Bungeni Live: Juni 3, 2012 [Morning Session]

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,867
Mkasomali na Mnyika waomba mwongozo kufuatia mgogoro wa madaktari na uendeshwaji wa Bunge hapo jana

Mwenyekiti bi Jesta Mhagama awazima, Mnyika aomba mwongozo

Mh. Machali na Mnyika wameomba mwongozo kuhusu sakata la madaktari, kwamba imefika wakati sasa liruhusiwe kujadiliwa bungeni kwani serikali bado inafanya maamuzi kibabe wakati swala lipo mahakamani na Madaktari wanaendelea kugoma huku wananchi wakizidi kuathirika.

Pia Mh. Mnyika amelalamika kuwa jana Mwenyekiti aliwatolea kauli mbaya kwa Mbunge Machali na yeye yaliyokiuka kukiuka kanuni mbalimbali kwa kuwaambia kauli za matusi, maudhi na kashfa kufuatia kumwambia Mkasomali kwamba aache kimbelembele, anadandia hoja na anajitafutia umaarufu. Na kwa mnyika kuwa ameshindwa kujibu taarifa (kufatia hoja za Mwigulu ambazo sikubahatika kuzisikia) ambapo hajapewa nafasi ya kujibu na kuwa eti Mnyika anawashwa (kauli amabyo aliitafasiri kama ni tusi).

Majibu ya Mwenyekiti: Kuhusu sakata la madaktari hakutolea jibu lolote la maana, bali Mwenyekiti amemgeuzia kibao Machali na kusema yeye ndiye alivunja kanuni kwanza (hakutaja zipi), ila kuhusu Mnyika amesema atalijibu baadaye ama siku atakayoona inafaa.

Kama na mhimili huu utabaki kimya kwenye huu mgogoro wa madaktari na serikali, basi itabidi wananchi tutumie nguvu ya UMMA.
 
Mbunge wa Kisesa CCM anawashangaa takukuru na Pcb walio iba fedha BOT wanawajua mbona wako kimya?

Anadai hakuna Akounti inayofunguliwa nje ya nchi bila kujulikana na BOT
 
Mh. Machali na Mnyika wameomba mwongozo kuhusu sakata la madaktari, kwamba imefika wakati sasa liruhusiwe kujadiliwa bungeni kwani serikali bado inafanya maamuzi kibabe wakati swala lipo mahakamani na Madaktari wanaendelea kugoma huku wananchi wakizidi kuathirika.

Pia Mh. Mnyika amelalamika kuwa jana Mwenyekiti aliwatolea kauli mbaya kwa Mbunge Machali na yeye yaliyokiuka kukiuka kanuni mbalimbali kwa kuwaambia kauli za matusi, maudhi na kashfa kufuatia kumwambia Mkasomali kwamba aache kimbelembele, anadandia hoja na anajitafutia umaarufu. Na kwa mnyika kuwa ameshindwa kujibu taarifa (kufatia hoja za Mwigulu ambazo sikubahatika kuzisikia) ambapo hajapewa nafasi ya kujibu na kuwa eti Mnyika anawashwa (kauli amabyo aliitafasiri kama ni tusi).

Majibu ya Mwenyekiti: Kuhusu sakata la madaktari hakutolea jibu lolote la maana, bali Mwenyekiti amemgeuzia kibao Machali na kusema yeye ndiye alivunja kanuni kwanza (hakutaja zipi), ila kuhusu Mnyika amesema atalijibu baadaye ama siku atakayoona inafaa.

Kama na mhimili huu utabaki kimya kwenye huu mgogoro wa madaktari na serikali, basi itabidi wananchi tutumie nguvu ya UMMA.

ni Machali na si mkosamali aliyeambiwa jana anakieleele.
 
Hii nchi nadhani ilipata uhuru wa kujitawala prematurely, sitegemei wabunge kutumia muda mrefu kuzungumzia haya mambo sasa zaidi ya kujitikita kwenye kupitisha bajeti ya kutuletea unafuu wananchi.

Hawa CCM ni wanafiki sana hawa, wamepitisha bajeti yenye mapungufu mengi majuzi alafu wanakuja kuhoji vitu ambavyo wanajua hakuna aliyetayari kuyafanyia kazi.
 
Dawa yao ni kufufuwa lile kundi la wapiga nondo wa Mbeya sasa waamishiwe Dodoma, hakuna dawa nyingine kwa hawa magamba.
 
kwa hali ya sasa CCM hawana ujasiri wakuruhusu swala la madaktari likajadiliwa bungeni.
 
Mnyaa anawapasha kama serikali kuu ni wachafu aka wanzinzi, walevi je wanauwezo gani wa kuwakataza watoto (halmashauri) nae akifanya alifanyacho mkubwa aka serikali kuu?
 
Mwisho wa CCM umefika. Hawana tena ujasiri na weledi wa kujibu hoja kwa hoja, wamejikita kwenye matusi na kutoa tuhuma ambazo hata spika anashindwa kuwaambia wazithibitishe licha ya kutaka wapinzani wathibitishe hata kile ambacho hawajasema [mfano jana amemlazimisha Sugu athibitishe kitu ambacho hakukisema huku akimwacha Manyanya atoe tuhuma nzito bila kumlazimisha azithibitishe hata baada ya kuombwa afanye hivyo na wabunge wa upinzani]
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom