Buriani Amina Chifupa!

Status
Not open for further replies.
wewe jibu swali bana !

Kadampinzani,

Naona tunakwenda mbali sana. Kama huwezi kuelewa ninaloandika basi niulize nifafanue, na usipokubaliana nami pia useme na kwa kwa nini hukubalini nami; hiyo itanisadia na mimi kujifunza kutoka kwako. Mambo ya kushambuliana hayatusadii lolote. Nilipotofautisha science na scientism ulinielewa kweli? Kama umenielewa hayo maneno ya "kuna mtu kasema science na uchawi sijui nini na nini" na hapa kunishupalia kuwa "wewe jibu swali bwana" yanatoka wapi.


Mwanzoni nilichukulia swali lako kama swali la kawaida na nikakujibu very sincerely kwenye post yangu hapa. Lakini sasa naona umezidi kuwa too personal na nadhani kuwa hatuwezi kuendelea kujadiliana namna hiyo. Afterall hayo mambo haya hayana uhusiano sana na mada hii, tunai-dilute bure.
 
Baada ya maelezo hayo mafupi, ninakujibu kuwa mimi ninaamini kuwa uchawi upo. Watu wasiomcha Mungu ni wafuasi wa shetani na mojawapo ya zawadi zao kutoka kwa shetani ni nguvu za uchawi.

Hii imenifurahisha kweli!


wewe jibu swali bana !
Will it make any difference anywhere? hii itahamisha mjadala kwa mhusika na familia yake na kwenda kwa mwana JF... sidhani kama itasaidia zaidi ya kuleta ugomvi usio na sababu
 
mmmh!--God Help Me!......This is weed..Think I have started to smock it before I know is weed...In my languaje is called (((Bange)))) Much more funny with beer and wine!! but is still sound dangerous!! I need to be perfect!..

Please God Help Me! as easy as I'nm comming!!

Had similar thoughts goind through my mind some while back in here JF, and was about to ask 'what's up man?' Need to be strong and get away by all means possible. Anyways, can get help if need it. Just get courage.
 
Dah!

Kada umenikwida shati kweli kweli mzee wangu. Nitatoa maelezo kidogo kabla ya kujibu swali lako.

Mimi niseme ukweli ni mwanasayansi; ugali wangu weote unatokana na sayansi, na naamini kabisa kuwa chembe ndogo sana ya maisha yoyote inatengezezwa kwa carbon, oxygen, nitrogen, helium,hydrogen na phosphorus. Lakini majua limitations za science kuwa huwezi kupika hizi elements kwenye maabara na kupata maisha. Kazi ya kutengeza maisha siyo kazi ya binadamu, ni kazi ya nguvu kubwa zaidi ya binadamu. Kwa hiyo ninaamini kabisa presense ya nguvu zaidi ya Sayansi ndiyo maana naamini kuwa Mungu yupo. Hata ninapokuwa nakabiliana na tatizo kubwa sana la kisayansi huwa namwomba Mungu anisaidie kunifungulia jibu la tatizo hilo kwani naamini kuwa yeye ana uwezo wa kuona nisikoweza kuona.

Chini ya imani hiyo hiyo ya kuwapo kwa Mungu na uwezo wake, ninaamini pia kuwa kuna Shetani. Sasa kati ya nguvu za kishetani ni pamoja na uchawi.

Baada ya maelezo hayo mafupi, ninakujibu kuwa mimi ninaamini kuwa uchawi upo. Watu wasiomcha Mungu ni wafuasi wa shetani na mojawapo ya zawadi zao kutoka kwa shetani ni nguvu za uchawi.


Hii umeielezea kwa makini sana...good work.
 
Hili la kifo cha Amina lisiwe siri

Tahariri: Tanzania Daima, jumapili, 15 Julai 2007

LIKO tatizo, ndani ya Chama Cha Mapinzudi (CCM). Tatizo hili ni la usiri katika kila jambo. Tatizo hili pia liko serikalini na haina shaka chanzo chake ni viongozi wakuu wa CCM ambao ndio wale wale wanaoongoza serikali.

Hili ni la kifo cha Amina Chifupa, ambaye wakati akiugua kuliwa na viji-maneno maneno kuhusu kuugua kwake na hata alifariki, uvumi ulizidi kusambaa kuwa kifo chake kina mkono wa baadhi ya viongozi wa CCM na serikali.

Kauli ya baba yake Amina, Mzee Hamis Chifupa mara tu baada ya kufariki kwa mwanae kuwa kifo hicho kisihusishwe na mambo ya kishirikiana au wauza mihadarati, kwa sababu kimetokana na mapenzi ya Mungu, nayo ilipokelewa kwa hisia tofauti na baadhi ya watu na hata baadhi ya vyombo vya habari ambavyo pengine kwa kutokubaliana naye, viliendelea kuandika habari za utata kuhusu kifo hicho.

Lakini kauli ya karibuni kabisa ya mzee Chifupa, ambayo inatofautina na ile aliyoitoa awali, imezidisha maswali kuhusu usiri uliopo katika kifo cha Amina.

Mzee Chifupa sasa anadai kuwa kifo cha Amina kilisababishwa na ugonjwa wa Kiswahili na kisukari, na kwamba kabla ya kifo chake, alikuwa akiwataja sana baadhi ya viongozi kadhaa.

Ni mzee Chifupa aliyewatangazia Watanzania kuwa amemzuia binti yake kujitokeza hadharani kulipua bomu lililosababisha ndoa yake kuvunjika, na kuwataja watu waliokuwa wakimuandama katika maisha yake. Haina shaka huu ni mlolongo wa kile kinachoitwa usiri, tukizingatia kuwa Mzee Chifupa ni kada wa siku nyingi wa CCM.

Hivyo Amina amekufa na siri nzito moyoni mwake, ambayo kama angepata nafasi ya kuiweka hadharani, huenda leo hii mambo yangekuwa tofauti na ilivyo sasa, kwa sababu wangejua ni nani bingwa wa fitina na majungu ndani ya CCM na serikali.

Ili kuondoa utata wa kifo hiki, tunaishauri serikali, ichukue hatua kukichunguza na viongozi wanaotajwa tajwa kuhusika nacho wawekwe bayana ili nao waeleze wanachokijua dhidi ya Amina.

Vinginevyo, hili la Amina lisipochunguzwa, sisi tunadhani litazidisha shaka ya wengi dhidi ya usiri katika mambo ya hatari na huenda CCM na serikali vikazidi kujiweka katika nafasi mbaya.

http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/7/15/tahariri.php
 
wana jf naona tumeingiza mada nyingine ambayo nadhani ni bora kuifungulia thread inayojitegemea nayo kuwepo ama kutokuwepo kwa uchawi,kutumika ama kutotumika kwa uchawi katika kufikia mafanikio
 
Heshima zenu watanzania,

Natumaini hii imefikia tamati, naiweka Kabrasha kwa sasa na ikihitajika tafadhalini fanya kutukumbusha tutairejesha HARAKA iwezekanavyo.

Wasalaam
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom