Mzanzibari Huru
JF-Expert Member
- Apr 17, 2014
- 373
- 225
Ndugu wana jamii
Wizi serikalini na katika mashirika ya umma ni tatizo sugu. Tatizo hili lipo miaka nenda miaka rudi. Tatizo hili ni shida sana kulitatuwa kwasabu ni tatizo lililomo kwenye damu ya watendaji.
Ikiwa kazi ya CAG ni kutowa ripoti kila mwaka juu ya wizi ulifanyika kila mwaka jana, hii haitokuwa tafauti sana na zile taarifa za habari tu na basi wizi hauwezi kung'oka. katika maiaka ya 80 wizi ulikuwa kwa milioni 4 au 5, sasa umekuwa kwa milioni 100 hadi mabilioni.
Njia ya kuzuia wizi 100% haipo na haiwezekani kabisa hata kufikiria hatuwa hizo, yaani hata ripoti ya CAG ya mwaka ujao itaonesha vile vile kuna wizi mzigo lala salama ulofanyika katika vitengo mbali mbali. Lakini uwezo wa kupunguza wizi huo hadi asilimia 80% upo.
Kinachotakiwa kufanywa ni kuigeuza CAG badala ya kuhesabu wizi ulofanyika kila mwaka jana, sasa wazuie wizi unawoweza kufanyika mwaka huu na mwaka kesho. Njia pekee ni kubadilisha mfumo mzima wa ununuzi serikalini na katika mashirika ya umma. Ikiwa manunuzi yote yanapitia CAG na kupata approval ya CAG basi wizi ule wa kununua vitu hewa au kudai huduma hewa utazuilika hapo hapo. Tunajuwa hili inawezekana kwasababu hakuna manunuzi ya kila siku na CAG itajipanga kiuajari, kimajukumu na kitaalamu.
Pia tender zote za serikali na mashirika ya umma zipitie CAG. Hapo tender hewa na malipo yasiokua ya lazima yataweza kuzuiliwa moja kwa moja. Mfano zile riba zinazoongezeka kwasababu walipaji walizembea au walifanya kusudi ili wavune kidogo katika ile riba.
Ikiwa si hivyo kila mwaka tutakuwa tunazidi kulalamika kuliko mwka ulopia.