Bungeni Live: Juni 3, 2012 [Morning Session]

Bungeni Live: Juni 3, 2012 [Morning Session]

Mfumo unaotumika ndiyo mbovu, mwenyekiti ni mfuasi wa chama cha Chemba kwahiyo hata kama Chemba ataongea Ujinga kama kawaida yake Mwenyekiti atasimama kutetea ujinga huo kwa sababu wanatoka chama kimoja.
Cha msingi pale mwenyekiti angemwambia Chemba achangie kilichokuwa mezani kwa siku ya leo badala yake mwenyekiti amemuacha Chemba apoteze muda wake hakuna alichochangia
 
Leo Mnyika amekuwa mbogo baada ya Mwigulu Nchemba kuleta propaganda bungeni badala ya kujadili bajeti ya serikali anajadili bajeti ya kambi ya upinzani na akagusia suala usalama wa taifa kutofanya kazi ipasavyo, ndipo Mnyika aliposimamia hapo kuwa usalama wa taifa wamezuia kujadili suala la EPA, kagoda na ufisadi mwingine bungeni na pia alisema katika wizi wa EPA Anahusika na ndipo alipopewa siku saba kuleta ushahidi.

Nawasilisha.


mbona baada ya ushahidi kupelekwa bungeni hatupati FEEDBACK AU HATUA ZINAZO CHUKULIWA NA BUNGE
 
Taasisi hii kwa sasa naona imeshindwa Kazi ya Kulilinda Taifa pamoja na rasilimali zake. Nachofahamu hawa jamaa ilibidi wawe proactive kwenye kuibua pamoja na kupangua njama mbalimbali zenye athari kwa Taifa. Kazi ambayo inatakiwa kufanyika kwa siri huku wakiweka uadilifu mbele ili kuepuka mazingira ya uonevu kwa namna yeyote ile.
Kwa matukio ya hivi karibuni nashawishika kusema ya kwamba hawa jamaa hawafanyi kazi kwa kufuata misingi ya sheria na haki. Badala yake wanatumika na wanasiasa kwa jinsi wapendavyo. Watu wanaogharimiwa na kodi za wavuja jasho wa nchi hii kwa sasa wamegeuka wasaliti na watu wa hatari dhidi ya wanyonge.
Aidha nashawishika kusema wanafanya yote haya kwa makusudi au bila ya kupenda. Kikubwa ninachokiona hapa ni mpasuko uliopo ndani ya jeshi hili kwa sasa " wapo wasiopenda mwenendo wa serikali - lakini ukishaingia humu kutoka sahau .....na hukumu ya usaliti inajulikana na wote" ...kwa upande mwingine " wapo wanaopenda huu mwenendo wa serikali - hawa ni wale wanaofaidika na actions za serkali kwa namna moja au ingine".
Mgawanyiko uliopo ndani ya TISS kwa sasa unatokana na sababu nyingi: kikubwa kikiwa ni usiri uliopo kwenye mambo mengi - angalia hawapendi hata kuhojiwa au kuweka hadharani ufanisi wao wa kazi. Hivi waziri wa ulinzi na usalama akisimama hadharani akasema " mwezi june - TISS imefanikiwa kuchunguza na hivyo kufanikisha urejeshwaji wa Tsh. Billion 300 zilizofichwa uswis nchini TZ" hapo kutakuwa na kipi kilichoharibika?. Ni mambo mengi sana yanayotakiwa yahojiwe kuhusu uhalali wa uwepo wa TISS katika kulisaidia taifa kwenye utatuzi wa mambo mbalimbali yaliyolikumba taifa hili. Mpaka leo hatuna majibu sahihi ya madubwana kama vile RICHMOND, DOWAN's, EPA, Meremeta, n.k.
Ukisoma heading yangu nauliza hivi ni sahihi kuendelea kusema tuna usalama wa taifa au tumetengeneza hatari nyingine kubwa zaidi. Nasema hivyo kwa sababu naliona hili ni joka lingine litakaloleta machafuko ndani ya nchi hii. Angalia matukio wanayohusishwa nayo kuya- engineer kila siku:
1) Kutuhumiwa kuvuruga chaguzi mbalimbali
2) Kutuhumiwa kufanya attempts mbalimbali za piga, kujeruhi na mara ingine vifo vyenye utata.
3) Kutuhumiwa kwenye wizi wa kiasi kikubwa cha fedha za wananchi
4) Kutuhumiwa ku- create matukio yanayo divert minds za watu na hivyo kuacha kujadili mijadala ya kitaifa mfano: kikombe cha babu nchi nzima.

Yote hayo kwa uchache tu ni kinyume na sheria ya uanzishwaji wa usalama wa Taifa inavyowataka kuenenda. Lakini watawala wanafanya yote haya kwa kupitia loophole ya usiri uliopo kwenye hiyo taasisi, wamesahau ya kuwa wanaongeza mpasuko uliopo. Haya yote yatakuja kuwarudi, wajiulize swali dogo sana - kwanini siri za serikali zinavuja? Jibu langu binafsi ni kwa sababu baadhi ya members wa TISS hawaridhishwi na ukiukwaji wa misingi ya Taasisi za usalama wa Taifa.

Kwa kumazia ndugu zangu, naombeni tuelezane ukweli....tutakuwa tunafanya makosa kusema hii ni taasisi hatarishi kwa usalama wa Taifa kutokana na mwenendo wa matukio ya sasa?


NB:
"Anayejimilikisha hati ya kutoa roho za wengine ajue nayeye hataishi milele ndani ya dunia hii iliyoumbwa na mwenyezi Mungu"
 
Sijakuelewa hapa mkuu..come again plz
Du mzee yaani hapo hujaelewa? Poa ni kwamba kama ulipitia stage zote hizo ukiwa TZ hutapata kitu zaidi ya kufa maskini na kupoteza muda wako ulioishi duniani.

Bora uzaliwe palestina ujue moja tu kwamba hakuna amani kuliko TZ kwenye amani ya kinafki.
 
CDM hawajajipanga namna ya kukabili ukiukwaji wa sheria za kuendesha bunge nje ya bunge.Ndani ya bunge tayari wananchi wanachanganywa tu. CDM Must do something very aggressive against this shit! Waache kucheza ngoma kama CCM.
Mipasho ya CCM inasaidia kununua muda bunge liishe bila kujadili na kuchukua hatua mambo ya msingi.CDM mpo bungeni miaka zaidi ya miwili sasa tunataka muwakabili CCM kwa namna yoyote ile hata ya kuwasusia bunge kuliko kuishia kupigizana kelele kama wao.

Enough is enough!

I agree with you, it seems CDM wamekuwa-ambushed na really they seem like surrendered.They must retreat and return to their normal standard we used to see them.Mnyika usikubali kutekwa nyara kama timu ya taifa Italy a.k.a Azzuri dhidi ya spain,mtapigwa mabao.Tadhali tundu lissu, Mbowe na wengine achaneni na hoizo propaganda za ccm.kUANZIA BAJETI itakyofuata tunawaomba sisi wananchi mrudi ktk mstari, tunahitaji mthibitisha kuwa you always deserve to be frontliners in critical issues.
 
Hii siyo mchango bali MATUSI KWA JAMII KUBWA YA WATZ ambao ndio walio wengi. Kama wewe umebahatika kupelekwa nje kifisadi au kwa kupewa ufadhili au msaada usije hapa ukatukana wenzako. Kuna waliozaliwa TZ, wakasoma TZ na kufanya kazi TZ wako vema mno hata kuliko waliokwenda huko usemako. Acha ushamba bwana mdogo!!!

Kwenye AMANI ya kinafki? Serikali inayouwa wananchi? Kule Mara kule songea? leo ya ulimboka? Na mengine ambayo huyajui?
Umefaidika nini na rasilimali zako? Dhahabu? Tanzanite?
Haujawahi sikia watu wanaingiza inchi kwenye mikataba hewa? EPA? Richmond? Kiwira?
Upo kaka?
 
Ushahidi Mhe. Mnyika atautoa tena mbaya zaidi sehemu ya ushahidi ni picha ya za video . Ushahidi huo utawaathiri wetu wengi sana wasiwasi wangu ni kwamba Mh Chogo Chemba awekewe ulinzi wa karibu sana maana aweza kujinyonga maana yeye ndio anajua zaidi ndani ya ushahidi huo ataonekena akijibinjua na mke wa kada mwenzake.
 
nimewahi kuandika hapa na leo narudia "SIKU HIZI SISOME TENA RIWAYA ZA AKINA JAMES HADLEY CHASE KN, KWA KUWA HABARI ZA BUNGE HASA WABUNGE WA CCM NI RIWAYA TOSHA" HUWEZI KUAMINNI MKUU WA MKOA KAMA MANYANYA ANSIMAMA BUNGENI NA KUDAI KUWA POLISI NI CCM NA NDO MAANA WALIMKAMATA ULIMBOKA KWA KUWA ETI CDM HUVAA MAGWANDA
 
Hoja ya Mh. Mnyika aka Mh. Washwa washwa iliishia wapi ? au ndio alikuwa anajitafutia umaarufu km kawaida yake?

Mbona waziri wenu washawasha hadi Kameroun kawaambia muwe huru.Hakuna kulala hadi M4C itwae madaraka ukitaka ndo hivyo ukikataa ndo hivyo.
 
Sijui kama wanchi wa singida kwenye jimbo la mgulu nchemba walimpigia kura huyu jamaa, huenda alishinda kwa kura za anavyojua yeye ,make angekuwa amepigiwa kura na wananchi asingekuwa anasimama na kujibizana mambo ya kipuuzi anaacha kuwakilisha vilio vya wapiga kura wake. Kama kuna mtu anajua vizuri jimbo la mgulu nchemba atujuze kwa ufasha waishivyo wananchi wake.
 
Mh. Mwigulu ni kiboko cha cdm kwa kweli, jamaa anawaendesha sana cdm anawapa mateso mabaya sana sana cdm bungeni

Hivi huyu jamaa alikuwa anaimbia kundi gani la taarabu vile? Mwiingizie Chemba sio jina geni masikioni mwangu! Ahhh naanza kuzeeka sijui kundi gani tena! Daaaaaaah!
 
Kwani wewe hujui siku hizi bongo movie zimehamia bungeni, hao wote ni wasanii. Wanapiga kelele na hakuna linaloendelea.

Kelele zao za kishabiki zaidi sasa ivi, na hizina tija kabisa
 
Back
Top Bottom