Burundi nao waitosa Tanzania!

Burundi nao waitosa Tanzania!

Umshasikia Sheria za EU? Kuna Mbongo kasoma hizo sheria. Baadhi ya Nationalist huwa wanalalamika kuwa nchi zao ziliuzwa na kupoteza Uhuru wake. Ndiyo maana Britain wakataka kujitoa na Barroso anasema FULL, ikiwa na maana wameshaingia tayari ila siyo full. Siyo kama kamuungano ketu ka EAU. Wenzetu wana hadi mahakama ambako nchi dhaifu hushindwa kesi kila siku, you know what i mean.

Barroso:
"This is about the economic and monetary union but for the EU as a whole," he said.

"The commission will, therefore, set out its views and explicit ideas for treaty change in order for them to be debated before the European elections."

"We want to put all the elements on the table, in a clear and consistent way, even if some of them may sound like political science fiction today. They will be reality in a few years' time."

Mr Barroso's announcement that he will set out plans for a European federation next spring, before elections to the European Parliament in May 2014, will further deepen Conservative divisions over the EU.
 
Mkuu timbilimu vipi tena, sina shaka unajua vizuri majirani zetu hawa tuko karibu nao sana miaka nenda rudi, wahamiaji wanatakiwa wawe na kibali ni hilo tu, tunapo zungumzia Wanyarwanda tuna maanisha Wahutu, Watutsi na Watwa - tatizo linatokana na a few ethnic group yenye mawazo hatarishi kwa mstakabali wa great lakes ni hilo tu, kwa bahati mbaya ni watu wachache sana wanao lifahamu hilo! Nawashauri kwa nia njema kwamba wahachane na ndoto zao za kutaka ku-annex sehemu za nchi jirani na inbuilt traits zao za kutowathamini binadamu wenzao wakitekeleza hilo hakuna ambaye atawanyoshea kidole. Wanyarwanda hasa Watutsi watabaki ni Wafrica kama Wafrica wengine, haya mawazo ya kuji-equate na Wayahudi ndio kunawapoteza kwa kwendeleza na vita vya on and off ndani ya DRC kwa karibu miaka ishirini bila ya kupata amani ya kudumu. Narudia kusisitiza kwamba ni kikudi kidogo tu cha Watutsi ndio chenye misimano ya U-Neo-colonialism and a watered down Fascism, lakini majority ya Watutsi ni binadamu wahungwana tu, labda tukiwa tuna watisha tisha kwa maneno wachache wao watajirudi - nimewahi kukaa nao bila matatizo yoyote, binafsi nisingependa kuwa sema sema lakini nina wajibu wa kujaribu kuwarudisha kwenye mstari wa watu wastaarabu na wapenda amani, in other words siwezi kukaa kimya na kuhacha kikundi cha binadamu wachache watuingize kwenye vita vya kijinga kwa kukosa kwao kutafakali mambo kwa kina, tukijifanya sitofahamu watazingiza nchi za East and Central Africa kwenye conflagration of a century - the threat is real sio imaginary. Sina shaka mkuu Rushasha hawachukii Watutsi per se na inaonekana anawajua vizuri na aliwahi kusema ana jamaa zake wa karibu walio oana na Watutsi, Rushasha kama mzalendo anacho fanya ni kutoa tahadhali kuhusu tabia zao ambazo wakati mwingine ziko highly umpredictable na mifano ya kudhilisha hilo hiko tele.

Very well said ndugu!
 
Wakubaliana kuunda rasimu ya shirikisho la EAC
By James Gashumba, EANA
Arusha, Septemba 20 , 2013 (EANA)- Mkutano wa maafisa waandamizi kutoka Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi wa kuharakisha Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki umekubaliana kuanza kuandaa rasimu ya katiba ya shirikisho hilo.

Kama ilivyokuwa kwa timu ya wataalamu walioandaa Itifaki ya Soko la Pamoja, timu ya kuaada rasimu ya katiba ya shirikisho la kisiasa itajumuisha wataalamu mbalimbali kutoka nchi zote tano wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

''Tumekubaliana juu ya taratibu na jinsi ya kuhakikisha kwamba ipo miongozo iliyowazi juu ya kuandaa rasimu hiyo ambayo hatimaye itafikia katika hatua ya mwisho ya kuundwa kwa shirikisho la kisiasa,'' Waziri wa Serikali za Mitaa wa Rwanda, James Musoni alisema baada ya mkutano wa mawaziri mjini Kampala mwishoni mwa wiki.

Wakuu wa nchi za Rwanda, Kenya na Uganda Juni mwaka huu walikubaliana kuongeza kasi ya kufikia lengo la shirikisho la Afrika mashariki.
Pia katika mkutano uliofanyika Mombasa,Kenya, Agosti mwaka huu, Burundi nayo iliunga mkono hatua hiyo ambayo pia inalenga kuimairisha miundombinu chakavu ndani ya kanda hiyo ya Afrika Mashariki.

Mkutano huo wa Kampala juu ya shirikisho la kisiasa ni wa kwanza wa aina yake ambapo maafisa waandamizi kutoka Rwanda, Kenya,Burundi na Uganda wamehudhuria tangu kikao cha utatu kilichofanyika mjini Entebe, Uganda Juni, mwaka huu.

Mawaziri kutoka nchi mbalimbali wananchama wa EAC waliopewa dhamana ya maandalizi ya shirikisho la kisiasa watatoa ripoti ya hatua iliyofikiwa mbele ya mkutano wa wakuu wa nchi za EAC utakaofanyika Oktoba, mjini Kigali, Rwanda.

Tanzania haimo katika mchakato wa shirikisho
Nchi hizo nne za EAC zinatumia baadhi ya vipembele katika mtangamano wa Afrika Mashariki ambavyo vinaeleza kwamba baadhi ya wananchama ndani ya jumuiya wanaweza kwenda kasi zaidi kuliko wengine katika baadhi ya masuala yanayohusu mtangamano.

Mahakama ya Afrika ya Mashariki (EACJ) ilitoa uamuzi mwaka 2009 kwamba hatua ya aina hii inaendana sawia na mahitaji ya muafaka katika kufikia maamuzi ndani ya EAC.

JG/IM/NI
Nashangaa baadhi ya watanzania tunahamaki kuachwa kando. Ni haki yao wacha waendelee kumtafutia mu7 post. Uzoefu wetu na zanzibar bila shaka hautupi hamu kurukia muungano na nchi jirani.
 
Kwa sasa hivi mustakabali wa Tanganyika na Zanzibar unahitaji kipaumbele. Watanganyika wapate nafasi ya kuamua juu ya ardhi yao na rasilimali zilizomo.


Nasikia zanzibar inajito Tanzania inakwenda EAC
 
You have expelled all of them now what? Anything changed in your life? Did you get any richer? Did you get more oxygen than what you were getting before? Did life get any better for you? Noooooo. You are still the same poor soul that you are and actually poorer for hating.

Do you have a family anyway? How many members? When the number increases /decreases does it affect your budget? Start thinking from that level and then go to national level.. By the way does your immigration laws support illegal immigration???? Chako chetu ; chetu chetu......
 
Mkuu Wacha1, muulize GOOGLE atakupa majibu yote.....

Barack Obama: Britain should stay in the EU - Telegraph

EU exit would put US trade deal at risk, Britain warned | World news | The Guardian

BBC News - Brazil 'overtakes UK's economy'

Story za Mchina huwezi kuziona kwenye hizo Media zenu zinazotawala dunia nzima. Wengine tunachambua hadi Media ndogo ndogo za nchi tofauti na huko ndiyo waweza kusikia News za Mchina. Mchina aliingilia hata kuokoa uchumi wa Greece kwa sababu tu EU ikivunjika, Ulaya itakuwa matatani na siyo siri, EU ndiyo soko kubwa sana la Mchina.

Mchina siyo MJINGA kama tunavyomuona hapo Tanzania. Sisi wanatuletea Wadhaifu hadi wanavalishwa bendera ya CCM na Kinana/Nape. Ovyo kabisa hawa wanaoletwa Africa/Tanzania.

Mkuu naona unakimbilia google, hivi hizo links ulizoweka zinaonyesha statistics zozote au basi ndio umburukenge wenyewe?

Kama unataka tuamini maneno yako unaweza kutujibu swali hili kwa nini majority ya EU members wanataka kwenda kukaa UK na sio France au Germany? Je, ni nani wamewekeza vitega-uchumi vyao zaidi kule China? Uchina kama hawatauza kwa USA au Ulaya kwa nchi kama UK wataporomoka kama ngedere. Nakuomba uchukue pesa ya China au Brazil halafu nenda Kilosa au Ifakara kama unaweza kununua chungwa.

Nafahamu wabongo wengi wanawaponda sana Waingereza wakati hata hawaelewi jinsi UK Government machinery inavyofanya shughuli zake. UK hawawezi kuamrishwa na nchi yoyote ile fact, EU pamoja na kujaribu kuwashurutisha waingie kwenye Euro wamegonga mwamba na bado EU wanawategemea sana UK kuwa-bail out kwenye matatizo yao.

Kuhusu ma-tabloids hao waandishi wanaandika kutokana na mwenye gazeti anavyotaka nini kiandikwe, usiwe mwepesi wa kufikiria kila kilichopo kwenye google ndio sahihi. Ukiangalia tangu mtikisiko wa uchumi 2008 kuanzia mwaka juzi UK economy inakuwa na sio hoi unavyoandika hapa. Hiyo imetokana na factors nyingi tu, i.e. mashindano ya Olympics pamoja na kuwa na watalii wengi kwenda kwenye kisiwa kile. Vile vile usisahau UK ni financial centre ya hali ya juu. Chijui Sikonge unaishi dunia ipi.
Wacha yupo Alaska tu anakula kuku na biscuti.

Leta stats za maana mjadala utakolea sio hizo za kuokoteza kwenye google.


BTW hizi nchi zinazojiita EA wanatuchelewesha tu kwenye mipango yetu ya maendeleo, tuna uzoefu wa ushirikiano zaidi ya hawa majirani zetu uchwara ambao wanafikiri tutawamalizia matatizo yao. Imekula kwao.
 
Kuna mambo mengi yanayofanya majirani watutenge, wengine wanatuchukia kwa sababu wanadhani ziwa Nyasa lina gesi na petroli hivyo wakituengua watafaidi peke yao, wengine wanatutenga kwa sababu ya neema ambazo Mwenyezi Mungu alimjalia mama yetu Tanzania, wengine wanatutenga ati tu kwa sababu tuna ardhi kubwa kuliko wao kiasi kwamba hatujui tutaitumiaje, wengine wanatutenga ati tu kwa sababu Rais wa China mara baada ya kuapa Tanzania ilikuwa nchi ya pili kuitembelea baada ya Urusi, wengine wanatutenga ati tu kwa sababu kati ya nchi tatu za Afrika alizozitembelea Obama Tanzania ilikuwa moja wapo wengine wanatuchukia kwa sababu Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani zenye kiasi kikubwa cha gasi, urani makaa ya mawe, chuma nk. Sasa mtu akikuchukia kwa sababu hizo nilizozitaja hapo juu ambazo kwa bahati mbaya ni za kweli unafanyaje, unawaita na kuwagawia baadhi au unakomaa tu. Mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe
 
HATA NCHI ZOTE ZIJITENGE BADO TZ ITASIMAMA KWA MTAZAMO HUU:
Mataifa yote ya Afrika Mashariki yameiona Tanzania kama taifa lisilojua umuhimu wa kutumia na kusimamia rasilimali zake kwa maendeleo ya taifa na watu wake lakini hili si jambo la kubezwa kwa mlango mwingine wa kufikiri.

Tanzania ni taifa ambalo kwa udhaifu wake limejikuta likijijenga vizuri kwa kuongeza vyanzo vingi vya ndani vya uchumi tofauti na mataifa mengine katika ukanda huu achilia mbali usaidizi wa bajeti ambao kila nchi katika ukanda huu unapata toka nchi za ughaibuni tofauti na mataifa mengine kama Kenya na Uganda ambayo yanategemea sana uwekezaji walioufanya nje ya nchi zao na hasa Tanzania.

Angalia vizuri, Tanzania inauwezo kiasi gani wa kuajiri watu wake katika sekta binafsi na sekta za umma, ongezeko la pato la taifa, ongezeko la uwekezaji wa ndani kutoka kwa wazawa, mataifa yote ya Afrika mashariki yanaona kuwa Tanzania ndio mahali sahihi pa kufanya uwekezaji mkubwa.

Kama viongozi wetu wataona jambo hili na kujua namna ya kutumia mianya hii, hata waungane na kuunda umoja wao ndani ya umoja bado Tanzania itaendelea kuwa ndio mama kwao na taifa kubwa sio tu kwa ukubwa wa eneo la ardhi bali lenye uwezo wa kuamua taswira za mataifa mengine.

Uhuru Kenyata(UK), Paul Kagame(PK) na Museveni(M7) wote wanajua kuwa bila Tanzania hakuna Afrika mashariki na kujitoa kwa Tanzania katika jumuiya hii ni kiama kwa mataifa yote yaliyobakia.

Tatizo ni kujisahau kwa Waziri husika na nina mashaka sana na nini anamshauri JK juu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki au yuko bize na mbio za urais 2015.

Mkuu kwanza salamu, alafu huo hapo juu ni ukweli kabisa sababu sio lazima muungane kisiasa tunaweza tu kuishia kiuchumi katika hatua ya sarafu kama mataifa ya Uingereza, Uswisi na Norway. Hizo ni mbinu za kutufanya tuone tunaachwa na tukurupuke tujiunge nadhani kama niko sahihi Mh. Sitta waziri mhusika wa Afrika Mashariki alisema Tanzania haitakubali kubuluzwa nadhani huo ndo uwe msimamo wetu na nchi yetu.

Shirikisho linatakiwa kuwa la wananchi na sio viongozi kama wanavyofanya hao wengine; hii itasaidia kupunguza lawama kwa wananchi ya kutonufaika. Hivyo serikali inatakiwa ifanye nini? Serikali inatakiwa iwaandae watu wake kiujasiliamali na kizalendo kupitia mifumo ya elimu na ufundi ili tuweze kuwa na nguvu kazi imara itakayo shindana na kuwekeza katika jumuiya kizalendo kwa manufaa ya nchi.

Ni bora uchelewe kufika lakini ufike mzima kuliko kuwahi alafu ufike vipande vipande. Wito wangu kwetu sisi wenye nchi kwamba tupaze sauti zetu kwamba hatutaki kuburuzwa katika shirikisho la Afrika Mashariki hadi pale sisi wananchi tutakapo amua tuko tayari sababu shirikisho ni letu sio la viongozi!
 
Mkuu uliona wapi Political federation inatangulia Economic integration?

Hebu tueleze kwanini interest ipo kwenye federation na sio economic integration?

Swali la muhimu na la maana, embu jibuni!!!!!!!!! mnaolalamikia uamuzi wa Tanzania
 
Bahti mbaya hatuna mipango ya scenario km hizi..yaani scenario wakikutona hatuna mvuto, na scenario wakituon tuna mvuto.....tulihitaji mipango ya kupelelezi, mipango ya kuweka maizngira ya kufanya siku zote wasikose ch akutegemea kwetu ili muungano wao siku zote uwe na unafiki..hiii itatusaidia ktk usalama zaidi ya tunavyodhani..aani kuliko itokee watupige vita kwa pamoja ni bora tuwe na control ya kuwagawa na kuwatumia wengine.


Burundi nio wa kwanza ktk miaka ya karibu kuwa na malumbano kabla haya ya malawi na tayari majeshi yetu yalikuw ana mahcmabulizi kadhaa ziwa Tanganyika na Mpakani.
 
Nashangaa baadhi ya watanzania tunahamaki kuachwa kando. Ni haki yao wacha waendelee kumtafutia mu7 post. Uzoefu wetu na zanzibar bila shaka hautupi hamu kurukia muungano na nchi jirani.
Spot on mkuu, muungano wa nchi mbili imekuwa issue mpaka leo - tukiongeza nchi nne si ndio itakuwa balaa!!
 
kagame tena?jamani nimeshasema watz tumewekewa maneno 3 ili tusione mambo yanayotendeka huku nyuma ya pazia maneno yenyewe ni Rwanda,Kagame,M23......sipendi kuyasikia tena please....

ivi wewe mbona unapenda kuigiza as if wewe ni MTZ???kwani ukichangia kama mnyarwanda utapungukiwa nini,hamjiamini watutsi!!?
 
Hakuna ugonjwa mbaya kama ukosefu wa fikra huru, Je wote mnaosupport hao walio tutenga na kuona kuwa mkuru/ watz wana mtatizo mmeshawahi kusoma kitabu cha "An Enemy of the People "? Basi kitafuteni kama mtakielewa na kukipeg kwenye scenario iliyopo hamtabwabwaja kama mnavyofanya.

Spar Bath,Dr. Stockmani or?
 
