CCJ kuanza Charm offensive! - Ask your questions!

CCJ kuanza Charm offensive! - Ask your questions!

labda tuna uwezo mdogo wa kukuelewa mkuu maana mawazo yako yamepita uwezo wetu wa kufahamu au kukuelewa; ila usikate tamaa kujaribu kuendelea kutufahamisha.
Ni vigumu sana kwa watu wanaoamini kwamba Unity inaweza kuwa ni Udhaifu..Kwanza ni Imani kisha unafuata kuelewa au kuelimika.
 
Ni vigumu sana kwa watu wanaoamini kwamba Unity inaweza kuwa ni Udhaifu..Kwanza ni Imani kisha unafuata kuelewa au kuelimika.

labda hapo ndipo tatizo; sidhani kama watu wanaamini unity inaweza kuwa ni udhaifu. Ila huwezi kuwa na muungano kwenye udhaifu. Kuna tofauti hapo.
 
Kwa kuongezea tu nitakupa ukweli ambao wengi hatupendi kuuweka maanani leo hii. Waislaam waliutaka Uhuru wa Tanzania mapema lakini wasingeweza kufanikiwa pasipo support ya Wakristu. Ndipo walipokuja na plan ya kuwavuta Wakristu na mwalimu akapewa Uenyekiti.

Haya ni maelezo ambayo yana walakini kidogo kwa sababu yanataka tuamini kwamba wapo watu ambao leo hawataki kuweka maanani ‘ukweli' kwamba "Waislamu ndio walioutaka Uhuru wa Tanzania mapema kabla ya Wakristu kwa hiyo ikabidi watafute support ya Wakristu ili wafanikiwe. Ndipo walipokuja na plan ya kuwavuta Wakristu na Mwalimu akapewa Uenyekiti."

Baadhi yetu humu ambao hatujui vyema yaliyotokea huko nyuma kabla ya Uhuru moja kwa moja tutaamini kwamba hivyo ndivyo ilivyokuwa - Waislamu waliwavuta Wakristu. Ingawa in the first place "ukweli' huu hauna ubaya wowote kuweza kufanya wengi wasipende kuuweka maanani leo, kwa sababu kama ndivyo ilivyokuwa basi ilikuwa ni hatua nzuri ya kutufikisha kule tulikokuwa tukitaka kwenda – kupata Uhuru.

Lakini, yapo maelezo yaliyowahi kutolewa na watafiti na kuthibitishwa na Mwalimu pamoja na viongozi wa Chama cha TANU ambayo yanadhihirisha kwamba katika kuutaka Uhuru na kufanikisha kupatikana kwake kulikuwa hakuna uhusiano wa moja kwa moja na suala la Waislamu kuwa mbele ama kuutaka mapema kuliko Wakristu. Kutokana na adha ya kutawaliwa na wakoloni, vuguvugu la kuutaka Uhuru lilikuwa limezagaa nchi nzima (kwa Waislamu, Wakristu na Wapagani) tangu mwaka 1925 vilipoanzishwa vyama mbalimbali vya kupigania haki vya wakulima na wafanyakazi nchini, pamoja na vyama vya kikabila vilivyoshughulikia zaidi shida zilizokuwa zikiwapata wanachama wa makabila hayo. Dar es Salaam kulianzishwa chama cha wafanyabiashara – African Commercial Association mwaka 1934. Ni dhahiri vilianzishwa vyama vya aina aina jinsi vuguvugu la kudai haki kutoka kwa wakoloni lilivyoendelea kukua. Hatimaye, matokeo yakawa ni kuanzishwa kwa chama kimoja cha TAA.

Wapo wasomi wazalendo waliofanya kazi ya kutafiti historia ya Chama cha TAA na TANU na kutoa kitabu mwaka 1981 Katika kitabu hicho watafiti hao wameandika hivi:

"Kwa ujumla chama hiki (TAA) kilitokana na vyama vingine vidogo vidogo vya awali kama vile vyama vya kikabila. Buhaya Union huko Bukoba kwa mfano ndicho kilichobadilishwa na kuwa African Association. Mahali pengine kama Dodoma chama hiki kilitokana na kikundi kidogo cha wafanyakazi serikalini. Huko Zanzibar kilitokana na juhudi za wasomi waliotaka kuunganisha Wakristu na Waislamu"(Labda huu ndio ‘ukweli' unaozungumziwa). "Hadi kufikia mwaka 1940 Chama hiki (TAA) kilikuwa kimeanza kushughulikia mambo muhimu ya kisiasa kama vile kutaka Waafrika wapate sauti katika serikali. Baada ya vita vya Pili vya Mabeberu madai ya Chama hiki yalilenga zaidi katika kupata wanachama wengi kutoka kila sehemu ya nchi, wanaume kwa wanawake. Katika Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika Dodoma tarehe 29 Machi, 1945 iliamuliwa kuwa juhudi zifanywe kuhakikisha kuwa katika kila mji mkuu wa jimbo kunakuwa na tawi la African Association lenye nguvu. Jukumu hili liliendelea hadi 1948 wakati Chama hiki kilipogawanyika katika matawi mawili – la Tanganyika na la Zanzibar. Tawi la Tanganyika liliitwa Tanganyika African Association (TAA) na la Zanzibar likaitwa African Association – Zanzibar…….
Baada ya vita Tanganyika iliendelea kuwekwa chini ya Baraza la Udhamini ikiangaliwa na Uingereza. Waingereza walijaribu kuleta mabadiliko kadhaa katika mambo ya uchumi na siasa ili waonekane kuwa wanaiendeleza Tanganyika. Kisiasa, kwa mfano, walijaribu kuwaingiza machifu ambao hawakuwa wawakilishi halisi wa wananchi…… Katika uchumi pia Waingereza walianzisha miradi mingi bila kufanya utafiti kamili hivyo kuwakera sana wananchi. Upinzani kama ulivyotokea huko Upare wakati wa Mbiru, au ule wa Wahehe kukataa kuogesha ng'ombe zao, au umoja wa Waluguru katika kupinga juhudi za kuhifadhi mapori na kulima matuta inadhihirisha kwamba ilipokaribia miaka ya 1950 wananchi walikuwa imara kukabiliana na wakoloni….

