CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!

CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!

Ndugu Mkandara,

siamini kuwa wabunge wa CUF wa Zanzibar wanaweza wakatengana na wenzao wa Bara; hili jamani tuwe realistic. Yaani ni kuunda kambi ambayo unajua haitkuwa na mwelekeo ili mradi tu huko nje uonekane umeungana? Wabunge wa CUF kutokea Zanzibar ndo wanaoifanya CUF iwe na nguvu ndani ya Bunge la jamhuri ya muungano. Wabunge wa bara ni wawili tu!! Sasa Chadema iungane na CUF kwenye kambi ya upinzani wakati CUF wameshapewa maelekezo kutoka Zanzibar kuwa waiunge mkono CCM. Yaani Chadema iseme, aaa unajua ninyi CUF ni upinzani, hata kama mnaiunga mkono CCM, tuwe kambi moja halafu wale wabunge wenu wawili wa bara ndo wasiwe wanaiunga mkono CCM! Kweli unaamini hii ni practical? Yaani wabunge wa CUF wana maelekezo kutoka kwenye chama chao yanayowataka waiunge mkono CCM, halafu bado unaona kuna hoja, kwa mfano ya katiba, ambayo unaamini CUF wataiacha CCM waiunge mkono Chadema.

Ohh, as much as tunapenda kuona nguvu ya upinzani ikiongezeka, tuwe wakweli na tuangalie mambo kwa hali halisi. CCM wameshanusa harufu ya kushindwa, wako tayari kutoa sacrifice, na sacrifice hiyo ni kuwa embrace baadhi ya wapinzani. Haikuwa rahisi kwa Mahafidhina wa uingereza kukubali kuungana na waliberali. Lilikuwa jambo gumu, lakini when madaraka is at stake, lolote laweza kutokea! CUF wameambiwa kutoka Zanzibar (ilipo ngome yao) kuwa waiunge mkono CCM; kwa hivyo voting zao zote itakuwa ni pro CCM. Itakuwa ni kujaribu kuzoa maji yaliyomwagika kwa Chadema kujaribu kuwang'ang'ania CUF. Hata mie sioni haja ya kufanya hivyo, unless Chadema nayo ikubali kuwa itapiga kura zake kuiunga mkono CCM. Hapo tutakao umia ni wapiga kura, kwani mtawala atakuwa amejihakikishia kutawala bila hata kelele.

Kwa numbers zilivyo huko bungeni, bado upinzani ni noise tu kwa hapa Tanzania. CCM bado wanaweza wakafanya chochote bila kuhitaji mpinzani yeyote. Lakini noise zikiwa genuine, itakuwa ngumu kwa CCM kutawala kwa mtindo ule ule wa business as usual. Tumeona mfano wa mambo ya EPA na Richmond. Ingawa bado wahusika wakubwa wako at large, lakini noise za wapinzani zilisaidia angalau kuwafunua macho wabongo walio usingizini. Kwa hiyo, tunahitaji upinzani genuine, hata kama utakuwa na wabunge wachache, cha muhimu uwe upinzani wa kweli usio na chembe au ukakasi wa kushirikiana na utawala. Only then nguvu ya hoja itasimama. Upinzani nusu, utawala nusu (Status ya CUF leo) haiwezi kuwa kitu tunachotamani kuona wengi.
Maneno yako sawa kabisa mkuu wangu isipokuwa unasahau kwamba hawa Wabunge wa Zanzibar walipewa maagizo hayo kuhusiana na jambo moja tu - Wamchague nani kuwa Spika for the interest ya CUF na WaZanzibar , kwani kupitia CCM ndio wamepata huo ulaji wa kuunda kwa serikali ya mseto. Na Yawezekana hofu yao kubwa wakimchagua spika wa Chadema anaweza kuwakwamisha ktk baadhi ya makubaliano walofanya na CCM kuhusiana na mabadiliko yaliyokwisha tangulia iwe muundo wa serikali, katiba na mengine tusoyajua. Kifupi, tumeona CUF wakiwapa support CCM ktk swala linalogusa maslahi ya Zanzibar na utetezi wa makubaliano haya wameujengea ukuta kumchagua Spika wa CCM. Na ndio maana nikasema tusiwaliaumu sana CUF kwani wao sasa hivi wanatafuta Ulaji ingawa picha nzima inaonyesha wajiunga na CCM kwa maslahi ya Wazanzibar.

Sasa yapo maswala ya msingi na ya kimuungano ambayo wao wanaweza kusimama nasi kwa kupata maagizo hayo hayo. Ifahamike tu kwamba miaka mitano iliyopita Chadema ilikuwa na wabunge wangapi?. Kwa nini wao wasijiulize maswali kama haya hali Chadema haina mbunge hata mmoja zanzibar au ndio tunarudi palepale kwamba wao hawakuwa na hesabu ya wabunge wa kutosha kuunda kambi ya Upinzani.. Na kama ndivyo hivyo basi wangeacha kabisa kusiwekpo na kambi ya Upinzani maadam wao hawataki kuwa na Chadema ambao muda wote wamekuwa wapinzani wa Tanzania au Zanzibar kujiunga na OIC.

Lakini haikuwa hivyo, waliunda kambi hiyo kwa maslahi ya Watanzania na Chadema wakapata mahala pa kujivunia masifa ambayo ndio sababu kubwa ya leo chama hiki kuwa hapa kilipo. Wangetaka wangempiga chini Dr.Slaa au Zitto kutokuwa wasemaji wa Upinzani na wakaweka watu wao. Na wakati wote huo CUF haikuwa na mbunge hata mmoja toka bara kama sikosei kwa hyo hawakuwa na sababu ya kujali kabisa maslahi ya Chadema kama chama.

Tena basi CUF hawakunufaika na lolote zaidi ya kuona maswala yao mengi yakitupwa nje na hata hapa JF tumekuwa wapinzani wakubwa ktk maswala mengi ya CUF kuhusu matakwa ya WaZanzibar na yanayohusu muungano. Hivyo inawezekana pia kuwa hizi ndio sababu zilizowasukuma CUF kujiunga na CCM ili wapate japo ulaji maana wameshindwa kupewa ushindi walostahili toka mwaka 1995.

Na tumejenga uhasama mkubwa kiasi kwamba Bara na Zanzibar zimekuwa nchi mbili tofauti kabisa inapofikia maswala mengi ya muungano japokuwa Chadema kama chama inawaunga mkono lakini wananchi wengi wa bara hawakubaliani na matakwa ya CUF kuhusiana na Zanzibar.

Kweli kabisa Tanzania leo hatuna Upinzani na CCM wataendelea kufanya wanayotaka kufanya ikiwa Upinzani hauwezi kujijenga lakini kumbuka tu moja ya njia bora ya kujenga Upinzani huanzia ktk ushirika unaojengwa na sio ushirika unaovunjika. Leo hii Upinzani wapo mbali zaidi kuliko mwaka jana au juzi kwa sababu tumevunja ushirikiano nje ya Bunge na sasa tumevunja bungeni hivyo safari ya kupata Upinzani wa kweli inazidi kuwa ndefu zaidi. Kwa mafanikio ya Chadema tunasahamu kwamba hata CUF wameongeza viti bungeni pia na vyama vingine vimepata kiti bungeni hali bunge lililopita walikuwa hawana kitu, kifupi kila chama kimegain kutoka CCM baada ya kushuka toka asilimia 80 hadi 61. Kila chama cha Upinzani kinajiona kimeongeza nguvu zake mwaka huu.

Na kibaya zaidi kutokana na kiburi cha Watanzania kila chama kitajiona wao wanaweza kufika mahala pasipo mwingine na hakika watakao umia zaidi ni wananchi. Haya nimesikia Mafisadi wanarudi kupitia viti maalum, hivi kweli kuna tegemeo lolote ambalko wewe una hakika Chadema watafanikiwa bungeni.. Watapiga kelele zipi ikiwa maswala yote yatafagiliwa uvunguni? kwenye magazeti na vyombo vya habari ambayo CCM wanaweza wafungia na wakapoteza biashara zao!

Ni wapi sauti ya mwananchi itasikika kesho? Aaaah mkuu wangu nitaonekana mbishi sana hivyo tuyaache kama yalivyo lakini kumbuka tu nachoweza kusema ni kwamba Upinzani bungeni siku zote hauna maana mtakubaliana kwa kila kitu baina yenu wenyewe. Kila mmoja wenu ndani ya Upinzani ana agenda zake kuwakilisha wananchi wake na sio lazima nyote mpigiane kura isipokuwa mnaunda Upinzani against chama tawala na yapo maswala Chadema inaweza kuwa against CUF kama ilivyotokea ktk swala la Spika lakini kipaumbele ni kuweka Upinzani kwa chama tawala kwa manufaa ya wnaanchi.
 
Pengine mimi ndio sielewi..
Hivi kosa la Pasco ni lipi hapa?..Kujiita yeye ni Political analyst kisha akamshambulia Dr.Slaa na Chadema ktk uchambuzi wake ambao wengi hatukubaliani!..Sasa kama hatuukubali kwa nini tusiandike ukweli wenyewe ni upi na kwa nini haikuwa hivyo badala yake tunamshambulia Pasco na utafiti wake binafsi hadi kumvika kofia za njano/kijani..

Mkandara,

Tunaacha kujadili hoja tunaanza kumshambulia mtu, ndio utamaduni wetu. Umesahau CCM waliposhindwa kujibu hoja za Dr. Slaa walianza kumshambulia kuwa ni Mdini na amepora mke wa mtu?

Mbaya ni hili la kudai usomi kuwa ni lazima uwe political analyst mwenye kufanya research maabara kuchanganya maandiko ya Marx na Churchil ndipo tukubali kuwa wewe ni kichwa. Ask Karl Rove au James Carvile wao mchezo wao ukoje. Infact I salute Pasco hata kwa hiyo "limited intellectualism" watu wanayodai hana ameweza kufikisha ujumbe wake vizuri na reaction ya watu is a proof kuwa kafanikiwa kwenye lengo lake na badala ya watu kujenga hoja kupinga hoja yake, wanamtazama nani huyu anayenena!

Yale yale Bungeni wanaambiwa kuna mtu anaiba almasi na dhahabu zetu, wanaulizana hivi huyu anaongea kwani ni Polisi au ana uwezo gani wa kujua kuwa dhahabu zinaibiwa.

miye najiuliziaGA uchumi wetu unakwenda wapi na deni kufumuka zaidi, kila mtu anauliza wewe ulisomea Uchumi wapi? Gademu angalia misafara ya kuomba saidia masikini na njaa watu wanavyokula mizizi, there natural born economist sihitaji M1, M2 au some theory to tell me kuwa 3% tunayolipwa kwa dhahabu ni dhuluma!
 
Rev.Kishoka,
Mkuu shukran sana kwani alichosema Pasco kuhusu Chadema ni mawazo mazuri tu na pengine kazungumza vibaya kuhusu CCM kuliko Chadema. Pasco Aliandika kama ifuatavyo:-

1. Kichama, wanachadema mkubali msiku chama chenu bado hamjajipanga kwa sura ya kitaifa, Kwa vile CCM imekaa mkao wa kifo, hii ndio opportunity yenu kujipanga muwe na sura ya kitaifa, Watanzania wawamini wawakabidhi nchi mwaka 2015.

Angalio langu:- sidhani kama kuna kosa kwa Chadema kujipanga kwa sura ya Kitaifa kama chama hata kama Chadema imepata viti 22 mikoani hii bado ni hesabu ndogo sana na sababu ya kufikia mafanikio haya inawezekana haitokani na chama bali nguvu ya Ujumbe wa Dr.Slaa. Na hata kama ni chama chenyewe lakini ujumbe mkubwa hapa ni kwamba CCM imechokwa hivyo Chadema watumie nafasi hii. Nilitegemea wana CCM kubisha zaidi kuhusu utafiti huu kwani hata mimi hapa siamini kama CCM imekaa mkao wa kufa bali ni Simba aliyejeruhiwa. CCM inaweza kuwa hatari zaidi kwa vyama vya Upinzani kuliko wakati wowote ule. Ni lazima na muhimu sana kwa Chadema wajipange kupambana na Simba alojeruhiwa.

2. Kwanza Freeman Mbowe, ajiuzulu uenyekiti, ampishe Dr. Slaa kwenye Usukani, Katibu Mkuu mpeni Zitto, hii itaifuta ile dhana ya nepotisim kwenye chama chenu, ili Walioichoka CCM wawafungulie mikono kwa kujitokeza kuwapigia kura 2015.

Angalio langu:- Hapa ndio vichekesho vikubwa kwani wapo wengi waliompinga Pasco ktk mada hii lakini wanakubaliana na mtazamo huu hasa ktk nafasi ya mwenyekiti (mada nyingine) ingawa mimi bado nina imani kwamba chama kinaweza kujitangaza Kitaifa pasipo umaarufu wa mwenyekiti, isipokuwa wakifahamu kwamba Dr.Slaa ataendelea kugombea kiti cha Urais mwaka 2015.
Kumbuka tu Dr. Slaa alisema yeye hatagombea tena kiti hicho jambo ambalo linawapa wasiwasi mkubwa wapenzi wa Chadema. Hivyo hata akiwa mwenyekiti bado kazi kubwa itakuwa sii kukitangaza chama bali mgombea kiti cha Urais ndio silaha kubwa ya Chadema. Labda nisema kwamba Chadema inatakiwa kuwashirikisha kikamilifu wageni wengi walioonyesha mapenzi ya dhati kwa chama na wapo tayari kujitoa mhanga kwa manufaa ya chama hicho. Uchaguzi huu umewafundisha Chadema kina nani wamesimama na chama na kina nani ni mapandikizi. Chadema isirudie makosa waliyoyafanya kuendea uchaguzi huu.

3. Kitendo cha kuihodhi kambi ya upinzani Bungeni, huu ni udhaifu mkubwa ambao hautawafikisha mbali. Pamoja na kanuni za bunge kuruhusu Chadema kuunda kambi rasmi ya upinzani, Chadema peke yenu hamuwezi!. Kama CCM iko ICU na Chadema haijajipanga, spika ndio huyo mama ma over confidence na over reaction, 2015 tutegemee nini?.

Angalio langu:- Nakubaliana na Pasco kabisa kwamba Chadema inatakiwa kutafuta kura za wabunge wa vyama vyote iwezekanavyo hivyo kuunda kambi ya Upinzani inayowajumuisha vyama vingine ni hatua ya kwanza, pili wapo wabunge wa CCM ambao pia ni wazalendo wafuatwe kupata kura zao na muhimu zaidi kwa Chadema kujenga mtandao ambao zaidi utasimamia maslahi ya taifa. Upinzani wa kichama wakati wa uchaguzi umekwisha sasa hivi Upinzani uliopo bungeni ni Wazalendo against Mafisadi au niseme chama tawala wanaokumbatia Ufisadi. Na ikumbukwe tu hao wabunge wote walioko bungeni wapo pale kusimamia maslahi ya wananchi mkiunda uadui wa kichama mtawaponza wananchi.

Sasa sielewi hizi analysis zake zilihitaji kipi zaidi ikiwa hali halisi inajionesha hivyo kulingana na mtazamo wa Pasco! Je, alihitaji kuwa na kitu gani zaidi ili apate mtazamo tofauti ikiwa hivyo ndivyo alivyo!
 
Mkandara,

Tunaacha kujadili hoja tunaanza kumshambulia mtu, ndio utamaduni wetu. Umesahau CCM waliposhindwa kujibu hoja za Dr. Slaa walianza kumshambulia kuwa ni Mdini na amepora mke wa mtu?

Mbaya ni hili la kudai usomi kuwa ni lazima uwe political analyst mwenye kufanya research maabara kuchanganya maandiko ya Marx na Churchil ndipo tukubali kuwa wewe ni kichwa. Ask Karl Rove au James Carvile wao mchezo wao ukoje. Infact I salute Pasco hata kwa hiyo "limited intellectualism" watu wanayodai hana ameweza kufikisha ujumbe wake vizuri na reaction ya watu is a proof kuwa kafanikiwa kwenye lengo lake na badala ya watu kujenga hoja kupinga hoja yake, wanamtazama nani huyu anayenena!

Yale yale Bungeni wanaambiwa kuna mtu anaiba almasi na dhahabu zetu, wanaulizana hivi huyu anaongea kwani ni Polisi au ana uwezo gani wa kujua kuwa dhahabu zinaibiwa.

miye najiuliziaGA uchumi wetu unakwenda wapi na deni kufumuka zaidi, kila mtu anauliza wewe ulisomea Uchumi wapi? Gademu angalia misafara ya kuomba saidia masikini na njaa watu wanavyokula mizizi, there natural born economist sihitaji M1, M2 au some theory to tell me kuwa 3% tunayolipwa kwa dhahabu ni dhuluma!

Tumeachia akili zetu ziliwe na mashindano ya nani msomi na kama ni msomi kasoma wapi na huko alikosomea amesomea nini badala ya kuhakikisha tunawekeza kwenye kujadili maslahi ya taifa yetu kwa kutumia mantiki yakinifu. Lazima tukubali kwamba hakuna taasisi yoyote ile inayoongozwa na binadamu ambayo haina mapungufu.
 
Dr.W.Slaa,

Wapukutikwa wa CHADEMA kamwe hawakotayari kukosolewa,leo hii kwakuwa tu wamapta wabunge wa idadi ambayo hawakuitarajia na hii inatokana kwa kuwa watu wameichoka CCM, leo hii watu hao hao wa cdm, wanataka tujifunze kwa Mh Satta wa Zambia, yeye pamoja na yota ameteua mawaziri sita toka nje ya chama chake,hao cdm wameshindwa kufanya hivyo hata kwenye serikali kivuli,hao ni kupayuka na kuropokwa kama walivyo viongozi wao. Hawana jipya,na hicho chama ni cha itikadi na kanada fulani tu,na kinachofanyika nicheza na vyombo vya habari,mmeshapukutika ninyi ni wa msimu tu.
 
Last edited by a moderator:
Wapukutikwa wa CHADEMA kamwe hawakotayari kukosolewa,leo hii kwakuwa tu wamapta wabunge wa idadi ambayo hawakuitarajia na hii inatokana kwa kuwa watu wameichoka CCM, leo hii watu hao hao wa cdm, wanataka tujifunze kwa Mh Satta wa Zambia, yeye pamoja na yota ameteua mawaziri sita toka nje ya chama chake,hao cdm wameshindwa kufanya hivyo hata kwenye serikali kivuli, hao ni kupayuka na kuropokwa kama walivyo viongozi wao. Hawana jipya,na hicho chama ni cha itikadi na kanada fulani tu,na kinachofanyika nicheza na vyombo vya habari,mmeshapukutika ninyi ni wa msimu tu.
Kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake na si kila mtu maoni yake ni constructive kama yalivyo maoni yako. Unarudi kwenye yale yale ya udini na ukabila/ukanda. Watu kama nyinyi mpo wengi na siasa hizi watanzania walishazijua toka enzi na enzi. Humpati mtu wa kubuluza huko unakotaka twende.

Asante kwa kuchangia.
 
Naomba nisieleweke kama nampigia chapuo Zitto, nimemtaja tuu kwa sababu nina uhakika na uwezo wake, kumfukuza kafulila was a mistake, lili lilikuwa jimbo lenu, kumuengua Mwera was a mistake, jimba mmelitoa sadaka, sasa vitu kama hivi ni vi cancer vidogo vidogo vinavyoitafuna Chadema from within, cancer ikigundulika, inakatwa kabla haijasaambaa, ama nayo isubiri uchaguzi?.

Nashukuru kwa mchango wako mzuri. Ninayo imani kuwa ingawa si kila kitu ulichosema kinaweza kuwa na manufaa, bado CDM na wananchi kwa jumla wanaweza kunufaika na jambo fulani katika mchango wako.

Hata hivyo napinga hoja ya kujenga watu au chama kutumia watu fulani kama msingi wake wa kukua na kukubalika kwa jamii. Jambo la aina hii ni hatari na wala siyo endelevu. Kwanza utaratibu wa aina hii hujenga kiburi kwa kumfanya mtu huyo ajione kwamba yeye ndio chama na bila yeye hakuna chama. Pili utaratibu huu hujenga ufalme na udikteta ndani ya chama.

Kwa hiyo pamoja na kwamba Dr. Slaa na Mh. Mbowe ndio viongozi wakuu wa CDM kwa sasa na tunaona mafanikio lakini hawawezi kusimama hadharani na kudai kwamba mafanikio yaliyopo yameletwa na wao pekee. Kila kiongozi ndani ya CDM kwa namna moja au nyingine amechangia mafanikio yaliyopo.

Kama kiongozi ana mapenzi mema kwa wananchi na hana ubinafsi, na anaona anao mvuto ndani ya jamii basi atumie mvuto wake kujenga chama na aepuke kujiona sasa yeye ndo chama, akifanya hivyo maisha yake ya siasa yatakuwa na si marefu. Wahenga walisema ngoma ikilia sana mwishowe hupasuka. Mtu makini huwa anafurahi zaidi akiambiwa umefanya vibaya kwa vile ni mara chache mtu kuona makosa yake kuliko mazuri na pia hupata wasaa wa kujifunza na kujirekebisha.

