Bibi Titi na Historia ya Mnazi Mmoja 1950s

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,918
30,259
BIBI TITI MOHAMED NA HISTORIA YA UWANJA WA MNAZI MMOJA 1950s

Katika uwanja huu mwaka wa 1949 walikusanyika makuli wa Bandari ya Dar-es-Salaam wanachama wa Dar-es-Salaam Dockworkers Union.

Walikusanyika hapo wakitokea kwenye ofisi ya chama chao iliyokuwa katikati ya uwanja wa wazi nyuma ya Acacia Avenue (Sasa Samora Avenue) ofisi ikikabiliana na Avalon Cinema.

Ofisi hii ilijengwa kwa mabati chini hadi juu.

Makuli wa Bandari ya Dar-es-Salaam walikuja Mnazi Mmoja kwa maandamano ya amani kuja kujadili mgogoro ndani ya chama chao ambacho General Secretary alikuwa Abdulwahid Kleist Sykes.

Kwa bahati mbaya sana kwa yale yaliyokuja kutokea baadae nafasi hii Abdul Sykes alipewa na Waingereza.

Wanachama walikuwa wanataka kuanzisha mgomo lakini Abdul Sykes alikuwa akizuia mgomo akidai lazima pawepo majadiliano kwanza baina yao na wenye meli.

Hiki ni kisa kirefu.
Kipo katika kitabu cha maisha yake.

Kwa ufupi ni kuwa chama kilikuwa kinaelekea katika vurugu na kuna baadhi ya wanachama waliomuona Abdul kuwa kikwazo kwa hiyo atolewe katika uongozi.

Abdul Sykes akiishi na baba yake Mzee Kleist na alikuwa kitandani mgonjwa lakini akipata na kufuatilia taarifa zote za mjini akiwa kiongozi wa Waafrika.

Taarifa alizokuwanazo kuhusu Dockworkers Union hazikumfurahisha na uamuzi wake ulikuwa Abdul ajiuzulu uongozi atoe fursa kwa chama kupata kiongozi mwingine.

Haikuwa siri kuwa Erica Fiah mhariri wa gazeti maarufu Kwetu na adui wa muda mrefu wa Kleist alikuwa akichochea uasi na akiitaka sana nafasi aliyokuwanayo Abdul.

Kleist akamuamrisha Abdul kujiuzulu.
Siku alipojiuzulu wanachama baadhi yao wakataka abakie.

Kilichofanyika wakambeba Abdul mabegani wakawa wanakujanae Mnazi Mmoja kwa maandamano na nyimbo wapate kufanya mkutano.

Abdul hakuweza kumkiuka baba yake.

Mkusanyiko huu wa makuli wa bandari pale Mnazi Mmoja ulikuwa kiashiria cha mambo makubwa yatakayofanyika katika viwanja vile si miaka mingi mbele baadae.

Erica Fiah mtu mzima wa najamo alichukua nafasi ya Abdul Sykes kijana mdogo wa miaka 25.

Erica Fiah akaitisha mgomo.

Makuli wakapambana askari wa kuzuia fujo maarufu kwa jina la kavirondo.

Damu ikamwagika pande zote mbili.
Serikali ikaipiga marufuku Dockworkers Union.

Mwaka wa 1954 TANU ikaundwa.

Bibi Titi alihutubia mikutano miwili ya TANU Mnazi Mmoja wala hamjui Julius Nyerere.

Tupa jicho kwenye picha mkono wa kushoto utaona kuna sehemu rangi nyeusi imetanda.

Hiyo ilikuwa sehemu maalum imetengwa kwa wanawake na huo weusi hayo ni mabaibui.

Picha: Bibi Titi Mohamed na Tatu bint Mzee wakiwa wamevaa mabaibui.

1701685263951.jpeg

1701685329069.jpeg



 
Back
Top Bottom