Nikitafakari huu msiba, naanza kukumbuka post za mwanakijiji kuhusu hili jambo nikianzia na ile ya free Amina. Mwanakijiji alitutahadharisha juu ya hatari iliyokuwa inamkabili huyu binti kwa kuzuiwa kuongea. Nitakuwa wa mwisho kuamini kwamba kifo hiki ni mapenzi ya bwana!
Nilitoka kidogo wenye ushauri kwangu nimesikia. niliaombwa na Dua mwanzoni niache nikakubali, wakaja vidudu mtu wakasema sina data ndio nikaamua kuendelea si nia yangu kuwakwaza watu. all in all file bado ninalo la mheshimiwa.
siku chache nilieleza kuwa hali ya Amina sio nzuri hamjui nani anaingia na nani anatoka nikaomba waheshimiwa wakamsalimie mgonjwa lakini naona wako busy na kutizama protocal jinsi ilivyokosewa wakati timu ya Taifa inaenda bungeni. wenye nia ya kumpa pole mgonjwa waniPM niwape mobile yake mumtumie salamu za kuimfariji. sisi tuwe rafiki wa shida kwenye uhondo tuwaachie wenzetu.
But, nina promise one thing!, kuwa hapa forum tuta-get to the bottom of this thing, enough, hiki kifo kinafanana sana na Marehemu Ipyana, ambaye in his case ilikuwa sambusa, nasikia safari hii ilikuwa ni samaki!
Sasa fasten Your Belt, kuna mzee mmoja ambaye amekuwa akiwatumia text message watu mabli mbali toka kifo kilipotokea, tunauliza baba kulikoni ya Ngoswe yakakuhusu mpaka kutumia hela zako zote hizo kutuma hizo message?
Mungu amlaze pema marehemu, Amina!