Chama cha TAA kilitumia mambo haya yote katika kuwaunganisha watu na kuwaelekeza pamoja katika kutafuta haki zao. Juhudi hizi ziliendelea katika kila jimbo hadi mwaka 1953 ambapo kulifanyika mkutano mjini Dar es Salaam na Mwalimu Julius K. Nyerere akachaguliwa kuwa kiongozi wa TAA. Kwa wakati huu TAA likuwa bado haijaweka madhumuni yake wazi ya kupigania uhuru hivyo Mwalimu Nyerere alipopendekeza umuhimu wa kuandaa chombo cha kupigana na mkoloni wajumbe waliafiki na kumpa kazi ya kuandaa katika ya Chama, Mkutano wa mwaka ulifanyika Dar es Salaam kuanzia tarehe 7 hadi 9 Julai, 1954 na kuhudhuriwa na wajumbe kumi na saba. Wajumbe hao ni:
1. Julius K. Nyerere – Rais wa Chama
2. Germano H. Pacha – Jimbo la Magharibi
3. Joseph Limalando – Jimbo la Kaskazini
4. Abubakari Ilanga – Jimbo la Ziwa
5. Said Kitwana – Jimbo la Ziwa
6. Japhet Kirilo – Jimbo la Kaskazini
7. C. Millinga – Jimbo la Mashariki
8. L. Makaranga – Jimbo la Ziwa
9. Saadani Kandoro – Jimbo la Ziwa
10. Kisung'uta Gabara – Jimbo la Ziwa
11. Saidi Tewa Saidi – Jimbo la Mashariki
12. Dossa Azizi – Jimbo la Mashariki
13. Ally W. Sykes – Jimbo la Mashariki
14. Patrick P. Kunambi – Jimbo la Mashariki
15. Joseph Kassela-Bantu – Jimbo la Mashariki
16. Abdul K. Sykes – Jimbo la Mashariki
17. John Rupia – Jimbo la Mashariki

Wajumbe wa Chama hiki cha TAA walikubali kukibadilisha jina lake na kuitwa Tanganyika African National Union (TANU)"
.

Katika orodha hii ya Wajumbe wa TAA walioanzisha TANU kuna majina 7 yanayoashirika kwamba ni Wakristu, 7 Waislamu na majina matatu hayashirii chochote maana mawili yana initials tu za kwanza na moja la kikablia (Kisung'uti).

Labda tumekuwa tukielewa vibaya maelezo kuhusu Mwalimu alivyokuwa akishirikiana na Wazee wa Kiislamu wa Dar es Salaam waliokuwa kwenye chama hicho akina Mzee Dossa Aziz, akina Sykes na wengine na kudhani kwamba ndio waanzilishi wa TAA Waislamu waliomvuta Mwalimu mkristu kujiunga nao.
 
Bibi Ntilie,
Sielewi lengo la swala hili kama ni kuthibitisha kwamba maneno yangu hayana ukweli au unachambua historia kwa kutafuta mikutano ya chama wa mwaka 1954 wakati Nyerere ali join chama hicho miaka miwili kabla, sasa sijui unajaribu ku prove kitu gani kwa kuorodhesha wajumbe wa mkutano huo hali wakati huo azma wa waanzilishi ipo ktk hatua ya utekelezaji wake. Je, unaweza kunambia hesabu ya wajumbe Wakristu ktk TAA before say in 40s au kufikia mwaka 1952 kabla ya mwalimu kujiunga?.

Je ulitegemea mkutano wa mwaka 1954 uwe na wajumbe Waislaam wengi kuliko Wakristu hali lengo kubwa la waasisi wa TAA mpya iliyozaa TANU kina Abdul Wahid Sykes na Hamza Mwapachu ilikuwa kuunganisha nguvu za Watanzania iweje tena hawa watu wapunguze nguvu za ushiriki wa wakristu ktk kikao kikubwa kama hicho!.

Pili, ulivyoelewa wewe walipoandika hivi:- Huko mikoani Chama TAA kilitokana na vyama vidogo vidogo ina maana kwamba hao ndio wanzilishi au waliojiunga na chama kilichokwisha anzishwa!..Leo hii CCJ imeanzishwa na kina Mwanakijiji umuhimu wa kupata wanachama na kufungua Ofisi zao mikoani wanaweza kutumia jumuiya zozote zile kwa malengo waliyokusudia wao. CCJ wanavyodai wao ni chama pekee kilichokuja na Itikadi tofauti na pinzani ya chama CCM....Could be true or not but the history will tell. Lakini nachoweza kusema ni ufanisi wa malengo yao kiitikadi ndiyo yatakayo onyesha tofauti hizo.

On the other hand, mimi najaribu kumuomba sana Mwanakijiji na wanachama wote wa Upinzani waunde UMOJA wa vyama lakini yeye na CCJ wanazo njia zao za kuunda UMOJA huo bila kuunganisha nguvu ya wanachama wa vyama vya Upinzani. Lakini let's say kama wao watakuwa wa kwanza kuwezesha umoja huu naozungumzia mimi (hypothetically).
Kujiunga kwa vyama, wanachama, vikundi vya jumuiya na kadhalika ktk umoja huu hakuwezi kubadilisha maana kwa kutazama Uuwiano wa wajumbe wa mkutano mkuu mwaka kesho..Tena ukiona uuwiano mkubwa wa wanachama wenye itikadi tofauti hii itakuwa ishara nzuri kwamba lengo la CCJ limekamilika zaidi kuliko tukiona wajumbe wa CCJ ndio wamejaa mkutano mkuu. Au nakosea bibie?
 
Mkandara kwenye suala la Mama Ntilia nadhani kauli yako hii hakutaka iiche pasipo kuiangalia kwa ukaribu kwa sababu imedai "Ukweli" kuondoa ukweli mwingine wote:

Kwa kuongezea tu nitakupa ukweli ambao wengi hatupendi kuuweka maanani leo hii. Waislaam waliutaka Uhuru wa Tanzania mapema lakini wasingeweza kufanikiwa pasipo support ya Wakristu. Ndipo walipokuja na plan ya kuwavuta Wakristu na mwalimu akapewa Uenyekiti.

Kwa mtu yeyote ambaye ameisoma kauli yako ilikuwa inataka kusema kuwa

a. Waislamu walitaka Uhuru wakristu walikuwa hawataki - ndio maana ya kutumia neno "mapema"
b. Wasingeweza kufanikiwa wenyewe - sielewi msingi wa hili ni nini, kwa sababu wangeweza kupata uhuru lakini sijui kama ungekuwa ni waislamu peke yao na wakristu wangeendelea kuw wakoloni au walitaka uhuru wa Watanzania wote kwani wote walikuwa chini ya mkoloni?
c. Walihitaji support (kuungwa mkono) na Wakristu - kana kwamba Wakristu wao hawakuwa na maslahi katika uhuru huo.
d. Waislamu walilpoona (a-c)wakabuni mpango wa kuwavuta Wakristu - kwa maneno mengine kabla yake wakristu hawakuwa katika mpango huo na wao walikaribishwa kutoa support
e. Mwalimu alipewa Uenyekiti kwa sababu ya Ukristu wake (ukizingatia d). Yaani, walimpa hivyo bila kujali uwezo wa kuongoza, uwezo wa kushawishi au yeye mwenyewe kutaka uhuru wa Tanganyika vile vile. Kama Mkristu inaonekana Nyerere hakutaka Uhuru wa TAnganyika hadi alipokutana na Waislamu wa Dar ambao kama wengine huko nyuma wamewahi kudai (kimzaha au ukweli) alifundishwa kuvaa kaptula - kana kwamba alipokuwa anaishi Butiama alikuwa anavaa manyasi.

Ni kutokana na hilo ndio mama Ntilie amekuja na jibu lake hilo. Hii haiondoi hata kidogo mchango wa Watanganyika wa awali katika kupigania uhuru bila ya kujali dini zao, au hadhi zao kwani hoja yako ikikubaliwa kama ulivyoiweka awali inaashiria (na mara nyingine imesikika hivyo inapotolewa na watu wengi) kuwa waislamu ndio wana haki zaidi na Tanganyika kwa sababu "walitaka uhuru wa tanganyika mapema").


Kwenye suala la umoja, huu umoja unaoupendekza msingi wake uwe ni nini? NI vitu gani ambavyo tunaweza kusema 1, 2, 3, 4, 5 na 6 tunakubaliana na hivyo tuunde umoja. Sidhani kama unataka watu waungane tu kwenye jina au chama kimoja for the sake of being able to say "we are united". Ni lazima kuwe na mambo fulani ya kuunganisha. Zaidi ya kuondoa CCM madarakani ni vitu gani vinapaswa viwe msingi wa muungano wa upinzani Tanzania?
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu wangu maneno yako ni pamoja ya kudhihirisha kwamba Ukweli huo hupendi kuiwekea maanani kama nilivyotanguliza usemi wangu.. Ni kitu gani kinachokufanya ufikirie kwamba Wakristu walikuwa hawataki Uhuru?.. Mkuu wangu naanza kufikiria kwamba wewe unavuta fikra za Udini mbele ya ukweli.

Mkuu wangu leo hii sisi wote tunataka kuondokana na Utawala wa CCM lakini juhudi hizo zitahesabika tu ikiwa kuna kundi la watu wataanza harakati hizo. Mapema inasimama kama watu waliojipanga kwanza kuutafuta Uhuru wa nchi yetu na bahati mbaya au nzuri walikuwa Waislaam. Lakini haya sio Mashindano ya kidini kwani yapo makabila yaliyo resist against ukoloni na naweza kusema kabila fulani lilikuwa la kwanza haina maana makabila mengine hawakutaka.

Kipengele cha B hadi mwisho ni uzushi wako mwenyewe... Ni fikra zako duni tu (Inferiority complex) mkuu wangu ktk udini kwa sababu hapa tunazungumzia Uhuru wa nchi nzima ambapo kulitakiwa uchaguzi wa nchi nzima na kulikuwa na masharti yake kama haya ya leo mnayojiandikisha ambayo ushindi usingewezekana kwa TAA pasipo kuwaunganisha nguvu za Wakristu hasa kutoka bara ili kupata kura za wananchi za kutosha.
Tatizo la kwanza sio Wakristu ila ni chama chenyewe kuwa na Waislaam wengi. Ni matatizo kama ya CUF au Chadema uchaguzi uliopita ambao walishindwa kupata ushindi kitaifa kutokana na shuku za Udini au Ukabila tena basi hawa tuhuma hizi sio za kweli lakini zimeweza kufanya kazi kuwapotezea kura nyingi sana. TAA ya miaka ya nyuma kabla ya kuunganisha nguvu hizi ilikuwa dhahiri na Waislaam wengi sana na imeshamiri Pwani.

Pengine rudia kusoma ile mada tulowahi kuizungumza sana humu - WATU MUHIMU KTK HISTORIA YETU. Utagundua ukweli na kwamba mimi sina fikra za kidini ila kuutafiti ukweli wa historia ya harakati za Uhuru wetu..
 
Ni lazima kuwe na mambo fulani ya kuunganisha. Zaidi ya kuondoa CCM madarakani ni vitu gani vinapaswa viwe msingi wa muungano wa upinzani Tanzania?
Turudi kwenye mada yetu...Hakuna zaidi ya kuwaondoa CCM madarakani..Kama lengo lenu CCJ sio kuwaondoa CCM madarakani why form a party 18 years after demokrasia imetangazwa?. Again utasema pengine hiyo ITIKADI yenu, hapa mkuu nataka kujua hiyo itikadi itafanya kitu gani tofauti ikiwa CCM wataendelea kuongoza nchi?
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu wangu maneno yako ni pamoja ya kudhihirisha kwamba Ukweli huo hupendi kuiwekea maanani kama nilivyotanguliza usemi wangu.. Ni kitu gani kinachokufanya ufikirie kwamba Wakristu walikuwa hawataki Uhuru?.. Mkuu wangu naanza kufikiria kwamba wewe unavuta fikra za Udini mbele ya ukweli.

ehe..!



Kipengele cha B hadi mwisho ni uzushi wako mwenyewe... Ni fikra zako duni tu (Inferiority complex) mkuu wangu ktk udini kwa sababu hapa tunazungumzia Uhuru wa nchi nzima ambapo kulitakiwa uchaguzi wa nchi nzima na kulikuwa na masharti yake kama haya ya leo mnayojiandikisha ambayo ushindi usingewezekana kwa TAA pasipo kuwaunganisha nguvu za Wakristu hasa kutoka bara ili kupata kura za wananchi za kutosha.
ehe!


Pengine rudia kusoma ile mada tulowahi kuizungumza sana humu - WATU MUHIMU KTK HISTORIA YETU. Utagundua ukweli na kwamba mimi sina fikra za kidini ila kuutafiti ukweli wa historia ya harakati za Uhuru wetu..
This is very interesting; wewe ukizungumzia mambo ya dini (kwa jina la ukweli excluding all others) ni kuwa uko objective. Mimi nikigusa mada hiyo hiyo na kudai ukweli ninakuwa mdini! Unataka tuamini kuwa wewe katika kuzungumzia kile unachokiita "ukweli" basi ur the only undisputed authority katika mambo haya ya "historia" na mtu mwingine akijaribu kuyapinga basi ni "mdini".

Labda yawezekana unauona kwa urahisi udini wa wengine kwa sababu wewe mwenyewe unaongozwa na udini huo huo unaowatuhumu wengine. Ni lazima tujifunze kuangalia mambo na kujadiliana bila kushutumiana na kuhisiana nani anahisia gani. Kwa sababu kama vile unavyoweza kuuona "udini" wangu kwa vile nimeenda kinyume na "ukweli" wako vivyo hivyo nami (au mtu mwingine) anaweza kabisa kuona "udini" wako kwa vile ummenda kinyume na "ukweli" wangu au wake.

Kuwaita watu wadini kwa vile hawakubaliani nawe hakufanyi hoja yako kuwa na nguvu ni kuwashambulia watu tu (ad hominem) zisizo za lazima. Vinginevyo mkiingiza mambo yanayohusu dini sisi wengine mtatutaka tukae mbali tusitoe mawazo yetu kwa sababu tukitoa na yasipokubaliana na yenu mtatuita wadini.

Hatutafika.
 
Mzee Mwanakijiji,
Katika maelezo yangu, I can back up na fact na ndio maana nimekuomba usome mada ile ya Watu muhimu ktk Historia yetu. Sikuandika mimi habari hizi wala kutunga historia. Unaweza kwenda library, kukutana na historian kutafuta ukweli. Na kama utapata majibu tofauti njoo hapa tuzungumze na sio kuandika hisia zako kwa kufikiria Mkandara alikuwa na maana hii. Nimekwambia sikuwa na maana hata moja ya maandishi yako uloandika bado unasema oooh mimi ndiye undisputed authority... nimesema wapi hivyo. Yote uloandika hapo juu toka kifungu B hadi mwisho ni maneno yako mwenyewe ambayo wewe pekee ndio unaamini hivyo na hata umefikia kusema Bibie Ntilie alikuwa na maana hiyo. Wee nani kusoma vichwani mwa watu? Labda unataka kunambia Bibie Ntilie ni wewe mwenyewe.. Nitarudia niliyoandika mwanzoni sikuwa na maana uloandika wewe hata chembe ni unyonge wako mwenyewe wa kutojiamini.
 
Mzee Mwanakijiji,
Katika maelezo yangu, I can back up na fact na ndio maana nimekuomba usome mada ile ya Watu muhimu ktk Historia yetu. Sikuandika mimi habari hizi wala kutunga historia. Unaweza kwenda library, kukutana na historian kutafuta ukweli. Na kama utapata majibu tofauti njoo hapa tuzungumze na sio kuandika hisia zako kwa kufikiria Mkandara alikuwa na maana hii. Nimekwambia sikuwa na maana hata moja ya maandishi yako uloandika bado unasema oooh mimi ndiye undisputed authority... nimesema wapi hivyo. Yote uloandika hapo juu toka kifungu B hadi mwisho ni maneno yako mwenyewe ambayo wewe pekee ndio unaamini hivyo na hata umefikia kusema Bibie Ntilie alikuwa na maana hiyo. Wee nani kusoma vichwani mwa watu? Labda unataka kunambia Bibie Ntilie ni wewe mwenyewe.. Nitarudia niliyoandika mwanzoni sikuwa na maana uloandika wewe hata chembe ni unyonge wako mwenyewe wa kutojiamini.

Yaani ile mada ni authority yako? Nipe kitabu cha watu independent ambao naweza kukipata library ambacho kitaniambia madai uliyoyasema kuwa Waislamu ndio walitaka uhuru "mapema" na kuwa walifanya mipangu kuwahusisha Wakristu kwani bila wao wasingeweza kupata uhuru. Maneno unayoyasema yana maana na yale uliyoyasema ulikuwa na uchaguzi wa kusema kuwa siyo maana yake lakini ndicho ulichomaanisha kwa sababu hujapinga tafsiri yangu. Yawezekana mimi nimekosea tafsiri yangu lakini ni wewe tu ndiye uliyemaanisha ulichosema na kwa vile bado kinasimama madai yako jinsi nilivyooesha kuanzia a to d yanasimama kukuhumu wewe mwenyewe siyo mimi.

Au unakataa kuwa:

Waislamu hawakutaka uhuru mapema - kwamba wakristu hawakuta, wapagani au watu wengine?

kwamba Nyerere alipewa uenyekiti kwa sababu waislamu walihitaji Mkristu na siyo kiongozi mwenye uwezo na kukubalika na watu wengi zaidi (maana walikuwepo wakristu wengine vile vile ambao wangeweza kabisa kupewa nafasi hiyo)

Mimi binafsi sijawahi kubishana kwenye masuala ya watu muhimu wa taifa letu kwa sababu kwangu wote ni muhimu na wanamchango usioweza kufutwa wala kusahaulika. Ninachokataa ni kujaribu kufuta michango ya watu wengine kwa sababu hawakuwa wakristu au kukubali michango yao kwa sababu waislamu waliwakaribisha kuchangia kana kwamba watu hao hawakuwa na mawazo yao wenyewe. Huu si uduni ni kujaribu kuiweka historia sawasawa.

Hakuna mtu ambaye anaweza kuzungumzia historia ya uhuru wetu bila kuzungumzia michango ya watu wa pwani ambako serikali za kikoloni ndiko zilikuwa na makao makuu na ambapo waislamu walikuwa ni majority! Ingechekesha isingekuwa hivyo! Na vile vile hatuwezi kufanya mchango wa wale wasiokuwa wakristu kuwa ulikuwa nyuma kwa sababu hawakuwa prominent au hawakuwa mstari wa mbele. Kama vile mababu zetu katika majimaji na uasi mwingine dhidi ya wakoloni naamini kilchoongoza kukataa ukoloni na utawala wa watu wengine ni zaidi ya suala la dini tu.

Kama inakufanya ujisikie vizuri wote tukisema waislamu ndio waliotaka uhuru zaidi na mapema, ndio waliongoza mapambano ya uhuru ndio waliwakaribisha wakristu kushiriki furaha hiyo au waliamua kutoa nafasi kwa watu wengine basi tutasema. Sasa katika kufanya hivyo inawezekana hatuthibitishi uduni wangu mimi bali uduni wako wewe kwa kisingizio kuwa ndiyo "historia".

Sikutaka kuchangia mada ile kwa sababu kama kawaida watu kama wewe wasingeangalia hoja zangu wangekimbilia kwa mbinu yao ya kawaida ya "udini" ili kuzima mijadala ya kushawishiana kwani ni rahisi zaidi kumuita mtu mdini, duni, mpumbagu, mjinga au what have you kuliko kuangalia hoja zake na kuzipinga.
 
Mie sitaki kuingia sana katika hili! Ila siku moja professor mmoja jina ninalihofgdahi alipokuwa akiwakilisha paper ya juu ya hali ya kisiasa nchini tanzania ilikuwa mwaka jana. ALISEMA WAISLAM WALITAKA UHURU UCHELEWESHWE KWA KUWA WASOMI WENYE IMANI YA KIISALAM WALIKUWA NI WACHACHE BY THEN, KWA HIYO KUHARAKISHA UHURU KUNGEWAATHIRI WAO! PAPER HIYO INAPATIKANA.
 
Mkandara, kwanini vyama vilivyoop vya upinzani visiungane au kwanini vimeshindwa kuungana? na kwanini bila ya CCJ haviwezi kuungana bado?

Naomba niulize swali dogo(japo litaonekana la ajabu).....Vipi Katiba yetu inaruhusu vyama kuungana na kuwa kama ile ya NARC ya Kenya(National Rainbow Coalition) kisha vikasimamisha mgombea kama ilivyo kuwa kwa Kibaki?..............Ama vyapaswa kuungana na kuunda chama kimoja chenye nguvu na kukisajili upya??????........Naomba kueleweshwa hapa wakuu
 
Mzee Mwanakijiji, yote uloandika hapo juu toka kifungu B hadi mwisho ni maneno yako mwenyewe ambayo wewe pekee ndio unaamini hivyo na hata umefikia kusema Bibie Ntilie alikuwa na maana hiyo. Wee nani kusoma vichwani mwa watu? Labda unataka kunambia Bibie Ntilie ni wewe mwenyewe.. ni unyonge wako mwenyewe wa kutojiamini.
Mkandara, nafuatilia majadiliano haya kwa makini sana, ila pia huyu Bibi Ntilie anazama deep in very interesting way haswa anapokuja kuwa backed.

Kufuatia interest zangu kwake, (Bibi Ntilie), nikamsoma kidogo baadhi ya post zake za nyuma nikazikuta very interesting. Nothing is imposible under the sun!.

Huu ubishi na upinzani wa kukataa general premise ya 'Umoja ni Nguvu na Utengano ni Udhaifu", unanipa posibility ya baadhi ya wapinzani hawana lengo la dhati la ukombozi, bali ama wako 'kazini' kutimiza wajibu wao, ama wanapigania nafsi zao katika mwelekeo wa kutapata kujizuia wasizame, hivyo wako tayari hata kukumbatia chelewa (CCJ) na kuyaepuka mabua (Chadema, CUF, etc ) ambayo tayari yanaelea (Vimeshasajiliwa).

Ukitapatapa kwenye maji na kujifariji kwa kukumbatia chelewa, ni hakika utazama!.

Tuendelee na mjadala.
 
Katika Tanzania ya sasa sidhani kama ni busara kuanza kuizungumzia historia ya nchi hii katika misingi ya ukabila na udini kwa sababu hakuna faida yoyote itakayopatikana kutokana na mijadala ya namna hiyo. Hapa naomba kieleweke kitu kimoja ni kwamba mnamo karne ya 19 matabaka ya watu mbalimbali hapa tanzania walikuwa tayari wameshajiingiza katika harakati za kudai uhuru wetu kutoka kwa wakoloni. Na katika kipindi hicho na kuendelea vuguvugu lilitandaa taratibu karibu Tanzania yote (Tanganyika na Zanzibar). Kwa hali hiyo basi hili vuguvugu halikuhusisha kwa namna yoyote ile ukombozi wa nchi hii kwa njia ya dini ama kabila. Hapa ningependa ieleweke kwamba kwa jamii ya watu wa pwani ambayo zaidi ya asilimia 90 ni waislamu wakijiunga na kutaka kudai uhuru wao si sahihi kusema kwamba waislamu walidai uhuru na vile vile jamii ya watu wa bara ambao zaidi ya asilimia 90 ni wakristu na wapagani wakijikusanya na kudai uhuru haina maana kwamba uhuru ule ulidaiwa na wakristu ama wapagani.
Pia ikumbukwe kwamba katika kuunganisha nguvu katika mapambano ya aina yoyote lazima kuwepo na "initiator" na muanzilishi huyo akitoka upande wa tabaka lolote baina ya yale ambayo yalitakiwa kuungana haimaanishi kwamba wao ndo walikuwa mbele katika harakati za kudai lile jambo. Ili watu wauungane lazima kuwe na lengo la pamoja na kwa namna yoyote ile ilikuwa ni lazima kwa watanganyika kuungana ili wadai uhuru. Haikuweza kuwa sahihi kwa chama cha TAA cha wakati huo ambacho kilikuwa na nguvu zaidi huko pwani kudai uhuru wa Tanganyika wakati kulikuwa na watanganyika wengine wengi ambao walikuwa wakidai uhuru kwa kipindi kile lakini si wanachama wa TAA. Hapo basi ndo dhana nzima ya kuungana kuongeza nguvu ikaja na kuunda chama ambacho kina sura ya kutaka kuikomboa Tanganyika na Zanzibar.
Pia ifahamike kuwa katika historia ya afrika mashariki kama si afrika yote miji ya pwani ambayo watu wake wengi ni waislamu ndio iliyokuwa miji ya kwanza kuendelea. Kwa haraka haraka utafahamu kwamba maendeleo ya aina yoyote yale yalikuwa lazima yotokee pwani kuelekea bara. Kwa hiyo basi hata vuguvugu la kujiunga kudai uhuru wa Tanganyika kwa namna yoyote ilikuwa lazima lianzie pwani kuja bara ila hapa haimaanishi kwamba watu wa bara ambao wengi ni wakristo hawakuwa na vuguvugu la kudai uhuru.
Mimi ni muislam na sipendezwi namna maada hii inavyowekwa either kwa makusudi ama kwa bahati mbaya ila ukweli ni kwamba hakukuwa na ushahidi ni nani hasa walianza vuguvugu la kudai uhuru wa nchi hii baina ya waislam na wakristo, na hata kama kukiwa na hiyo kumbukumbu haitasaidia kitu katika mapambano haya ya kutaka kuikomboa tena nchi yetu kutoka kwa wakoloni weusi.
Turudi kwenye maada yetu ya msingi, Mwanakijiji kwa namna yoyote ile bila kubisha wala kukataa imejidhihirisha zaidi katika maada zako za hivi karibuni kwamba wewe ni mfuasi kama sio mwanachama wa CCJ. Sijajua haswa ni kipi kilichokosekana katika vyama vingine ambavyo vipo CCJ ambavyo vinatufanya sisi wenye mitazamo ya kati tuamini kwamba chama hiki si miongoni mwa vile vingi vilivyopo ambavyo tija yake kwa mtanzania ni ndogo zaidi ya ulafi na uroho wa madaraka wa viongozi wake?? Pili, tukiwa tunafahamu kwamba utitiri wa vyama vya siasa si njia sahihi ya kujikomboa na kupata kile tunachokihitaji zaidi ya kuwasumbua na kuwachanganya wananchi wa kawaida ni kipi hasa kilichowafanya muanzishe chama kipya badala ya kukusanya nguvu zenu katika vyama vilivyokuwa tayari vipi?? Je hii inamaana miongoni mwa utitiri wa vyama vilivyopo hakuna waliokuwa na nia ya dhati kabisa kuleta maendeleo ya kweli isipokuwa CCJ?? Ni kwa kiasi gani mnaweza kutuhakikishia kwamba CCJ si CCM B kwa maana kwamba inajengwa na watu walewale waliokaa CCM kwa miaka mingi sasa wameamua kutoka na kujidai wapinzani. hofu yangu hapa ni kwamba isije ikawa nusu ya mafisadi wa CCM wamehamia CCJ, maana kwa mtazamo wangu binafsi sijamuona wa kumuita msafi ndani ya CCM na kama wapo unaweza kunitajia japo majina mawili? mtajikwamua ki vipi na hilo. Naomba ufafanuzi....
 
Mkandara, nafuatilia majadiliano haya kwa makini sana, ila pia huyu Bibi Ntilie anazama deep in very interesting way haswa anapokuja kuwa backed.

Kufuatia interest zangu kwake, (Bibi Ntilie), nikamsoma kidogo baadhi ya post zake za nyuma nikazikuta very interesting. Nothing is imposible under the sun!.

Huu ubishi na upinzani wa kukataa general premise ya 'Umoja ni Nguvu na Utengano ni Udhaifu", unanipa posibility ya baadhi ya wapinzani hawana lengo la dhati la ukombozi, bali ama wako 'kazini' kutimiza wajibu wao, ama wanapigania nafsi zao katika mwelekeo wa kutapata kujizuia wasizame, hivyo wako tayari hata kukumbatia chelewa (CCJ) na kuyaepuka mabua (Chadema, CUF, etc ) ambayo tayari yanaelea (Vimeshasajiliwa).

Ukitapatapa kwenye maji na kujifariji kwa kukumbatia chelewa, ni hakika utazama!.

Tuendelee na mjadala.

Pasco...........

Katiba inasemaje juu ya chama kujiunga na kusimamisha mgombea mmoja.....Je wanaweza kuungana na kufanya 'rainbow' coalition kama ilivyokuwa Kenya(inaruhusiwa?,ama wakiungana inabidi waisajili upya hiyo coalition yao.......Ikoje hii?

Ama wanaweza kuwa na muungano usio rasmi...kwamba wote wanaamua let say kuiunga mkono CHADEMA katika uchaguzi(sijui kama litawezekana hili,kwa Tanzania)
 
Itikadi ni ya mlengo wa kulia, nitafafanua zaidi wiki ijayo: Kwa ufupi:

- Limited but responsible government
- Minimal gvt spending
- promotion of free enterprise
- Self - Reliance
- African Socialism as corrected by the new understanding in economics, social justice
- Rule of law
- Restoration and promotion of founding principles of our nation(among them equality of status, accessibility to wealth and of opportunity, african unity - we are not afraid of Kenyas or Ugandans!, etc)
- Defense of the traditional family
- Absolutely and categorical opposition of all forms of exploitation of man by man!
- Fighting for the rights of workers and peasants of our country to give them opportunity to prosper in the globalized economy.
.. na mengine mengi..

kama uko 99% in tandem na hayo hapo juu consider urself an ideological member!

Kwa huu mchanyato wa ki-ideolojia hapo juu ninacoclude kuwa CCJ is just another mediocry, bigoted, populist, oppurtunistic gang to ensure UFISADI ENDELEVU....

Omarilyas
 
I am also here guys following the discussion which is getting hot as time goes on. I salute all commentators for their valuable contributions in the topic of "CCJ kuanza Charm offensive! - Ask your questions! ".

From my own perspective, It is now clear that comments of many people reflects their tribes, religion, political ideology, exposure and educational background. It is thus difficult to doge to reveal who you are and what kind of belief you have when giving out opinions. Nevertheless, it is not bad or sinful to reveal what you believe, but you have to be careful with opinions given in religious perspectives, they always cause problem. Opinions given in a religious context need to be presented in a neutral manner because there are very few people who are willing to surrender their beliefs because that may appear as a defeate of your faith. Tugs of war in religions is there to stay and God Himself will come to resolve them but Mkandara nad Mwanakiji will never because of three reasons
1. There are different reference books to explain belief in God
2. Different way of understanding or interpretation of verses from the reference books
3. Human different interests


Mkandara is advocating that
  1. CCM has lost vision and capability to continue ruling Tanzania and that it is high time now it has to be substituted with another capable political party
  2. The only effective strategy to remove CCM from power is through ballot box
  3. Political parties need to be united so as to consolidate their political fans into one big movement so as to vote out CCM in the coming election
  4. CCJ alone cannot pose big threat to CCM unless it is unites with theother 18 opposition parties
Mwanakijiji believes that
  1. CCM is no longer a party which stands for the poor people, the peasants and civil workers of the nation therefore it has to be replaced now
  2. The 18 opposition parties with permanent registration have failed to deliver and therefore cannot bring the hopes required by Tanzanians
  3. CCJ can bring the hope because it has the policies which reflect Nyerere's policies which stood for the poor workers and peasants of this country
  4. CCJ cannot unite with the current 18 opposition parties to form a STRONG union of oppositio parties because of the differences in their VISIONs, POLICIES and whose would like not to relinquish them
  5. Therefore, CCJ has intended to do it alone and believe that they can win the coming election provided they are permanently registered by Mr Tandwa. They believe that they have the right policies, vision which can attract many supporters to vote fot them
Nobody knows what actually will ensue in October, but one of the above two guys will fulfill the reality. Right now we can keep on speculating through powers of our beliefs, imagination and theories. So keep on the discussion and I am enjoying it. However, I want to see CCJ given its permanent registration because there is no limit of number of political parties required by the law. On the other hand I want the opposition parties to unite if they can agree on the right and workable policy to facilitate for a stronger union.
 
Huu ubishi na upinzani wa kukataa general premise ya 'Umoja ni Nguvu na Utengano ni Udhaifu", unanipa posibility ya baadhi ya wapinzani hawana lengo la dhati la ukombozi, bali ama wako 'kazini' kutimiza wajibu wao, ama wanapigania nafsi zao katika mwelekeo wa kutapata kujizuia wasizame, hivyo wako tayari hata kukumbatia chelewa (CCJ) na kuyaepuka mabua (Chadema, CUF, etc ) ambayo tayari yanaelea (Vimeshasajiliwa).

Ukitapatapa kwenye maji na kujifariji kwa kukumbatia chelewa, ni hakika utazama!.

Tuendelee na mjadala.

Ideally kila mmoja wetu angependa kuwe na chama kimoja cha upinzani chenye nguvu ili kuleta upinzani wenye nguvu dhidi ya CCM, lakini implementation ya jambo hilo sio rahisi kama mnavyotaka kuaminisha, bado tuna tatizo la "viongozi asili kuwa na hurka ya kutopenda kufunikwa na wageni na kupoteza ushawishi wao ndani ya vyama vyao", bado tunashuhudia viongozi wa vyama wakifukuzana, na bado tunashuhudia ufinywaji wa democrasia ndani ya vyama, na sio busara kuyafumbia macho matatizo haya.

Kwa Tanzania bara, hakuna chama cha upinzani kinachoweza kusema "hawa ni watu wangu" bado tuna "Yanga-CCM" lakini bado "Simba" haijajitokeza na kujenga upinzani wa dhati japo kuna watanzania wa sehemu mbalimbali, wa kada mbalimbali wanaounga mkono vyama vya upinzani, na wapo wengine ambao wamekatishwa tama na CCM lakin bado hawajashawishika kuviunga mkono vyama vilivyopo;

Msingi wa muungano uwe ni kuwaweka watu hawa pamoja, kujenga mazingira ya watu hawa kujiunga na chama na kujisikia ni sehemu na wadau wa movement hiyo katika kuleta mabadiliko wanayoyahitaji ndani ya nchi yao, lakini hili kufanyika SIO LAZIMA kuunganisha vyama bali kujenga imani na matumaini ya watu hawa kwa chama, na kwa viongozi wa chama chao.

Wakati mwingine gharama za kuunganisha vyama ni kubwa sana kuliko kuanzisha harakati mpya.
 
Kwa huu mchanyato wa ki-ideolojia hapo juu ninacoclude kuwa CCJ is just another mediocry, bigoted, populist, oppurtunistic gang to ensure UFISADI ENDELEVU....

Omarilyas

Ni wazi unaweza kusema hivyo kwa sababu hauna idiolojia mbadala ambayo siyo "mediocre, bigoted, populist, opportunistic gang to ensure ufisadi endelevu". Kwa sababu hauna itikadi mbadala yenye tofauti na hiyo yenye uwezo wa kushawishi akili basi itikadi inayokuongoza ni ile ile ya twisted sense of elitism, entitlement and absurd propositions of the worst kind!
 

Msingi wa muungano uwe ni kuwaweka watu hawa pamoja, kujenga mazingira ya watu hawa kujiunga na chama na kujisikia ni sehemu na wadau wa movement hiyo katika kuleta mabadiliko wanayoyahitaji ndani ya nchi yao, lakini hili kufanyika SIO LAZIMA kuunganisha vyama bali kujenga imani na matumaini ya watu hawa kwa chama, na kwa viongozi wa chama chao.

Wakati mwingine gharama za kuunganisha vyama ni kubwa sana kuliko kuanzisha harakati mpya.


haya yote hayawezi kuwa msingi; ni matokeo tu ya huo muungano au ushirikiano. Msingi ni lazima uwe katika mambo ambayo mnataka kufanya na matokeo yake, madaraka, itikadi na mahusiano ya kiungozi vile vile. Mnapoungana mnataka kutekeleza sera gani, za nani, kwa vipi na kwanini sera hizo?
 
Back
Top Bottom