Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,240
- 44,487
- Thread starter
-
- #261
Nobody knows what actually will ensue in October, but one of the above two guys will fulfill the reality. Right now we can keep on speculating through powers of our beliefs, imagination and theories. So keep on the discussion and I am enjoying it. However, I want to see CCJ given its permanent registration because there is no limit of number of political parties required by the law. On the other hand I want the opposition parties to unite if they can agree on the right and workable policy to facilitate for a stronger union.
Pasco...........
Katiba inasemaje juu ya chama kujiunga na kusimamisha mgombea mmoja.....Je wanaweza kuungana na kufanya 'rainbow' coalition kama ilivyokuwa Kenya(inaruhusiwa?,ama wakiungana inabidi waisajili upya hiyo coalition yao.......Ikoje hii?
Ama wanaweza kuwa na muungano usio rasmi...kwamba wote wanaamua let say kuiunga mkono CHADEMA katika uchaguzi(sijui kama litawezekana hili,kwa Tanzania)
.Pasco,
Mkuu nakumbuka huko nyuma ulitoa shukran kwa kukupa taarifa ya mpango wa waislaam kumvuta mwalimu ili kutuwezesha kupata Uhuru..Kisha akafuatia Bibi Ntilie na hoja yenye nukuu za mkutano wa 1954, nilimwelewa vizuri na nikamjibu vizuri sana kiasi kwamba hakurudi kuuliza zaidi aidha alielewa au bado alikuwa akitafuta hoja zaidi. Hoja ya Ntilie ilihusu zaidi uuwiano wa waislaam na Wakristu ktk mkutano wa mwaka 1954 na kuuliza mbona walikuwa wajumbe sawa pande zote mbili? na nikamjibu kwamba mwaka 1954 ilikuwa ni miaka miwili baada ya Mwalimu kujiunga na TAA, hivyo ushawishi mikoani tayari ulikwisha anza na hakika watu hawajui kazi kubwa ya ushawishi aloifanya mwalimu kwa muda wa miaka miwili tu kufikia kuundwa kwa TANU ktk mkutano huo wa 1954.
Hata hivyo, harakati za Uhuru wetu na wanaTAA zilianza mapema na wapiganaji wetu walipokuwa India..Kwa bahati kubwa sana nimewahi kuzungumza na Mzee Ally Sykes kwa mapana zaidi. Nakumbuka aliniuliza kama najua kuwa Ule wimbo wa Taaanzaniiia - Tanzania, nakupenda kwa moyo woote - waliutunga wao wakiwa kambini India..Nilibakia domo wazi nikifikiria uchungu waliokuwa nao hawa watu wakiwa vitani tena nchi za wageni.
Lakini hata yeye niliweza kuchambua pumba toka ktk maelezo yake alipodai baadhi ya vitu kwa lengo la Ubinafsi zaidi... nikaweza kujumlisha mengi hata kuelewa pengine hizi ndio sababu zinazofanya historia hii isipate kuwekwa wazi kwani itakuwa na madhara yake, madhara kama haya hapa JF tunavyoyaona...
Nashindwa kumwelekeza Mwanakijiji mambo muhimu kwa sababu tayari kisha ingia uchungu wa kidini akifikira kwamba maadam Waislaam ndio walianza mapema basi ina maana Wakristu walikuwa hawautaki Uhuru. Nimemwambia sio kweli bado hataki kuelewa - Jazba!
Kuna historia mbili ambazo Tanzania hatutaki kuzizungumzia ama kuziwekea maanani (kumbukumbu) kwa sababu maalum....1. Harakati za Uhuru wa Bara na 2. Mapinduzi ya Zanzibar.
Katika historia hizi, ukweli utabakia ukweli hata kama Historia haikubaliki ktk umma wa leo. I bet U mkuu hakuna mtu humu anajua historia ya TAA iliyoanzishwa mwaka 1929 Nyerere akiwa na umri wa miaka 7 kuja hadi kufikia 1953 kwa undani zaidi.. hakuna na kama wapo ni wachache sana..Na bahati mbaya wengi wetu hatupendi kutafuta ukweli wa historia yetu.
Kama Katiba yao ndivyo ilivyo, I can say with absolute confidence; CCJ is nothing but a disappointment in the making.
mkuu.. you might be very right.. wakati mwingine ili kujua maji ya moto kiasi gani inabidi utumbukize mkono. CCJ ilivyo na itikadi yake haijatoa sababu ya kwanini inataka kuwa chama kipya! Karibu malengo, nia, madhumuni, muundo na mfano ni carbon copy ya CCM tofauti ni herufi tu "J" na "M".. wao wameelezea yale yale yaliyoelezewa na CCM kwa maneno mengine!Labda ningependa kujua zaidi ni ajenda yao hasa ni nini?
Binafsi ningemshauri mtu yeyote anayetaka kujiunga na CCJ kufikiria kwanza.
Mkuu nakumbuka huko nyuma ulitoa shukran kwa kukupa taarifa ya mpango wa waislaam kumvuta mwalimu ili kutuwezesha kupata Uhuru..Kisha akafuatia Bibi Ntilie na hoja yenye nukuu za mkutano wa 1954, nilimwelewa vizuri na nikamjibu vizuri sana kiasi kwamba hakurudi kuuliza zaidi aidha alielewa au bado alikuwa akitafuta hoja zaidi. Hoja ya Ntilie ilihusu zaidi uuwiano wa waislaam na Wakristu ktk mkutano wa mwaka 1954 na kuuliza mbona walikuwa wajumbe sawa pande zote mbili? na nikamjibu kwamba mwaka 1954 ilikuwa ni miaka miwili baada ya Mwalimu kujiunga na TAA, hivyo ushawishi mikoani tayari ulikwisha anza na hakika watu hawajui kazi kubwa ya ushawishi aloifanya mwalimu kwa muda wa miaka miwili tu kufikia kuundwa kwa TANU ktk mkutano huo wa 1954.
Bibi Ntilie,
Sielewi lengo la swala hili kama ni kuthibitisha kwamba maneno yangu hayana ukweli au unachambua historia kwa kutafuta mikutano ya chama wa mwaka 1954 wakati Nyerere ali join chama hicho miaka miwili kabla, sasa sijui unajaribu ku prove kitu gani kwa kuorodhesha wajumbe wa mkutano huo hali wakati huo azma wa waanzilishi ipo ktk hatua ya utekelezaji wake. Je, unaweza kunambia hesabu ya wajumbe Wakristu ktk TAA before say in 40s au kufikia mwaka 1952 kabla ya mwalimu kujiunga?
Je ulitegemea mkutano wa mwaka 1954 uwe na wajumbe Waislaam wengi kuliko Wakristu hali lengo kubwa la waasisi wa TAA mpya iliyozaa TANU kina Abdul Wahid Sykes na Hamza Mwapachu ilikuwa kuunganisha nguvu za Watanzania iweje tena hawa watu wapunguze nguvu za ushiriki wa wakristu ktk kikao kikubwa kama hicho!
Pili, ulivyoelewa wewe walipoandika hivi:- Huko mikoani Chama TAA kilitokana na vyama vidogo vidogo ina maana kwamba hao ndio wanzilishi au waliojiunga na chama kilichokwisha anzishwa!..
Leo hii CCJ imeanzishwa na kina Mwanakijiji umuhimu wa kupata wanachama na kufungua Ofisi zao mikoani wanaweza kutumia jumuiya zozote zile kwa malengo waliyokusudia wao. CCJ wanavyodai wao ni chama pekee kilichokuja na Itikadi tofauti na pinzani ya chama CCM....Could be true or not but the history will tell. Lakini nachoweza kusema ni ufanisi wa malengo yao kiitikadi ndiyo yatakayo onyesha tofauti hizo.
On the other hand, mimi najaribu kumuomba sana Mwanakijiji na wanachama wote wa Upinzani waunde UMOJA wa vyama lakini yeye na CCJ wanazo njia zao za kuunda UMOJA huo bila kuunganisha nguvu ya wanachama wa vyama vya Upinzani. Lakini let's say kama wao watakuwa wa kwanza kuwezesha umoja huu naozungumzia mimi (hypothetically).
Kujiunga kwa vyama, wanachama, vikundi vya jumuiya na kadhalika ktk umoja huu hakuwezi kubadilisha maana kwa kutazama Uuwiano wa wajumbe wa mkutano mkuu mwaka kesho..Tena ukiona uuwiano mkubwa wa wanachama wenye itikadi tofauti hii itakuwa ishara nzuri kwamba lengo la CCJ limekamilika zaidi kuliko tukiona wajumbe wa CCJ ndio wamejaa mkutano mkuu. Au nakosea bibie?
.Mkuu Mkandara, you are too obvious kwamba una 'unafsi' dhidi ya Mwanakijiji na pia nadhani mabandiko yako dhidi ya CCJ yana "unafsi" pia ndani yake. Una tatizo gani na CCJ, if I may ask? Kama huoni sababu wala mantiki ya ujio wake then let CCJ be. Kama wewe ni CHADEMA ama TLP you had your oportunity and chances kuunganisha vyama vyote vilivyopo nchini humu. Miaka 15 na hamkuweza kufanikiwa kuifanyia nchi hii yaliyotakikana wala hamkuona kwamba kuungana ni jambo muhimu sana mpaka CCJ kilipojitokeza ndio mnauona umuhimu wake na ku-amplify! Najua wewe binafsi umekuwa ukilipigia kelele jambo hili muhimu. Lakini ni juhudi zipi ulizozionyesha wewe kama wewe nje ya JF kufanikisha au ni michango ya hoja kali ndani ya JF? Kama kweli nia yako ni kuona vyama vinaungana basi ungana na Mwanakijiji (anayefanya kweli) kujaribu upya, huenda this time CCJ wanaweza kula mfupa uliomshinda fisi. Who knows!
.
Bibi Ntilie, tusiupersonalize huu mjadada ukafikia kiwango cha kuonekana ni Mkandala vs Mwanakijiji. Hapo tunabishana kwa hoja, tena ni hoja muhimu sana kwa mustakabali wa taifa letu. Hoja ya Mwanakijiji kuwa CCJ peke yake wanaweza, na hoja ya Mkandala CCJ peke yenu hamuwezi, nami kwa upande wangu, ninasimama na hoja ya Mkandala kuwa CCJ peke yenu hamuwezi hata kwa dawa.
Hoja ya harakati za kupigania uhuru tangu TAA mpaka TANU imeibuliwa na lengo la kusisitiza umuhimu wa ushirikiano na umoja ni nguvu ikijumlisha 'managing divesity' towards the common enemy, ndipo ilipokuja hoja kwanini Julius alipewa ukuu TAA na Hatimaye TANU.
Kuna mambo mengi kwenye historia hayajaandikwa na hayajasemwa hadharani. Hakuna ubishi kuhusu uwezo wa Mwalimu kwenye tasnia ya uongozi, ila wengi wanaamini ni Mwalimu kwa utashi wake mwenyewe, sio wengi wanaojua kuwa Mwalimu alishawishiwa na kupatiwa ahadi fulani ndipo akakubali.
Sio wengi wanaofahamu kuwa Mwalimu alipotoka Pugu, alikuwa hana pa kuishi, bali alifikia moja kwa moja nyumbani kwa kina Sykes pale Ilala Boma, wakati huo John Rupia tayari akiwa ni mmiliki wa yale maghorofa yote matatu yanayozunguka Uhuru Round About. Hakuna watu wanaofahamu Mama Maria alifanya biashara ya kuuza mafuta ya Taa na alifundishwa kupika Chapati na Vitumbua na Mama Sykes for survival.
Pamoja na hitaji la kuutumia uwezo wa Mwalimu, pia umuhimu wa kuutumia Ukristo wake, Ukatoliki kwenye kuwavuta Wakristo pia ulizingatiwa (Rupia ni Anglicana). Hoja hii ndio iliyoingizwa sentments za kidini na kunyumbulishwa, kupinduliwa na kugeuzwa kuwa Wakristu hawakudai uhuru, hoja hapa sio nani alidai uhuru, hoja hapa ni need ya wapinzani kufanya kazi pamoja towards common enemy.
Mwanakijiji anaheshima yake kwa jamii kutokana na maandishi yake, ana nguvu kubwa ya ushawishi, hivyo kitendo tuu cha Mzee Mwanakijiji, kujitanabaisha hadharani kuwa ni miongoni mwa CCJ, kumeleta tumaini jipya kwa watu kama mimi kuwa kama hata Mzee Mwanakijiji anaweza kujiunga CCJ na kupigia debe, then CCJ ni substance is not nothing. Kwangu mimi hata Mpendazoe ni Nothing lakini Mzee Mwanakijiji ni something, ndio maana nikaunga mkono juhudi za Mkandala kumuelimisha Mwanakijiji umuhimu wa 'United we Stand' na akatolea mifano ya kushindwa kwa wapinzani kwenye chaguzi za huko nyuma.
Bibi Ntilie mimi nakusoma kwa great interest haswa unavyokwenda Sambamba na Mwanakijiji in Mwanakijiji Syle " Kama kweli nia yako ni kuona vyama vinaungana basi ungana na Mwanakijiji (anayefanya kweli) kujaribu upya, huenda this time CCJ wanaweza kula mfupa uliomshinda fisi. Who knows!". Ni CCJ gani hiyo inayoweza kuula mfupa uliomshinda fisi ili hali hiyo CCJ hata meno hayajaota, unless otherwize itaota meno ya chuma, hivyo na uchanga wake ndipo ifanikishe huo ufupa uliomshinda fisi, ila kumbuka fisi hawindi mwenyewe, hata simba ambaye ni mnyama mwenye nguvu, hukaa kwa makundi.
Jamani jamani, lets work together, CCJ peke yenu hamuwezi?.
Mkandara, you are too obvious kwamba una 'unafsi' dhidi ya Mwanakijiji na pia nadhani mabandiko yako dhidi ya CCJ yana "unafsi" pia ndani yake. Una tatizo gani na CCJ, if I may ask? Kama huoni sababu wala mantiki ya ujio wake then let CCJ be. Kama wewe ni CHADEMA ama TLP you had your oportunity and chances kuunganisha vyama vyote vilivyopo nchini humu. Miaka 15 na hamkuweza kufanikiwa kuifanyia nchi hii yaliyotakikana wala hamkuona kwamba kuungana ni jambo muhimu sana mpaka CCJ kilipojitokeza ndio mnauona umuhimu wake na ku-amplify! Najua wewe binafsi umekuwa ukilipigia kelele jambo hili muhimu. Lakini ni juhudi zipi ulizozionyesha wewe kama wewe nje ya JF kufanikisha au ni michango ya hoja kali ndani ya JF tu? Kama kweli nia yako ni kuona vyama vinaungana basi ungana na Mwanakijiji (anayefanya kweli) kujaribu upya, huenda this time CCJ wanaweza kula mfupa uliomshinda fisi. Who knows!
.
Bibi Ntilie, tusiupersonalize huu mjadada ukafikia kiwango cha kuonekana ni Mkandala vs Mwanakijiji. Hapo tunabishana kwa hoja, tena ni hoja muhimu sana kwa mustakabali wa taifa letu. Hoja ya Mwanakijiji kuwa CCJ peke yake wanaweza, na hoja ya Mkandala CCJ peke yenu hamuwezi, nami kwa upande wangu, ninasimama na hoja ya Mkandala kuwa CCJ peke yenu hamuwezi hata kwa dawa..
Kinachohitajika nchini dhidi ya CCM ni chama kingine chenye nguvu, chenya sera inayokubalika, maono ya kitaifa, uongozi uliokomaa, na mwelekeo usio na shaka. Chama hicho kingetumia muda kujijenga peke yake kingeweza kabisa kuiangusha CCM. Hata hivyo siyo chadema wala cuf wala tlp ambavyo vimetaka kutumia muda uliopita kujijenga kuweza kushika uongozi wa taifa. Wote wana malengo ya kuindoa CCM madarakani na hawaoni tatizo la kifalsafa la mawazo hayo.
Hebu tukubaliane kwa sekunde chache kuwa CCJ haiwezi, haipaswi kuweza na haitoweza hata "kwa dawa". Nani anaweza? Tunaambiwa kuwa muungano wa vyama vya upinzani peke yake utaweza. Hii ina sauti nzuri na inavutia hisia kwa sababu haina lengo la kusema ukweli. Tunatakiwa kupendekezewa kuwa ati vya vikiungana ndio itawezekena really?
a. Kwa miaka 15 haja ya muungano wa vyama vya upinzani imekuwepo na wengine tulikuwa nayo vile vile lakini kwa miaka 15 huu muungano haujafanikiwa. Ndugu zetu watetezi wa muungano huu wa upinzani hawawajaribu kutuambia kwa kina kwanini umeshindikana lakini sasa hivi unawezekana.
b. Tangu vyama vingi virejee nchini kumekuwepo na uchaguzi, 1995, 2000, na 2005 katika chaguzi hizo zote wimbo wa "wapinzani waungane" umerudiwa na kuwa kibwagizo cha kisiasa nchini na kama muziki usio na ala wapinzani wameshindwa kuungana. Hatuambiwi kwanini ila katika uchaguzi huu 2010 ati muungano utakuwa ni bora na unafaa na utawezekana.
c. Najua hoja nyingi zinazotolewa juu ya kushindikana kwa muungano zinakimbilia kudai ni "ubinafsi wa viongozi" kwani kila kiongozi wa upinzani "anataka kuwa yeye". Jibu laweza kuvuta hisia lakini halina msingi katika uhalasia. Na watu hawataki kukubali kuwa kuna makubwa zaidi ya ubinafsi. Watetezi hawa wa muungano wanataka tuamini kuwa sasa hivi huo "ubinafsi" mwaka huu umeisha. Kwamba mwaka huu kwa sababu watu wameamka na kujua zaidi basi muungano utafanikiwa. Tunawauliza huo ubinafsi umeisha lini?
Sasa licha ya hayo yote hapo juu watetezi wetu wa muungano "usio na msingi" wanataka upinzani uungane ili tu uing'oe CCM. Kwa haraka na kwa wengi hili ni lengo zuri, lakini ni lengo hafifu na lisilo na msingi wa kusimamia. Ati "kuindoa CCM madarakani" ndio liwe lengo la msingi vinginevyo itaendelea kutawala. Well.. kwa haraka na kwa wenye hisia hili ni jambo jema. Lakini tukiliangalia kwa ukaribu tutaona hatari yake na ni kwanini ni jambo la kuepuka.
- Huwezi kuunganisha vyama kwa lengo la kuondoa chama kingine madarakani wakati vyama hivyo vina tofauti za itikadi na sera. Vikishinda vitaongoza kwa sera za chama gani?
- Huwezi kuunganisha watu wenye malengo tofauti yanayotokana na vyama vyao huku vikiwa vimeahidiana nafasi mbalimbali halafu vikiingia madarakani baada ya kuiangusha CCM vianze kuulizana na kudaiana na baadaye kuvutana huku Watanzania wanaanza kulalamika tena kwanini "wapinzani hawapatani". Muungano wa kuindoa CCM ni muungano hatari.
- Huwezi kuunganisha vyama vyenye mitazamo tofauti na sera tofauti za kushughulikia matatizo ya nchi ukatarajia ati vikiingia madarakani vitapatana jinsi ya kufanya hivyo. Hii ni kuwa naive. Nchi huongozwa kwa sera na sera hujenga sheria na sheria hujenga maamuzi mbalimbali ya kiutendaji. Sasa mnapokuwa na vyama vyenye sera tofauti wakati mmekiondoa chama chenye sera moja hivyo vyama vitaweza vipi kutawala taifa huku kimoja bado kikiwa na malengo na sera zake?
