Mifuko ya Hifadhi ya Jamii yapewa siku 60 kuwalipa Wanachama wake

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1687428767894.png
Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, imetoa agizo hilo ikiwa ni siku moja tangu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson kuitaka Serikali kuwawajibisha Waajiri wanaoshindwa kuwasilisha Michango pamoja na Mifuko kutolipa madeni ya Wanachama wake.

Wizara hiyo imeagiza Majina ya Waajiri wote Sugu wasiowasilisha na wanaodaiwa Michango ya Wafanyakazi kupelekwa kwa Mameneja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa Mikoa ndani ya siku 7 kuanzia leo Juni 22, 2023.

Aidha, Serikali imeitaka mifuko yote kukamilisha zoezi la kusaini mikataba ya kulipa madeni yote ya michango ya wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kabla ya Juni 30, 2023.

==========

Serikali imeagiza mameneja wa mifuko ya hifadhi ya jamii kuwasilisha majina ya waajiri sugu wanaodaiwa michango ya wafanyakazi wao ndani ya siku saba kuanzia leo.

Agizo hilo limekuja siku moja baada ya Spika wa Bunge, Dk Ackson Tulia kuagiza kuchukuliwa kwa hatua kwa waajiri walioshindwa kupeleka michango ya wafanyakazi katika mifuko ya hifadhi ya jamii, hali ilinayosabisha kero kwa wastaafu nchini.

Akizungumza Jumanne Juni 20,2023 akiongozana na wawakilishi wa Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Katambi amewataka mameneja wa mikoa kuhakikisha kuwa hakuna malalamiko ya wanachama katika mikoa wanayoiongoza.

“Sasa hii ni kipimo kwamba badala Rais (Rais Samia Suluhu Hassan) kupokea ujumbe kutoka kwa wastaafu kumlalamikia tafsiri yake ni kuwa mstaafu hajahudumiwa ipasavyo hajapata elimu ama amepuuzwa,”amesema.

Amesema malalamiko hayo kwa viongozi pia yanatafsiri kuwa hajapewa huduma inayostahili na ndio maana wanakata rufaa kwenda ngazi za juu.

Pia Katambi ameagiza mifuko hiyo kuhakikisha kuwa inawalipa wanachama ndani ya siku 60 za kisheria wanachama ambao nyaraka zao zimewasilishwa kwa ukamilifu.

“Mameneja wahakikishe kuwa hakuna malalamiko ya wanacham akatika mikoa wanayoiongoza na kuhakikisha kuwa waajiri wote wanalipa na kuwasilisha madeni ya michango ya watumishi wao kila mwezi,”amesema.

Mbali na hilo, Serikali imeagiza mifuko ya hifadhi ya jamii kukamilisha zoezi la kusaini mikataba ya kulipa madeni ya michango ya wanachama kabla ya Juni 30, 2023.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom