Tetesi: CHADEMA kuitisha kikao cha kamati kuu kwa dharura kupanga mikakati ya kukabiliana na nguvu ya Makonda

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,321
9,745
Ndugu zangu Watanzania,

Nimepenyezewa taarifa kuwa CHADEMA hakukaliki wala hakuendeki wala hakupangiki mikakati ya aina yoyote ile. Hii ni baada ya ujio wa Makonda kuonekana kuwa tishio kwa uhai wa chama hicho cha upinzani ambacho kinaendelea kusambaratika na kudhoofika kila uchwao.

Inasemekana kikao cha dharura cha kamati kuu kinakwenda kuitishwa muda wowote ule kujadili namna ya kukabiliana na nguvu kubwa na ushawishi wa Makonda ulionekana kuteka mijadala ya kisiasa hapa nchini na kuonekana kuwa na nguvu ya ushawishi kwa wananchi wanaopenda siku zote mtu na kiongozi wa maamuzi magumu, ujasiri na kujiamini aina ya Paul Makonda.

Mtoa taarifa wangu amenieleza kuwa viongozi wote kwa sasa ndani ya kamati kuu ya CHADEMA hadi kanda wamevurugwa akili na kuchanganyikiwa ghafla kutokana na ujio wa Makonda unaoendelea kuzima taarifa zao na kukiweka chama cha mapinduzi midomoni mwa watanzania muda wote.

Kwa sasa CHADEMA haieleweki kama ipo stoo au kabatini au mfukoni mwa Mwenyekiti mwenyewe, haieleweki nini kinaendelea juu ya CHADEMA maana Makonda kateka anga lote la siasa na kuvishika mateka vyama vyote vya upinzani ambapo mpaka muda huu vipo chini ya ulinzi mkali sana wa komandoo na jasusi wa siasa ndugu Paul Makonda huku vikiwa mikono juu kichwa chini mwendo wa mateka.

Mtoa taarifa wangu anasema viongozi mbalimbali wa CHADEMA wanataka wakutane kwa dharura ili waone wafanyeje kumkabili Makonda, wengine wakadai kuwa GIA ya kumchafua kwa tuhuma za uzushi imegonga mwamba masikioni mwa watanzania na badala yake ameendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya Watanzania ambao wameonekana kuwa na shauku kubwa sana ya kumsikiliza Makonda na kutaka aanze ziara zake mikoani anakosubiliwa kwa hamu kubwa sana ili wamlaki kwa kishindo.

Wanajiuliza kama hajaanza ziara za mikoani tayari jina lake limeshatangulia na kuwatetemesha watu na kuteka mijdala yote mitaani na watu kuwa na hamu ya kumuona na kumsikiliza ,vipi akifika na kuanza kuvurumisha makombora? Nani atasalimika? CHADEMA itaficha wapi sura zao? Habari zao zitasikika wapi? Nani ataandika au kutangaza habari za chadema katika magazeti na hata TVs?

Inasemekana CHADEMA wapo katika wakati mgumu sana na hawaelewi wafanye nini hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa CHADEMA inapenda sana kutembelea matukio tukio ya mpito. Kwa hakika Makonda anawalaza na viatu chadema nzima kwa sasa. Hawahemi wala kupumua, ni roho juu juu tu kama wagonjwa mahututi.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Upumbavu tu hakuna lolote uliloandika hapo ya kumdanganya mtu. Alikuwa Mkuu wa mkoa na nguvu za ziada ya kuweza kuvamia Clouds fm na hata kupoteza watu na CHADEMA haikufa Wala kusambaratika. Itakuwa ss hivi kuwa mropikaji wa chama ndo CDM kisambaratike? Punguza uzuzu humu jukwaani
 
Upumbavu tu hakuna lolote uliloandika hapo ya kumdanganya mtu. Alikuwa Mkuu wa mkoa na nguvu za ziada ya kuweza kuvamia Clouds fm na hata kupoteza watu na CHADEMA haikufa Wala kusambaratika. Itakuwa ss hivi kuwa mropikaji wa chama ndo CDM kisambaratike? Punguza uzuzu humu jukwaani
Ni kwa kuwa hupo ndani ya Chadema lakini waliopo ndani ya chadema wameshachanganyikiwa na kukosa amani mioyoni mwao
 
Ha ha ha kwani ukiwataja CCM Tu unaogopa nn?

Hayo uliyosema wao ndio wanafanya Kwa sasa wanaona kijana anakuja kuharibu ugali wao

Sasa ndugu yangu ungekuwa muwazi Tu kuwataja ccm ambao wako chimbo moja dodoma

Kumkabili mwenezi anaegusa mtaafu wao 😂
 
Huo ndio ukweli subiri utaona muda wowote CHADEMA ikiitisha kamati kuu yake kwa dharura ili kujadili hali ya kisiasa hapa nchini maana kwa sasa ni maji ya shingo imebanwa koo na kuzimwa habari zake kama mshumaa
Una uhakika ulikuwa nyeg..e iliyoshinda ikatungisha mimba?
 
Ha ha ha kwani ukiwataja CCM Tu unaogopa nn?

Hayo uliyosema wao ndio wanafanya Kwa sasa wanaona kijana anakuja kuharibu ugali wao

Sasa ndugu yangu ungekuwa muwazi Tu kuwataja ccm ambao wako chimbo moja dodoma

Kumkabili mwenezi anaegusa mtaafu wao 😂
CCM Ndio iliyompitisha na kumchagua komandoo Makonda kuwa mwenezi wake.ndio maana unaona ikiendelea kumuunga mkono na kumpa ushirikiano wote.sasa upande wa pili kibanda chao kina waka moto na kuteketeza kila kitu kilicho ndani yake. Sasa ni mayowee tu kutoka CHADEMA.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nimepenyezewa taarifa kuwa CHADEMA hakukaliki wala hakuendeki wala hakupangiki mikakati ya aina yoyote ile.hii ni baada ya ujio wa Makonda kuonekana kuwa tishio kwa uhai wa chama hicho cha upinzani ambacho kinaendelea kusambaratika na kudhoofika kila uchwao. Inasemekana kikao cha dharura cha kamati kuu kinakwenda kuitishwa muda wowote ule kujadili namna ya kukabiliana na nguvu kubwa na ushawishi wa Makonda ulionekana kuteka mijadala ya kisiasa hapa nchini na kuonekana kuwa na nguvu ya ushawishi kwa wananchi wanaopenda siku zote mtu na kiongozi wa maamuzi magumu,ujasiri na kujiamini aina ya Paul Makonda.

Mtoa taarifa wangu amenieleza kuwa viongozi wote kwa sasa ndani ya kamati kuu ya CHADEMA hadi kanda wamevurugwa akili na kuchanganyikiwa ghafla kutokana na ujio wa Makonda unaoendelea kuzima taarifa zao na kukiweka chama cha mapinduzi midomoni mwa watanzania muda wote.kwa sasa CHADEMA haieleweki kama ipo stoo au kabatini au mfukoni mwa mwenyekiti mwenyewe,haieleweki nini kinaendelea juu ya CHADEMA maana Makonda kateka anga lote la siasa na kuvishika mateka vyama vyote vya upinzani ambapo mpaka muda huu vipo chini ya ulinzi mkali sana wa komandoo na jasusi wa siasa ndugu Paul Makonda huku vikiwa mikono juu kichwa chini mwendo wa mateka.

Mtoa taarifa wangu anasema viongozi mbalimbali wa CHADEMA wanataka wakutane kwa dharura ili waone wafanyeje kumkabili Makonda ,wengine wakadai kuwa GIA ya kumchafua kwa tuhuma za uzushi imegonga mwamba masikioni mwa watanzania na badala yake ameendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya watanzania ambao wameonekana kuwa na shauku kubwa sana ya kumsikiliza Makonda na kutaka aanze ziara zake mikoani anakosubiliwa kwa hamu kubwa sana ili wamlaki kwa kishindo.

Wanajiuliza kama hajaanza ziara za mikoani tayari jina lake limeshatangulia na kuwatetemesha watu na kuteka mijdala yote mitaani na watu kuwa na hamu ya kumuona na kumsikiliza ,vipi akifika na kuanza kuvurumisha makombora? Nani atasalimika? CHADEMA itaficha wapi sura zao? Habari zao zitasikika wapi? Nani ataandika au kutangaza habari za chadema katika magazeti na hata TVs?

Inasemekana CHADEMA wapo katika wakati mgumu sana na hawaelewi wafanye nini hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa CHADEMA inapenda sana kutembelea matukio tukio ya mpito. Kwa hakika Makonda anawalaza na viatu chadema nzima kwa sasa.hawahemi wala kupumua .ni roho juu juu tu kama wagonjwa mahututi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Nimegundua wewe ni kiumbe unayependa sana kutukanwa.
 
Nimegundua wewe ni kiumbe unayependa sana kutukanwa.
Mimi siogopi wala kuhofia matusi kwa kuusema ukweli.kuna watu ukiongea na kuandika ukweli huwa wanaumia sana na kukimbilia matusi kama ngao yao.mimi nitaendelea kuwaambieni ukweli hata kama mtatukana matusi kama walevi wa gongo.wala sitawatukana wala kuwajibu zaidi ya kuendelea kuwaelimisha kwa utulivu na upendo mkubwa
 
Back
Top Bottom