Lakini zaidi cha kushangaza ambacho watetezi hawa wa muungano wanashindwa kutuambia ni kuwa haya "maslahi ya taifa" ya taifa yatakayotokana na kuondolewa CCM madarakani na kuingia kwa muungnao wa upinzani usiokuwa na madhumuni, sera, malengo, au njia wanazokubaliana kutawala taifa ni maslahi yapi? Haiwezekani kusema ati kuondoka CCM madarakani ndio "maslahi ya taifa". Hizo ni semantics mumbo jumbo! Maslahi ya taifa ni mambo mema ambayo yatatokea kwa CCM kutoka madarakani siyo CCM KUTOKA MADARAKANI. Naomba watetezi wa muungano mtuanishie maslahi ya taifa ambayo yatatokea kwa CCM kuondolewa madarakani na muungano ambao haujaunganisha malengo, madhumuni, itikadi, sera wala mwelekeo wa taifa:
Sasa, binafsi nilishaandika huko nyuma vile vile kuwa Chadema isiungane na chama kingine. Kanuni ile ile ndio imeniongoza wakati huu. Kinachohitajika nchini dhidi ya CCM ni chama kingine chenye nguvu, chenya sera inayokubalika, maono ya kitaifa, uongozi uliokomaa, na mwelekeo usio na shaka. Chama hicho kingetumia muda kujijenga peke yake kingeweza kabisa kuiangusha CCM. Hata hivyo siyo chadema wala cuf wala tlp ambavyo vimetaka kutumia muda uliopita kujijenga kuweza kushika uongozi wa taifa. Wote wana malengo ya kuindoa CCM madarakani na hawaoni tatizo la kifalsafa la mawazo hayo.
KUONDOLEWA CCM MADARAKANI ni lazima kuwe ni MATOKEO na siyo LENGO la chama cha upinzani. Kwamba, kutokana na kukubalika kwa sera, mipango, uongozi, siasa na mapendekezo ya kushughulikia matatizo ya wananchi na kujenga taifa basi wananchi wanaamua kuchagua chama hicho kingine na kwa kufanya kwao hivyo wanajikuta wameiondoa CCM madarakani. Hivyo, CCM itaondolewa kwa sababu wananchi wamepata kitu bora na cha kuwafaa kwa maisha yao; wamepata mbadala wa kweli wa kisiasa na kiuongozi na wakauchagua.
Naomba nieleweke vizuri. Kama CCJ itashindwa kupewa usajili wa kudumu au nafasi ya kushindwa kushiriki uchaguzi bado nitaunga mkono upinzani. Lakini sitounga mkono umoja wa upinzani usio na msingi. Nitachagua chama kingine ambacho naamini kinaweza kuja na sera, mikakati na itikadi inayolifaa taifa. SIWEZI kuunga mkono upinzani kwa minajili tu ya kuiangusha CCM; huo ni mtazamo wa hatari. Siwezi kuunga mkono upinzani ilimradi nionekane niko kinyume na CCM wakati sikubaliani na sera, mikakati au itikadi zao; siwezi kuunga mkono upinzani kwa sababu ati nachukia CCM. Muungano wa chuki hauwezi kudumu kwa sababu chuki kama chuki inatabia ya kumtafuna mwenye nayo.
Sasa, naomba nitoe changamoto kwa watetezi wa muungano wa upinzani; NAOMBA mchague mambo matano tu ya msingi ambayo yawe sababu ya vyama vya upinzani kukubaliana kuungana na mambo hayo yakigombaniwa kwa pamoja yatasababisha wananchi wauchague umoja wa upinzani na kwa kufanya hivyo watakuwa wameichagulia CCM kuondoka madarakani. Katika mambo hayo matano - KUINDOA CCM MADARAKANI kusiwe mojapo. Yaani, mambo matano ambayo wapinzani wakikubaliana kuhusu muundo wa serikali yao, kuhusu namna ya kutawala, kuhusu kugawana madaraka kati yao, kuhusu sera za elimu, afya, miundo mbinu, kilimo, sayansi na teknolojia, na kuhusu mambo ya uongozi wa juu wa taifa. Naomba mnipe mambo MATANO TU ambayo yaweza kuwa msingi wa ushirikiano au muungano wa upinzani ambayo yanaweza kusababisha CCM itolewe madarakani kwenye sanduku la kura.
Msiendelee kuniimbia wimbo kuwa hakiingii kichwani, au kichwa changu kigumu, au ni mdini au maneno mengine yoyote ya kushambulia nafsi yangu badala ya hoja. JENGENI HOJA YA MSINGI WA USHIRIKIANO WA UPINZANI AMBAYO INAWEZA KUSABABISHA CCM KUONDOLEWA MADARAKANI. Msiimbe tu "tuungane tuungane" maana kama ingekuwa rahisi hivyo na muhimu hivyo kwanini vyama vilivyopo sasa vimeshindwa kuungana hadi hivi sasa? Kwanini hata kwenye chaguzi ndogo ambapo ingekuwa rahisi zaidi kama kule Mbeya Vijiji walishindwa kuungana? Kwanini hata kama wameshindwa kuungana Tanzania nzima wameshindwa kuungana Jiji la Dar tu au Arusha au Mwanza kuiangusha CCM kwenye maeneo hayo?
Watetezi hamtaki kujua sababu?
Mkuu Mwanakijiji Kimsingi nakubaliana na Hoja zako nyingi, napingana na wewe kama msimamo wako ni kwamba Vyama viende kwenye Uchaguzi kila mtu kivyake hapana mkuu hilo litakuwa ni kosa kubwa sana, mimi naomba niwe kati kati yaani napenda kuwe na Partial Muungano hasa katika Nafasi Za Ubunge.
Mimi naungalia Uchaguzi huu kama Msingi wa Kuleta Mabadiliko makubwa katika kipindi cha 2010/2015. Na Mabadiliko hayo hayawezi kuwepo kama tutaruhusu Kamati ya CCM ( Namaanisha bunge lililosheheni CCM) itutungie sheria katika kipindi hicho. Ni Lazima tukubali kwamba tunahitaji bunge lenye nguvu ili tuweke bases kuelekea Mabadiliko ya Kimfumo tunayoyahitaji na hilo halitowezekana kwa Vyama vya Upinzani kwenda man to man katika Majimbo yote si CHADEMA si CUF si CCJ watakaoweza kupata wabunge wengi bila ya KUACHIANA MAJIMBO.
Mkuu Nataka USHIRIKIANO na SI KUUNGANISHA vyama ili tuwe na Uwakilishi wenye Nguvu
Mwanakijiji nakubaliana na wewe na baadhi ya hoja zako..
Za kutounga mkono chama chochote cha upinzani kwasababu ya kuion'goa CCM madarakani kwani naamini lengo si kuwa madarakani tu.Mrengo wa CHADEMA ni Center Right....Ni vema vigogo wote wa CCJ wakaunga mkono CHADEMA kwakuwa vinafanana sana kimtazamo na hata kiitikadi..Ni baadhi ya hoja zipi unakubaliana nazo? Binafsi kama Chadema inataka kwenda ilivyo (endapo CCJ itanyimwa) niko tayari kuinga mkono lakini siwezi kuiunga mkono kwa lengo la kuiondoa CCM madarakani kwani ni msingi mbovu wa kuchagua watu. Ni lazima uwe ni uungwaji mkono wa kukubaliana na sera na itikadi yao. Kwa sasa ni ngumu mno kufanya hivyo kwa sababu wao wana mwelekeo wa Kiliberali na mimi nina mwelekeo wa wa mrengo wa kulia.