mwita ke mwita
JF-Expert Member
- Aug 13, 2010
- 8,058
- 3,755
Mkuu uliona wapi Political federation inatangulia Economic integration?Woga utatumaliza Wa-Tanzania.
HATA NCHI ZOTE ZIJITENGE BADO TZ ITASIMAMA KWA MTAZAMO HUU:
Mataifa yote ya Afrika Mashariki yameiona Tanzania kama taifa lisilojua umuhimu wa kutumia na kusimamia rasilimali zake kwa maendeleo ya taifa na watu wake lakini hili si jambo la kubezwa kwa mlango mwingine wa kufikiri.
Tanzania ni taifa ambalo kwa udhaifu wake limejikuta likijijenga vizuri kwa kuongeza vyanzo vingi vya ndani vya uchumi tofauti na mataifa mengine katika ukanda huu achilia mbali usaidizi wa bajeti ambao kila nchi katika ukanda huu unapata toka nchi za ughaibuni tofauti na mataifa mengine kama Kenya na Uganda ambayo yanategemea sana uwekezaji walioufanya nje ya nchi zao na hasa Tanzania.
Angalia vizuri, Tanzania inauwezo kiasi gani wa kuajiri watu wake katika sekta binafsi na sekta za umma, ongezeko la pato la taifa, ongezeko la uwekezaji wa ndani kutoka kwa wazawa, mataifa yote ya Afrika mashariki yanaona kuwa Tanzania ndio mahali sahihi pa kufanya uwekezaji mkubwa.
Kama viongozi wetu wataona jambo hili na kujua namna ya kutumia mianya hii, hata waungane na kuunda umoja wao ndani ya umoja bado Tanzania itaendelea kuwa ndio mama kwao na taifa kubwa sio tu kwa ukubwa wa eneo la ardhi bali lenye uwezo wa kuamua taswira za mataifa mengine.
Uhuru Kenyata(UK), Paul Kagame(PK) na Museveni(M7) wote wanajua kuwa bila Tanzania hakuna Afrika mashariki na kujitoa kwa Tanzania katika jumuiya hii ni kiama kwa mataifa yote yaliyobakia.
Tatizo ni kujisahau kwa Waziri husika na nina mashaka sana na nini anamshauri JK juu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki au yuko bize na mbio za urais 2015.
Kuna wakati Kikwete alikuwa Marekani, akazungumzia kuhusu matatizo ya Kenya, serikali ya Kibaki ikachukia kuwa kwanini kana alikuwa na kitu cha kuzungumza kuhusu matatizo ya Kenya asiongee na viongozi wa Kenya bali akasubiri akaenda Marekani na kuongea na wamarekani kuhusu matatizo ya Kenya. Ndio ntindo wake.
Hatuna haraka sana, ngoja kwanza tumalize oparesheni Kimbunga halafu tupeane vitambulisho vya Uraia.
Baadae tuweke kura ya maoni ili wote tutoe maamuzi kwa pamoja kama tuingie huko au tuendelee kusubiri!
murutongore........hizi zao nin tabia za msichana mwenye hajavunja ungo!...SA watawamaliza (SA makes all economic decisions kwa SADC!) China imeingia and i hear wanakuja with everything (as investors they are supposed to atleast boost local economy) hata mpishi wa chai ni mchina! aaaargh! now Obama wants a piece ....where there is keen western interest chungeni! dont be fooled..TZ maybe ver rich and so is Nigeria with oil, Congo with minerals, etc mmm...my brothers msidanganyike ..tanganyika na zinj zahitaji warwanda, waganda warundi na wakenya!Exactly the same scenario happened with Rwanda. Ila kagame huwa hamung'unyi maneno. Anakupa hapo hapo.
Woga utatumaliza Wa-Tanzania.
Kuna watu umu walisema sisi tujitoe EAC tutaungana na Burundi.nawasubiri mje apa kuchangia
name naungana nawe mkuu naona haya mataifa yanaionea wivu Tanzania maana viongozi wa mataifa makubwa wanatia nanga hapa sasa wakiona hivyo wanasikia wivu! shine shine shine my beautiful country!Hizi ndoa za mkeka zina matatizo yake, sijafahamu utafiti wa kina uliofanywa nao zaidi ya kufikiria msukumo tu wa kiitifaki kutokana na wimbi la Tanzania kujitangaza katika anga za mataifa mbalimbali duniani na kuonekana kukubalika na kuvutia viongozi mbalimbali kuitembelea.
Kuna nchi kama Uingereza, na pengine hata Uswizi hazikujihusisha kwa undani katika shirikisho la Ulaya, hata hivyo pamoja na kugomea kuingia katika sarafu ya Ulaya na kuruhusu tu mzunguko wa sarafu hiyo katika nchi, bado sijaona kuathirika na bado inaonekana kiuchumi kuendelea kutengamaa.
Kwa vile Tanzania ni mwanachama wa nchi za ushirikiano wa kiuchumi nchi za kusini mwa Afrika, sioni haja ya kuhangaika na ndo ya mkeka ya hawa Museveni, Kenyata Wanyarwanda. Tuwaache waendelee na yao, ipo siku watakapokuja kugutuka kuingia kichwakichwa ndipo wakapofahamu kwa nini Tanzania tumekuwa muhimu kwao na kwamba uzoefu katika masuala ya shirikisho baina ya nchi na nchi si kama kukaribisha jirani wakutanapo kwenye kilabu cha pombe kukaa meza moja, ni mambo mazito yanayohitaji uchambuzi, utafiti na kupima kwa kina vinginevyo ni kumnufaisha fulani ambaye ameshindwa kutupa kete kwa Mtanzania aliye makini na kuhitaji muda wa kupima na kutafakari kabla ya kuchukua hatua.
Tanzania kuna kila la kujivunia na nyota inaendelea kumulika kwani tukituliza kichwa kuna kila dalili ya kuwa taifa la viwanda tokana na utajiri wa chuma huko wilayani Ludewa, chuma ambacho pia ni moja ya nguzo kubwa katika uundwaji wa viwanda vikubwa. Vigumu kuchukua chuma kukisafirisha nje ni ghali bora kujenga viwanda nchini na hivyo kulinufaisha taifa kiuchumi. Tuwaache waendelee na ndoa ya mkeka, ipo siku watajua na kurudi wenyewe kuanzia njia za vichochoro kwa aibu kabla hawajapiga hodi mlangoni.
Adui yangu mokala1989 yuko wapi? Eti tutabaki na burundi :heh::heh:. Kwa kifupi, sisi (EAC) tunaogelea downstream, nyie ndo mnaogelea upstream. Mtachoka tu.
[Jamaa wanatuona watu wasio makini na very slow kuchukua uamuzi,mtu asikuongopee hawa jamaa wako fast kupita maelezo when it comes kwenye business.
Sisi tutakalia kulalamika tu wakati jamaa wanachupa,tuache uswahili TUKANYAGE TWENDE.
murutongore........hizi zao nin tabia za msichana mwenye hajavunja ungo!...SA watawamaliza (SA makes all economic decisions kwa SADC!) China imeingia and i hear wanakuja with everything (as investors they are supposed to atleast boost local economy) hata mpishi wa chai ni mchina! aaaargh! now Obama wants a piece ....where there is keen western interest chungeni! dont be fooled..TZ maybe ver rich and so is Nigeria with oil, Congo with minerals, etc mmm...my brothers msidanganyike ..tanganyika na zinj zahitaji warwanda, waganda warundi na wakenya!
Wakubaliana kuunda rasimu ya shirikisho la EAC
By James Gashumba, EANA
Arusha, Septemba 20 , 2013 (EANA)- Mkutano wa maafisa waandamizi kutoka Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi wa kuharakisha Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki umekubaliana kuanza kuandaa rasimu ya katiba ya shirikisho hilo.
Kama ilivyokuwa kwa timu ya wataalamu walioandaa Itifaki ya Soko la Pamoja, timu ya kuaada rasimu ya katiba ya shirikisho la kisiasa itajumuisha wataalamu mbalimbali kutoka nchi zote tano wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
''Tumekubaliana juu ya taratibu na jinsi ya kuhakikisha kwamba ipo miongozo iliyowazi juu ya kuandaa rasimu hiyo ambayo hatimaye itafikia katika hatua ya mwisho ya kuundwa kwa shirikisho la kisiasa,'' Waziri wa Serikali za Mitaa wa Rwanda, James Musoni alisema baada ya mkutano wa mawaziri mjini Kampala mwishoni mwa wiki.
Wakuu wa nchi za Rwanda, Kenya na Uganda Juni mwaka huu walikubaliana kuongeza kasi ya kufikia lengo la shirikisho la Afrika mashariki.
Pia katika mkutano uliofanyika Mombasa,Kenya, Agosti mwaka huu, Burundi nayo iliunga mkono hatua hiyo ambayo pia inalenga kuimairisha miundombinu chakavu ndani ya kanda hiyo ya Afrika Mashariki.
Mkutano huo wa Kampala juu ya shirikisho la kisiasa ni wa kwanza wa aina yake ambapo maafisa waandamizi kutoka Rwanda, Kenya,Burundi na Uganda wamehudhuria tangu kikao cha utatu kilichofanyika mjini Entebe, Uganda Juni, mwaka huu.
Mawaziri kutoka nchi mbalimbali wananchama wa EAC waliopewa dhamana ya maandalizi ya shirikisho la kisiasa watatoa ripoti ya hatua iliyofikiwa mbele ya mkutano wa wakuu wa nchi za EAC utakaofanyika Oktoba, mjini Kigali, Rwanda.
Tanzania haimo katika mchakato wa shirikisho
Nchi hizo nne za EAC zinatumia baadhi ya vipembele katika mtangamano wa Afrika Mashariki ambavyo vinaeleza kwamba baadhi ya wananchama ndani ya jumuiya wanaweza kwenda kasi zaidi kuliko wengine katika baadhi ya masuala yanayohusu mtangamano.
Mahakama ya Afrika ya Mashariki (EACJ) ilitoa uamuzi mwaka 2009 kwamba hatua ya aina hii inaendana sawia na mahitaji ya muafaka katika kufikia maamuzi ndani ya EAC.
JG/IM/NI
Mkuu uliona wapi Political federation inatangulia Economic integration?
Hebu tueleze kwanini interest ipo kwenye federation na sio economic integration?
Whtz burundi by the way??!!
Surely, you swim down stream towards the deep ocean where you'll be drowned for ever never to be seen again.. as for us, we swim upstream towards the shore..
Surely, you swim down stream towards the deep ocean where you'll be drowned for ever never to be seen again.. as for us, we swim upstream towards the shore..