Tahadhari kwa CHADEMA: Pamoja na kuwa hamjasuguana sana na polisi kuelekea maandamo yasiyo na kikomo kuanzia DSM tarehe 24/01/2024 lakini...........

Uzima Tele

JF-Expert Member
Jan 20, 2023
1,101
2,344
CHADEMA ina maana mmesahau ya Arusha miaka kadhaa iliyopita? Hamkumbuki kuwa mamluki wa UVCCM na baadhi ya polisi walitumiwa na CCM kwa kuwavalisha mabomu na kuyalipua mkutanoni na kujeruhi na kuua baadhi ya watu baadae kuanza kuitwa nyie ni chama cha kigaidi?

Haya. Hebu fuatilia andiko hili 👇👇👇mpaka mwisho;

1. Niko hapa Mwanza. Nimemsikiliza Naibu Katibu Mkuu CHADEMA (Tanganyika) kupitia online TVs mbalimbali Ndugu Singo Kigaila akitoa updates za maandalizi ya maandamano ya umma yasiyo na ukomo. Sasa nimeamini kuwa kumbe ni kweli yatafanyika. Niliposikia tu kuwa yatapokelewa na mwakilishi wa UN ofisi ya Tanzania nikaridhika kabisa kuwa sasa mambo yameiva.

Lengo la maandamano hayo ni;

👉Kushinikiza serikali kuiondoa toka bungeni miswaada mitatu ya sheria inayohusu mabadiliko ya sheria za uchaguzi ili ikai - draft upya kwa kuingiza maoni ya wananchi, taasisi za dini, NGOs, CBOs, vyama vya siasa na hukumu za mahakama Afrika na Afrika Mashariki kuhusu wakurugenzi wa serikali za mitaa (wilaya, miji, manispaa na majiji) kutojihusisha na usimamizi wa chaguzi zetu pamoja na kuingiza kifungu ktk sheria cha kuruhusu wagombea binafsi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi bila kulazimika kudhaminiwa na chama cha siasa..

👉 Kuishinikiza serikali kuchukua hatua za makusudi kupunguza gharama za maisha kwa wananchi kwa serikali kuondoa au kupunguza baadhi ya kodi na tozo mbalimbali, serikali kuuambia ni nini hasa tatizo la umeme wa tatizo ambapo ni kama vile nchi Haina umeme kabisa na serikali kupunguza matumizi yake ya anasa nk nk..

2. Pamoja na kuwa CHADEMA mmekubaliana na polisi lakini hampaswi kuwaamini moja kwa moja...

Wapeni imani ya mashaka (benefit of doubt) huku mkiwa na tahadhari zote. Kumbukeni maandamano haya kwa DSM ni mwanzo tu lakini yataendelea ktk miji mingine ktk mikoa mingine Tanganyika na Zanzibar. Ni wazi kuwa mpaka hapa tulipo DSM yatafanyika na itapita na serikali this time itaiona nguvu ya umma..

Lakini mnaweza kutegwa kwa jeshi hilohilo kuingiza mamluki wa chipukizi maelfu wa UVCCM tena wengine wakiwa ni polisi wenyewe ili kuleta vurugu katikati ya maandamano. Ina maana nyie hamuijui CCM?

Hamjui kuwa ma - RCs, DCs na RPCs na OCDs karibu wote ni makada kindakindaki wa CCM na wako tayari kukipigania chama chao na ulaji kwa gharama zozote zile?

Mmesahau mkutano na maandamano ya kule Arusha mwaka 2013 ambayo polisi waliovaa kiraia walikuja mkutanoni wakijifanya ni wana mkutano lakini kumbe ni wavurugaji na wauaji wakiwa wamevaa mabomu na kuyaripua katikati ya mkutano?

Kuweni makini. Kubalini watulinde lakini wakati huohuo na tumie intelejensia yenu kutafuta habari muhimu toka humo na ndani ya CCM kujua wanapanga nini. Walinde maandamano na wakati huohuo nao wakilindwa ili yake ya Arusha mwaka 2013 yasijirudie..

Wakifanikiwa kujeruhi au kuua mtu hata mmoja tu, nawaambia mapema kabisa CHADEMA kuwa watatumia kigezo hicho, kutoendelea na maandamano katika miji ya mikoa mingine nchi nzima..!

Msidhani kuwa CCM hawajui impact ya nguvu ya umma Kwa njia hii ya maandamano. Wanajua fikana watafanya kila njia kujaribu kuuzima moto huu hata ikibidi kumwaga damu zisizo na hatua..
 
Back
Top Bottom