Mnabuduhe
JF-Expert Member
- May 8, 2015
- 352
- 590
Salaam!
Tarehe 26/03/2021 Ni siku ya Kumpumzisha Aliyekuwa Rais wetu John Pombe Magufuli huko kwao Chato.
Nawapongeza sana JamiiForums Facebook page kwa Kuelewa na Kumuenzi kwa Nukuuu Nkutu alizowahi kuzisema wakati wa uhai wake.
Na moja ya nukuu hizo ina maneno haya "Siku moja mtanikumbuka, na Mimi najua Mtanikumbuka kwa mazuri si mabaya"
Sasa naona watu wengi bado hawajaelewa Kiswahili hiki,kumkumbuka kwa mazuri wala si kwa mabaya.
Mh. Rais alimaanisha kuwa anatambua fika kuwa kuna mambo ambayo aliyafanya sio mazuri - na yawezekana aliyafanya kwa nia njema kabisa lakini hayo yasiwe sehemu ya jinsi mtakavyo mkumbuka.
-Kufuta Wafanyakazi Hewa ( Lilikuwa Jambo zuri kwa Afya na ustawi wa taasisi za serikali) lakini Je unadhani wale walioathirika walilipokea vipi zoezi hilo?
- Kuvunja mikataba ya kilaghai,Vita vya Wauza madawa ya kulevya na Uhujumu uchumi ( watu walioathirika na maamuzi hayo hawawezi kufurahi kamwe)
-Bomoa Bomoa kupisha Ujenzi wa miundo mbinu,Kusimamisha Ajira na Maslahi ya Wafanyakazi wa Serikali,Kusitisha Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.
- Vyombo vya Habari kuminywa Uhuru wao! na mengine mengi .
Alijua kuwa katika Kuimarisha Uchumi lazima mambo kama hayo yangetokea,hutokea na yalishatokea hata kabla ya yeye kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakati fulani Mh. Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliitisha Press Conference IKULU,na Mwandishi mmoja toka kanda ya Ziwa alimuuliza swali kuwa kwanini Mh. Mzee Benjamini Mkapa(Hayati) asishtakiwe kwa sababu alifanya biashara Ikulu.
Kikwete alimjibu yule Mwandishi kuwa Iwapo tutaamua kuwashtaki Viongozi waliopita basi Itabidi Tuanze na Awamu ya Kwanza.
Kikwete alikuwa Sahihi - Nyerere alifanya Mabaya, Mwinyi Alifanya Makosa,Kikwete alifanya Mabaya na JPM alifanya Mabaya - Hakuna Aliyekamilika katika suala la Uongozi - hajawahi kutokea na wala hatakuja kuwepo.
James Madison (Rais wa nne wa Marekani) aliwahi kusema" If men were angels no government would be necessary,If angels were to govern men,neither external or internal controls on government would be necessary." Tafsiri yangu ya kikalimani ni Kuwa - Iwapo Binadamu wangekuwa Malaika Hakungekuwa na haja ya kuwa na Serikali (DORA) na iwapo Malaika wangekuwa watawala wa Binadamu basi kusingekuwa na haja ya Udhibiti wa Ndani au nje Katika Utawala(Serikali)
Rais alikuwa na Shortcoming zake kama Binadamu,lakini ameshapumzika - Kilichobaki kwake ni Hukumu ya Haki kwa Muumba wake.
Tumkubuke kwa Mema yake aliyotufanyia Watanzania, Kathubutu mambo magumu sana! Kuna watu walituaminisha kuwa Huwezi Kuvunja Mikataba ya Madini, akaivunja ikawezekana.
Kuna watu walituaminisha kuwa hatuwezi kununua ndege kwa Fedha Taslim - Ikawezekana.
Kuna watu walituaminisha mambo mengi kuwa hayawezekani, lakini amejaribu kwa Uthubutu mkubwa sana.
Kiswahili ni rahisi ila kuna watu hawataki kuelewa kabisa - TUMUENZI KWA YALE MEMA ALIYOTUFANYIA.
Lakini wapo ambao hawatataka kuelewa maana ya haya na ni haki yao kufanya hivyo ila haina Afya kwao - Amepumzika JPM,Shujaa wa Majira haya.
Nawasilisha.