Napenda kuhitimisha kwa kusema kuwa:

Chama makini hakijengi viongozi bali hujenga mfumo wa uongozi. Watu huja na kupita bali chama kipo na kitaendelea kuwepo.

Iwapo kiongozi yeyote akikiuka misingi na mfumo wa uongozi, na kama kiongozi anakubali kujirekebisha apewe onyo. Kama yeye hataki basi atimuliwe tu hata kama kiongozi huyo ni Dr. Slaa au Mh. Mbowe. Unaweza kupoteza jimbo moja kwa uamuzi huo lakini ukapata mengine matano kwa uamuzi huo huo.

Wananchi hapo mwanzo walikuwa wanaunga mkono CCM au TANU si kwa sababu Mwl J.K.Nyerere alikuwa kiongozi bali kwa sababu ya misingi iliyokuwa imewekwa. Hata kama JKN angekuwa ndio kiongozi wa CCM ya leo nina uhakika wananchi wangemkataa yeye na CCM yake kutokana na kukiuka misingi ambayo inakubalika na umma wa watu anaowaongoza.

Asanteni sana,
Namshukuru mtoa mada na pia nashukuru kupata nafasi ya kuchangia.
 
Maneno yako sawa kabisa mkuu wangu isipokuwa unasahau kwamba hawa Wabunge wa Zanzibar walipewa maagizo hayo kuhusiana na jambo moja tu - Wamchague nani kuwa Spika for the interest ya CUF na WaZanzibar , kwani kupitia CCM ndio wamepata huo ulaji wa kuunda kwa serikali ya mseto. Na Yawezekana hofu yao kubwa wakimchagua spika wa Chadema anaweza kuwakwamisha ktk baadhi ya makubaliano walofanya na CCM kuhusiana na mabadiliko yaliyokwisha tangulia iwe muundo wa serikali, katiba na mengine tusoyajua. Kifupi, tumeona CUF wakiwapa support CCM ktk swala linalogusa maslahi ya Zanzibar na utetezi wa makubaliano haya wameujengea ukuta kumchagua Spika wa CCM. Na ndio maana nikasema tusiwaliaumu sana CUF kwani wao sasa hivi wanatafuta Ulaji ingawa picha nzima inaonyesha wajiunga na CCM kwa maslahi ya Wazanzibar.

Sasa yapo maswala ya msingi na ya kimuungano ambayo wao wanaweza kusimama nasi kwa kupata maagizo hayo hayo. Ifahamike tu kwamba miaka mitano iliyopita Chadema ilikuwa na wabunge wangapi?. Kwa nini wao wasijiulize maswali kama haya hali Chadema haina mbunge hata mmoja zanzibar au ndio tunarudi palepale kwamba wao hawakuwa na hesabu ya wabunge wa kutosha kuunda kambi ya Upinzani.. Na kama ndivyo hivyo basi wangeacha kabisa kusiwekpo na kambi ya Upinzani maadam wao hawataki kuwa na Chadema ambao muda wote wamekuwa wapinzani wa Tanzania au Zanzibar kujiunga na OIC.

Lakini haikuwa hivyo, waliunda kambi hiyo kwa maslahi ya Watanzania na Chadema wakapata mahala pa kujivunia masifa ambayo ndio sababu kubwa ya leo chama hiki kuwa hapa kilipo. Wangetaka wangempiga chini Dr.Slaa au Zitto kutokuwa wasemaji wa Upinzani na wakaweka watu wao. Na wakati wote huo CUF haikuwa na mbunge hata mmoja toka bara kama sikosei kwa hyo hawakuwa na sababu ya kujali kabisa maslahi ya Chadema kama chama.

Tena basi CUF hawakunufaika na lolote zaidi ya kuona maswala yao mengi yakitupwa nje na hata hapa JF tumekuwa wapinzani wakubwa ktk maswala mengi ya CUF kuhusu matakwa ya WaZanzibar na yanayohusu muungano. Hivyo inawezekana pia kuwa hizi ndio sababu zilizowasukuma CUF kujiunga na CCM ili wapate japo ulaji maana wameshindwa kupewa ushindi walostahili toka mwaka 1995.

Na tumejenga uhasama mkubwa kiasi kwamba Bara na Zanzibar zimekuwa nchi mbili tofauti kabisa inapofikia maswala mengi ya muungano japokuwa Chadema kama chama inawaunga mkono lakini wananchi wengi wa bara hawakubaliani na matakwa ya CUF kuhusiana na Zanzibar.

Kweli kabisa Tanzania leo hatuna Upinzani na CCM wataendelea kufanya wanayotaka kufanya ikiwa Upinzani hauwezi kujijenga lakini kumbuka tu moja ya njia bora ya kujenga Upinzani huanzia ktk ushirika unaojengwa na sio ushirika unaovunjika. Leo hii Upinzani wapo mbali zaidi kuliko mwaka jana au juzi kwa sababu tumevunja ushirikiano nje ya Bunge na sasa tumevunja bungeni hivyo safari ya kupata Upinzani wa kweli inazidi kuwa ndefu zaidi. Kwa mafanikio ya Chadema tunasahamu kwamba hata CUF wameongeza viti bungeni pia na vyama vingine vimepata kiti bungeni hali bunge lililopita walikuwa hawana kitu, kifupi kila chama kimegain kutoka CCM baada ya kushuka toka asilimia 80 hadi 61. Kila chama cha Upinzani kinajiona kimeongeza nguvu zake mwaka huu.

Na kibaya zaidi kutokana na kiburi cha Watanzania kila chama kitajiona wao wanaweza kufika mahala pasipo mwingine na hakika watakao umia zaidi ni wananchi. Haya nimesikia Mafisadi wanarudi kupitia viti maalum, hivi kweli kuna tegemeo lolote ambalko wewe una hakika Chadema watafanikiwa bungeni.. Watapiga kelele zipi ikiwa maswala yote yatafagiliwa uvunguni? kwenye magazeti na vyombo vya habari ambayo CCM wanaweza wafungia na wakapoteza biashara zao!

Ni wapi sauti ya mwananchi itasikika kesho? Aaaah mkuu wangu nitaonekana mbishi sana hivyo tuyaache kama yalivyo lakini kumbuka tu nachoweza kusema ni kwamba Upinzani bungeni siku zote hauna maana mtakubaliana kwa kila kitu baina yenu wenyewe. Kila mmoja wenu ndani ya Upinzani ana agenda zake kuwakilisha wananchi wake na sio lazima nyote mpigiane kura isipokuwa mnaunda Upinzani against chama tawala na yapo maswala Chadema inaweza kuwa against CUF kama ilivyotokea ktk swala la Spika lakini kipaumbele ni kuweka Upinzani kwa chama tawala kwa manufaa ya wnaanchi.

mi nimependa ulipowakumbusha wana cdm cuf ilikuwa na uwezo wa kuwa fanya watu kama slaa na zitto kutosikika pamoja walikuwa hawana wabunge bara ila walikuwapo wanawake wakuteuliwa cuf ilikuwa na uwezo wakuwaweka wanawake wale dhaifu ilikudhoofisha upinzani lakini walikuwa nania ya kweli naupinzani wa kweli wakamuweka zitto na slaa hichi kitendo bahati nzuri ama mbaya uchaguzi wa 2015 cuf ikaongeza viti zenji na bara wakapata fursa hii halafu wakawaambia cdm ni ccm b kwakuwa mlikwenda kuongea na kikwete. Tutawaona humu wote mtalowa maji. Tusiongee kishabiki cuf ni chama cha upinzani kitendo ilichofanya cdm kutotaka kuijumuisha cuf ktk kambi ya upinzani kwa visingizio vya kijinga eti kwakuwa nyinyi mpo serikali moja ya zanzibar itakuwaje mbowe anaongea nakujitia kutafakari huku akijua fika nini kimetendeka na watu wavivu wakufikiri basi wamevishwa shuka hilo la la kuwa cuf naSUK watu wameamini na kuona sawa.
 
Tusiongee kishabiki cuf ni chama cha upinzani kitendo ilichofanya cdm kutotaka kuijumuisha cuf ktk kambi ya upinzani kwa visingizio vya kijinga eti kwakuwa nyinyi mpo serikali moja ya zanzibar itakuwaje mbowe anaongea nakujitia kutafakari huku akijua fika nini kimetendeka na watu wavivu wakufikiri basi wamevishwa shuka hilo la la kuwa cuf naSUK watu wameamini na kuona sawa.

Ni wewe tu na wengine wachache ndio bado mnaiona CUF kama chama cha upinzani.

Haiwezekani uwe na sura mbele na nyuma. Daima sura itakuwa mbele na nyuma kitakaa kisogo. Mbunge huyo huyo akienda kwenye baraza la wawakilishi anakuwa sehemu ya serikali ya CCM huyo huyo akija bunge la muungano awe mpinzani wa CCM.

CUF wameshapima kina cha maji sasa... next time wanaingia wazima wazima ndani ya CCM.

CUF no more..
 
Kama watu wameichoka ccm wadhihirishe kwa kupigia kura chadema katika kila uchaguzi unaofanyika wakianzia na arumeru mashariki.
 
Wanabodi,

Nikiwa hapa Dom, nimebahatika kukutana baadhi ya wabunge wapya wa CCM na wa kambi ya upinzani, kujaribu kufahamiana, sio siri, baadhi yao hawana hata substance ya ni nini kilichowafanya washinde, na viti maalum ndio usiseme kabisa, wengi ni makapi tuu, kama sio vidumu, basi ni kwa ajili ya kutoa huduma na kibinaadamu, na hili litathibitishwa na michango yao kikao cha Januari.!

Leo nilikuwa nafanya mapitio ya hii thread nilichokisema miaka miwili iliyopita kuhusu wabunge wa CCM. Nilisema baadhi ya wabunge wapya wa CCM wengi ni makapi tuu, hawana substance!. Hili limethibitishwa na JK, katika kulisuka upya baraza lake, kwenye hao wabunge waliopo, amesaka sana akakuta patupu!, yaani hamna kitu mle!, ndipo akajaribu kuvikombeleza vile vichwa vichache vilivyomo na kulazimika kufanya uteuzi mpya wa wabunge wa kumsaidia.

Hivi nyinyi wabunge wa CCM ulioko bungeni, mnajisikiaje rais wenu anapokosa msaada wenu na kulazimika kukopa ili ajenge timu yake?!. Ki ukweli ni bure kabisa nyinyi!. Mnatuangusha sana!.
 
Pasco unaonekana una akili lakini hutaki kuitumia vizuri,umeandika kama umetoka kulala,cdm ni chama makini cha upinzani ndio maana magamba wamejaribu kukiua na kujikuta wanakufa wao.

Mbowe na slaa kiungozi na kiutendaji wamefiti. Huyo zitto huwa nampenda ila anatamaa ya uongozi abakie alipo na kama hataki ajiondokee, cdm wanachonikera hawapendi kwenda kwenye sehemu ambazo wanajiona hawapendwi kama dar, pwani, mafia, lindi, mtwara, pemba, Z'bar etc. Mwanza, arusha kila leo wanaenda hadi mwishoe watachokwa.
 
Unajua wakati mwingine usim-judge mtu kwa ukimya wake wakati mwingine ukimya wa Mbowe ndo unaiweka CHADEMA pale ilipo! japo unaafiki ya kuwa CHADEMA imeongezeka viti unasahau kuwa imeongeza viti hivyo chini ya uenyekiti wa Mbowe na viongozi wengine kuanzia Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu (mikakati na mipango ilifanyika chini ya uongozi wake kwa kushirikiana na wengine)!

Jamani tuache kunyanyapaa.. Zitto itafika wakati atapata huo Uenyekiti au Ukatibu Mkuu anaoutaka! uchaguzi wa vyama utakuja tena! na si kwa jinsi anayotumia sasa kwa ku-discredit the current leaders (naomba ajifunze hili)! Meanwhile siwezi afiki mtu mwingine yeyote kupewa uongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni zaidi ya Mbowe maana hiyo itakuwa ni kum-discredit kiongozi wa chama ilhali yupo Bungeni na nathani wenzetu walioanza demokrasia mapema waliliona hili ndo maana kama chairman wa chama ni Mbunge anakuwa kiongozi pia wa chama hata Bungeni!

Tuache ku-pin point individuals unfit for our personal weaknessses like judging someone on identities! na kuwa-discredit for misjudging their merits, uongozi si kupayuka tu! na busara ya kuwaweka wenzako woote pamoja na kusikiliza mawazo ya wengine jamani! Hebu imagine kama Mh Zitto angekuwa Chairman wa chama katika lile suala la Dowans halafu akatofautiana na wenzie juu ya Msimamo; what would have happened? si chama kingalifia mbali kama NCCR-Mageuzi (Mchawi angetafutwa!) lakini impact yake ilikuwa ndogo kwa vile position yake si nzito kama ya chairman...!

Jamani tuwe na subira, Zitto anapaswa kukomaa zaidi haswa kwenye maswala ya ndani ya chama na overall party stands vs public affairs! Kuna mambo hayapaswi kuenda nje na personal stands without reservation of other opinions ni sumu kwa chama haswa kama ukiwa kiongozi wake! nasema hivi kwa sababu so far sijaona issue zozote ambazo zingeweza kuleta mtafaruku kama uliotokea hapo kabla ukimhusisha huyu ndugu yetu..! Ajifunze na uchaguzi unakuja ajipange vizuri na ajaribu kuepuka media katika baadhi ya maswala!

nashukuru sana kwa majibu yako mazuri, kwani mbowe yeye ana tatizo gani kwenye uongozi wake? huyo unayemwona anafaa mpeleke nyumbani kwako.
 
Pasco unaonekana una akili lakini hutaki kuitumia vizuri,umeandika kama umetoka kulala,cdm ni chama makini cha upinzani ndio maana magamba wamejaribu kukiua na kujikuta wanakufa wao.

Mbowe na slaa kiungozi na kiutendaji wamefiti. Huyo zitto huwa nampenda ila anatamaa ya uongozi abakie alipo na kama hataki ajiondokee, cdm wanachonikera hawapendi kwenda kwenye sehemu ambazo wanajiona hawapendwi kama dar, pwani, mafia, lindi, mtwara, pemba, Z'bar etc. Mwanza, arusha kila leo wanaenda hadi mwishoe watachokwa.

Marire, hii ilikuwa ni mwaka 2010 leo ni 2012 kujipanga kumeanza!.
 
Leo nilikuwa nafanya mapitio ya hii thread nilichokisema miaka miwili iliyopita kuhusu wabunge wa CCM. Nilisema baadhi ya wabunge wapya wa CCM wengi ni makapi tuu, hawana substance!. Hili limethibitishwa na JK, katika kulisuka upya baraza lake, kwenye hao wabunge waliopo, amesaka sana akakuta patupu!, yaani hamna kitu mle!, ndipo akajaribu kuvikombeleza vile vichwa vichache vilivyomo na kulazimika kufanya uteuzi mpya wa wabunge wa kumsaidia.

Hivi nyinyi wabunge wa CCM ulioko bungeni, mnajisikiaje rais wenu anapokosa msaada wenu na kulazimika kukopa ili ajenge timu yake?!. Ki ukweli ni bure kabisa nyinyi!. Mnatuangusha sana!.

Pasco
Lakini Huyo Huyo JK kwenye hotuba yake kwenye teuzi za mawaziri si alisema . Nanukuuu "Uwazirii hauna shule"
  • Alikuwa na maana gani

JK hajakosa hao unaoita vichwa . Anakosa watu loyal kwake . Na kateua disloyal wachache kwa ajili ya PR tu machoni pa wananchi.

Abadilishe Priority ya seletion . Loyality na urafiki visiwe vgezo vya muhimu. Mbona kwenye Pool la CCM wamo wamo japo ni magamba

Mfano mtukama January kumuweka wizara yasayansi naona kigezo cha vichwa siochamuhimu kwake. Yes Naunga Mkono 90.% Kijana mwenzetu January kwa kwenye uwaziri lakini sio kunazia kwenye sekta ya Sayansi. Zipo Wizara zinafaa mtu kuanza kujenga na kujengewa uwezo.
 
ndugu zangu watanzania,leo nimeona si vibaya kuja na tafakuri ya kina kuhusu chama cha mapinduzi wengine tunakilaumu bila kufikiria kwa makini ni nini kimekifikisha hiki chama mkombozi wa bara la afrika hapa kilipofikia.
Mimi nina mambo mawili matatu kuhusu hali hii na ni nini hatma yake,naomba wale waliokiona kwa jicho la tofauti na mimi si vibaya na wao wakaniweka sawa ila huu ni mtizamo wangu.
1.kilichoimaliza ccm ni malengo yake,nifafanue kidogo.
Ccm kama taasisi yoyote duniani ilianzishwa kwa sababu na ninapoongelea ccm mtaniwia radhi nikiiunganisha na tanu kwa sababu hakuna mahali tulipoambiwa kuwa ni chama kipya bali tuliambiwa sababu ilikuwa ni kuunganisha vyama tu kwa hiyo malengo ni yaleyale ya tanu.
Hiki chama kilikuwa na malengo ya uhuru tu.mifano ni mingi tazama kila ikifika 9 desember nchi inazizima majeshi yafanya mazoezi karibu mwezi mzima bajeti yake inashangaza(hata kama haijaidhinishwa na bunge) tukimaliza hapo tunasubiri mwaka mmoja tena tunasherehekea tena kwa mbwembwe zaidi ya mwaka uliopita,sasa nini maaana yake?
Maana yake hata tumalize miaka 200 hakuna la ziada kwa sababu malengo aliyoweka dereva wetu yameshatimia sasa ni kunywa na kushrehekea mpaka kiama,ulevi si ulevi ulafi si ulafi.sasa mnataka tufanye nini tena?

2.hata binaadamu asipojiwekea malengo na kuyahuisha ataishia kuyasifu mafanikio ya malengo ya awali hata kama yamepitwa na wakati,tuchukue mfano huu,kila binadamu hapa naomba tuchukue mwanaume anaanza na lengo la kuoa ni wachache wanaopanga watoto kabla ya kuoa sasa wakati unapotafuta mke huo ni mpango a.
Mungu anaweza kukupa mke mzuri mwenye heshima zote sasa ukikosea baada ya kuoa usipoweka mpango b nini kitafuata baada ya kuoa utakuta miaka nenda rudi unshehekea mke wakati huo watoto wanaongezeka mwisho unajikuta familia ina watoto tisa bila kujua uifanyie nini familia hiyo kwa sababu bado umebaki kwenye lengo la mke.

3.mfano wa tatu ni mazao,tunategemea wakati wa kulima lazima utakuwa na lengo huwezi kulima tu mradi umelima.
Lengo lako ni kulima mahindi unaanza mchakato wa kulima,kupanda,kupalilia,kuweka mbolea kama inahitajika,kulinda wanyama waharibifu na mwisho kuyaondoa mavuno shambani.
Kama mazao yakishakomaa kama hujayaondoa shambani tegemea yafuatayo;
shamba kuvamiwa na wanyama waharibifu huingia na kuharibu shamba.
Mazao kuoza na kuota bila utaratibu na hivyo shamba kuwa kichaka humo huwa maficho ya nyoka,panya nk.

Ccm kama taasisi na kwa kuwa imetuonyesha imeshafikia malengo yake miaka 50 iliyopita na haiwezi kuhuisha malengo yake imefikia wakati tutafute chama kitakachokuja na malengo ya wakati huu na wakati ujao.
Tusafishe shamba tupande mazao upya na ikifikia yakiiva tuvune na kusubiri msimu mpya.kama binadamu baada ya ndoa tukae na mke wetu tuanze kupanga familia na maendeleo yetu na kila wakati tuhuishe malengo kutokana na wakati.
Ccm tuipumzishe si kwa lengo baya ila ni kkawaida mbona mzee akizeeka tunamhudumia kila kitu bila kufanya kazi tena?mbona tunapata baraka kwa kupumzisha wazee na kuwafanyia kazi?tutafute blanketi kwa ajili ya babu(ccm)tumwashie moto apumzike vijana tukabiliane na shangamoto mpya za karne mpya.
Kwa babu tusikilize hadithi za uhuru na muungano tu na hapo tutapata hata radhi yake.

kama thread za mwanakijiji vile!!!!!!!
 
Good perception...but unafikiri kuwa ccm itaamua yenyewe kupumzika? Hawa watu wanahitaji nguvu, tena nguvu sana kuwaondoa madarakani its not as simple and politely as you talk....

TOGETHER WE CAN BRING THE CHANGES WE NEED.....YES WE CAN...!!!!
 
tunajua kweli ccm imechokwa! Lakini ni kweli kuwa cdm bado haijajipanga?
 
Nilikuwa napita sehemu pembeni yake kuna Jalala (Shimo La Taka Taka), Nilichokiona ilibidi nichukue simu yangu na kukipiga picha ili angalau na nyie wana JF mshuhudie ni kwa kiasi gani watu wamechoka huu mtandao wa Magamba, naona huyu mwenye hii kadi hakutaka ku complicate sijui kuirudisha wala kushikwa na hasira yoyote, kaamua kutupa jalalani kuonyesha kwamba ni worthless kwake.

Kazi kwenu mliotumwa na mavuvuzela ya NAPE and co,
ccm2.jpg
ccm1.jpg
HAMIA CHADEMA >> www.hamiachadema.com
 
Back
Top Bottom