Buriani Amina Chifupa!

Status
Not open for further replies.
wewe yebo yebo nakwambia, mie nilikuwa nikianza kusafiri nje ya nchi tokea miaka ya 1979 na sina ulimbukeni wa teknolojia na mambo ya uchawi yapo angalau siuamini, siuabudu lakini naamini upo na kuna watu wanaufanya tena kwa utaaluma. sasa sijui mwenzangu weye kuja nje miaka hii ya karibuni ndio unaona unajua kila kitu i dont know ( am not rude ) lakini mambo ya uchawi yapo, sasa turudi katika kifo cha amina, mimi sijui kama alikuwa anaumwa ukimwi au alirogwa but i guess i just have to go with the flow of her daddy's commnets ! lakini uchawi upooooooooooooooo !! kwani unajua nini kilichotokea kigamboni wewe ?
 
Jamani mnaopingana na theory ya uchawi,

Tofautisheni kati ya science na scientism katika kuijadili hiyo theory ya uchawi. Science inafafanua mambo mbalimbali ya kiasili kwa kutumia sheria za kisayasi, scientism ni kuamini kuwa kila jambo hapa duniani linafafanuliwa kisayansi.

Kwa bahati mbaya scientism iko wrong: kuna matukio mengi ambayo hayafafanuliwi kisayansi. Mambo yasiyoelezeka kisayansi yameweka katika makundi mbalimbali kama humanism (ubinadamu), philosophy, religion or spiritual, mythology na mengineyo. Vitu kama mapenzi, furaha, huzuni hayaelezeki kisayansi ni mambo humanistic. Uchawi pia hauelezeki kisayansi, uko kwenye mythology.

Kwa hiyo, hata kama wewe ni mwanasayansi, jitahid kuwa makini sana unapojadiliana na wenzako katika maswala haya. Wanasayansi wengi walijua limitations za sayansi na ndio maana wengi wao walikuwa waja Mungu sana.
 
kichuguu,
wewe binafsi unaamini uchawi upo au haupo ? ( simaanishi kama unatumia ila nataka tu kujua kama unadhani upo na unafanya kazi au la )
 
Timing na sababu za kifo chake bado vinanitatiza. kwa nini kama ni uchawi atupiwe mara baada ya talaka? Au kama ni ukimwi uje siku moja baada ya kupewa talaka? Bado nadhani kilichomuua huyu dada ni depression. Alimpenda sana mume wake, na hakuwa tayari kuachika!
 
kichuguu,
wewe binafsi unaamini uchawi upo au haupo ? ( simaanishi kama unatumia ila nataka tu kujua kama unadhani upo na unafanya kazi au la )

KadaM

Naheshimu hili swali umelielekeza kwa Mhe Kichuguu...lakini nalifananisha na lile la kujiuliza Mungu yupo au Hayupo? Nadhani yote ni jinsi unavyoamini wewe na nafsi yako...sio black & white.
 
Kuna haja sana ya kuwa makini hasa inapotokea kifo kama hiki; wananchi kuelezwa kuwa Marehemu alikufariki kwa uchawi...iko siku jamii itaanza kuonyeshana vidole kumtafuta mchawi ni nani miongoni mwetu; tukajikuta tunachinjana wenyewe kwa wenyewe. Ni tahadhari tu.
 
Dah!

Kada umenikwida shati kweli kweli mzee wangu. Nitatoa maelezo kidogo kabla ya kujibu swali lako.

Mimi niseme ukweli ni mwanasayansi; ugali wangu weote unatokana na sayansi, na naamini kabisa kuwa chembe ndogo sana ya maisha yoyote inatengezezwa kwa carbon, oxygen, nitrogen, helium,hydrogen na phosphorus. Lakini majua limitations za science kuwa huwezi kupika hizi elements kwenye maabara na kupata maisha. Kazi ya kutengeza maisha siyo kazi ya binadamu, ni kazi ya nguvu kubwa zaidi ya binadamu. Kwa hiyo ninaamini kabisa presense ya nguvu zaidi ya Sayansi ndiyo maana naamini kuwa Mungu yupo. Hata ninapokuwa nakabiliana na tatizo kubwa sana la kisayansi huwa namwomba Mungu anisaidie kunifungulia jibu la tatizo hilo kwani naamini kuwa yeye ana uwezo wa kuona nisikoweza kuona.

