Burundi nao waitosa Tanzania!

Burundi nao waitosa Tanzania!

Tatizo tumewakataza Aridhi yetu. Acha waende zao watajuta siku moja kwani hata wao wanatutegemea sana. Kilichopo sasa tuangalie ni jinsi gani tutaungana na DRC, Zambia na Mozambique kama kunaulazima wakuwepo kwenye shilikisho.
 
Wenzetu walitaka ardhi tu,hakuna CHA EAC wala nini?Kama hao wazamani walishindwa wa leo tutaweza?Hapo EAC ndio imeishaingia ICU tusubiri kifo chake rasmi muda mfupi ujao.Na hao wanaokimbilia huko wasubirini tu ,baada yamuda mfupi moshi wake utakuwa mzito na hatimaye moto kuwaka.
 
Tanzania siyo kwamba haipo kwenye jumuiya yoyote . Tupo SADC na tuko commited kweli na SADC. Hii EAC imekaa kishabiki mno. Tukijipanga , we wont lose anything. Let them go. After all nchi zote nne na hata South Sudan ziko politically unstable....zitavutana tu. Kila nchi pale imekaa mkao wa kula tu...

Uelewa wako wa mambo ni wa chini sana kujadili mada kama hii! Nchi inaingia ktk ushirikiano na nchi nyingine kwa madhumuni gani kama siyo kufaidika? Unazungumzia SADC,toka juzi nauliza tunauza nini ktk nchi za SADC? Sijapewa jibu!

Siyo kwamba nadharau nchi yetu kuwepo ktk SADC lakini sioni maendeleo endelevu ktk jumuiya hiyo sana sana sisi kuwa soko la bidhaa za SA! Sioni hata kama tunalikwepa tatizo la ardhi kwasababu ktk jumuiya hii ndiko nchi nyingi zina matatizo ya kweli ya ukosefu wa ardhi!

Sekta ya kilimo ndiyo mwajiri namba moja Tanzania,kwa maana wananchi wengi wanajishughulisha na kilimo. Wakulima wetu wakiwekewa utaratibu mzuri wa masoko na bei wana uwezo wa kulisha ukanda wa EAC,lakini hawana ubavu wa kupambana na wakulima wakubwa wa kizungu ktk SADC!

Kama wafanyabiashara wa Kariakoo wanadhani biashara yao na Wazimbabwe ni endelevu,basi wanajidanganya. Kwasababu Zimbabwe ikisha ondolewa vikwazo na USA na EU mambo yatabadilika sana!
 
Candid Scope,

Siyo kweli hayo unayoyasema. Muingereza kwa sasa anaporomoka si kawaida. Hata huduma zao za kulisha watu bure na kuwapa nyumba sasa wameanza kuzibana. Kiuchumi ameshazidiwa na Brazil na alipotaka kujitoa EU, China na USA walimwambia hata asiote kufanya hivyo.

Kuhusu Swis, hata wao wamejiingiza kimya kimya kwenye Schengen maana walikuwa wanakosa pesa kibao. Kujiondoa kwa Rwanda, Burundi na Uganda, kutakuwa na madhara makubwa sana kwetu na hapo mtu asikudanganye. Labda na sisi tuje tujifanye kawa Waswizi kwa kujiingiza kimya kimya kwenye Schengen na Uganda, Rwanda na Burundi huko mbeleni maana itakuwa na faida kwao na sisi.

Anyway, siasa za Africa zinabadilika badilika kutokana na Rais. Kesho wakija Marais wengine, watagombana na watarudisha ndoa na Tanzania. Inabidi katiba zetu kwanza zibadilike na nchi iwe na msimamo na siyo RAIS.

Unaweza kutupatia Statistics za uchumi wa UK kuporomoka kwa kiasi unachosema? Je, unaweza kuthibitisha kwamba USA na China waliwashurutisha UK kutoondoka EU?
 
You are not serious! Unalinganisha Norway na Tanzania iliyojichokea?

Siyo huyo pekee,wapo wengi wanatoa mifano hapa,ukisoma unajiuliza kiwango chake cha uelewa wa mambo kama hata amemaliza darasa la Saba! Kumbe eti wengine wahitimu wa Chuo Kikuu! Mpaka jana nimeandika kwamba kama hawa nawasoma hapa ni wasomi wa nchi hii,basi CCM bado wana muda mrefu wa kuendelea kutawala nchi hii!
 
Safi sana hatuhitaji kujiunga na majirani ili kuendelea tunahitaji mipango bora tu, maana tuna kila kitu kuanzia soko na rasilimali. Kwa hili nampongeza Kikwete na wa kulaumiwa ni Che nkapa ambaye tamaa zake za fisi ndizo zimetufikisha hapa pamoja na Mwinyi.
 
Kwanza kiingereza hujui eti you'll be drowned..go back to school. halafu if we can swim downstream it means we are good swimmers you dimwit. we will not "be drowned".

Nyie wakikuyu ni tajiri wa kingereza maskini wa ardhi. Sasa kuleni hiyo kingereza chenu cha kikikuyu.
 
You have expelled all of them now what? Anything changed in your life? Did you get any richer? Did you get more oxygen than what you were getting before? Did life get any better for you? Noooooo. You are still the same poor soul that you are and actually poorer for hating.

Hasira za nini wewe?... ni vibaya mtu akiambiwa arudi kwao? Hakika MUNGU wa Mbinguni atazidi kuuanika uovu wenu. Na huyo shetani mnayemtumikia naye kawachoka maana maovu mnayoyafanya mmemzidi hata yeye! Poor tutsis! Mnatia huruma sana...
 
Safi sana hatuhitaji kujiunga na majirani ili kuendelea tunahitaji mipango bora tu, maana tuna kila kitu kuanzia soko na rasilimali. Kwa hili nampongeza Kikwete na wa kulaumiwa ni Che nkapa ambaye tamaa zake za fisi ndizo zimetufikisha hapa pamoja na Mwinyi.

Licha ya baadhi ya makosa ya Mkapa lakini alikua mtawala smart ambaye huwezi compare na jamaa yenu!
 
Hasira za nini wewe?... ni vibaya mtu akiambiwa arudi kwao? Hakika MUNGU wa Mbinguni atazidi kuuanika uovu wenu. Na huyo shetani mnayemtumikia naye kawachoka maana maovu mnayoyafanya mmemzidi hata yeye! Poor tutsis! Mnatia huruma sana...

Nadhani una matatizo binafsi na Wanyarwanda. Uliachwa?
 
Licha ya baadhi ya makosa ya Mkapa lakini alikua mtawala smart ambaye huwezi compare na jamaa yenu!

Labda wewe ni mgeni angalia jinsi ambavyo namwandika JK ni rais wa kwanza kuwa mwizi unaweza search hiyo topic nilianzisha mara matokeo ya urais yalipotangazwa.

BTW Are you from Rwanda?

Search .... .When a president becomes a thief .... .... ..
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mbona majirani wanatushitukia hivi kulikoni? inawezekana tuna matatizo!!
Mkuu, Watanzania hatuna matatizo yoyote, nilishasema humu kwamba wote wale wanao taka kulitenga Taifa letu kila mmoja wao ana ajenda yake katika mjumuhiko huo, jaribu kuchunguza walivyo ingia madarakani! Wote walitumia mabavu kushika madaraka, nakwambia it's a question of time kabla hawajakumbwa na kisanga cha "SENE-GAMBIA". Chukulia mfano mdogo wa mapigano ya majeshi ya Rwanda na Uganda nchini DRC, sasa tujiulize hivi hawa ni jamaa wenye mshikamano wa kweli au ni marriages of convenience? tuje Kenya na Uganda wamewahi kukwaluzana kwa kijisiwa kidogo kwenye ziwa Victoria, je dhamila iliyo msukuma M7 kudai kisiwa kile in the first place kwamba ni sehemu ya Uganda wanataka kutueleza dhamila hiyo imekufa? Incidents nilizo taja hapo juu zinaweza kuonekana ni insignificant lakini they speak volumes about Psyche za utatu mtakatifu.
 
kagame tena?jamani nimeshasema watz tumewekewa maneno 3 ili tusione mambo yanayotendeka huku nyuma ya pazia maneno yenyewe ni Rwanda,Kagame,M23......sipendi kuyasikia tena please....

Hakuna anayemzidi Mbongo kwa kutengeneza propoganda za ku-justify udhaifu, uzembe, uswahili, ufikira mgando wake, na mamabo kama hayo! Tu mabingwa duniani. Kwa hivyo huyo Kagame, Rwanda, M23 utazidi kuwasikia sana (hadi tutakapopata chanzo kingine cha propoganda) iwe ni katika ufisadi, rushwa, ujambazi wa kutumia nguvu, na hata vibaka wa Dar watakawambia wametumwa na Kagame! Watu ambao wanafisidi hazina ya taifa ni 'wahamiaji haramu'.
 
Woga gani? TZ haina cha kuogopa wala wa kumuogopa!

Lazima waTZ sijui WaTanganyika tukubali kujitathimini. Tukubali kuwa pengine ni siasa za ujamaa au cho chote kile kilichotokea hatuna moyo ama ujasiri wa kuthubutu (kitu ambacho waingereza wanakiita to take risk). Huwezi kuwa mjasiriamali na papo hapo ukaogopa ku-take risk ukatarajia kufanikiwa. Tunapenda sana kujiletea mabadiliko na mfanikio lakini tunaogopa kuchukua hatua zinazohitajika. Tumekubali kuwa na mfumo wa vyama vingi lakini tunapiga propoganda kuua vyama vingi. Tumekubali na pia kufurahia kuunda katiba mpya iliyobora lakini wakati huo huo tunataka iwe Katiba ya CCM. Tunataka kuunda jumuiya ya Afrika ya Mashariki lakini wakati huo huo hatutaki mchakato uende kwa spidi inayofaa, wenzetu wameamua kwenda kwa spidi inayofaa basi kama kawaida yetu tunaanza kulalama na kutamba kuwa wanatuonea wivu tena wa kike. Kwa mipasho ya kanga hakuna anyetuingia! Tunataka lakini wakati huo huo hatutaki, tuna wasiwasi 'hawa wanataka kutuibia ardhi yetu' - kama sio woga ni nini?
 
Hizi ndoa za mkeka zina matatizo yake, sijafahamu utafiti wa kina uliofanywa nao zaidi ya kufikiria msukumo tu wa kiitifaki kutokana na wimbi la Tanzania kujitangaza katika anga za mataifa mbalimbali duniani na kuonekana kukubalika na kuvutia viongozi mbalimbali kuitembelea.

Kuna nchi kama Uingereza, na pengine hata Uswizi hazikujihusisha kwa undani katika shirikisho la Ulaya, hata hivyo pamoja na kugomea kuingia katika sarafu ya Ulaya na kuruhusu tu mzunguko wa sarafu hiyo katika nchi, bado sijaona kuathirika na bado inaonekana kiuchumi kuendelea kutengamaa.

Kwa vile Tanzania ni mwanachama wa nchi za ushirikiano wa kiuchumi nchi za kusini mwa Afrika, sioni haja ya kuhangaika na ndo ya mkeka ya hawa Museveni, Kenyata Wanyarwanda. Tuwaache waendelee na yao, ipo siku watakapokuja kugutuka kuingia kichwakichwa ndipo wakapofahamu kwa nini Tanzania tumekuwa muhimu kwao na kwamba uzoefu katika masuala ya shirikisho baina ya nchi na nchi si kama kukaribisha jirani wakutanapo kwenye kilabu cha pombe kukaa meza moja, ni mambo mazito yanayohitaji uchambuzi, utafiti na kupima kwa kina vinginevyo ni kumnufaisha fulani ambaye ameshindwa kutupa kete kwa Mtanzania aliye makini na kuhitaji muda wa kupima na kutafakari kabla ya kuchukua hatua.

Tanzania kuna kila la kujivunia na nyota inaendelea kumulika kwani tukituliza kichwa kuna kila dalili ya kuwa taifa la viwanda tokana na utajiri wa chuma huko wilayani Ludewa, chuma ambacho pia ni moja ya nguzo kubwa katika uundwaji wa viwanda vikubwa. Vigumu kuchukua chuma kukisafirisha nje ni ghali bora kujenga viwanda nchini na hivyo kulinufaisha taifa kiuchumi. Tuwaache waendelee na ndoa ya mkeka, ipo siku watajua na kurudi wenyewe kuanzia njia za vichochoro kwa aibu kabla hawajapiga hodi mlangoni.
Viwanda gani unavyozungumzia bwana Candid Scope? Nyerere alituwekea misingi ya viwanda vya kutupeleka mbele tumevigawa na baadhi kubadilishwa kuwa ma go down. Leo tunategemea Mchina aje atujengee kiwanda cha nguo. Hiyo gesi wala hatuna sera za kuitumia kuinua maisha ya watanzania waachane na kutumia kuni na mkaa wapike kwa gesi. Badala yake tumesaini mkataba wa kuiuza yote nje. Vivyo hivyo chuma. Tutakuwa tunasifika tu kwamba Tanzania inazalisha chuma lakini matunda yake wanavuna wengine kama ilivyo na dhahabu yetu. Wenzetu wametushtukia waache waendelee na mipango ya ushirikiano sisi tukijichimbia chini kama mbuni. Waingereza na Waswiss hawakujiunga na shirikisho la Ulaya kwa sababu ya arrogance lakini nchi makini kama Ufaransa na Ujerumani wametambua umuhimu wa ushirikiano.
 
Nadhani una matatizo binafsi na Wanyarwanda. Uliachwa?
Mkuu timbilimu vipi tena, sina shaka unajua vizuri majirani zetu hawa tuko karibu nao sana miaka nenda rudi, wahamiaji wanatakiwa wawe na kibali ni hilo tu, tunapo zungumzia Wanyarwanda tuna maanisha Wahutu, Watutsi na Watwa - tatizo linatokana na a few ethnic group yenye mawazo hatarishi kwa mstakabali wa great lakes ni hilo tu, kwa bahati mbaya ni watu wachache sana wanao lifahamu hilo! Nawashauri kwa nia njema kwamba wahachane na ndoto zao za kutaka ku-annex sehemu za nchi jirani na inbuilt traits zao za kutowathamini binadamu wenzao wakitekeleza hilo hakuna ambaye atawanyoshea kidole. Wanyarwanda hasa Watutsi watabaki ni Wafrica kama Wafrica wengine, haya mawazo ya kuji-equate na Wayahudi ndio kunawapoteza kwa kwendeleza na vita vya on and off ndani ya DRC kwa karibu miaka ishirini bila ya kupata amani ya kudumu. Narudia kusisitiza kwamba ni kikudi kidogo tu cha Watutsi ndio chenye misimano ya U-Neo-colonialism and a watered down Fascism, lakini majority ya Watutsi ni binadamu wahungwana tu, labda tukiwa tuna watisha tisha kwa maneno wachache wao watajirudi - nimewahi kukaa nao bila matatizo yoyote, binafsi nisingependa kuwa sema sema lakini nina wajibu wa kujaribu kuwarudisha kwenye mstari wa watu wastaarabu na wapenda amani, in other words siwezi kukaa kimya na kuhacha kikundi cha binadamu wachache watuingize kwenye vita vya kijinga kwa kukosa kwao kutafakali mambo kwa kina, tukijifanya sitofahamu watazingiza nchi za East and Central Africa kwenye conflagration of a century - the threat is real sio imaginary. Sina shaka mkuu Rushasha hawachukii Watutsi per se na inaonekana anawajua vizuri na aliwahi kusema ana jamaa zake wa karibu walio oana na Watutsi, Rushasha kama mzalendo anacho fanya ni kutoa tahadhali kuhusu tabia zao ambazo wakati mwingine ziko highly umpredictable na mifano ya kudhilisha hilo hiko tele.
 
Ahsante sana Mkuu Jasusi. Vitu kama hivi ndivyo vinatupa raha kurudi jamvini mara kwa mara ili kuzisoma hekima na busara za watu ambao wanaweza kuangalia upande mwingine wa shilingi na siyo kutetea/kupinga tu bila kutafakari kwa kina.

Viwanda gani unavyozungumzia bwana Candid Scope? Nyerere alituwekea misingi ya viwanda vya kutupeleka mbele tumevigawa na baadhi kubadilishwa kuwa ma go down. Leo tunategemea Mchina aje atujengee kiwanda cha nguo. Hiyo gesi wala hatuna sera za kuitumia kuinua maisha ya watanzania waachane na kutumia kuni na mkaa wapike kwa gesi. Badala yake tumesaini mkataba wa kuiuza yote nje. Vivyo hivyo chuma. Tutakuwa tunasifika tu kwamba Tanzania inazalisha chuma lakini matunda yake wanavuna wengine kama ilivyo na dhahabu yetu. Wenzetu wametushtukia waache waendelee na mipango ya ushirikiano sisi tukijichimbia chini kama mbuni. Waingereza na Waswiss hawakujiunga na shirikisho la Ulaya kwa sababu ya arrogance lakini nchi makini kama Ufaransa na Ujerumani wametambua umuhimu wa ushirikiano.
 
Last edited by a moderator:
Wakubaliana kuunda rasimu ya shirikisho la EAC
By James Gashumba, EANA
Arusha, Septemba 20 , 2013 (EANA)- Mkutano wa maafisa waandamizi kutoka Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi wa kuharakisha Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki umekubaliana kuanza kuandaa rasimu ya katiba ya shirikisho hilo.

Kama ilivyokuwa kwa timu ya wataalamu walioandaa Itifaki ya Soko la Pamoja, timu ya kuaada rasimu ya katiba ya shirikisho la kisiasa itajumuisha wataalamu mbalimbali kutoka nchi zote tano wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

''Tumekubaliana juu ya taratibu na jinsi ya kuhakikisha kwamba ipo miongozo iliyowazi juu ya kuandaa rasimu hiyo ambayo hatimaye itafikia katika hatua ya mwisho ya kuundwa kwa shirikisho la kisiasa,'' Waziri wa Serikali za Mitaa wa Rwanda, James Musoni alisema baada ya mkutano wa mawaziri mjini Kampala mwishoni mwa wiki.

Wakuu wa nchi za Rwanda, Kenya na Uganda Juni mwaka huu walikubaliana kuongeza kasi ya kufikia lengo la shirikisho la Afrika mashariki.
Hii kitu wanafanya sio kitu kipya. Kwa kweli wamechelewa sana kulingana na ratiba ya awali Utaipata hapa: https://www.jamiiforums.com/katiba-...;-sema-ndiyo-serikali-moja-3.html#post6510457 Kwa ufupi: Mchakato wa kuunganisha Afrika Mashariki unasema hivi:

Kuhusu hatua ya mwisho ya shirikisho la kisiasa, katika Mkutano Usio wa Kawaida mwaka 2004 Wakuu wa Nchi wa Kenya, Tanzania na Uganda waliazimia kuunda Kamati ya Kuharakisha Shirikisho la Afrika Mashariki. Kamati hiyo inayoongozwa na Amos Wako iliwasilisha taarifa yake kwa Wakuu wa Nchi mwezi November mwaka huo huo katika Mkutano wa Sita wa Wakuu wa Nchi.
Miongoni mwa mambo mingine, kamati hiyo ilitengeneza ratiba iliyotaka mambo yafuatayo:


a. Rasimu ya katiba ya shirikisho la Afrika Mashariki ifi kapo Desemba 2007
b. Kupitishwa katiba na mkutano wa Wakuu wa Nchi mwezi Januari 2009
c. Kura ya maoni kuhusu katiba ifi kapo Desemba 2009
d. Shirikisho la kisiasa lenye urais wa mzunguko ifi kapo 2010 na uchaguzi wa rais ifi kapo 2013
Mkutano wa Wakuu wa Nchi Usio wa Kawaida uliofanyika Dar es Salaam mwezi Mei 2005 ulielekeza kuundwa kwa utaratibu wa mashauriano ya kitaifa kukusanya maoni kutoka kwa Waafrika Mashariki juu ya Shirikisho la Afrika Mashariki na kuharakisha mchakato huo. Uk 90 -92
 
Back
Top Bottom