LATRA anzisheni route ya Kibaha Kariakoo, Ferry Mbezi Luois papumue

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,638
697,929
Sheria na kanuni za LATRA si kwamba ni msahafu kwamba haziwezi kubadilishwa ama kutenguliwa ndio maana wametoa tena ruti ya Mbezi Mnazi mmoja .. Hii ruti ilikuwepo lakini ikafutwa baada ya ujio wa mradi wa mwendokasi unapoelekea kufeli kwa speed ya kutisha..

Sekta ya usafiri inapaswa kubadilika kulingana na mahitaji ya nyakati.. Kama kwasasa kuna daladala za Gongo la mboto Ferry nina imani kuwa na ruti hizi inawezekana kabisa na itasaidia sana kupunguza mrundikano wa abiria kwenye vituo Vikubwa
1. Bagamoyo Ferry/ Mnazi mmoja
2. Kibaha Ferry/ Mnazi mmoja
3. Kibaha Mbagala/ Gongo la mboto
4. Chanika Temeke/Buzz nknk

Hizi ruti ndefu zitapunguza misongamano vituo vya kubadilisha magari
Vitaokoa muda wa wasafiri, kumbuka muda ni mali
Vitapunguza nauli na kuleta unafuu kwa wananchi
Vita boost uchumi na kuleta matokeo chanya

Kwasasa alfajiri pale kituo kipya maili moja kuna mwendokasi wa moja kwa moja Kariakoo hii imepunguza usumbufu mwingi sana wa kubadilishwa na kusubiria magari pale Kimara

Vilevile kuna ruti ya saa nane usiku ya coaster isiyo rasmi ya wafanyabiashara inayoanzia Mlandizi na kuwachukua wa njiani mpaka maili moja.. Kwakuwa ruti kama hizi zimeonesha matokeo chanya LATRA itafakari upya kwa manufaa mapana ya Tanganyika.

IMG-20240229-WA0031.jpg
 
Hii nchi kwa visheria haijambo..

Wao wangeacha tuu watu wavurugane wenyewe,
Mmoja akitaka kutoka kibaha mpka chanika sawa,
Huyu Bagamoyo mpka kisukulu sawa,
Mwingine Mlandizi to Kijichi, Poa.
China plaza Karume, twendee.
 
shida ya ruti ndefu hawafiki mwisho, na kipindi cha rush hours huyaoni
kuna mpaka chanika mbezi, kwanza huyapati, yanaishia hukoo Gomes

mloganzila - makumbusho, kuyapata pale makumbusho ni kwa tochi
Kibaha haijawahi kukosa abiria Aisee kuanzia saa nane usiku mpaka saa saba usiku
 
Napendekeza
Chanika to Masaki
Chanika to Kigamboni
Chanika to Bunju
Chanika to Kiluvya

Tabata to Kigamboni
Tabata to Mbagala
Tabata to Chanika

In short kutokana na mahitaji ya wakati, mtandao wa usafiri wa daladala uwe ni kama utandu wa buibui ili kupunguza watu kutumia daladala zaidi ya moja kwa uelekeo mmoja
 
walitangaza mwaka jana segerea to vijibweni (kigamboni) ila sijaona mpaka leo daladala
 
Back
Top Bottom