Tanzania inajitegeme? Du! Mnauza nini sadc?

..chungulia hapa wana data za exports za Tanzania.
The Observatory of Economic Complexity :: Tanzania Exports, Imports and Trade Partners

..katika majirani zetu, Kenya[eac], na Congo[sadc], ndiyo waagizaji wakubwa wa bidhaa zetu.

..pia ktk nchi za Kiafrika, South Africa[eac] ndiyo anaongoza kwa kuagiza bidhaa za Tanzania.

NB:

..wako wanaopinga data za exports zetu kwa South Africa wakidai kwamba tunauza madini, hivyo wanatunyonya.
 
Sikujua kuwa The Guardian na BBC ni Tabloid. Asante kwa kufungua macho.....

Ntakujibu moja tu: Watu walikuwa wanakimbilia UK kwa Sababu walikuwa walikuwa wanagawa nyumba na fedha za bure. Ila sasa Uk wameishiwa hela, njaa kali..... Soma hapa:

The Coalition will end the benefits 'free-for-all' for migrants, Mark Harper says - Telegraph

Migrants must get benefits say EU: Brussels threatens to stop new crackdown | UK | News | Daily Express

Kuhusu pesa ya Mchina, fanya utafiti ujuwe mashirika makubwa wanavyonunua vitu China, malipo wanadaiwa hela gani.


Mkuu naona unakimbilia google, hivi hizo links ulizoweka zinaonyesha statistics zozote au basi ndio umburukenge wenyewe?

Kama unataka tuamini maneno yako unaweza kutujibu swali hili kwa nini majority ya EU members wanataka kwenda kukaa UK na sio France au Germany? Je, ni nani wamewekeza vitega-uchumi vyao zaidi kule China? Uchina kama hawatauza kwa USA au Ulaya kwa nchi kama UK wataporomoka kama ngedere. Nakuomba uchukue pesa ya China au Brazil halafu nenda Kilosa au Ifakara kama unaweza kununua chungwa.

Nafahamu wabongo wengi wanawaponda sana Waingereza wakati hata hawaelewi jinsi UK Government machinery inavyofanya shughuli zake. UK hawawezi kuamrishwa na nchi yoyote ile fact, EU pamoja na kujaribu kuwashurutisha waingie kwenye Euro wamegonga mwamba na bado EU wanawategemea sana UK kuwa-bail out kwenye matatizo yao.

Kuhusu ma-tabloids hao waandishi wanaandika kutokana na mwenye gazeti anavyotaka nini kiandikwe, usiwe mwepesi wa kufikiria kila kilichopo kwenye google ndio sahihi. Ukiangalia tangu mtikisiko wa uchumi 2008 kuanzia mwaka juzi UK economy inakuwa na sio hoi unavyoandika hapa. Hiyo imetokana na factors nyingi tu, i.e. mashindano ya Olympics pamoja na kuwa na watalii wengi kwenda kwenye kisiwa kile. Vile vile usisahau UK ni financial centre ya hali ya juu. Chijui Sikonge unaishi dunia ipi.
Wacha yupo Alaska tu anakula kuku na biscuti.

Leta stats za maana mjadala utakolea sio hizo za kuokoteza kwenye google.


BTW hizi nchi zinazojiita EA wanatuchelewesha tu kwenye mipango yetu ya maendeleo, tuna uzoefu wa ushirikiano zaidi ya hawa majirani zetu uchwara ambao wanafikiri tutawamalizia matatizo yao. Imekula kwao.
 
Hapa vipi??????
half-full.jpg


Barroso:
"This is about the economic and monetary union but for the EU as a whole," he said.

"The commission will, therefore, set out its views and explicit ideas for treaty change in order for them to be debated before the European elections."

"We want to put all the elements on the table, in a clear and consistent way, even if some of them may sound like political science fiction today. They will be reality in a few years' time."

Mr Barroso's announcement that he will set out plans for a European federation next spring, before elections to the European Parliament in May 2014, will further deepen Conservative divisions over the EU.
 
ivi wewe mbona unapenda kuigiza as if wewe ni MTZ???kwani ukichangia kama mnyarwanda utapungukiwa nini,hamjiamini watutsi!!?

mmh....una lako jambo!tofauti na wewe unadhaani hakuna mtz mwingine mwenye akili ya kuona hili?
 
Back
Top Bottom