Bungeni Live: Juni 3, 2012 [Morning Session]

Bungeni Live: Juni 3, 2012 [Morning Session]

Uamuzi gani mgumu wa LIWALO NA LIWE? Huu wa KUENDELEZA UTEKAJI NYARA NA MAUAJI YA MADAKTARI??
KILA SIKU IENDAYO KWA MUNGU CCM INAZIDI KUDHIHIRISHA UDHAIFU WAKE. Tumeanza kuona udhaifu wa KIWETE, tukaona UDHAIFU wa PINDA,tukaona UDHAIFU wa BI MKORA MAKINDA,tukaona UDHAIFU wa BUNGE. Ukijumlisha UDHAIFU WOTE HUU unapata UDHAIFU +WA SERIKALI YA MAGAMBA!!!

Poleni sana Watanzania kwa kukosa serikali IMARA. Endeleeni kuomba sana ili Mungu awapatie serikali IMARA TOKA CHADEMA. M4C HOYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!
 
Na kweli aisee, Km Mh. WASHWA WASHWA vile anatutetea ili vyakuwashwa vikunwe au sio ?

:A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down:
 
I agree with you, it seems CDM wamekuwa-ambushed na really they seem like surrendered.They must retreat and return to their normal standard we used to see them.Mnyika usikubali kutekwa nyara kama timu ya taifa Italy a.k.a Azzuri dhidi ya spain,mtapigwa mabao.Tadhali tundu lissu, Mbowe na wengine achaneni na hoizo propaganda za ccm.kUANZIA BAJETI itakyofuata tunawaomba sisi wananchi mrudi ktk mstari, tunahitaji mthibitisha kuwa you always deserve to be frontliners in critical issues.

Mkuu! ulicho ongea ni sawa, lakini wanacho fanya CDM ni kumpa kamba ndefu ccm ambayo inataka kujinyonga, wasije wakarudi na madai kwamba kamba ilikuwa fupi!
 
naomba maoni ya wadau kuhusu kauli za jana za wabunge wa CCM wakati wa kikao cha jioni.
 
Da. Wewe kweli nunge boya
Nunge = mtu asiye hamnazo kabisa
Boya = fuata upepo, asiye na msimamo
 
wapuuzi wote wale; hakuna haja ya kupoteza muda kuwajadili.

Washwa washwa at work na dawa ya kitu kinacho washwa ni kukunwa tu hakuna dawa zaidi ya hiyo. Na jana Mh. Mnyika aka mh. washwa washwa aliumbuliwa jana bungeni kwa kujitafutia umaarufu wa rahisi
 
Bunge letu sasa limegeuka uwanja wa vijembe na kutupiana lawama, nawasihi wabunge wafuate kilicho wapeleka Dodoma.
 
Bunge letu sasa limegeuka uwanja wa vijembe na kutupiana lawama, nawasihi wabunge wafuate kilicho wapeleka Dodoma.
Wakati Bunge lilipokuwa halina vijembe nini kilifanyika ambacho
kiliinufaisha nchi hii?
 
Kulindana,kutokubali kukosolewa na kutokuwa na utamaduni wa kuwajibika ndo kunakopelekea hayo yote kutokea.
wananchi INABIDI TUWE WAPOLE TU!Maana tushayakororoga wenyewe na sidhani kama tutaacha kuyakoroga. Wanachokifanya kiukweli kinaonyesha sisi tuliowatuma tulivyo maana hawa ni wawakilishi wetu sisi wananchi tulioona wanafaa.Swali la kizushi Je watanzania wenzangu hamkuwa na watu wenye hekima zaidi ya hawa na mkaacha kuwachagua kwa sababu mzijuazo ninyi.Mmelima bangi mnataka mvune mahindi! wapi na wapi!!!!.
 
ulimboka%284%29.jpg

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk. Stephen Ulimboka.


Kambi ya Upinzani Bungeni imeituhumu Idara ya Usalama wa Taifa kwa kushindwa kuzuia matukio ya wahamiaji haramu kutoka Ethopia na kitendo cha kutekwa na kutweswa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk. Stephen Ulimboka.

Shtuma hizo zimetolewa jana na Msemaji wa kambi ya upinzani wa ofisi ya Rais, Profesa Kulikoyela Kahigi, alipokuwa akiwasilisha maoni ya kambi hiyo, kuhusu mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2011/12 na Makadirio ya Mapitio na Matumizi ya Ofisi ya Rais kwa mwaka wa fedha 2012/13.