Chini ya imani hiyo hiyo ya kuwapo kwa Mungu na uwezo wake, ninaamini pia kuwa kuna Shetani. Sasa kati ya nguvu za kishetani ni pamoja na uchawi.

Baada ya maelezo hayo mafupi, ninakujibu kuwa mimi ninaamini kuwa uchawi upo. Watu wasiomcha Mungu ni wafuasi wa shetani na mojawapo ya zawadi zao kutoka kwa shetani ni nguvu za uchawi.
 
Yes, nakubaliana kabisa na wewe. Katika jamii ya kistaarabu tusitangulize sana uchawi hata kama tunaamini kuwa upo. Sababu ya kwanza ni ugumu wa ku-prove kuwa kweli uchawi ulitumika na nani mchawi. Mzee Chifupa asingeongea swala la uchawi hadharani, badala yake ni afadhali angebaki nalo moyoni na kama na yeye anaamini uchawei basi alishughulikie kichawi kuko kwa huko kwa vile uchawi siyo jambo la hadharani.
 
unajua wengi wetu tuliopo nje tunasema kwamba katika jamii hii tusiendekeze mambo ya uchawi, lakini mnaposema jamii hii mnarefer kwa jamii ipi ? najua sio ya tanzania, ebu niambie watu gani wasioendekeza uchawi bongo ( kati ya hao waliofanikiwa na simaanishi wote waliofanikiwa wametumia uchawi ) ( na hao wanaotumia uchawi kwa njia mbaya ya kuondoa viumbe vya mungu duniani )nyie mnataka kusema katika hiyo jamii "kwa mfano ya tz" mzee jk akupitia kwa wazee fulani hivi wakati anagombea urais,? kama jibu ni NDIO basi kuna kila sababu ya kuweka mbele mambo ya uswahili katika hiyo the so called "jamii". hapa ishu ni kwamba, wengi tupo nje na tumekuwa americanised au britishenalized if there's such a word, katika kufikiria kiasi kwamba tuna-apply science katika kila jambo.na ndio maana kuna mwanachama hapa akasema vitu kama furaha, huzuni havihusiana na sayansi.naweza nikasema uchawi ni kama taaluma nyingine tu na upo tena ni effective, angalau sijawahi kumroga mtu and hopefully never will, lakini tuwaulize hao wanaotumia wakwambie.
 
Kuna haja sana ya kuwa makini hasa inapotokea kifo kama hiki; wananchi kuelezwa kuwa Marehemu alikufariki kwa uchawi...iko siku jamii itaanza kuonyeshana vidole kumtafuta mchawi ni nani miongoni mwetu; tukajikuta tunachinjana wenyewe kwa wenyewe. Ni tahadhari tu.

ndio kama mambo ya kule salem, boston massachusetts kipindi hicho, watu walikuwa wakinyongwa kuhofiwa kuwa ni wachawi, more info soma the crucible by arthur miller.
 
kuna mtu kasema science na uchawi sijui nini na nini, sasa nauliza swali: which came first, uchawi au sayansi ?" ona hapo watu watakapoteleza, mie siendelei zaidi lakini naombeni mnijibu !
 
KadaM

Naheshimu hili swali umelielekeza kwa Mhe Kichuguu...lakini nalifananisha na lile la kujiuliza Mungu yupo au Hayupo? Nadhani yote ni jinsi unavyoamini wewe na nafsi yako...sio black & white.

ningeomba hapa kupingana na wewe, unapoongelea suala la mungu yupo au hayupo, nadhani hata tu sio kidini, unaweza ukafikiria tu mwenyewe milima, maji, binadamu, miti, there must be someone behind this nature mzee, na vitu hivi HAVIWEZI kuexist kama mtu mkubwa in this case ni MUNGU wakati suala la uchawi ni kwamba bila ya uchawi watu WANAEXIST and we dont need it, simple !

labda ungesema suala la uchawi ni kama la osama, wengine wanasema huyu jamaa anaexist na wengine hawaamini kama kuna mtu anayeitwa osama bali ni myth !
 
kuna mtu kasema science na uchawi sijui nini na nini, sasa nauliza swali: which came first, uchawi au sayansi ?" ona hapo watu watakapoteleza, mie siendelei zaidi lakini naombeni mnijibu !

