Carol Ndosi: Rais Samia aache kusisitiza kila mara kuwa yeye ni Rais mwanamke, haipendezi

Je kama kuna wanaomchezea wakiwa na fikra ni mwanamama atawahurumia...wabongo ukiwadekezadekeza utaingia nao msikitini...
Bashiru alimwambia asiwe Rais baada ya JPM kuanza kuugua akawa mbishi akisema anasubiri kauli ya kutumbuliwa ya rais mwenyewe.

Kistaarabu Bashiru hakupaswa kuwepo hata mle bungeni na ni sehemu ya “mfumo dume” unaomtesa Mama akiwa Rais pale ikulu.
 
Mwana harakati na Mjasiriamali carol Ndosi kupitia kipindi cha Joto Kali la Asubuhi TV-E ameweka wazi kukerwa kwake na kitendo cha Rais Samia kila anapopata nafasi kuongea na Watanzania basi lazima aseme kuwa yeye ni Rais mwanamke na yeye ni mwanamke. Amesema kuwa amekuwa akirudia mara kwa mara kila apatapo nafasi kuwa yeye ni mwanamke wakati kila mtanzania anajua kuwa yeye ni mwanamke.

Carol Ndosi anasema kuwa Rais Samia yeye ni Rais hapaswi kuendelea kujificha nyuma ya kimvuli cha uanamke kwani hilo si jambo zuri na haipendezi kwa Rais kuwa na hofu ya uanamke wake bali anatakiwa ajue watu wanamuamini kama Rais si kama mwanamke.

Amesema pengine Rais Samia anapitia mambo mengi kwenye chama chake au kwa watu wanaomzunguka kwa sababu ya uanamke wake lakini yeye kama Rais hatakiwi kuitumia kama ngao kwani yeye ni Rais na watu wanajua ni mwanamke hatakiwi kuwakumbusha watu, haipendezi.

Chanzo: TV-E/E-FM
We mwache tu miaka 5 itaisha yupo kwenye kuwaambia watu kuwa yeye ni mwanamke.
 
Umesema kweli. Kuna voice note ya akina Bashiru na Sukuma Gang wenzie wakati JPM yuko amekufa na hawataki kutangaza. Anasikika Bashiru akisema "Yule Samia ni Mwanamke Hajui Kitu".

Ukiona Samia anasema mara kwa mara hayo maneno, na wewe huelewi, ujue hayakuhusu. Walengwa wanajuwa
Acheni kumzushia Bashiru mambo ya kijinga.

Hamuwezi kufanya mambo yenu bila kumuhusisha.
 
Yes maana kina Bashiru walimwambia mama a step down Tanzania haiko tayari kuongozwa na mwanamke, Sasa obviously hayo maneno yalimuumiza na sioni shida mtu kutoa dukuduku la moyoni as long as haumizi mtu, so I wonder wanaomshambulia eti anatumia uanauke wake ka excuse na Carol bila kutafakari akalibeba Hilo neno la ma clout chaser wa kisiasa bila kujua hicho ni kijembe kwa wahusika flani.
Bashiru muongo muongo
 
Kwa maoni yako mkuu. JPM unayemuamini wewe alimuamini yeye akampa umakamu wa rais.
Wapi nimesema namuamini JPM?

Humu ndani eatu sijui mnafikiri kwa kutumia makalio ama kitu gani, unashindwa kuelewa. Kwamba kila anaempinga huyo mama basi ni mfuasi wa JPM, aisee!

Jambo la pili ujue umakamu wa rais ni ceremonial figure, mtu yeyote anaweza kua makamu wa rais.
 
Wapi nimesema namuamini JPM?

Humu ndani eatu sijui mnafikiri kwa kutumia makalio ama kitu gani, unashindwa kuelewa. Kwamba kila anaempinga huyo mama basi ni mfuasi wa JPM, aisee!

Jambo la pili ujue umakamu wa rais ni ceremonial figure, mtu yeyote anaweza kua makamu wa rais.
Tulia mkuu Rais Samia afanye kazi yake. Hizi kelele hazina msaada wowote kwa nchi na kwake pia.
 
UPUUZI TU ....UDHAIFU WA KATIBA YETU NDIYO CHANZO CHA KUWEPO HAYA MAUZA×2 YOTE ......


NB: chief mkuda hangaya hana uwezo wa kuongoza ...
Ataongoza na atamaliza muhula wake, atakuja Rais mwingine na utalalamika hivi hivi

Funzo: HUWEZI KUMRIDHISHA KILA BINADAMU
 
Kwa katiba ya Tanzania hata ukimpa mtoto urais mtaendeshwa hovyo hovyo tu.

Hivyo usidhani mama ni dhaifu na anatumia kichaka cha jinsi.

Kuna namna anawakumbusha tu lakini si udhaifu.

Mamlala aliyonayo yanatosha kabisa kuamua lolote na hakuna atakayeleta fyoko fyoko.
Carol Ndosi ni opposition members
Ambae alikuwa anaogopa kujitokeza wakati wa jiwe..naona sasa ana launch her political career upya...
Huu nao ni ule ujinga wa jiwe, kila anayekosoa mpinzani.
 
Hata Nyerere tuna mu attack humu na alishakufa....
Viongozi hujadiliwa hata baada ya kifo..
But wewe Una attack anaechangia hoja simply sababu kaongea tofauti na unacho amini....

Actually sijasema alichoongea Ndosi sio sahihi
Nimetazama angle ingine mbona hakuwahi kukosoa chochote wakati wa Magufuli?
Why anakosoa now?
Ohhh sababu Uhuru wa kukosoa umerudi?
Ohhh nani kaurudisha?Ohhh Samia....


There you are
Kwa hiyo wewe ndio unapanga nini akosoe na nini asikosoe!? Ile statement yako kwenye post yako ya kwanza juu ya freedom of speech ina maana gani sasa!?
 
Kama mtu kutwa anakusakama kwa maneno ya hivyo mwisho unakuwa na inferiority complex
Inauma sana ukipitia hali kama hiyo
 
Hivi yule dogo wa Mbeya cha Matusi mbona simsikii tena,kwa hii hali ya mbowe kufungwa kwa kesi ya ugaidi na ingekuwa enzi za Magu angetukana mpaka atapike nyongo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom