CCJ kuanza Charm offensive! - Ask your questions!

Za kutounga mkono chama chochote cha upinzani kwasababu ya kuion'goa CCM madarakani kwani naamini lengo si kuwa madarakani tu.Mrengo wa CHADEMA ni Center Right....Ni vema vigogo wote wa CCJ wakaunga mkono CHADEMA kwakuwa vinafanana sana kimtazamo na hata kiitikadi..

center right ina sifa gani?
 
Bibi Ntilie,
Kwanza samahani sana kama nilikukwaza lakini hakuna mahala nimekuseng'enya hata kidogo kwani JF ni uwanja wa wazi kwa watu wote hata wasiokuwa wanachama..Ni ktk fikra kama hizi ndipo tunapokosana.. watu kutotumia facts bali kuzua jambo ili mradi tunabishana..halafu mimi na Mwakijiji hatukuanza jana, ni wapiganaji kwa njia tofauti na hakika tuna tofauti zetu ktk dini, kabila,malezi na mengine mengi tu ambayo yanamfanya yeye kuwa mwanakijiji na mimi Mkandara..Lakini bado tuna umoja wa nguvu kubwa ktk mapambano haya toka zamani.

Hatuwezi kuwa sawa hata siku moja ila tunaweza kuafikiana ktk mambo kadhaa na pengine hata kufanana. Nimewahi kukutana na Mwanakijiji na hakika ana mwamko mkubwa ktk harakati za ukombozi wa Tanzania kupitia maandishi yake na fikra zake lakini ukombozi huu sii wake peke yake, ni weetu sote na ndio sababu kubwa inayonisukuma mimi kuchangia mawazo yangu ktk kutafuta ufumbuzi..Hii hofu ya kutokubaliana nadhani inawasumbua sana lakini ndivyo kijiwe hiki kinavyotakiwa kiwe kwani mjadala siku zote hutupa nafasi ya kujadili vitu kwa mapana zaidi, lengo likiwa kuelimishana, kufahamishana na pengine kuchukua maamuzi yaliyo sahihi kuhusiana na mada.

Nakumbuka mwaka 2005, nilikuwa na mjadala kama huu hapa lakini wakati ule walikuwa Chadema na sera yao za Majimbo na matumizi ya helikopta kupambana na CCM. Tulitumia muda mrefu sana kubishana juu ya uwezo wa Chadema kushinda kama wasipojiunga na wapamnbanaji wengine na niliambiwa hivi hivi kuwa nina Uhasama na Mbowe. Jambo ambalo wengi hawakufahamu kwamba Mbowe alikuwa mshikaji na tunafahamiana zaidi ya kumtaja hapa kijiweni..wakashindwa pia kufahamu kwamba ushindi wa Chadema ni ushindi wangu na watanzania wote pasipo kuwa wanachama wa Chadema kwani ukombozi wa nchi haulazimishi watu wote kushika Bunduki..

Leo hii Mwanakijiji ameshika Bunduki kubwa (Itikadi) na tunampa kila sifa za kujitoa mhanga kuwa mstari wa mbele ktk Upiganaji lakini pia tukumbuke kwamba hakuna mpiganaji anayekwenda vitani na silaha kubwa pasipo plan. Tunachojaribu kujenga hapa ni plan ya ushindi laa sivyo ya nini kubeba bunduki kubwa kuingia vitani ukijua hakuna ushindi. Hii sio vita ya Mwanakijiji au CCJ, vile vile kushindwa kwa wapiganaji wengine kina Chadema, NCCR,CUF na wengineo wote hakuwezi kuondoa haki na tumaini la CCJ kuingia vitani isipokuwa CCJ pasipo plan safi, silaha hiyo haiwezi kushinda vita hivi..

Na kama ujuavyo nilitoa mchango wangu ambao Mwanakijiji hakuupokea vema kama walivyokataa Chadema, na hata CUF niliwahi kuzungumzia kuhusu imani yangu na Seif Sharrif Hamad kuwa ni kiongozi dhaifu mwenye agenda ya kupigania haki za Wapemba (Zanzibar) zaidi kuliko suhindani na CCM...Nimepinga pia maswala mengi ya chama CCM na sijasikia mtu akisema kama hutaki anayofanya JK tuwaache wafanye wanavyotaka wao...hii lugha hata nashindwa kuielewa.

Kwa hiyo haya ndio mawazo yangu yaliyotangulia sikuwa na wala sintakuwa na ugonvi na Mwanakijiji isipokuwa huwa tunarushiana tope hapa na pale tunapokutana viwanja. Namheshimu sana na nashukuru Mungu tuna watu kama yeye ktk kijiwe hiki pamoja na kwamba tunatofautiana sana kimtazamo ktk baadhi ya maswala. Much respect kwake, ila najua humkera sana napomkosoa ktk hoja zenye utata.

Hayo ndio yangu Bibi Ntilie, na katika issue ya TAA nadhani tuache kama ilivyo kwa sababu kama nilivyozungumza hapo awali. Kutokuwa na historia ya Uhuru wety kabla ya mwaka 1952 kuna sababu na sababu zenyewe ndio kama hizi hapa. lakini nakuambia nilichoandika ndio Ukweli wenyewe na kutowekea maanani ni pamoja na majibu yenu.

Baada ya kufikiria kwa muda nimefanya editing habari iliyofuata... mtanisamehe kwa kuiondoa ili turudi ktk mada husika....samahani sana.
 
Za kutounga mkono chama chochote cha upinzani kwasababu ya kuion'goa CCM madarakani kwani naamini lengo si kuwa madarakani tu.Mrengo wa CHADEMA ni Center Right....Ni vema vigogo wote wa CCJ wakaunga mkono CHADEMA kwakuwa vinafanana sana kimtazamo na hata kiitikadi..

GS

Asante kwa kuelezea vizuri eti Chadema ni chama cha kilibelari na CCJ ni chama cha mlengo wa kulia. Kama ujamaa ni mlengo wa kulia basi mlengo wa kushoto haupo duniani. Kuna watu humu wana flip flop sana kuliko hata john kerry. ukirudi nyuma kidogo tu utaona wanasema kuwa CCJ haiwezi kuungana na CHADEMA kwa sababu CCJ ni chama cha kijamaa na CDM ni chama cha kibepari leo tena kinyume.

M=J
 
Mojawapo ya matatizo ambayo wakosoaji wa Nyerere walikutana nayo ni kudhania tunapozungumzia "Ujamaa" tunazungumzia "Marxist ideology" ambayo Magharibi inajulikana kama "socialism". Sasa nikisema ni "mrengo wa kulia" inaweza kukupa shida kwa sababu mawazoni unafikiria nazungumzia marxist ideology of socialism which to a very large extent is a very liberal (leftist) ideology.

Nyerere's Ujamaa is a distinct social-political and economic system that is founded on some very certain principles that are enshrined in African psyche. You have to read these principles to understand that indeed "Ujamaa" is to the right of capitalism. I mean far right.
 
Mwanakijiji na Shalom CHADEMA sio chama cha kiribelari..Soma hapa Falsafa na Itikadi ya CHADEMA..Huu ndio mtazamo wetu.

  1. Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika "Nguvu na Mamlaka ya Umma" (The People's Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.
  2. Aidha falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.
  3. Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.
  4. Historia inaonyesha kuwa "UMMA" wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.
  5. CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka "Nguvu ya Umma". Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.
  6. CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa "kuchaguliwa" kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza "waliowachagua" kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.
  7. Hivyo basi, falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.
  8. Falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.
  9. CHADEMA ni chama cha itikadi ya MRENGO WA KATI (center party).
  10. CHADEMA ni chama kinachoamini kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi kwa kutumia raslimali za nchi yetu bila kuathiri uhuru wa Taifa, na kuhakikisha kuwa umma kwa ujumla unanufaika na raslimali zao.
  11. CHADEMA inaamini katika kujenga na kuimarisha uchumi wa soko huru, utakaoheshimu na kulinda haki na mali za watu, biashara huru na sekta ya watu binafsi bila kupoka mamlaka ya umma katika maeneo nyeti hususani pale penye hitilafu ya soko au penye maeneo nyeti ya kiuchumi. Tunaamini katika soko huru sio soko holela.
  12. CHADEMA inaamini kuhakikisha matumizi bora ya raslimali asilia za nchi ili zichangie kikamilifu katika pato la taifa na hasa kuboresha huduma za kiuchumi zinazotumiwa na wananchi wote.
  13. CHADEMA inaamini katika uzalendo na kuthamini mila na desturi zetu zilizo nzuri.
  14. CHADEMA inaamini katika uhuru chini ya sheria zilizo za haki.
  15. CHADEMA inaamini katika siasa ambazo ziko juu ya vyama zenye kusimamia zaidi maslahi ya Taifa.
  16. CHADEMA inaweka umuhimu wa pekee katika familia kama moja ya taasisi muhimu ya kijamii.
  17. CHADEMA inaamini katika umuhimu wa uhuru wa kuamini katika kujenga maadili ya mwanajamii mmoja mmoja bila kuifanya dini kuwa sehemu ya dola.
  18. CHADEMA inaamini taifa linaundwa na watu, hivyo uhai wake unawategemea watu, na mabadiliko yake yanatokana na watu.
  19. CHADEMA inaamini katika kujenga uwezo wa wazawa katika kumiliki na kuendesha uchumi.
  20. CHADEMA inaamini kumiliki raslimali na mali miongoni mwa wananchi kunawapa uhuru zaidi hivyo tunataka kujenga chama na baadaye taifa lenye kutoa fursa, ambapo kila mtu bila kujali asili na hali yake anaweza kutimiza na kufanikiwa kadiri ya vipaji vyake.
 
Bibi Ntilie,
Kwanza samahani sana kama nilikukwaza lakini hakuna mahala nimekuseng'enya hata kidogo kwani JF ni uwanja wa wazi kwa watu wote hata wasiokuwa wanachama..Ni ktk fikra kama hizi ndipo tunapokosana.. watu kutotumia facts bali kuzua jambo ili mradi tunabishana..halafu mimi na Mwakijiji hatukuanza jana, ni wapiganaji kwa njia tofauti na hakika tuna tofauti zetu ktk dini, kabila,malezi na mengine mengi tu ambayo yanamfanya yeye kuwa mwanakijiji na mimi Mkandara..Lakini bado tuna umoja wa nguvu kubwa ktk mapambano haya toka zamani.

Mkuu Mkandara,
Asante. Pole sana. Sikuwa na maana yoyote ya kwamba umenisengenya in the real sense/meaning of the word. Unajua wakati mwingine akina 'bibi kizee' mara nyingi tunapenda kuweka mambo - with 'a light touch' tuliyojifunza kwa Adam Lusekelo!! No hard feelings I hope.

Narudia kusema ninaipenda sana michango yako humu na kama tunatofautiana basi ni katika ile hali ya kawaida ya kwamba kila mtu ana mtazamo wake kuhusu mambo fulani fulani. Naamini nimesamehewa!
 
Hapa kina Mkandara tupo wengi sana....CCJ!!! Mhhhh

omarilyas

Omarilyas. He, he, heeeee! How are you?
Kwani tatizo lako na CCJ ni lipi hasa? Waanzilishi wa CCJ ni Wazalendo kama ulivyo wewe na wengine wote walio na uchungu na nchi hii na hawakubaliani na status quo au mwenzetu unaona tambarare tu?
 
Mwanakijiji na Shalom CHADEMA sio chama cha kiribelari..Soma hapa Falsafa na Itikadi ya CHADEMA..Huu ndio mtazamo wetu.

  1. Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika "Nguvu na Mamlaka ya Umma" (The People's Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.
  2. Aidha falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.
  3. Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.
  4. Historia inaonyesha kuwa "UMMA" wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.
  5. CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka "Nguvu ya Umma". Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.
  6. CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa "kuchaguliwa" kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza "waliowachagua" kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.
  7. Hivyo basi, falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.
  8. Falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.
  9. CHADEMA ni chama cha itikadi ya MRENGO WA KATI (center party).
  10. CHADEMA ni chama kinachoamini kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi kwa kutumia raslimali za nchi yetu bila kuathiri uhuru wa Taifa, na kuhakikisha kuwa umma kwa ujumla unanufaika na raslimali zao.
  11. CHADEMA inaamini katika kujenga na kuimarisha uchumi wa soko huru, utakaoheshimu na kulinda haki na mali za watu, biashara huru na sekta ya watu binafsi bila kupoka mamlaka ya umma katika maeneo nyeti hususani pale penye hitilafu ya soko au penye maeneo nyeti ya kiuchumi. Tunaamini katika soko huru sio soko holela.
  12. CHADEMA inaamini kuhakikisha matumizi bora ya raslimali asilia za nchi ili zichangie kikamilifu katika pato la taifa na hasa kuboresha huduma za kiuchumi zinazotumiwa na wananchi wote.
  13. CHADEMA inaamini katika uzalendo na kuthamini mila na desturi zetu zilizo nzuri.
  14. CHADEMA inaamini katika uhuru chini ya sheria zilizo za haki.
  15. CHADEMA inaamini katika siasa ambazo ziko juu ya vyama zenye kusimamia zaidi maslahi ya Taifa.
  16. CHADEMA inaweka umuhimu wa pekee katika familia kama moja ya taasisi muhimu ya kijamii.
  17. CHADEMA inaamini katika umuhimu wa uhuru wa kuamini katika kujenga maadili ya mwanajamii mmoja mmoja bila kuifanya dini kuwa sehemu ya dola.
  18. CHADEMA inaamini taifa linaundwa na watu, hivyo uhai wake unawategemea watu, na mabadiliko yake yanatokana na watu.
  19. CHADEMA inaamini katika kujenga uwezo wa wazawa katika kumiliki na kuendesha uchumi.
  20. CHADEMA inaamini kumiliki raslimali na mali miongoni mwa wananchi kunawapa uhuru zaidi hivyo tunataka kujenga chama na baadaye taifa lenye kutoa fursa, ambapo kila mtu bila kujali asili na hali yake anaweza kutimiza na kufanikiwa kadiri ya vipaji vyake.
Bibi Ntilie,
Mkuu hayo yote tuyaache nyuma tugange yaliyopo na yajayo maanake mzigo huu unatuelemea sote.

Kama Chadema ni chama cha CENTRAL, meaning a Reform Party sijui Mwanakijiji na hao CCJ wao wanakuja na itikadi gani tofauti...
Nijuavyo mimi Central party mara zote huundwa kwa sababu ya haikubaliani na uongozi mzima wa serikali unavyoendeshwa.. Mara nyingi ni pale nchi inapokotoka ktk dira au inapokosa DIRA, mambo yanaendeshwa KIUTAWALA zaidi ya KUONGOZA kwani Kutawala huhitaji dira wala idiology isipokuwa deceitful and control ya Utawala wako, usokuwa na Uhuru.

Hivyo kiitikadi Chadema wanataka ku reform serikali kuu, kurudisha Haki ya wananchi, kurudisha uhuru wao ili waongozwe na sii kutawaliwa kufuatana na dira ya taifa na kikubwa zaidi wananchi wawe ndio wenye control ya serikali kuu kwani hiyo ndio maana halisi ya wananchi walio UHURU..as to say Chadema noble cause ni true reform of the government..
Hii lugha naisikia tena CCJ! - what's up yaani tuna cenral party ngapi maanake nasikia hata Mtikila anajiiweka central..

Hapa ndipo napopigwa bao na siasa za Bongo maanake kila mtu ni reformist, ebu nitafutie mtu au kiongozi yeyote toka chama chochote Tanzania asome ya Chadema kisha anambie wapi anapingana na Itikadi ya Chadema! sidhani kama utampata...Kifupi Tanzania hatuna chama chochote chenye itikadi zaidi ya porojo..hakuna kitu Iitikadi za Kushoto wala Kulia, ila ni mapana ya fikra ktk muundo wa HAKI za jamii baada ya matokeo ndani ya nchi huru badala ya - Itikadi kuwa biblia ya mfumo wa maisha yao - way of life...

Utunzi wa Itikadi kidogo unafanana na Imani ya dini zetu ambazo kimsingi binadamu wote tunatafuta kutoingia motoni..Sasa hizi imani ziwe ni hadithi au kuna ukweli ndivyo siasa za Itikadi zinavyoaminiwa pia...Kila dini imetupa dira ya kuishi ili upate uzima wa milele, na tumepewa pia mamlaka ya kuchagua imani na umayoiamini wewe na haki ya kuyaendesha maisha yako kufuatana na imani ulokuwa nayo. Mwisho wa siku mhukumiwa ni wewe mmoja. Tofauti baina ya dini, Demokrasia huja na mfumo wa itikadi (Biblia) ambayo tunapewa dira ya kwenda sote peponi (maendeleo) na mamlaka ya sisi kuchagua itikadi gani tutaifuata kwa kupiga kura zetu haki ya wengi ktk ushindi hupewa nafasi ya kutuongoza, na sote tunafuata dira hiyo kuelekea huko kuzimuni.

Hivi ndivyo inavyotakiwa kuwa, Chama CCM wawe na Katiba yao ambayo CUF,NCCR au CCJ wakiisoma wanaona hakuna maendeleo kama tutafuata path hiyo.. CCM vile vile wakisoma za wenzao.. wapo wengine wanaweza kubaliana na nguzo za itkadi lakini kuna vipengele ambavyo havikubaliki na ndipo hujitenga na kuunda Central Right au Left. Ni kama kama dini moja ilojitenga ktk dhehebu fulani....

Ukija kwetu hakika sisi tumeuvaa mkenge, tumevamia mfumo huu Demokrasia kwa sababu Uongozi bora na mbaya kwa nchi zetu ni Mtawala mwenyewe...Aidha ana sifa za Dikteta, Corrupt, Kiongozi asiyependa madaraka ya kiutawala ila a kuongoza umma wake (hawa ni aghlabu kuwapata) but all of them huchaguliwa regardless of Idiology kwa sababu hatuna kitu hicho ila tunzi za haki za binadamu waliokuwa huru..Sawa na kuwa na Biblia au Kuran mkononi lakini sifa ya maisha ni kubembea kwa sana..
 
Mkandara nashukuru sana kwa kuchanganua hili kwa kina..Umeeleza vizuri sana sina cha kujazia nitaharibu.CCJ wamekuja na yale yale ya CHADEMA kimsingi hata mengine ni copy and paste ya CHADEMA na ndio maana nimekuwa nikisisitiza na kusema humu kuwa hakukuwa na sababu ya kuanzisha CCJ kwani kinafanana kabisa na CHADEMA.Ndio maana nimekuwa nikisisitiza na ninaendelea kusisitiza kuwa vigogo wanounda CCJ wajipange mapema kuwa na alternative ya kujiunga na CHADEMA watakapokosa usajili,wafanye hivyo mapema kabla ya kukosa usajili kwani maandalizi yanaanza sasa sio mpaka wasubiri wakose usajili.Na hata CCJ wakikosa usajili mwaka huu basi chama hiki kife natural death na nguvu zielekezwe kwa CHADEMA..Siipigii debe CHADEMA ila naeleza facts..
 
GS, ngoja nikae chini na kuchanganua matatizo ya sera za CHADEMA na ni kwanini ni kinyume na zile za CCJ. Kuamini vitu vile vile au kwa karibu haina maana mtatumia njia zile zile kwa sababu yote uliyoyasema kuhusu imani za Chadema yaweza kuwa ni imani ya CCM vile viile!
 
Gender Sensitive,
Shukran sana kwani hata mimi ambaye nimesema sana hapa kuwa mfuasi wa mrengo wa kulia sikupendelea flip ya Chadema toka KULIA kwenda KATI ambako hukubaliani na mwongozo wa kushoto au kulia ikiwa nchi imepoteza dira. Kusema kweli ilinipumbaza nikabakia domo wazi na siasa za Bongo lakini I guess, wana kila sababu kufanya hivyo kwani imani pasipo dira ni sawa na kutokuwa na imani kabisa.
Pili, ktk nchi ambayo siasa za magharibi haziwezi kufanya kazi ipaswavyo kutokana na watu na mazingira (maskini) nadhani pia ni muhimu kuweka nguvu ktk kusimamisha dira, majukumu ya Utawala bora na kuwaelimisha wananchi kwanza pasipo kuzingatia itikadi hizi za kulia na kushoto...

Kwa kiasi fulani nakubaliana na Chadema katika hatua yao ila sielewi kama wanayafanya haya wakiwa bado social conservative au watabakia reformist hata baada ya Ushindi kupatikana..Nakumbuka serikali ya Harper nchini Canada walifuata utaratibu huu kwa kujimega toka Conservative wakaunda Reform Party within Conservative kwa sababu chama kilikosa dira, viongozi walivunja miiko na maadili ya chama. Kwa hiyo wakajiengua wenyewe kuunda reform party kurudisha utamaduni wao kama wanavyotaka kufanya CCJ kutoka CCM. Kwa Canada waliweza kupata ushindi na wakarudisha Conservative kwenye madaraka baada ya kuganga njaa ya ushindi kwa chaguzi 3 kupita - miaka 12.

Sasa nikirudi nyumbani nakuta CCJ wanataka ku reform (changes) within - Chama cha Mapinduzi, na Chadema wanataka mageuzi ya Political structure nzima kwa malengo ya kuboresha maisha ya wananchi wote..Hivyo, kuna tofauti ya msingi wa malengo baina ya vyama hivi kama alivyokuwa akidai Mwanakijiji na sii kwamba sikumwelewa isipokuwa alichoshindwa kuelewa ni kwamba Ushindi wa CCJ utakuwa mgumu sana ikiwa hawa WATU wapiga kura wanachotaka kuona ni Kina nani wapo nyuma ya harakati hizi (Hatuaminiani).
Pili, Mazingira waliyoyaweka CCM tayari ni kutugawa ktk makundi ili tusiweze kufikia kura zinazotakiwa kupata Ushindi.. The winner take all ni mtego wa CCM ambao tayari wamekwisha jenga wanachama na wapenzi mara 2 ya jumla ya vyama vyote.

Mkoloni hakuwa mjinga kutumia divide and rule, tazama huko Iraq. Marekani walisema wazi kwamba Wakisha mwondoa Saadam watajaribu kuweka serikali moja wanayoipenda wao (demokrasia) na wakishindwa itabidi kuwagawa kwa kutumia imani zao za dini..Wairaq walijua fika azma hii na sisi wote tulijua hilo lakini kwa sababu Wairaq waliamini haiwezi kutokea leo wamegawanyika na hawana nguvu tena ila kupigana wenyewe kwa wenyewe..Na hawapendani kabisaaa yaani Uadui umekuwa mkubwa kuliko wakati wa Saadam.

Haya Tazama Palestine, wamegawanywa ktk makundi mawili, nguvu yao imekwisha kabisaa na watatawaliwa hadi Yesu arudi.. Hii ni mifano hai kabisa ambayo hatuwezi kuitazama kwa dharau kwani mfumo wa kuwagawa watu works na unaendelea kutumiwa na kila mwenye nguvu (power) na tamaa ya utajiri iwe ktk Familia, jamii au dunia. Umoja sii nguvu only apply kama some or all of you are doing nothing! Yale yaliyotutokea wakati wa Umtumwa kuchukuliwa na warabu wawili wenye migobole..Sasa hivi tuondokane na ujinga ule UMOJA ni NGUVU kama sote tutaweka nguvu zetu ktk kuleta mageuzi..
 
Ukweli ni kuwa wote CCJ, CUF na Chadema hawana ubavu by themself kuwang'oa CCM madarakani, pamoja na kuwa kwamba hivo vyama vyote vina sera nzuri na endelevu pengine kuzidi zile za chama tawala.

Nafikiri cha msingi ni kuangalia namna ya kuitoa CCM madarakani kwanza. Na wote tunajua kuwa as is uwezekano huo ni mdogo, sababu kuu ni kuwa kura za wapinzani zimegawanyika sana. Mimi bado maoni yangu ni kuwa hawa wapinzani wote waungane regardless ya itikadi zao, waungane kwenye majimbo ya uchaguzi na kusimamisha mtu mmoja kwenye nafasi ya urais.

Muungano huu sio lazima kwamba yaani waue vyama vyao hapana iwe ni coliation kama ilivo sasa UK, Ujerumani na nchi nyingine ulaya.

Hapa tutaendela kujadili wedha ni CCJ au Chadema ilhali hii ni nafasi nyingine ya kuwarudisha CCM madarakani kwa kishindo. WanaCCm hivi sasa wanazidi kutabasama na hili suala la CCJ kwa sababu wanajua wengi wa watu watakaoenda huko ni toka CUF na Chadema (of course na CCM pia wamo).

Sasa hivi utitiri wa vyama kweli ndio tija? au kama kweli waTz tunataka mabadiliko ya kweli ni lazima viongozi wetu wa upinzani wakae chini pamoja na kuona namna gani wanaweza kufanya kazi kwa umoja.
 
Nafikiri cha msingi ni kuangalia namna ya kuitoa CCM madarakani kwanza. Na wote tunajua kuwa as is uwezekano huo ni mdogo, sababu kuu ni kuwa kura za wapinzani zimegawanyika sana. Mimi bado maoni yangu ni kuwa hawa wapinzani wote waungane regardless ya itikadi zao, waungane kwenye majimbo ya uchaguzi na kusimamisha mtu mmoja kwenye nafasi ya urais.

kuna maswali nimeyauliza huko nyuma juu ya huu muungano usio muungano utafanya kazi vipi... lakini kwa vile tunapenda mazingaombwe basi tuko tayari kuwa na muungano usio muungano alimradi wote tunakubaliana ni muungano hadi tutakapogundua kumbe hatujaungana!
 
Mkuu Mwanakijiji Binafsi sipigii Chapuo any kind of Muungano ila nasema ni Lazima Vyama viwe na Strategies za Kauchiana Majimbo ili visigawane Kura, I don't care hata Rais akitoka CCM, CCJ au CHADEMA what I care about is a strong parliament. Sasa kwa hali ilivyo si CCJ, si CHADEMA wa si CUF peke yao wanaweza kupata 50% ya Viti vya Ubunge. Mimi Nataka vyama vitambue ni majimbo ypi CCJ ina Nguvu, wapi CUF ina Nguvu na wapi CHADEMA ina nguvu nk then vyama vingine visisimamishe Mgombea wa Ubunge katika hayo majimbo.

Nasisitiza tena bila ya kutengeneza Bunge lenye Nguvu CCM itaendeleza Undava tu kama kawaida
 
GS, ngoja nikae chini na kuchanganua matatizo ya sera za CHADEMA na ni kwanini ni kinyume na zile za CCJ. Kuamini vitu vile vile au kwa karibu haina maana mtatumia njia zile zile kwa sababu yote uliyoyasema kuhusu imani za Chadema yaweza kuwa ni imani ya CCM vile viile!

Huna sababu ya kupoteza muda kuangalia matatizo ya sera ya CHADEMA kwani ofcoz natambua hakuna sera zilizo perfect duniani kote,cha msingi ni falsafa na itikadi na utekelezaji wa sera zenyewe.Sera zaweza kuwa njema lakini utekelezaji hovyo..CCM Ujamaa lakini tunacheza ngoma nyingine kabisa..Itikadi inabeba kila kitu kwa mtazamo wangu..
 
Gender Sensitive,
Shukran sana kwani hata mimi ambaye nimesema sana hapa kuwa mfuasi wa mrengo wa kulia sikupendelea flip ya Chadema toka KULIA kwenda KATI ambako hukubaliani na mwongozo wa kushoto au kulia ikiwa nchi imepoteza dira. Kusema kweli ilinipumbaza nikabakia domo wazi na siasa za Bongo lakini I guess, wana kila sababu kufanya hivyo kwani imani pasipo dira ni sawa na kutokuwa na imani kabisa.
Pili, ktk nchi ambayo siasa za magharibi haziwezi kufanya kazi ipaswavyo kutokana na watu na mazingira (maskini) nadhani pia ni muhimu kuweka nguvu ktk kusimamisha dira, majukumu ya Utawala bora na kuwaelimisha wananchi kwanza pasipo kuzingatia itikadi hizi za kulia na kushoto...

Kwa kiasi fulani nakubaliana na Chadema katika hatua yao ila sielewi kama wanayafanya haya wakiwa bado social conservative au watabakia reformist hata baada ya Ushindi kupatikana..Nakumbuka serikali ya Harper nchini Canada walifuata utaratibu huu kwa kujimega toka Conservative wakaunda Reform Party within Conservative kwa sababu chama kilikosa dira, viongozi walivunja miiko na maadili ya chama. Kwa hiyo wakajiengua wenyewe kuunda reform party kurudisha utamaduni wao kama wanavyotaka kufanya CCJ kutoka CCM. Kwa Canada waliweza kupata ushindi na wakarudisha Conservative kwenye madaraka baada ya kuganga njaa ya ushindi kwa chaguzi 3 kupita - miaka 12.

Sasa nikirudi nyumbani nakuta CCJ wanataka ku reform (changes) within - Chama cha Mapinduzi, na Chadema wanataka mageuzi ya Political structure nzima kwa malengo ya kuboresha maisha ya wananchi wote..Hivyo, kuna tofauti ya msingi wa malengo baina ya vyama hivi kama alivyokuwa akidai Mwanakijiji na sii kwamba sikumwelewa isipokuwa alichoshindwa kuelewa ni kwamba Ushindi wa CCJ utakuwa mgumu sana ikiwa hawa WATU wapiga kura wanachotaka kuona ni Kina nani wapo nyuma ya harakati hizi (Hatuaminiani).
Pili, Mazingira waliyoyaweka CCM tayari ni kutugawa ktk makundi ili tusiweze kufikia kura zinazotakiwa kupata Ushindi.. The winner take all ni mtego wa CCM ambao tayari wamekwisha jenga wanachama na wapenzi mara 2 ya jumla ya vyama vyote.

Mkoloni hakuwa mjinga kutumia divide and rule, tazama huko Iraq. Marekani walisema wazi kwamba Wakisha mwondoa Saadam watajaribu kuweka serikali moja wanayoipenda wao (demokrasia) na wakishindwa itabidi kuwagawa kwa kutumia imani zao za dini..Wairaq walijua fika azma hii na sisi wote tulijua hilo lakini kwa sababu Wairaq waliamini haiwezi kutokea leo wamegawanyika na hawana nguvu tena ila kupigana wenyewe kwa wenyewe..Na hawapendani kabisaaa yaani Uadui umekuwa mkubwa kuliko wakati wa Saadam.

Haya Tazama Palestine, wamegawanywa ktk makundi mawili, nguvu yao imekwisha kabisaa na watatawaliwa hadi Yesu arudi.. Hii ni mifano hai kabisa ambayo hatuwezi kuitazama kwa dharau kwani mfumo wa kuwagawa watu works na unaendelea kutumiwa na kila mwenye nguvu (power) na tamaa ya utajiri iwe ktk Familia, jamii au dunia. Umoja sii nguvu only apply kama some or all of you are doing nothing! Yale yaliyotutokea wakati wa Umtumwa kuchukuliwa na warabu wawili wenye migobole..Sasa hivi tuondokane na ujinga ule UMOJA ni NGUVU kama sote tutaweka nguvu zetu ktk kuleta mageuzi..

Mkandara asante kwa shule nyingine,nimejifunza kitu kikubwa hapa..Naamini kabisa hata tukiingia madarakani tutabaki vile vile hatutaenda kwenye mrengo mwingine.It is so hard to deviete toka tulipo kwenda tusikoamini,naamini tunajifunza kutoka kwa wenzetu na tunachukua tahadhari.
 
Mkuu Mwanakijiji Binafsi sipigii Chapuo any kind of Muungano ila nasema ni Lazima Vyama viwe na Strategies za Kauchiana Majimbo ili visigawane Kura, I don't care hata Rais akitoka CCM, CCJ au CHADEMA what I care about is a strong parliament. Sasa kwa hali ilivyo si CCJ, si CHADEMA wa si CUF peke yao wanaweza kupata 50% ya Viti vya Ubunge. Mimi Nataka vyama vitambue ni majimbo ypi CCJ ina Nguvu, wapi CUF ina Nguvu na wapi CHADEMA ina nguvu nk then vyama vingine visisimamishe Mgombea wa Ubunge katika hayo majimbo.

Nasisitiza tena bila ya kutengeneza Bunge lenye Nguvu CCM itaendeleza Undava tu kama kawaida

Mzee Mwanakijiji,

Muungano niliokua nazungumzia ni more or less kama ndege ya Uchumi anaozungumzia hapo juu. Actually muungano sio neno sahihi bali tuite Ushirikiano yaani kama mkuu alivoweka wazi hapo ni muhimu vyama vya upinzani viangalia kwenye majimbo wapi kila chama kina nguvu basi vile venye udhaifu viache visisimaishe watu wao bali viunge mkono wengine . Mfano Kigoma waachiwe Chadema, Tanga na Zanzibar waachiwe CUf na kadhalika. Hii itaongeza idadi ya wabunge wa upinzani bungeni na kuwaongezea nguvu hivo hivo kwenye urais waangalie nani kati yao anakubalika zaidi (Slaa, Mpendazoe, Kabwe, Maalim, Lipumba) basi asimamishwe.

Chadema walifanaya hivi 1995, 2000 hawakusimamisha mtu kwenye urais bali wali support CUf. 2005 waliweka mtu lakini bado alikuwa nyuma ya Lipumba in third place, surely kama kweli Chadema wako serious na mgombea urais ni budi kushirikiana na CUF, peke yao ubavu hawana.
 
kuna maswali nimeyauliza huko nyuma juu ya huu muungano usio muungano utafanya kazi vipi... lakini kwa vile tunapenda mazingaombwe basi tuko tayari kuwa na muungano usio muungano alimradi wote tunakubaliana ni muungano hadi tutakapogundua kumbe hatujaungana!
Mkuu hayo maswali yako yanachanganya kwa sababu wewe hutaki kusema malengo yako isipokuwa ya wengine. Sema wewe malengo ya CCJ kisha tuone kama kuna watu hawakubaliani nayo..Nijuavyo tunakubaliana na hoja zetu kama tunavyokubaliana na hizo za Chadema - REFORM inahitajika..Na sote hapa tumefikia kutoa ushauri wetu ni kwa sababu tunaamini katika vyama vyote wapo wananchama na watu wanaotaka mageuzi (changes) ambayo ndio msingi wa muungano huu.

Kama nilivyosema hapo awali hakuna chama Tanzania chenye itikadi, ila ni mawazo ya kutuwezesha kutoka ktk Umaskini. Mapungufu ya CCM sii mapungufu ya itikadi yenyewe ila makosa ya viongozi wake wameshindwa kutuondoa ktk Umaskini..Ndivyo wananchi wote wanaamini bila kujali itikadi. Navyojua mimi hili ndio chimbuko la vyama vyote vya Upinzani nchini kuzaliwa kwake.

Mzee Mtei kutokubaliana na Nyerere na Ujamaa haina maana ilikuwa itikadi ya kisiasa ila dhidi ya mfumo wa Uchumi. Mrema na NCCR haikuwa kupinga Ubepari bali kupinga mfumo wa Uongozi ktk kukuza uchumi wetu kwa kutumia wageni (Wakaburu). Hivyo hiyvo vyama vyote vimeundwa kwa kutazama zaidi mapungufu ya Uongozi na sio mapungufu ya Itikadi kwani hatujawahi kutumia itikadi yoyote kiutawala toka tumeacha Ujamaa.

Nadhani utarurahishia sote ukiweka malengo ya CCJ hapa ukumbini na vizuri zaidi ikiwa malengo hayo yatazungumzwa na wahusika (vyama vingine) zaidi yetu sisi kwani huko ndiko utapata majibu yenye kuthibitisha muungano huu utakuwa wa aina gani. Mkubaliane msikubaliane swala la ushindi dhidi ya CCM ni lazima kuwepo na UMOJA wenu ktk hatua za awali, kinyume cha hapo itakuwa kazi kubwa sana kuushawishi Umma ikiwa vyama vyote vinahadithia hadithi ile ile...Utawala wa CCM ni Mafisadi!
 
Mkuu Mwanakijiji Binafsi sipigii Chapuo any kind of Muungano ila nasema ni Lazima Vyama viwe na Strategies za Kauchiana Majimbo ili visigawane Kura, I don't care hata Rais akitoka CCM, CCJ au CHADEMA what I care about is a strong parliament. Sasa kwa hali ilivyo si CCJ, si CHADEMA wa si CUF peke yao wanaweza kupata 50% ya Viti vya Ubunge. Mimi Nataka vyama vitambue ni majimbo ypi CCJ ina Nguvu, wapi CUF ina Nguvu na wapi CHADEMA ina nguvu nk then vyama vingine visisimamishe Mgombea wa Ubunge katika hayo majimbo.

Ndege ya Umma, hata vyama vikiachana majimbo tatizo bado litakuwa lile lile; vinaachiana majimbo ili kiwe nini? Na vinaachiana kwa makubaliano gani? Sema kwa mfano kwenye jimbo moja wagombea wawili wa CUF na CHADEMA wote wanaoonekana kukubalika kila mmoja akivuta karibu kura asilimia 40 na yule wa CCM anavuta asilimia 20, sasa hao wawili wanapoamua kukubaliana ni kwa misingi gani? Naomba uanishe japo kanuni tu za makubaliano hayo ziwe vipi au mmoja anaamua tu kujitolea kuwa basi "mgombea wetu anakubali kumpisha wa kwenu"?

Nasisitiza tena bila ya kutengeneza Bunge lenye Nguvu CCM itaendeleza Undava tu kama kawaida

Unafikiri Bunge lenye vyama vingi vidogo vidogo vilivyoachiana majimbo litakuwa na nguvu au bunge lenye wabunge wengi wa chama kimoja cha upinzani ndio litakuwa na nguvu zaidi?
 
Nyerere's Ujamaa is a distinct social-political and economic system that is founded on some very certain principles that are enshrined in African psyche. You have to read these principles to understand that indeed "Ujamaa" is to the right of capitalism. I mean far right.

Really? This is certainly big news to me. I have to revisit my ideological class!!
 
Back
Top Bottom