"Hivi usalama wa taifa na vikosi vyote vya ulinzi na usalama vilikuwa wapi hadi wahabeshi wakavuka mpaka na kuendelea na safari hadi Kongwa,?" alihoji Profesa Kahigi na kuongeza:

"Kitendo cha kutekwa na kuteswa kwa kiongozi wa Chama cha Madaktari Nchini Dk. Stephen Ulimboka, na vyombo vya usalama vipo dhahiri kuwa hali ya usalama ni ya mashaka."

Alisema hali ya usalama ni tete pia katika mipaka ya mikoa ya Kigoma na Kagera hususani kuhusiana na wahamiaji haramu.

Alisema kambi hiyo inayasema hayo kwa kuwa Rais ambaye ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo vyote vya usalama hapa nchini lakini kwa matukio hayo, Ofisi ya Rais haijatoa kauli ya kina bungeni ni kwa vipi watu hao wameingia toka nje na wanasafiri hadi katikati ya nchi bila kujulikana.

"Au kuna mtandao wa vyombo vya usalama unaojihusisha na biashara hiyo ya kusafirisha watu, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa nchi yetu?" alihoji.

Alisema huo ni udhaifu mkubwa kwa idara ya usalama wa Taifa na kuhoji ni kutokana na watendaji kupata kazi bila ya kuzingatia vigezo na weledi au kutojua umuhimu wa maana halisi ya idara hiyo kwa taifa.

Alisema tatizo la rushwa linaloigusa serikali ndio msingi wa pendekezo la kambi ya upinzani kuhusu kufanya maboresho ya Idara ya Usalama wa Taifa.

Alisema taarifa kubwa kama kashfa ya rada, rushwa ya Richmond, sakata la EPA na Ufisadi wa IPTL ni ishara kuwa idara ya usalama ni ya baadhi ya viongozi wa serikali, chama na familia zao.

Aidha, alisema kambi ya upinzani inaitaka serikali kutoa taarifa kwa Bunge kuhusu uchunguzi wa ubadhirifu wa kashfa ya Kagoda, Meremeta na Deep Green.
TAKUKURU

Profesa Kahigi alisema kambi hiyo inapendekeza kuwa uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ufanywe na Kamati ya Taifa ya Uteuzi na ithibitishwe na Bunge.

Kambi hiyo ilitaka taarifa za taasisi hiyo ziwasilishwe bungeni kila mwaka na kujadiliwa na Bunge kama ilivyosasa ambapo taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Halikadhalika, kambi hiyo imehoji ni hatua gani ambazo Takukuru wameshachukua juu ya tuhuma dhidi ya Jairo na wenzake ambazo zilithibitishwa na Kamati ya Bunge.

SOURCE: NIPASHE
 
kama wanatuambia kuna ndege ya nchi nyingine hutua na kubeba wanyama bila usalama wa taifa kujua sasa hapo kuna usalama wa taifa kuna usalama wa mafisadi..kama msangi ana skedo kibao badala ya kukamatwa ndiyo wanapandishwa vyeo hapo kuna usalama...kama walishindwa kumsaidia dhaifu wao kujua mmiliki wa richmond hapo kuna usalama wa taifa...kama wapo basi raisi dhaifu..
 
Form IV failure na Form VI ndo wamejazana huko usalama wa taifa, intelligent people wanakwapuliwa na nchi zenye akili wanarudi hapa wanaanza kutuchunguza its crazy.

Lazima viongozi wetu wajue "Those days are over, make changes". Kuna watu smart mbaya lakini huwezi kukuta wanawafuatilia, wanawapa training na kuwaingiza kwenye vitengo nyeti.

I expected this country could be well networked kila sehemu, badala yake imejaza vilaza kwenye sekta nyeti kama hiyo. Matokeo yake wanaanza kutumaliza sisi ndugu zao badala ya maadui wa nchi.
 
That time Mwl, alipenda kuwaweka mazuzu na wasio na elimu ili wawe 'SIR YES SIR' na wasiweze kumsaliti na hao wanawapenyeza watoto wao humohumo Vilaza kibao kazi kutisha raia ' Mimi Usalama; hata ethics hakuna hopless TISS. hawana msaada tena. Hapo ina maana Al-shabaab walishafika mji mkuu wa tz.
 
Naamini kabisa kunaweza kuingia kikosi cha makamandoo kikafika hadi Dodoma na kuliteka bunge nalinganisha na ile squad iliyosemekana iliingia hadi ndani ya Pakistani na kummaliza Binladen kwa mahelikopta ila Tz magari yanatosha.
Kwa maana hii inaonyesha mipaka yetu ipo wazi aidha walio mipakani wakiachiwa vihela vidogo wanakuwa hawapekui kitu.

Ni aibu kubwa tena hatari,wale wanaosema wanalinda mipaka tunahitaji watupe jibu.
 
Back
Top Bottom