendelea kujijengea tabia itakayo pumbaza akili na fahamu zao kwa ujumla. Kitendo cha baadhi ya wafuasi wa chama hicho wanaojitahidi kwa nguvu zote kuendelea kuishabikia CCM richa ya maomvu na madudu mengi yanayofanywa na chama hicho ni kupungukiwa na maarifa na ufaham.

kama wewe ni mwnaCCM, ni wakati wako sasa kutafakari kwa kina kuhusu kuendelea ama kutoendelea kushabikia chama hicho kwani chama kimepoteza dira na hakitoweza tena kuliongoza taifa hili. Kuendelea kushabikia chama hicho ni kujiangamiza wewe mwenyewe.

TAFAKARI!, CHUKUA HATUA
 
Back
Top Bottom