Mbunge wa Maswa John Magale Shibuda ametumia nafasi aliyopewa kuchangia hotuba ya Mali Asili na Utalii kuwaponda viongozi wake wa Chadema na kwamba wananchi wa jimbo lake wapo nyuma yake. Aidha ametumia nafasi hiyo kuwaponda waandishi na wahariri wanaobeba ajenda za viongozi wa kisiasa akiwalenga hasa wa Chama chake wanaoendelea udhalimu na maslahi binafsi. <br />
<br />
Maneno kama kamati kuu ya Chadema, viongozi dhalimu, kukosekana kwa demokrasia yamejirudia sana kwenye hotuba yake. Wakati akisema hayo wabunge wengi wa Chadema kama Msigwa, Lucy Owenya na Christina Lissu wameonekana wanyonge sana