BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Nilishindwa kupiga picha lakini miundombinu mingi haipo sawa kwa maana ya ubora, vitu vingi vinaonekana vimechoka, ni kama vile hospitali imetelekezwa.
Mbali na huduma nyingine kuendelea kama kawaida kwa maana ya Watoa huduma kufanya shughuli zao na kusafisha mazingira kwa kufagia lakini wanaangushwa na miundombinu ambayo imechoka, kuanzia kwene ukuta, viti na vifaa vingine mbalimbali.
Pia sehemu ya vyoo nako hali si nzuri, mabomba na miundombinu mingine ipo hoi.
Hivi viongozi wetu wako wapi? Hawajui hiki kinachoendelea au wanafanya makusudi? Serikali ya Zanzibar ifanye kitu katika hili.
Hela zinazotolewa na Serikali kuboresha na kuendesha Taasisi hiyo zinaelekea wapi? Nani anahusika na jukumu la kuangalia ubora wa miundombinu na vifaa? Hatua zichukuliwe.
Sehemu ya kutolea huduma ya afya nayo inakuwa si salama kwa afya.
Pia soma: Inasikitisha: Tazama hali ya miundombinu Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, Unguja, Zanzibar