CCJ kuanza Charm offensive! - Ask your questions!

CCJ kuanza Charm offensive! - Ask your questions!

Kama uko dar unaweza kwenda Lumumba! ila uwe mwangalifu, wewe uliza wapiganaji ukioneshwa basi unamuuliza kadi, wanatembea nazo ili watakapopata tu usajiri waweze kuanza Charm Offensive na kutufundisha itikadi ya ujamaa (mlengo wa kulia) na kuchukua nchi kwa sababu chadema na vyama vin ginene havina itikadi -Did I say that?

yes u did and ur absolutely right!
 
Mkuu Mkjj, All the best na hicho chama chenu kipya na wengine wenye plan ya kuanzisha vyma vingine vipya mpaka vifike 100 all the best na ujinga na upumbavu uliokubuhu wa mgombea binafsi ili kwenye uchaguzi tuwe na wagombea wa urais kama 100 na nyie all the best.

Mimi huku kwetu Moshi ndani ndani naona kabisa jinsi CCM wanavyopiga magoli kilaini sababu tu ya watu kujifanya mambo ya itikadi, lakini mkoa wetu huu kuna wapinzani walishinda kwa gia moja tu ya ANTI CCM.

This is my last topic on this futile attempt ya kuanzisha CCJ eti kama chama mbadala.

Obama alishinda kwa Gear moja tu CHANGE WE CAN BELIEVE IN. Hii ndio nucleus ya ushindi wake, CHANGE FROM Status Quo hata kama na yeye ni status Quo, lakini gear ilikua CHANGE.

Zanzibar ni mfano hai kabisa wa jinsi ya kuishinda CCM. Zanzibar issue ni very simple CCM or not CCM (CUF). Kama wajanja( Wajuaji) wa bara na vyama utitiri wangeingia Zanzibar wala usingesikia possibility ya serikali ya mseto, sababu CCM na 48% wangeshinda kwani hiyo 52% wanayopata CUF ingegawanywa kwenye huo utitiri wa vyama.

Sasa Bongo na magenius wetu wanaotaka vyama vipya kila siku, hata ukileta gear ya change mkagawana kura vyama 10+, CCM Si bado mshindi??

Anyways, nitaumwa kichwa bure acha na mimi nifanye mipango ya kuanzisha chama kipya kwani ndio fashion bongo. Kila mtu mjuaji na mimi nisilale nyuma lazima niingie front na kuanzisha chama kipya.
 
Mkuu Mkjj, All the best na hicho chama chenu kipya na wengine wenye plan ya kuanzisha vyma vingine vipya mpaka vifike 100 all the best na ujinga na upumbavu uliokubuhu wa mgombea binafsi ili kwenye uchaguzi tuwe na wagombea wa urais kama 100 na nyie all the best.

Kuuita huu ni ujinga na upumbavu hakufanyi kung'ang'ania "CCM ingoke tu" kuwa ni hekima; inaweza kuwa ni version ya jambo lile lile la ujinga na upumbavu.

Mimi huku kwetu Moshi ndani ndani naona kabisa jinsi CCM wanavyopiga magoli kilaini sababu tu ya watu kujifanya mambo ya itikadi, lakini mkoa wetu huu kuna wapinzani walishinda kwa gia moja tu ya ANTI CCM.

Hilo laweza kuwa kweli; walishinda wapi na kwa ushindi wa aina gani? Naomba mifano tu ambayo imekufanya uchukulie "moshi" nzima iko hivyo.

This is my last topic on this futile attempt ya kuanzisha CCJ eti kama chama mbadala.

Of course.. yale yale... usianzishe hoja ambayo huwezi kuitetea.

Obama alishinda kwa Gear moja tu CHANGE WE CAN BELIEVE IN. Hii ndio nucleus ya ushindi wake, CHANGE FROM Status Quo hata kama na yeye ni status Quo, lakini gear ilikua CHANGE.

SI KWELI... alishindwa kwa sababu aliarticulate very clearly and boldy ni change gani aliyokuwa anaizungumzia... ! Hata kwa sisi ambao hatukukubaliana naye tulijua kabisa ni nini anataka kufanya. Sasa hamuwezi kusimama tu nakusema "CCM ing'oke" bila kutueleza halafu badala yake kiwe nini?

Zanzibar ni mfano hai kabisa wa jinsi ya kuishinda CCM. Zanzibar issue ni very simple CCM or not CCM (CUF). Kama wajanja( Wajuaji) wa bara na vyama utitiri wangeingia Zanzibar wala usingesikia possibility ya serikali ya mseto, sababu CCM na 48% wangeshinda kwani hiyo 52% wanayopata CUF ingegawanywa kwenye huo utitiri wa vyama.

Kama suala ni kungoa tu chama halafu mambo yawe yale yale kweli Zanzibar ni mfano mzuri! ni sawa kabisa na Chiluba na Kaunda! So.. kama lengo lenu ni alimradi mseme kuwa CCM imeondolewa madarakani na kukiingiza chama kingine chenye kumaintain status quo basi endeleeni.

Sasa Bongo na magenius wetu wanaotaka vyama vipya kila siku, hata ukileta gear ya change mkagawana kura vyama 10+, CCM Si bado mshindi.

Sasa hata msipogawana kura halafu mkashinda na kuendelea na kile kilichokuwepo au msikubaliane nini kiwepo kunaondoa vipi matatizo ya wananchi?

Anyways, nitaumwa kichwa bure acha na mimi nifanye mipango ya kuanzisha chama kipya kwani ndio fashion bongo. Kila mtu mjuaji na mimi nisilale nyuma lazima niingie front na kuanzisha chama kipya.

Jaribu tu na ukija na hoja tutakuunga mkono vile vile. Ndio uzuri wa demokrasia. Hadi kitakapopatikana kweli chama cha kweli cha upinzani nchini.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu nilijiunga na Chadema kwa sababu walikuwa mrengo wa kati kulia... Leo nawasikia nyie CCJ imekuja na mrengo wa Kulia...Mmmhhhhh! lakini maadam Chadema believe we need to REFORM the Government. I guess I will support them, will remain a Conservative til then!

Nakuomba pitia kwa makini kitu hiki HAPA
Kila la kheri mkuu..... tulikuwepo!
 
Wanaotaka kuingia madarakani ni lazima waje na wawe na sera na mipango inayoeleweka. Siamini kabisa katika muungano wa kutaka CCM iondoke madarakni bila wanaotaka kuiondoa kujulikana mipango yao nini kwa taifa na wataifanyaje? Wanasema the devil is in the detail. Obama hakusema tumuondoe tu Bush halafu tutajua cha kufanya mbele ya safari, Wamarekani wangemuona mzugaji. Aliwaambia kabisa atakachofanya na atakifanya vipi na kwa muda gani. Huo ndio msingi wa kuiondoa serikali iliyoko madarakani, siyo kusema tuiondoe tu alimradi turuke ruke mitaani kushangilia "CCM imeng'oka".. sasa mumuue Simba halafu mkaribishe CHui!? Well.. mtashangilia mmeua simba, lakini mtakuwa mmeondoa tatizo?

I thinK that is SUPERB. For sure mipango inayotekelezeka na Sera ni vitu vya msingi sana. But usisahau kuwa mipango na sera peke yake haviwezi kutufikisha pale tunapotaka Tanzania ifike, Pali Mipango na Sera lazima iende na Viongozi makini wenye nia ya dhati ndani ya taifa letu.

Tatizo lipo pia hapo kwenye red print, Viongozi makini, jasiri na wazalendo wanatakiwa ili taifa letu liendelee mbele. Kama CCJ au chama kikingi chochote hakitakuwa na Viongozi makini, Jasiri na Wazalendo nafikiri mvinyo utakuwa ni uleule but in a very new bottle
 
Firstcollina,
Mvinyo utakuwa ni uleule but in a very new bottle - Nimeipenda sana!
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu nilijiunga na Chadema kwa sababu walikuwa mrengo wa kati kulia... Leo nawasikia nyie CCJ imekuja na mrengo wa Kulia...Mmmhhhhh! lakini maadam Chadema believe we need to REFORM the Government. I guess I will support them, will remain a Conservative til then!

Nakuomba pitia kwa makini kitu hiki HAPA
Kila la kheri mkuu..... tulikuwepo!

true.. Chadema wako kati-kulia.. Tanzania naamini kabisa inahitaji a far right ideology kwa muda fulani. Centralist hawawezi kuipiku CCM, wataendelea kuwa wasindikizaji tu.
 
Mzee Mwanakijiji,
Kwanza matumizi ya hili neno KULIA ktk elimu ya itikadi tulofundishwa au kupumbazwa nayo unalitumia vibaya kwa sababu hapa sii mahala pake pamoja na kwamba mimi nakuelewa where U come from..
Maadam neno hili linatumika vinginevyo na unapolibadilisha kutokana na mazingira yetu nina hakika utawachanganya wengi. Hakuna mahala panasema ni lazima KULIA iwe pinzani na UJAMAA lakini ndivyo inavyofahamika kwa watu wote kutokana na mfumo mzima wa Demokrasia. Na hakuna mtu who cares na hizi habari za KULIA au KUSHOTO - hakuna mkuu wangu, watu hapa hawana dini (siii kulia wala kushoto)kutokana na Njaa kali.

Pili, Katika kampeni zenu mnapotumia neno UJAMAA mnapoteza nguvu na maana halisi ya UJAMAA, kwa sababu watu wengi wanajua kwamba UJAMAA ni Ukomunist na usoshalist, pale serikali ku control watu na Uchumi, njaa zaidi na machungu yote waliyoyapata wakati wa mwalimu yatarudi vile vile kama ilivyokuwa mwaka 1982 hata kama lengo la itikadi yenu ni kulinda Uhuru na maslahi ya Taifa kwanza.

Hivyo unaposema UJAMAA watu wengi watakukimbieni pasipo kufikiria mara mbili. Ni muhimu kutafuta neno jingine ambalo kwao haliambatanishi UJAMAA na UKOMUNIST, hii ni nchi ya wajinga na wengi wataamini mnataka kurudisha hali ile ya Kutaifishaji, vijiji vya Ujamaa, foleni ya vyakula na kadhalika...It reminds them of hardship!

Na kuhusu Chadema mkuu umeshindwa kuelewa kwamba Unahitaji mageuzi ya serikali kuu kwanza na sio mageuzi ndani ya chama..Kwa wajinga wengi watasema mnabadilsiha chupa lakini mvinyo ni ule ule..besides njia hii huchukua nguvu na muda mrefu kusimama..Again nitakukumbusha tu kwamba CCJ imekataliwa au kucheleweshwa kusajiliwa na yaonyesha hakuna plan B, siku zinayoyoma na hadi sasa CCM mshindi kwa sababu hii ni nchi ya WAJINGA hamuwezi kupata support ya wengi inabidi mfikirie kama wanavyofikiria wao. By the way wanasema wao ni lengo wa kati (wasiofungamana na upande wowote) na mimi ni mfuasi wa KULIA lakini nakubaliana na mageuzi yao kutokana na Watu/Mazingira tuliyopo.

Hapo ndipo CCM huwapiga bao Wapinzani wote kwa sababu huzungumzia vitu vinavyoonekana kwao..Elimu, Afya, Barabara, maji, Mawasiliano, ajira na kadhalika hata kama hawawezi kuvileta kuliko kutumia hizi lugha za itikadi, sera na Ilani. Watu hawajali sana kusoma maelezo mareefu yasiyokuwa na tija kwao.

Mkuu sijui ulikuwa Bongo mara ya mwisho lini lakini Ukimuuliza Mdanganyika yeyote nini maana ya Itikadi basi katika kila 1000 utapata mmoja!..lakini muulize kama anataka CCM iondoke kwa sababu imeshindwa ku deliver maendeleo kwa wananchi, utapata kura za watu 999 na mmoja atakayekataa ni kiongozi wa chama. Hivyo babuu ni muhimu sana kujua Wadanganyika wanafikiri nini - Mwenye NJAA mwambie atakula wapi na sii siasa za Utampa kazi aje kesho..Kamba hizi wanazijua vizuri na hata wao huzitumia ktk maisha yao ya kila siku.
 
true.. Chadema wako kati-kulia.. Tanzania naamini kabisa inahitaji a far right ideology kwa muda fulani. Centralist hawawezi kuipiku CCM, wataendelea kuwa wasindikizaji tu.

And what is far right in Tanzania aspects? What are the interests and philosophical stands of Tanzanian's Far right like the visioned CCJ? So who is the enemy to blame for all ''our miseries''? Muhindi? Muarabu? Mswahili?Mkaburu?Mchaga?Muangaza?Mpemba?Muislamu?Mkristo wa mrengo wa kati?M-CCM?Mwanamtandao? ......

Tuamsheni tuliolala

Omarilyas
 
saad!... maadui tuliwaanisha mapema; Ujinga, Maradhi, Umaskini na sasa tunaye Ufisadi..!!! Ukishaanza kufikiria maadui kwa misingi ya "watu" kama unavyoonesha basi ni vigumu sana kuelewa falsafa hii. Kwa sababu utakuwa unajaribu kupambana na watu.
 
Mkuu katika yote haya (Ujinga,Maradhi,Umaskini na UFISADI) hakuna hata moja CCM haija yaainisha. Na kwa uhakika zaidi JK anapewa sifa na vyombo vya madola kwa kuweka mkakati kupambana na Ufisadi. Yote yapo vitabuni na sheria zimetungwa. Mambo ndio mabaya zaidi!
Kwa hiyo, bado tatizo letu sii Itikadi ila ni WATU wanaoshindwa kutekelezwa majukumu waliyopewa ktk kupambana na maadui hao..Hizi hadithi za Umaskini,Ujinga,maradhi tumezisikia toka tupate Uhuru...tumefika wapi ? -The fact remain we dealing with UONGOZI MBAYA..
 
Ndio maana nawachukia sana wanasiasa. Hata hao wanaojiita wa UPINZANI, wote ni wanafiki!

Kipimo cha ukomavu wa kisiasa ni, kuwaambia wananchi wapange wao kipaumbele cha mikakati ya maendeleo, kisha wabunge watekeleze kama wananchi wanavyotaka, si wabunge kupanga wao kisha kusema kwamba wao ndio pekee wenye uwezo wa kupeleka maendeleo kwa wananchi. Huo ni unafiki! Pia, kama kweli chama kinajiamini na sera zake, hakitakuwa na shida ya fedha, kwani wanachama wake watatosha kukichangia kiendelee kuwa hai. Hili la kudai ruzuku ni unafiki. Huwezi kupeleka bakuli kwenye serikali unayopingana nayo, kisha ukaendelea kudai kwamba wewe ni mpinzani. Hilo haliwezekani.

Kati ya vyama vyote vya upinzani, kuna hata kimoja chenye ubavu wa kujiendesha bila ruzuku?

Hii hata siweki signature!
 
Mkuu katika yote haya (Ujinga,Maradhi,Umaskini na UFISADI) hakuna hata moja CCM haija yaainisha. Na kwa uhakika zaidi JK anapewa sifa na vyombo vya madola kwa kuweka mkakati kupambana na Ufisadi. Yote yapo vitabuni na sheria zimetungwa. Mambo ndio mabaya zaidi!
Kwa hiyo, bado tatizo letu sii Itikadi ila ni WATU wanaoshindwa kutekelezwa majukumu waliyopewa ktk kupambana na maadui hao..Hizi hadithi za Umaskini,Ujinga,maradhi tumezisikia toka tupate Uhuru...tumefika wapi ? -The fact remain we dealing with UONGOZI MBAYA..

of course.. nimerudia hilo la uongozi muda mrefu sana; lakini uongozi mzuri utashughulikia mambo gani? Manake huweki mzuri ili uusifie tu kuwa "tuna uongozi mzuri".
 
mzee mm i wish you all the best. Katika CCJ lipi mnaliona ni tatizo kubwa kati ya ujinga, maradhi, umaskini na ufisadi? Nimekuwa nikichukulia ujinga kama ni kubwa by far. What do you or CCJ perceive? How do you plan to tackle the problem and what are the expected levels of achievement?

cheers
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu nilijiunga na Chadema kwa sababu walikuwa mrengo wa kati kulia... Leo nawasikia nyie CCJ imekuja na mrengo wa Kulia...Mmmhhhhh! lakini maadam Chadema believe we need to REFORM the Government. I guess I will support them, will remain a Conservative til then!

Nakuomba pitia kwa makini kitu hiki HAPA
Kila la kheri mkuu..... tulikuwepo!

Mkandara
MBona unaonekana kama umekata tamaa, huyu mwanakijiji siku zote ni mwanachama wa ccm na ndiyo anataka kuhama sasa pamoja na wapiganaj baada ya kupigwa bao na mtandao. Fuatilia ile topic ya mbowe kusaini cheque ndiyo utamjua.
 
wengine wanasema niko Chadema
Wengine wanasema niko CCM
mwenyewe nimesema niko wapi na kwanini; hawataki!
 
Mzee Mwanakijiji,
Kina nani wanasema uko CCM au Chadema? madai yako hawa wote hawana Itikadi safi iweje wewe uwe vyama hivyo..na hata kama Ulikuwa CCM nadhani ilitokea kimakosa tu.....
 
Mzee Mwanakijiji,
Kina nani wanasema uko CCM au Chadema? madai yako hawa wote hawana Itikadi safi iweje wewe uwe vyama hivyo..na hata kama Ulikuwa CCM nadhani ilitokea kimakosa tu.....

Mimi nataka kujua M mwanakijiji, kabla alikuwa chama gani? Pia nasikia CCJ inatarajia kupokea wanachama wengi toka CCM, kama ni kweli, tutarajie uozo maaana hakuna kitakatifu kinachoweza kutoka CCM, wametufanyia ufisadi muda mrefu hivyo leo ndo washtuke wakati wenzao upinzani walishapigana vita vya kutosha. Na hao hao wana CCM walikuwa wanawakejeli kuwa wanawivu wa kushindwa.
 
Siku zote amekuwa ni mwanachama wa CCM(muulize pasco) labda sasa ndiyo anataka kuhama na wale wanajiita ni wapiganaji huku wananuka na wameukumbatia ufisadi miaka yote hii. Moja ya sifa ya chadema ni kule kuweza kuona mamluki. nilikuwa najiuliza kwa nini chadema wanamuacha huyu mpiganaji si wangempa hata kazi mojawapo? du jamaa ni smart
 
hiyo kadi ya CCM ulinipa wewe? yaani my validation ilitakiwa itoke Chadema? Nadhani unawapa clout ambayo bado hawaistahili.
 
Back
Top Bottom