I am not sure whether you understood my previous two posts or I am missing a point in your post.
 
But why the Lugalo doctors cannot come out to tell us the truth regarding the cause of AC's death? And why are we not questioning this part of this story? How long do we want the list of conspiracy theories to go before we knew the truth?

I think if we cannot push the Lugalo doctors to release the results of pm then I think we better close the chapter because we shall never know the truth. This mzee is simply suffering from guilt conscience; all he is doing is carthasis without which he may end up in the same direction as his daughter.
 
Kitila,

Hao madaktari labda wamepewa onyo la kutoongea na shirika lolote la habari.
 
Hivi Nchimbi Ni Nani? ana sifa gani...
-sasa NCHIMBI sijui atajisikiaje na sijui kama atakuja kwenye msiba wa DADA YETU bi Amina-
__________________
Hua sielewi vizuri!!
 
Dah!

Kada umenikwida shati kweli kweli mzee wangu. Nitatoa maelezo kidogo kabla ya kujibu swali lako.

Mimi niseme ukweli ni mwanasayansi; ugali wangu weote unatokana na sayansi, na naamini kabisa kuwa chembe ndogo sana ya maisha yoyote inatengezezwa kwa carbon, oxygen, nitrogen, helium,hydrogen na phosphorus. Lakini majua limitations za science kuwa huwezi kupika hizi elements kwenye maabara na kupata maisha. Kazi ya kutengeza maisha siyo kazi ya binadamu, ni kazi ya nguvu kubwa zaidi ya binadamu. Kwa hiyo ninaamini kabisa presense ya nguvu zaidi ya Sayansi ndiyo maana naamini kuwa Mungu yupo. Hata ninapokuwa nakabiliana na tatizo kubwa sana la kisayansi huwa namwomba Mungu anisaidie kunifungulia jibu la tatizo hilo kwani naamini kuwa yeye ana uwezo wa kuona nisikoweza kuona.

Chini ya imani hiyo hiyo ya kuwapo kwa Mungu na uwezo wake, ninaamini pia kuwa kuna Shetani. Sasa kati ya nguvu za kishetani ni pamoja na uchawi.

Baada ya maelezo hayo mafupi, ninakujibu kuwa mimi ninaamini kuwa uchawi upo. Watu wasiomcha Mungu ni wafuasi wa shetani na mojawapo ya zawadi zao kutoka kwa shetani ni nguvu za uchawi.

Kichuguu - huu ni mjadala tofauti kabisa, unahitaji mahali pake mbali na hapa ulipo.

Kutoweza kuunganisha C, N, O2 na mengineyo kuumba uhai kwa wakati huu haimaanishi haiwezekani milele! Sayansi imetoka mbali na itaendelea kwenda mbali, sasa hivi tumefikia kwenye chembe za uhai na nanotechnology, na gurudumu litaendelea kusukumwa mbele. Baada ya hapo pengine watu wataanza kuuliza: hiyo C, N vimetoka wapi? Je Sayansi itavitengeneza - actually vinatengenezeka kutokana na kujua viini vyake - electrons, protons, neutrons n.k. Baada ya hapo tutauliza hivyo viini vyake je, vinatengenezeka? Kwa kila hatua tutaendelea kusema ni Mungu ndiye aliyeviumba, au sayansi ya wakati huo italeta jibu jingine; and on and on, and on........
 
mmmh!--God Help Me!......This is weed..Think I have started to smock it before I know is weed...In my languaje is called (((Bange)))) Much more funny with beer and wine!! but is still sound dangerous!! I need to be perfect!..

Please God Help Me! as easy as I'nm comming!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom