Bunge na ubinafsishaji wa Bandari ya Dar es Salaam, huu ni ufisadi mkubwa

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,830
21,460
Bunge letu ni taasisi na muhimili wa kidola usiopaswa kuegemea mihimili mingine ya kidola katika taifa.

Kwa nini Bunge la JMT lielekezwe kubariki badala ya kusimamia (dhibiti) na kutoa mwongozo (rule of procedure) kuhusu namna ya serikali kuingia mikataba kama huu wa TPA?

Wadau tunaamini Bunge halipaswi kuwa reduced to that level of a government department endorsing the latter's contracts deals already entered by parties.

We would rather have seen the parliament pushing for disclosure of the said contracts, not the contrary.

Kama mkataba haupo Bungeni/hadharani, Bunge linaridhia nini?

Pili, ni jambo la kushangaza kuona Tanzania inaendelea kuwa taifa lisilojifunza. Kama ilivyokuwa wakati wa ghiliba za ABSA kurubuni serikali (na watanzania kwa ujumla) kisha kupewa NBC (1997) bure, mtindo huu umejirudia miaka 26 baadaye, ukitumiwa na Falme (Emirate) ya Dubai ikishirikiana na Kampuni ya DP World (DPW) kuchukua mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) kwa njia ya kuingia Hati ya Makubaliano (Memorandum of Understanding/MoU).

Tujuavyo sisi, ni kwa njia hii ya MoU, kama ilivyokuwa kwa NBC, TPA inaondoka pasipo waarabu hawa kulipa hata senti moja.

Wengi wa watanzania waliolilia NBC, wakiongozwa na Mwl. Nyerere, wamekwishafariki, TPA italiliwa na nani yarabi?

Ushauri kwa Wabunge Utaalam na teknolojia ni variables zinazonunuliwa sokoni. Core economic value ya TPA ni proximity ya nchi (geoeconomic advantage) katika bahari ya Hindi na maziwa Makuu ya Afrika. Hiyo advantage ndio inaitofautisha Tanzania na nchi nyingine. Tukiisha kuipoteza thamani hii we are worthless.

Option bora ya kuimarisha ufanisi TPA inatakiwa kwanza, kubadirisha management recruitment approach ili key management positions zote zijazwe kwa kuzingatia vigezo vya umahiri na matokeo ya ushindani katika soko la kazi, bila kujali iwapo mtendaji mkuu na team yake ya menejimenti ni raia wa watanzania au wageni, provided wameshindana na kudhihirisha mahiri wa kusimamia uendeshaji wa kazi za TPA.

Pili, mfumo na muundo wa TPA uwekwe bayana kuwa CEO na team yake wawe na mamlaka ya kupendekeza, kwa mujibu wa sheria ya manunuzi, kununua na kutumia teknolojia na vifaa (machinery & equipment) vya kuendesha bandari kwa ufanisi pasipo kuingiliwa na mamlaka za serikali.

Aidha, kama serikali inaona kuna umuhimu wa kubinafsisha TPA basi iweke na kutangaza utaratibu wa kuuza hisa za TPA kwenye soko la mitaji la Dar es Salaam (DSE) - hata cross-floating of shares - ambapo serikali inaweza ku-retain 51% ya hisa, kisha 49% ya hisa za mtaji wa TPA zikawa floated through IPO.

We need transparency in the governance of our national assets, properties and resources not otherwise.
 
Serikali yetu imejaa wezi na wapigaji wa kila aina pale Bandari. Kama suala la NBC lilikuja na majibu tofauti na matarajio yetu sio kigezo cha kuwanyima hawa jamaa wa Dubai wakaendesha bandari yetu.

Huko USA bandari nyingi tu zinaendeshwa na makampuni ya kukodisha, sisi tuna kipi chenye kuwazidi hao wamarekani kiuchumi na katika suala zima la tija itakayopatikana hapo bandarini?.

Kama mleta mada hatumiwi bila ya kujijua basi hana uwezo wa kutazama hasara tunayopata kama Taifa kwa bandari kuendelea kuendeshwa na kundi la wapigaji.

Maana uhalisia ni kwamba wapigaji huwa wanabadilishwa kadri ya awamu mpya ya uongozi inapoingia madarakani, madudu ni yale yale ya miaka yote.
 
Nilikuwa na matumaini na huyu mama, lakini ni wazi kuwa hana uzalendo wowote.

Haiwezekani nchi ikawa inarudia makosa yaleyale.
Marehemu JPM alikuja na mkwara wa kuweka kamera pale bandarini na kutangaza makontena zaidi ya elfu moja yaliyopiita bila ya kulipiwa ushuru, hakuna kipya cha maana alichoweza kukibadilisha mpaka anaaga dunia.

SSH ameona utumbo wetu wa uendeshaji na hivyo ni maamuzi sahihi kuja kivingine kuliko kujitetea kwa kete ya uzalendo wakati tija hailingani na rasilimali iliyopo.
 
Kama Tanzania tutabinafsisha bandari wakati huu ambao imeongeza makusanyo, volume ya mizigo imeongezeka, trilioni za fedha tumekopa na zitalipwa na walipa Kodi basi tukubali Kwamba Mwenyenzi Mungu aishiye asipotuadhibu atawaadhibu watoto na wajukuu zetu Kwa kuwarejesha utumwani

TUMEUZA MIGODI NA MADINI YOTE
TUMEUZA MBUGA ZA WANYAMA
TUMEKOPA TRILIONS
TUMEUZA VISIWA
LEO TUNAUZA BANDAR

NA HAYA YOTE YANAFANYIKA BILA UWAZI WALA USHIRIKISHAJI WANANCHI

KULIKUWA NA UMUHIMU GANI MAHUFULI KUWEKEZA TRILIONS BANDARI
Nchi yangu Tanzania na chama cha mapinduzi hapa mmekosea
 
Hivi kweli kama tutakuwa na Taifa la watu wanaomba Kura Kwa ajili ya kuja kuuza rasilimali na kukopa kuna umuhimu gani wakusomesha Watanzania, kaama wanasoma kuja kupangisha na kukodisha Mali za wananchi Kwa mataifa yanayotafuta ajira sisi tunasoma Kwa ajili gani

TICS JUZI TUMEWAONDOA KWA MAMBO HAYAHAYA
 
Bunge letu ni taasisi na muhimili wa kidola usiopaswa kuegemea mihimili mingine ya kidola katika taifa.

Kwa nini Bunge la JMT lielekezwe kubariki badala ya kusimamia (dhibiti) na kutoa mwongozo (rule of procedure) kuhusu namna ya serikali kuingia mikataba kama huu wa TPA?

Wadau tunaamini Bunge halipaswi kuwa reduced to that level of a government department endorsing the latter's contracts deals already entered by parties.

We would rather have seen the parliament pushing for disclosure of the said contracts, not the contrary.

Kama mkataba haupo Bungeni/hadharani, Bunge linaridhia nini?

Pili, ni jambo la kushangaza kuona Tanzania inaendelea kuwa taifa lisilojifunza. Kama ilivyokuwa wakati wa ghiliba za ABSA kurubuni serikali (na watanzania kwa ujumla) kisha kupewa NBC (1997) bure, mtindo huu umejirudia miaka 26 baadaye, ukitumiwa na Falme (Emirate) ya Dubai ikishirikiana na Kampuni ya DP World (DPW) kuchukua mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) kwa njia ya kuingia Hati ya Makubaliano (Memorandum of Understanding/MoU).

Tujuavyo sisi, ni kwa njia hii ya MoU, kama ilivyokuwa kwa NBC, TPA inaondoka pasipo waarabu hawa kulipa hata senti moja.

Wengi wa watanzania waliolilia NBC, wakiongozwa na Mwl. Nyerere, wamekwishafariki, TPA italiliwa na nani yarabi?

Ushauri kwa Wabunge Utaalam na teknolojia ni variables zinazonunuliwa sokoni. Core economic value ya TPA ni proximity ya nchi (geoeconomic advantage) katika bahari ya Hindi na maziwa Makuu ya Afrika. Hiyo advantage ndio inaitofautisha Tanzania na nchi nyingine. Tukiisha kuipoteza thamani hii we are worthless.

Option bora ya kuimarisha ufanisi TPA inatakiwa kwanza, kubadirisha management recruitment approach ili key management positions zote zijazwe kwa kuzingatia vigezo vya umahiri na matokeo ya ushindani katika soko la kazi, bila kujali iwapo mtendaji mkuu na team yake ya menejimenti ni raia wa watanzania au wageni, provided wameshindana na kudhihirisha mahiri wa kusimamia uendeshaji wa kazi za TPA.

Pili, mfumo na muundo wa TPA uwekwe bayana kuwa CEO na team yake wawe na mamlaka ya kupendekeza, kwa mujibu wa sheria ya manunuzi, kununua na kutumia teknolojia na vifaa (machinery & equipment) vya kuendesha bandari kwa ufanisi pasipo kuingiliwa na mamlaka za serikali.

Aidha, kama serikali inaona kuna umuhimu wa kubinafsisha TPA basi iweke na kutangaza utaratibu wa kuuza hisa za TPA kwenye soko la mitaji la Dar es Salaam (DSE) - hata cross-floating of shares - ambapo serikali inaweza ku-retain 51% ya hisa, kisha 49% ya hisa za mtaji wa TPA zikawa floated through IPO.

We need transparency in the governance of our national assets, properties and resources not otherwise.
Sisi Watanzania hatuwezi kujisimamia wenyewe ni WEZI, WABINAFSI, ROHO MBAYA na TUNAPENDA MILOLONGO MIREFU BILA SABABU.

Dunia ya sasa inakwenda spidi sana na bandari ni sehemu muhimu sana ya kuharakisha maendeleo, sasa sisi tunafikiria kujinufaisha binafsi.

Mimi naunga mkono wazo la Serikali la kubinafsisha bandari.
 
Fx7FF43WIAE7fKF.jpg

Fx7FGgRX0AAZuy0.jpg
 
"Bunge kuwa reduced to that level of a government depaetment"

Ukweli ni kwamba, bunge letu hata sio kama department ya serikali, bunge letu ni chawa wa serikali, house boys and girls wa serikali.
Harafu tunashauri wee, utafikiri hatuoni. Tanzania ni peculiar country duniani, shida ni kutaka kufananisha ni kwingine hapo utafeli tu! Acha mambo yaende tu uzuri nchi haiwezi kufutika hata tuuze kila kitu ikiwamo ikulu, maisha yataenda tu
 
Hivi kweli kama tutakuwa na Taifa la watu wanaomba Kura Kwa ajili ya kuja kuuza rasilimali na kukopa kuna umuhimu gani wakusomesha Watanzania, kaama wanasoma kuja kupangisha na kukodisha Mali za wananchi Kwa mataifa yanayotafuta ajira sisi tunasoma Kwa ajili gani

TICS JUZI TUMEWAONDOA KWA MAMBO HAYAHAYA

Unakosea uongozi wa kisiasa duniani kote kwa sasa hauombwi ni ulaghai na viini macho vya kuonesha sijui ni mchakato wa kidemokrasia.

Dunia ya leo unanunuliwa kwa rushwa amakuchuliwa kwa nguvu kwa kitumia majeshi au hayo majeshi yakijitambua na yakichoka kutumiwa na wanasiasa hujichukulia wakawa wao ndio watawala.
 
Sisi Watanzania hatuwezi kujisimamia wenyewe ni WEZI, WABINAFSI, ROHO MBAYA na TUNAPENDA MILOLONGO MIREFU BILA SABABU.

Dunia ya sasa inakwenda spidi sana na bandari ni sehemu muhimu sana ya kuharakisha maendeleo, sasa sisi tunafikiria kujinufaisha binafsi.

Mimi naunga mkono wazo la Serikali la kubinafsisha bandari.
Kibaya zaidi dunia ya sasa haimsubiri mtu, ni juhudi za mtu mwenyewe zinazokwenda kumuwezesha akawa sehemu ya dunia pana.
 
Back
Top Bottom