CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!

I regret why Dr. Slaa you are not my president. Ombi langu kwako na chama kwa ujumla. Una wabunge wengi sasa na wengi wao ni wageni na wachanga kwenye siasa. Watanzania wasingependa nafasi zao ziishie hapo kwa kushindwa kutekeleza yale muhimu amabayo yatawafanya warudi tena 2015 na zaid wawe mfano kwa majimbo mengine ili kuongeza idadi kubwa zaidi ya wabunge. Streghts mliyo nayo wote wamekwenda shule za uhakika na hivyo ni waelewa ukilinganisha na 82% ya vihiyo wa CCM.

Hapa ninamaanisha kwa uzoefu wako mwenyewe, Mh. Mbowe, Mh. Zito, Mh. Ndesamburo na wengine wakongwe ujitoe muda wenu kuwafunda na kuwafanya kuwa chachu ya mabadiliko bungeni na zaidi kwa wananchi waliowachagua. Kama nynyi wazoefu mlikubalika basi mnayo ya kuwafundisha wabunge wachanga na hata ku-share mawazo ambayo yatawafanya wabunge wa CHADEMA kuwa mfano kwa majimbo mengine na hatimae kuleta imani kwa wengine ambao walichagua CCM.

We wish you all the best na watanzania wengi tuliokuchagua wewe ndo raisi wetu tofauti na JK aliye wa tume yake ya uchaguzi NEC.

Ukipata muda zungumza na wananchi wako uwashukuru ili wasijisikie wapweke.
 
Rais wetu mtarajiwa Dr.Slaa umenikuna na ninakuahidi na watanzania ni mashihidi kuwa wanajua wewe ndio Rais wao mioyoni mwao,uendelee kutujuza mambo na kutupigania kwani tunaamini Marehemu Baba wa Taifa hili J.K.Nyerere amerudi kupitia kwako.
mmaroroi, kumbe Dr. Slaa bado ni rais wenu mtarajiwa?, uchaguzi wa 2010 umeisha na mshindi amershatangazwa, sasa huyu mtarajiwa ni kwa mwaka 2015?, maana uchaguzi huo haujatangazwa, unless amebadili nia na kutangaza rasmi kuwa mwaka 2015 hagombei au?.
Hilo la Watanzania kumkubali yeye ndio rais wao mioyoni mwao, ni la muhimu ila pia lazima muelewe Tanzania inae rais wa nchi ambaye sio lazima awe ni rais wa mionyoni mwa watu, rais huyu yupo kwa mujibu wa katiba, japo amechaguliwa kwa kura za kuchakachuliwa lakini ndie rais. Rais wa mionyoni mwenu kasema hamtambui, sijui ndio ushauri kwenu na nyinyi msimtambue?.
 
I regret why Dr. Slaa you are not my president. Ombi langu kwako na chama kwa ujumla, Ukipata muda zungumza na wananchi wako uwashukuru ili wasijisikie wapweke.
nginda, asante kwa hili, na hili ndilo mimi nimekuwa nikilisemea, anatakiwa aseme neno moja tuu na roho zao zitaponywa!, nilitamani aseme siku ile ile baada ya kazi, wala sio kushikana mikono na mtu, wala sio kukubali matokeo wala kuyasaini, bali kuwaambia waliompa kura zao, asanteni, na kuwaeleza tuwe wavumilivu, tuvute subira na ustahilivu wakati wakuu wa chama wakitafakari hatua muafaka za kuchukuchua.
 
Pasco, naamini kuwa wewe ni mchambuzi wa mambo ya siasa...

Naomba kukupa homework..

Fanya utafiti wa kina, kuhusu suala la CHADEMA kuunda kambi ya upinzani peke yake. Katika hili naomba uje na analysis inayoonyesha 'Ni kwa vipi, na kwa nini CHADEMA imeunda kambi ya upinzani peke yake? Je, wameamua au wamelazimika? Je, wamefanya hivyo kwa maslahi yao, au kwa maslahi ya Watanzania. Je, kulikuwa na alternative gani katika hili?

Naomba utafiti wako uwe na data halisi zikihusisha majibu toka kwa wadau wote wa hili jambo. Naomba uzuie sana hisia zako binafsi katika uchambuzi wako. Nimeainisha haya katika thread niliyoanzisha, ya homework kwa wachambuzi wa siasa...
 
Tuko, Asante sana kwa ushauri huu, ni kweli hapo mwanzo nilijiita mchambuzi wa siasa, baada ya kuelimishwa mchambuzi anatakiwa aweje, na moja ya sifa kuu ya mchambuzi ni kufanya scientific research kwa kutumia vile vigezo rasmi vya utafiti, kuanzia intro, preamble, then plausible major and minor ndipo unapata Scientific and logical conclusion toka kwenye "major and minor" na mwisho bila kusahau references.

Ndipo nikajigundua kumbe mimi sio mchambuzi, ili kuwa mchambuzi lazima uwe mtafiti, hivyo nimesharekebisha, mimi sio mtafiti, bali just a political comentator, yaani mzungumziaji tuu from the poit of view ya a layman, yaani yule mtu wa chini kabisa.

Kwa ndugu yangu Tuko, tuendelee kuwa Tuko pamoja, homework yako hiyo siwezi kuifanya si unajua elimu zenyewe zetu za Watanzania, ila pia naomba kwa vile tuna maresearchers wengi, wakiona inafaa, watatusaidia.

NB. Linapotokea jambo, kama mtu ni mhusika, unajua A-Z na husemi, unategemea wasiojua watajuaje?, mimi na wananchi wenzangu tunasubiri hao wajuaji waseme nasi tusikilize, ndio maana wengine wetu, hatuna shughuli yoyote ya kufanya, bali tunapenda kujiendea tuu viwanja vya Bunge hapa Dodoma, mfano nilidokezwa Bunge kukaa siku ya Jumanne, mpaka leo ni wiki mzima imepita, waheshimiwa wetu wako hapa kwenye vikao muhimu tena busy kweli kweli, ili nasi kujichotea mawili matatu tunayayasikia hapa na pale na kuwatupia wananchi na members wenzetu hapa JF.
 
Geza Ulole, amini usiamini, sina tatizo na Mbowe kuwa ndiye kiongozi wa upinzani bungeni tatizo langu ni si lazima awe yeye simply kwa sababu ni Mwenyekiti. Nimezungumzia point muhimu sana inaypotwa powers from within, Dr.Slaa anayo na Zitto anayo, sorry to say, Mhe. Mbowe hana!.

Victory yoyote hupatikana kwa consolidation of powers na kuzipangia strategies, ndio maana hata vitani, majemedari sio wakaao mstari wa mbele kwenye the line of fire, wanaokaa mbale ni wapiganaji, Mbowe ni Jemedari wenu, Zitto ni mpiganaji wetu. Nafasi ya kioungozi wa upinzani bungeni, haimuhitaji jemedari, inamhitaji mpiganaji kushusha vipigo tuu.

Bunge lililopita, Hamad Rashid ndio alikuwa kiongozi naye ni too diplomatic ila waelewa wanajua it was powers za Dr. Slaa ndizo zilizokuwa major factor of which I doubt kama Mbowe ataruhusu powers za Zitto zimbypass.

Dhana ikijengeka, hata kama ni ya uwongo, hugeuka sumu, maadamu chama Chenu Chadema, tayari kimegubikwa na dhana fulani fulani, msisubiri uchaguzi sijua miaka mingapi ijayo, you have to act fast, kama niliwashauri CCM, Makamba ni liability kwa chama chao, ameshawacost dearly, wakisubiri mpaka 2012 wakati wa uchaguzi wao mkuu, demage inazidi kuongezeka itafikia wakati itakuwa too little too late!.

Naomba nisieleweke kama nampigia chapuo Zitto, nimemtaja tuu kwa sababu nina uhakika na uwezo wake, kumfukuza kafulila was a mistake, lili lilikuwa jimbo lenu, kumuengua Mwera was a mistake, jimba mmelitoa sadaka, sasa vitu kama hivi ni vi cancer vidogo vidogo vinavyoitafuna Chadema from within, cancer ikigundulika, inakatwa kabla haijasaambaa, ama nayo isubiri uchaguzi?.
Pasco nadhani to be fair tuseme ukweli kwamba Kaulila Hakufukuzwa Chadema bali baada ya kumuondolea madaraka, kwa hasira alijiondoa yeye mwenyewe Chadema.

Na kwa kiongozi mwenye uongozi wa busara, hata mimi kwa behavior za Kafulila ningemuengua katika uongozi. Najua power yake katika siasa lakini kama hakujirekebisha don't be fooled na kuchaguliwa kwake sasa. Political career itakuwa jeopardized. Believe me ni lazima abadilike na akue kisiasa. Nilidhani ni vema niliweke hili sawa isionekane kwamba ni kweli Chadema walimfukuza Kafulila.

Simfahamu vizuri Mwera hivyo I have no comment.
 
Pengine mimi ndio sielewi..
Hivi kosa la Pasco ni lipi hapa?..Kujiita yeye ni Political analyst kisha akamshambulia Dr.Slaa na Chadema ktk uchambuzi wake ambao wengi hatukubaliani!..Sasa kama hatuukubali kwa nini tusiandike ukweli wenyewe ni upi na kwa nini haikuwa hivyo badala yake tunamshambulia Pasco na utafiti wake binafsi hadi kumvika kofia za njano/kijani.

Pengine hata mimi sielewi siana za Bongo lakini kuna tofauti kubwa sana kati ya vyama vya Upinzani kushirikiana nje ya Bunge (coalition) na kuunda ushiurikiano huo ndani ya bunge. Na maadam Pasco kazungumzia ushirikiano wao ndani ya Bunge nadhani ni jukumu letu sisi kuelewa ushirikiano wa Upinzani ndani ya bunge unahitajika kwa sababu gani..

Marekani kumetokea kundi la mageuzi wanaojiita Tea party hawa wamekuwa sumu ndani ya chama chao wenyewe na pengine kulingana na siasa za Bongo hawa wangeitwa wasaliti na kunyang'anywa uanachama.

Lakini mbali na hivyo leo hii ndani ya bunge lao Republican wanajaribu kila hali kushirikiana na kundi hili ili kuunda umoja wa Upinzani ambao Republican hata pasipo kundi hili wanaweza kabisa kuendesha Upinzani ndani ya Bunge kwa sababu wao ni majority tena kukizidi hata chama tawala lakini maadam maswala yanayokuja bungeni yatakuwa na ushawishi mkubwa wa kuendeleza ya Obama na serikali yake, Republican wanataka kuongeza nguvu ya Upinzani zaidi kwa sababu ndani ya bunge wapo wabunge ambao ni swingers pia.

Hivyo leo Chadema ina wabunge wasiofika 50, kweli wamepata nguvu ya kuunda Upinzani lakini idadi hii haina nguvu ya ushindani bungeni ikiwa wao Chadema hawatafuti support ktk maswala muhimu ambayo wao watasimamia Bungeni iwe hata kubadilisha katiba ya nchi. Chadema kama chama wanatakiwa kutafuta support ya wabunge wengine kuhusiana na hoja zao lakini sio ushirikiano utakao waunganisha na kuwa chama kimoja.

CUF wameweza kufanikiwa ktk maswala kutokana na support ya Chadema nje na ndani ya Bunge lakini wameshindwa kulipa fadhala baada ya kupata wao. Hii ni desturi ya mswahili siku zote hulia shida kabla hajapata na akisha pata hukuacha solemba hadi siku zitakapo mwishia ndipo huwatafuta marafiki zake. Hii ni Hulka yetu, hivyo tusiwalaumu CUF kwa yote waliokwisha Achieve kwani leo hii CUF wameweza kubadilisha katiba ya Muungano pasipo kupitishwa na bunge letu. wameweza kuunda serikali ya mseto kabla ya uchaguzi hivyo kuwafanya wao ni part of CCM na watatekeleza sera za CCM wakiwa CUF kiitikadi - Hatujayaona haya popote duniani lakini ndivyo ilivyokuwa na Chadema wamekaa kimyaa..

Pengine ukimya huu ndio ulomsukuma Pasco kuanza kuhoji uongozi wa Chadema, na pengine hata kuona ni udhaifu ktk siasa za Bongo lakini wakuu zangu ni vizuri sana kumwambia Pasco kile kilichofanyika na kwa sababu gani Chadema hawakufanya hivi ama vile kulingana na dhana yake. CUF kuungana na CCM haina maana Chadema wachoke kutafuta support yao ama ya vyama vingine kwa maslahi ya wananchi kwani tukitaka kuundwa kwa katiba mpya, ushirikiano wa wabunge wetu wa Upinzani hauwezi kuondoa ushirikiano baina ya CUF na CCM, au ushirikiano huo kuwaunganisha Chadema na CUF bali ni hoja yenyewe ndio inahitaji nguvu ya vyama hivyo vya Upinzani ili kuweza kusimama kwa maslahi ya Taifa... Na kama mlivyokwisha sema Bunge ni mhimili tofauti na ule wa serikali, waacheni CUF waungane na CCM ktk maswala ya kuunda serikali lakini tunapofika Bungeni, Upinzani unatafuta ushirikiano mwingine kabisa tofauti na ule wa kuunda serikali.
 
Tuko, Asante sana kwa ushauri huu, ni kweli hapo mwanzo nilijiita mchambuzi wa siasa, baada ya kuelimishwa mchambuzi anatakiwa aweje, na moja ya sifa kuu ya mchambuzi ni kufanya scientific research kwa kutumia vile vigezo rasmi vya utafiti, kuanzia intro, preamble, then plausible major and minor ndipo unapata Scientific and logical conclusion toka kwenye "major and minor" na mwisho bila kusahau references.

Ndipo nikajigundua kumbe mimi sio mchambuzi, ili kuwa mchambuzi lazima uwe mtafiti, hivyo nimesharekebisha, mimi sio mtafiti, bali just a political comentator, yaani mzungumziaji tuu from the poit of view ya a layman, yaani yule mtu wa chini kabisa.

Kwa ndugu yangu Tuko, tuendelee kuwa Tuko pamoja, homework yako hiyo siwezi kuifanya si unajua elimu zenyewe zetu za Watanzania, ila pia naomba kwa vile tuna maresearchers wengi, wakiona inafaa, watatusaidia.

NB. Linapotokea jambo, kama mtu ni mhusika, unajua A-Z na husemi, unategemea wasiojua watajuaje?, mimi na wananchi wenzangu tunasubiri hao wajuaji waseme nasi tusikilize, ndio maana wengine wetu, hatuna shughuli yoyote ya kufanya, bali tunapenda kujiendea tuu viwanja vya Bunge hapa Dodoma, mfano nilidokezwa Bunge kukaa siku ya Jumanne, mpaka leo ni wiki mzima imepita, waheshimiwa wetu wako hapa kwenye vikao muhimu tena busy kweli kweli, ili nasi kujichotea mawili matatu tunayayasikia hapa na pale na kuwatupia wananchi na members wenzetu hapa JF.

Sasa bwana mkubwa kama wewe ni layman unajiondolea mwenyewe credibility ya kutoa ushauri wa maana. Kwani ukisema tu wewe ni layman wale ambao wanaelewa zaidi wa mambo watakupuuza tu.

Kwa mfano ni kitu gani kinakufanya usema CHADEMA haina sura ya kitaifa? Kama ni wabunge ambao watu wengi wamekuwa wakitumia kama kigezo cha kusema CHADEMA si chama cha Taifa mwaka huu wametoka mikoa mbalimbali ya nchi mpaka Zanzibar. Of course hata kama wangetoka sehemu moja hilo si tatizo cha muhimu ni ufanisi wao. Na kwa ufahamu tu hata kule Marekani ambako kuna vyama viwili vikubwa kuna majimbo ambao siku zote ni ya chama fulani na chama kingine unakuta hakijawahi kushinda huko tangu enzi. Kutokana na hiyo sababu leo hii wamarekani wana kitu wanaita blue and red states.

Sura ya kitaifa ya CCM ipo lakini CCM hapa Tanzania inafaidi mfumo wa zamani wa chama kimoja. Miaka ijayo huko mbele kuna maeneo ambayo CCM itakuwa haina nguvu kabisa, kwa sasa ushahidi ni kule Pemba, CCM haina kitu kule.

Kimsingi tusitegemea kuwa chama cha siasa kitakubalika na kushinda kila mkoa ua jimbo. Kinacho matter kwa Tanzania ni wengi wa kura kwa ujumla wake na sio idadi ya majimbo. Kutokana na hilo kama mimi ningekuwa kwenye chama cha siasa ningefanya kazi ya kujenga chama kwenye yale majimbo yenye wapiga kura wengi zaidi. Kwa mfano kwa nini niangaike sana kufanya kampeni Zanzibar kwenye wapiga kura chini ya 500,000 wakati kuna mikoa kama Dar es Salaam, Mwanza, Kagera, Mbeya zenye wapiga kura zaidi ya milion moja kila mmoja. Mimi ningejikita kwenye hiyo mikoa kwanza.
 
Pengine mimi ndio sielewi..
Hivi kosa la Pasco ni lipi hapa?..Kujiita yeye ni Political analyst kisha akamshambulia Dr.Slaa na Chadema ktk uchambuzi wake ambao wengi hatukubaliani!..Sasa kama hatuukubali kwa nini tusiandike ukweli wenyewe ni upi na kwa nini haikuwa hivyo badala yake tunamshambulia Pasco na utafiti wake binafsi hadi kumvika kofia za njano/kijani.

Pengine hata mimi sielewi siana za Bongo lakini kuna tofauti kubwa sana kati ya vyama vya Upinzani kushirikiana nje ya Bunge (coalition) na kuunda ushiurikiano huo ndani ya bunge. Na maadam Pasco kazungumzia ushirikiano wao ndani ya Bunge nadhani ni jukumu letu sisi kuelewa ushirikiano wa Upinzani ndani ya bunge unahitajika kwa sababu gani..

Marekani kumetokea kundi la mageuzi wanaojiita Tea party hawa wamekuwa sumu ndani ya chama chao wenyewe na pengine kulingana na siasa za Bongo hawa wangeitwa wasaliti na kunyang'anywa uanachama.

Lakini mbali na hivyo leo hii ndani ya bunge lao Republican wanajaribu kila hali kushirikiana na kundi hili ili kuunda umoja wa Upinzani ambao Republican hata pasipo kundi hili wanaweza kabisa kuendesha Upinzani ndani ya Bunge kwa sababu wao ni majority tena kukizidi hata chama tawala lakini maadam maswala yanayokuja bungeni yatakuwa na ushawishi mkubwa wa kuendeleza ya Obama na serikali yake, Republican wanataka kuongeza nguvu ya Upinzani zaidi kwa sababu ndani ya bunge wapo wabunge ambao ni swingers pia.

Hivyo leo Chadema ina wabunge wasiofika 50, kweli wamepata nguvu ya kuunda Upinzani lakini idadi hii haina nguvu ya ushindani bungeni ikiwa wao Chadema hawatafuti support ktk maswala muhimu ambayo wao watasimamia Bungeni iwe hata kubadilisha katiba ya nchi. Chadema kama chama wanatakiwa kutafuta support ya wabunge wengine kuhusiana na hoja zao lakini sio ushirikiano utakao waunganisha na kuwa chama kimoja.

CUF wameweza kufanikiwa ktk maswala kutokana na support ya Chadema nje na ndani ya BUnge blakini wameshindwa kulipa fadhala baada ya kupata wao. Hii ni desturi ya mswahili siku zote hulia shida kabla hajapata na akisha pata hukuacha solemba hadi siku zitakapo mwioshia ndipo huwatafuta marafiki zake. Hii ni Hulka yetu, hivyo tusiwalaumu CUF kwa yote waliokwisha Achieve kwani leo hii CUF wameweza kubadilisha katiba ya Muungano pasipo kupitishwa na bunge letu. wameweza kuunda serikali ya mseto kabla ya uchaguzi hivyo kuwafanya wao ni part of CCM na watatekeleza sera za CCM wakiwa CUF kiitikadi - Hatujayaona haya popote duniani lakini ndivyo ilivyokuwa na Chadema wamekaa kimyaa..

Pengine ukimya huu ndio ulomsukuma Pasco kuanza kuhoji uongozi wa Chadema, na pengine hata kuona ni udhaifu ktk siasa za Bongo lakini wakuu zangu ni vizuri sana kumwambia Pasco kile kilichofanyika na kwa sababu gani Chadema hawakufanya hivi ama vile kulingana na dhana yake. CUF kuungana na CCM haina maana Chadema wachoke kutafuta support yao ama ya vyama vingine kwa maslahi ya wananchi kwani tukitaka kuundwa kwa katiba mpya, ushirikiano wa wabunge wetu wa Upinzani hauwezi kuondoa ushirikiano baina ya CUF na CCM, au ushirikiano huo kuwaunganisha Chadema na CUF bali ni hoja yenyewe ndio inahitaji nguvu ya vyama hivyo vya Upinzani ili kuweza kusimama kwa maslahi ya Taifa... Na kama mlivyokwisha sema Bunge ni mhimili tofauti na ule wa serikali, waacheni CUF waungane na CCM ktk maswala ya kuunda serikali lakini tunapofika Bungeni, Upinzani unatafuta ushirikiano mwingine kabisa tofauti na ule wa kuunda serikali.
Mkuu wangu Mkandara,
Nadhani labda umeelewa vibaya tu, sijaona mahali ambapo Pasco amejibiwa vibaya kiasi hicho unachojaribu kuonyesha. Ni kweli kwamba kumekuwa na maoni tofauti kuhusu maoni ya Pasco lakini hii haina maana Pasco ni mbaya hivyo. Mimi binafsi namheshimu sana kwa michango yake hapa JF na naheshimu sana kazi kubwa anayoifanya katika kutafuta mageuzi hapa nchini. Hata hivyo ni vema ujue hapa ni jukwaani na kuna baadhi ya members wanaandika vyovyote waonavyo. Hilo huwezi lizuia lakini wengi wetu wamemjibu vizuri tu including Dr Slaa. Kila mmoja alikuwa na mawazo yake na kama unavyojua mkuu wangu hapa huwa tunapishana mawazo lakini mwisho huwa tunapata kitu kimoja constructive. Si rahisi kukubaliana kila kitu, maana tukiruhusu kukubaliana kila kitu basi nalo litakuwa taabu nyingine.

Kuhusu suala la kuungana kwa Chadema na vyama vingine vya upinzani nadhani limezungumzwa sana hapa jamvini na wengi tumelichangia kila mtu kwa mawazo yake. Binafsi nimelieza sana hapa https://www.jamiiforums.com/uchaguz...lia-chadema-chama-cha-kushirikiana-nacho.html na najua kila mtu ana mawazo yake na nivizuri tukaja na hoja kwa nini tunadhani tuungane na je kwa nini pia tusiungane na je tulazimishane kuungana kama wengine kwa sababu zao hawawezi kutaka kuungana? Ninatilia mashaka sana hata na muungano na CUF kwa kauli zao. Nimeona mwenyewe hata mawazo ya Rashid Hamad kwenye program moja asubuhi Star Tv nadhani binafsi nina mashaka makubwa na misimamo ya CUF hasa kipindi hiki baada ya uchaguzi mkuu. Naona wamekuja na misimamo na kauli zinazonitia shaka kama kuna kweli kuaminiana tena.

Kama Chama chochote cha upinzani objective yao ni kuliondoa taifa hapa lilipo, na kuikosoa serikali mahali itakapo boronga na mwisho kushika dola. Sasa ndugu yangu kama wao wakiamua kuchukua msimamo tofauti kwa kuwa hawana ushirikiano bungeni hilo litakuwa kosa kubwa na nadhani sisi wananchi tutawahukumu. Siku zote agenda za kitaifa na zenye manufaa ya kitaifa hazitakiwi kupingwa tu kwa sababu eti hatuna ushirikiano bungeni. Hilo litakuwa ni kosa. Ninaamini yanaweza kuwapo mambo ya maana ambayo hata upinzani utayakubali na kuyapitisha bila shida kama vile walivyopitisha kwa pamoja na chama tawala mswada wa mfuko wa jimbo bila upinzani wa ndani ya bunge ingawa kulikuwa na upinzani mkubwa toka nje ya bunge. Lakini ukijaribu kupinga hoja ya maana iliyoanzishwa na CUF au na Chadema au na NCCR kwa sababu hamko pamoja kwenye alliance wakati kimsingi ni hoja ya muhimu nalo si jema na nilishauita huo kuwa ni wehu.

Nimesikia asubuhi kwa mfano Rashid Hamad akisema kuwa anaona issue ya Katiba mpya kama ni moja ya kitu muhimu kinatakiwa kishughulikiwe na bunge hili. Sasa ikitokea motion hii ya katiba mpya ikawa tabled na Chadema na CUF wakaipinga kwa sababu tu hawako pamoja kwenye kambi moja basi naweza kuuita huu kuwa ni wehu. Ushauri wangu ni kwamba hata huo ushirikiano lazima tuwe waangalifu sana. Nakumbuka game alilocheza John Cheyo kwenye bunge la tisa, na kama si busara ya spika aliyekuwepo Cheyo alionekana kafanya kitu cha kawaida maana ni haki yake kuamua anavyoona! Sasa kama spika angekuwa ni yule ambaye ana side one side kama tunavyoogopa kuwa bunge hili laweza kuwa, basi fikiri nini kingetokea. Tusiwalaumu tu Chadema lakini pia tuwasikilize na nimeona michango mingi hata toka kwa viongozi wa Chadema hapa wakitetea hoja zao.

Hata hivyo si vibaya kuwashauri, ila pia tusiwalaumu tu kwa maamuzi yao kila mara. Tushiriki kuleta mabadiliko kama ilivyokuwa siku zilizopita.
ASANTE
 
Kaa la Moto,
Mimi mtazamo wangu nadhani hatukutoa majibu mazuri isipokuwa tumezungumzia zaidi kwa mapenzi yetu ya chama Chadema. Leo hii akisoma mtu asiyekuwa mwanaChadema, asiyefahamu kwa nini Chadema imefanya kufanya kadhaa wa kadhaa akifuata maswali ya Pasco hataelewa lolote iwe kutoka majibu ya Dr.Slaa au wengineo kwani zaidi uchambuzi umekwenda ktk kazi yake yeye Pasco jinsi alivyoifanya. Ni sawa kabisa na kumuomba yeye ushahidi wa yale aloandika hivyo inatukwaza wengine tusiojua kitu.

Mambo mengi leo hii yanajitokeza baada ya mwanzo mbaya, mimi naamini kabisa Hamad katoa majibu yote hayo kutokana na wao kutegemea kwamba tungeshirikiana nao bungeni hivyo kupeana Ulaji. Utanisamehe lakini, kwani binafsi naamini sana kwamba wapo wabunge wengi pale bungeni wanatafuta ulaji zaidi ya uwakilishi wao kwani vyeo hivi vya haya mabaraza huja na ruzuku zake iwe posho zaidi ya vikao na kadhalika hivyo kwa CUF kukosa nafasi za Ulaji ama niseme kwa lugha ya kisiasa, kuwa part ya Wasemaji ndani ya kambi ya Upinzani, kumeweka dosari kubwa ktk ushirika wao, na ndio maana leo Hamad anabwabwaja yote haya ili mradi kuonyesha hasira zao kuwa Chadema imewaacha mataani.

Kama sikosei Dr.Slaa alisema CUF walikubali kuungana nasi ktk Upinzani na kuahidi kumpigia kura mgombea wa Chadema ktk kiti cha Uspika lakini matokeo yake yamekuwa tofauti pasipo sisi kupewa sababu. Je, makubaliano hayo yalitangulia kabla Chadema hawajachagua uongozi wa kambi ya Upinzani, hivyo CUF waliipona wametupwa nje ndio wakaja na hasira hizi..

Kumbuka Chadema hawana ulazima wa kuunda baraza la mseto, wao ndio wameshika nafasi ya pili na wana uwezo wa kuunda chombo hicho kisheria pasipo kuwahitaji CUF, lakini pia ikiwa ahadi hizi za ushirikiano kulitangulia kabla ya Chadema kuchagua safu ya viongozi wa Upinzani bungeni basi tukubali tumeamua kufanya hivyo kwa sababu Chadema haiwahitaji CUF wala vyama vingine ktk kuhitaji kura zao ktk mapendekezo ya kambi hiyo ya Upinzani.

Kuna hatari ya maamuzi kama haya hasa inapoingia uhasama bungeni kiasi kwamba wabunge wakashindwa kufikiri na kutimiza yale wananchi tulowatuma bungeni.. Hizo siasa za maji taka zikaingia hadi bungeni tena upande wa Upinzani wakawaacha CCM wakipeta na kuchekelea, jambo ambalo athari yake itakuwa kubwa zaidi kwa wananchi ambao wanategemea mageuzi ya hata policies zilizokuwepo.

Kwa hiyo mkuu wangu Yote unayoyasikia leo, Mbowe akizungumza kama kiongozi wa Upinzani na hamad kama msemaji wa kundi jingine ni baada ya matokeo ambayo kama sikosei hamad alisema CUF hawataungana na Chadema ikiwa vyama vingine havitashirikishwa..Na kwa mtazamo wangu sioni ubaya wake hata kidogo kwani Mrema pamoja na kuwa supporter wa CCM sidhani kama atapinga kuungana na Chadema inapofikia maswala ya katiba, NEC, Usalama wa Taifa na kadhalika, unless JK amchague yeye kushika Uwaziri wa mambo ya ndani. Hivyo wakati wao wakitazama nafasi zao za ulaji nadhani nasi tutazame maslahi yetu yataweza vipi kutetewa bungeni kwani napoandika hivi nimeuvua Uchadema na kuwa Mtanzania ambaye nataka mageuzi kupitia bungeni.
 
Last edited by a moderator:
Kaa la Moto,

Kumbuka Chadema hawana ulazima wa kuunda baraza la mseto, wao ndio wameshika nafasi ya pili na wana uwezo wa kuunda chombo hicho kisheria pasipo kuwahitaji CUF, lakini pia ikiwa ahadi hizi za ushirikiano kulitangulia kabla ya Chadema kuchagua safu ya viongozi wa Upinzani bungeni basi tukubali tumeamua kufanya hivyo kwa sababu Chadema haiwahitaji CUF wala vyama vingine ktk kuhitaji kura zao ktk mapendekezo ya kambi hiyo ya Upinzani.

Kuna hatari ya maamuzi kama haya hasa inapoingia uhasama bungeni kiasi kwamba wabunge wakashindwa kufikiri na kutimiza yale wananchi tulowatuma bungeni.. Hizo siasa za maji taka zikaingia hadi bungeni tena upande wa Upinzani wakawaacha CCM wakipeta na kuchekelea, jambo ambalo athari yake itakuwa kubwa zaidi kwa wananchi ambao wanategemea mageuzi ya hata policies zilizokuwepo.
Mkandara,

Nakumbuka nimesoma thread moja ambayo Dr Slaa mwenyewe alikuwa akiweka wazi kuhusu jambo hili. Alisema kuwa Chadema walilifanya jambo hili kwa CUF kabla hata hawajaamua kuunda serikali yao na inaelekea CUF walishachukua uamuzi wao kimya kimya. Tena akasema wazi kuna mambo mengi ambayo yalikuwa yakiendelea nje ya uelewa wa JF na wao kufikia uamuzi huo walisharidhika kuwa wenzao hawana haja na mashirikiano.

Hata hivyo aliweka bayana kuwa CUF waliwaandikia Chadema kuwa wao kama CUF watawaunga mkono Chadema kwenye issue ya usipika kwa Marando lakini hawakutaka kujibu lolote kuhusu serikali ya umoja katika upinzani. Lakini akasema pia Chadema wamepata habari kuwa CUF wamepewa orders toka Zanzibar kuwa wawa support CCM. Na akasema let us wait and see what will be the truth na bila shaka ukweli uko wazi na kila mmoja aliuona na hata leo umeonekana. so, jua kwamba Unaweza mpeleka ng'ombe bwawani lakini huwezi mlazimisha ng'ombe kunywa maji.

Inaelekea CUF tangu mwanzo hawakufurahia Chadema kusimamisha mgombea urais maana kuna mahali wali protest na walitaka instead Chadema wawaunge mkono, sasa wanaonyesha makali yao. hahahahahahahaha. Kwa hili hata nikijivua uchadema liko wazi!

So ulitegemea nini mkuu wangu?
 
Jamani kinachoendelea ni kawaida ingawa kinachochewa sana na siasa za tuhuma na kudharauliana kati ya vyama hivi viwili kwa muda mrefu sasa. Hata 2005, CUF pia waliunda serikali pekee yao hadi baada ya wiki kadhaa ndipo wakaweza kuongea kistaarabu na kukubaliana kushirikiana na ndio maana Hamad akaendelea kuwa kiongozi wa upinzani na Dr Slaa kuwa naibu wake huku Halima Mdee akiwa Naibu Chief Whip.

Lakini ni kweli hali ya sasa ni tofauti kidogo kwani CUF wanamakubaliano ya siasa za kistaarabu na CCM na huku CHADEMA imeamua kuchukua siasa za ngangari hadi kieleweke.....

Lakini pia wakati CUF walikuwa na Hamad Rashid ambaye ilikuwa ni rahisi kufanya naye kazi kwa nianjema kabisa. CHADEMA wanaye Freeman Mbowe ambaye hulka yake sio ya ushirikiano na zaidi kumuamini ni vigumu.....Wakiweza kuyazungumza haya kwa uwazi na lile la CHADEMA kuwaona CUF ni Waislamuwaislamu na CUF kuwaona CHADEMA Wakristowakristo...ni wazi hekima zinaweza kushika hatamu na Watanzania wote wakafaidika na mafanikio ya vyama hivi na wenzao wa NCCR mageuzi
 
Ni zipi hizi kijana! maana hizi unazosema zilitanguliwa na zile siasa za ngangali. Kwa hiyo almost everything has got its starting point. Bila shaka na Chadema kitaeleweka. Don't worry!
 
Big up Dr
Dr amejibu vizuri jamani.Watu ni vichwa.Sisi tumekaa tu tunafikiri viongozi wetu hawaoni mambo kumbe wako mbele sana kisayansi.
Yusuf makamba angeweza kutoa majibu hayo?si angeongea utumbo mtupu
 
Kaa la Moto,

Mkuu wangu pengine hukumsoma vizuri Dr.Slaa. nakumbuka alichosema ni kuhusiana na Uwakilishi wa CUF ktk swala la Uspika ndio wabunge wa Zanzibar walipewa maagizo kuwa support CCM. Hapa ndipo ujumbe wangu unapokuja ya kwamba maadam Wabunge wa Zanzibar walipewa amri ku support CCM haina maana wale wa bara nao watafuata hivyo hivyo kwa hiyo bado Chadema inaweza kupata kura na support kutoka CUF bara pamoja na vyama vingine.

Sasa iwe Hamad Rashid alidanganya kusema hivyo au walikuwa na mpango mwingine zaidi na CCM ktk hili bado sio mwisho wa hoja nyinginezo za bungeni ambazo Chadema wanawahitaji CUF na vyama vingine kupata kura zao. Kuwapachika CUF na wengineo ktk kambi ya Upinzani kunawaondolea ile nguvu ya kuwapa support CCM ktk issue zinazoandaliwa na Upinzani dhidi ya sera za CCM. Halafu unaweka picha kwa wananchi kwamba Chadema ipo tayari kushirikiana na chama chochote pasipo kujali tofauti za Ki itikadi au matokeo ya Uchaguzi kwa maslahi ya Taifa na sio ya chama.

Mkuu wangu point nyingi nilizozisoma mimi humu zinahusu Chadema na Uchadema zaidi ya sababu zinazojenga Taifa au ngome ya Upinzani kwa manufaa ya taifa. It's all about Chadema na kunufaika kwake wakifanya hivi ama vile..ndipo nami nasema tuwe makini na hizi siasa za majitaka bungeni kwani Upinzani wasipokuwa mstari mmoja dhidi ya chama tawala na kuanza kutupiana lawama mara nyingi kama sii zote faida kubwa huenda kwa chama tawala.

Na mwsiho wa siku miaka mitano itakwisha hatukubadilisha hata moja bungeni zaidi ya kupitisha miswada baada ya miswada na kuzidi kuwanyonga wananchi..Matokeo yake wananchi hawatakuwa na imani na vyama vyote iwe CCM, Chadema wala CUF na hapo ndipo hasira zao zinaweza kuwaangusha hata Chadema. Kinachoendelea leo baina ya Chadema na CUF ni aibu tupu kwa vyama vyote kwa sababu wote hawa wanatazama maslahi ya vyama vyao bungeni badala ya kuweka maslahi ya wananchi mbele ya uwakilishi wao.
 
Last edited by a moderator:
Izi hoja ni nzito kweli kweli, sijui ni Wa TZ. wangapi watakuwa na uwezo wa kuziaccess na kuzielewa. Ingawa watu wamehamasika sana na mambo ya kisiasa kwa sasa, uchache wa waliojitokeza kupiga kura unaonesha bado watu wengi hawataki kukubaliana na reality na wanaendelea kung'ang'ania emotions zao.

Hivyo nashawishika kuamini hata kama kitu hakina mantiki yoyote, kukifanyia kazi ni muhimu kama unataka kupata ushindi kwenye siasa za TZ sababu watu wengi hawana muda wa kufikiri au kusikiliza facts nzito zilizopo. Ni bora hoja za kwanini ni shida kuunganisha vyama vya upinzani au hata upinzani bungeni ziwekwe wazi kwa waTZ ili kufuta ile mentality ya kwamba watu ni wapinzani ni wabinafsi na hivyo hawana jipya katika matatizo kama ya ukosefu wa maadili.

Kweli Jamiiforums ni shule/chuo cha ukweli, nimekuwa nikijifunza na kupata habari nyingi sana humu, ila leo nimejifunza na kuelewa zaidi.

HONGERENI SANAAAA & keep it up.
 
Karibu mkuu endelea na wewe kuchangia kwa ajili ya ukombozi wa nchi yetu. Naona ni mchango wako wa kwanza na umejiunga hapa tangu Feb. tuendeleze mapambano.

Karibu sana.
 
Sasa bwana mkubwa kama wewe ni layman unajiondolea mwenyewe credibility ya kutoa ushauri wa maana. Kwani ukisema tu wewe ni layman wale ambao wanaelewa zaidi wa mambo watakupuuza tu.
HISIA KALI, kiukweli mimi ni just a layman, kwa hiyo nikiwa layman ndio nikose credibility ya kutoa maoni yangu au ushauri wa maana?.
Si kweli kuwa wale wenye uelewa zaidi,wanawapuuza ma laymen, ndio maana wewe ni shahidi, kwani wapiga kura wengi ni kinanani kama sio sisi ma layman, mbona wanakuja kuomba kura, wanatupigia mpaka magoti?, wengine hukaa nasi hadi kwenye mavumbi, kweli wanatupuuza?. Naamini wenzetu wanatusikiliza sana sisi ma layman ndio maana hata thread imejibiwa.
 
Ndugu Mkandara,

siamini kuwa wabunge wa CUF wa Zanzibar wanaweza wakatengana na wenzao wa Bara; hili jamani tuwe realistic. Yaani ni kuunda kambi ambayo unajua haitkuwa na mwelekeo ili mradi tu huko nje uonekane umeungana? Wabunge wa CUF kutokea Zanzibar ndo wanaoifanya CUF iwe na nguvu ndani ya Bunge la jamhuri ya muungano. Wabunge wa bara ni wawili tu!! Sasa Chadema iungane na CUF kwenye kambi ya upinzani wakati CUF wameshapewa maelekezo kutoka Zanzibar kuwa waiunge mkono CCM. Yaani Chadema iseme, aaa unajua ninyi CUF ni upinzani, hata kama mnaiunga mkono CCM, tuwe kambi moja halafu wale wabunge wenu wawili wa bara ndo wasiwe wanaiunga mkono CCM! Kweli unaamini hii ni practical? Yaani wabunge wa CUF wana maelekezo kutoka kwenye chama chao yanayowataka waiunge mkono CCM, halafu bado unaona kuna hoja, kwa mfano ya katiba, ambayo unaamini CUF wataiacha CCM waiunge mkono Chadema.

Ohh, as much as tunapenda kuona nguvu ya upinzani ikiongezeka, tuwe wakweli na tuangalie mambo kwa hali halisi. CCM wameshanusa harufu ya kushindwa, wako tayari kutoa sacrifice, na sacrifice hiyo ni kuwa embrace baadhi ya wapinzani. Haikuwa rahisi kwa Mahafidhina wa uingereza kukubali kuungana na waliberali. Lilikuwa jambo gumu, lakini when madaraka is at stake, lolote laweza kutokea! CUF wameambiwa kutoka Zanzibar (ilipo ngome yao) kuwa waiunge mkono CCM; kwa hivyo voting zao zote itakuwa ni pro CCM. Itakuwa ni kujaribu kuzoa maji yaliyomwagika kwa Chadema kujaribu kuwang'ang'ania CUF. Hata mie sioni haja ya kufanya hivyo, unless Chadema nayo ikubali kuwa itapiga kura zake kuiunga mkono CCM. Hapo tutakao umia ni wapiga kura, kwani mtawala atakuwa amejihakikishia kutawala bila hata kelele.

Kwa numbers zilivyo huko bungeni, bado upinzani ni noise tu kwa hapa Tanzania. CCM bado wanaweza wakafanya chochote bila kuhitaji mpinzani yeyote. Lakini noise zikiwa genuine, itakuwa ngumu kwa CCM kutawala kwa mtindo ule ule wa business as usual. Tumeona mfano wa mambo ya EPA na Richmond. Ingawa bado wahusika wakubwa wako at large, lakini noise za wapinzani zilisaidia angalau kuwafunua macho wabongo walio usingizini. Kwa hiyo, tunahitaji upinzani genuine, hata kama utakuwa na wabunge wachache, cha muhimu uwe upinzani wa kweli usio na chembe au ukakasi wa kushirikiana na utawala. Only then nguvu ya hoja itasimama. Upinzani nusu, utawala nusu (Status ya CUF leo) haiwezi kuwa kitu tunachotamani kuona wengi.
 
Back
Top Bottom