Bunge Litii Mahakama; Lisipotii Nani Aitii Basi?

Bunge Litii Mahakama; Lisipotii Nani Aitii Basi?

Kwamba kuna taarifa kuwa Mahakama Kuu imeweka zuio (injunction) ya kuzuia Bunge kujadili suala la escrow kwa sababu kuna watu wameenda mbele ya mahakama kutafuta 'relief' fulani ni taarifa ambazo zilitarajiwa na zimekuwa zikinong'onwa kwa siku kadhaa sasa wakati taifa linasubiria mjadala huo Bungeni. Tukikubali kuwa Mahakama imetoa zuio hilo basi swali ni je Bunge linatakiwa kutii au lisitii?

Kuna watu ambao wanaamini mjadala huu ni lazima uendelee kwa sababu Bunge linafanya kazi zake "bila kuingiliwa". Lakini pia tunafahamu kwenye masuala ya haki Mahakama nayo inatakiwa kufanya kazi zake "bila kuingiliwa". Je, hili lina maana pande hizi mbili zinaweza kujikuta kwenye stalemate (kukodoleana) hadi mmoja wao apepese macho?

Naomba kupendekeza kuwa katika masuala ya kutafuta haki Mahakama na maamuzi yake yako juu ya mtu yeyote; yako juu ya Bunge na hata juu ya Ikulu. Mahakama inapotoa uamuzi fulani uamuzi huo unatakiwa kutiiwa na wanaohusika. Kwamba sasa Bunge linataka kuendelea na mjadala wakati Mahakama imetoa zuio halali siyo tu ni kutengeneza mwelekeo mbaya (bad precedence) lakini pia utatuletea matatizo huko mbeleni pale ambapo ama Ikulu au watendaji wengine watakapoamua kupuuzia maamuzi ya mahakama kwa sababu hawayapendi au wanaona yanawazuia kupata manufaa fulani ya kisiasa.

Ni kwa sababu hii naamini Bunge litatambua hatari waliyo nayo kwa kutokutii amri ya mahakama. Mahakama haina majeshi na wala haina polisi lakini kama maamuzi yake hayawezi kutiiwa na watu ambao walitunga sheria nani basi ataweza kuyatii maamuzi ya mahakama? Kinachosikitisha ni kuwa hata baadhi ya watu ambao wanatarajiwa kuwa watetezi wa utawala wa sheria wanaonekana kukubali kutokutii huku kwa Bunge. Hii ni hatari.

Hata mwizi ana haki ya kwenda mbele ya mahakama kutafuta msaada; mafisadi na wezi wa mali za umma nao wana haki hiyo hiyo. Ni jukumu la wanaodai kuthibitisha madai yao. Na kwa vile serikali yetu kwa makusudi au kwa bahati mbaya hadi hivi sasa haijaanzisha uchunguzi wa kihalifu (criminal investigation) kuhusiana na escrow na kwa vile jukumu hilo linamuangukia DPP ambaye ofisi yake amekuwa dhaifu mara zote linapokuja suala la ufisadi basi wezi wetu wanapoenda mbele ya mahakama na kutumia mchakato wa mahakama kujilinda hatuwezi kuwakatalia ati kwa vile hatuwwapendi au tunaamini wanatumia mahakama vibaya. Ndio uzuri wa nchi ya kidemokrasia hata wezi wakikimbilia polisi lazima walindwe!

Hivyo basi, nasihi Bunge litii mahakama kwani kama halitotii hakuna mtu mwingine Tanzania ambaye atatakiwa kutii mahakama hasa kama inachukua uamuzi ambayo mtu huyo haupendi.

Kitu pekee ambacho Bunge linaweza kufanya na ninaamini ndio njia pekee ya kutokugongana na mahakama ni

a. Kuahirisha mjadala huo wa escrow
b. Mara moja kutuma wanasheria wake kutaka wasikilizwe ili kuondoa zuio hilo na hata ikibi kulikatia rufaa chini ya certificate of emergency ili lisikilizwe mara moja na kutolewa uamuzi kwani linahusiana na maslahi makubwa ya taifa.
c. Na kutii uamuzi utakaotolewa.
d. Kama Bunge kweli linataka kujadili mada hizi na kuwa na uwezo wa kuzuia masuala ya ufisadi lingengalia sheria zake ilizotunga ambazo baadhi yetu tunaamini ndio chanzo cha ufisadi. Hadi leo hii hawajafanyia mabadiliko sheria ya usalama wa taifa, bado hawajafanya mabadiliko sheria ya DPP na hata CAG mwenyewe na badala yake tunazunguka kwenye sheria zile zile mbovu. Binafsi ningeona la maana kama wabunge wangekaa kujadili kwa uhuru suala la udhaifu wa usalama wa taifa na haja ya mabadiliko kuliko kujadili kitu ambacho tayari tunajua nini kimetokea ila wapo baadhi ya watu wanaotafuta njia ya kutokea kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu. Usalama wa taifa kwangu ndio tatizo kubwa zaidi la kukabiliana na ufisadi nchini kuliko kitu kingine chochote.

Tusikubali Bunge nalo lijiinue dhidi ya mahakama, maana tukikubali basi mahakama zetu zitakuwa zimedhoofishwa kwa madhara makubwa sana katika suala la haki.

Kwa upande wa serikali tungetarajia hadi hivi sasa tayari uchunguzi wa kihalifu ungekuwa umeanza kufanyika badala ya kuacha uchunguzi wa kibunge (parliamentary inquiry) uliofanywa na Kamati ya PAC chini ya Zitto. Kama uchunguzi huu ungekuwa umeanza hata akaunti zinazodaiwa kugawiwa fedha zingewekwa chini ya ulinzi ili zisitoe fedha na wamiliki wake kuhojiwa. Na hata hili lingeweza kutumika kuzuia mjadala wa kisiasa Bungeni.
hakuna kafara escrow akaunt. Tusiwaingize watu wasio na hatia. Bora lisijadiliwe
 
Mwanakijiji unatumwa unatumika, sisi tunajua kuwa suala hilo ni la kibunge na mahakama haina haki ya kuzuia bunge kujadili suala ambalo bunge limekwishaanza kulijadili kufanya hivyo ni wazi mahakama inaliingilia bunge kinyume na maumbile ya katiba. Tatu suala hilo lina maslahi mapana ya kitaifa, yaani haki ya mtu mmoja haiwezi kuzuia haki za umma, nne pesa nyingi imetumika kutekeleza maagizo ya bunge kufanya uchunguzi, tano Mahakama inahusika na kesi hiyo, kwanini inataka kuwa hakimu wa kesi inayowahusu???

ZAIDI ya yote bunge ni kwa niaba ya wananchi, ambao ndo chanzo cha mamlaka yote.

Naona kama wanataka kutumia mwanya huo kufanya bunge lijadili juujuu ili PINDA apete, na hapo hapo bunge/makinda waseme wako serious sana ndo maana wametupilia mbali amri ya mahakama, win win situation.
 
mwanakijiji bwana, ulizama kijijini siku nyingi kuibuka umeibuka na haya.

au na ww kwenye ile payrol umo?
 
That's the only solution.

I smelt a rat from the day one when I saw people engineering this are the ones who has failed to join hands with those who were opposing CCM's hijack of Warioba's constitutional report. To me escrow and I concur with judge Warioba has said today is tip in the iceberg. Just imagine Katiba which is a supreme law the country when constitutional assembly was ongoing characterized by insults and abuses I expected to see those who claim to be patriotic to distance themselves and demonstrate their patriotism to mama Tanzania. Lakini wapi they were always seated in the bunge and pocketing 300k per day. These are the ones who could have set president by telling Sita that look what you doing is taking us astray. But now they speaking at the apex of their voices. They are not even talking issues but people. They are not even telling us if the due process was violated. No, they are talking about people. They don't even bother to talk how a system can be put in place which will see local investors protected against malicious investors the likes of Mechmar. They have just personalized escrow issue. I do not have a vocabulary to explain such a behaviour
 
Watawala siku zote huwa wako blind, hawazionagi warning signs kwa sababu wanajuaga tu "everything is gona be alright". Wakati Ghadafi anatoa yale mahotuba makali makali na kuwaita mende wale wanaompinga, alikuwa akijua kabisa kuwa yuko salama!!! Sisi tutaendelea kukenua meno bila kujua kuwa nchi hii si ile tuliyoizoea .... ni nchi yenye resource muhimu sana.
 
Mzee Mwanakijiji acha mahakama nayo idhoofishwe tu ili umuhimu wa kuifumua na kuisuka upya uonekane. Kwa sasa hatuna mahakama tuna genge la wezi ktk mhimili wa mahakama pia na ndio maana ktk list ya waliopewa pesa majaji wapo pia. By the way wee bado unategemea kupata haki yako mahakamani? watu siku hizi wanapata kwa kupitia vyombo vya habari. Hata ESCROW ni matokeo ya vyombo vya habari, Ms. Tanzania halisi kapata haki yake aliyokuwa ameporwa na Ms. Lundenga kwa presha ya media.
 
Mwanakijiji you must be kidding. Kwani mahakama inaogopa nini report ikijadiliwa wahusika wachukuliwe hatua maana hata kama wataresign itawazuia kupelekwa mahakamani,..
 
Hii amri ina mkono wa Kikwete mwenyewe kutoka US, anajua fika kuwa Mtoto wake Miraj Kikwete ndio mwenye Simba Trust ya Australia, so mwisho wa siku ishu ikijadiliwa na watu kuwajibishwa kuna wengine wataamua kumwaga ugali na kumtaja Miraj Kikwete, hivyo hii amri ya mahakama ina mkono wa tezi dume toka US. Pia ieleweke Kikwete yuko US, Mwanakijiji yuko US, upo uwezekano wa kumtuma kupima upepo hapa....

Usimsakisizie Rais mwache apone huko alipo. Hili swala limeghubikwa na unafiki mtupu. Kama leo ulimsikiliza Mzee Warioba ni kuwa we had God given opportunity kutafuta dawa kwa kuweka kwenye katiba mambo ambayo rasmu ya pili ya Warioba iliyapendekeza lakini kwa ushabiki na unafiki wa wabunge wa CCM we left that opportunity slip off the window kwa kumwacha Sita na wenziwe kubaka rasmu na kujitengenezea mambo yao. Leo waliokataa rasmu yenye maadili eti leo wanaungana na wapinzani kwenye escrow.Afadhali mahakama imesitisha maana hakuna maslahi ya taifa bali ya wachache kisiasa
 
Hivi, Bunge likiamuru Mahakama isisikilize kesi kwani wako kwenye mchakato wa kutunga sheria itakayogusa hiyo kesi; Mahakama ingekubali huo ujinga?
 
Mahakama inatakiwa itulize KITENESI make huu muziki ni mzito wanatakiwa wenye akiri zao wauchambue kwanza na kila kitu kiwe wazi.
 
Alooo si bure huyu mzee wa kijiji asha kula mlungula!
 
Demokrasia ya kiriberali inaleta matatizo kuliko faraja katika nchi masikini hasa nchi za kiafrika. Demokrasia imekuwa ndio mrija mkuu wa kutunyonya. Demokrasia na mtoto wake utawala wa sheria ndio vimekuwa nyundo ya kumkandamiza mnyonge. Mnyonge awe mtu, nchi ilmradi ashindane tu na mwenye nguvu. Masikini katika demokrasia hana haki mbele ya mwenye pesa hata iwaje chini ya demokrasia, taifa masikini halina chake mbele ya taifa tajiri linapokuja ya haki sawa. Halikadhalika hapa nchini mwetu wenye fedha ndio wenye haki, wenye kushinda uchaguzi, wenye kuweka court injuction, wenye kusamehewa makosa ya mauaji na DPP ndani ya wiki moja. Demokrsia, mihilimili, sijui na nini vilee vyote hivyo ni ugandamizaji wa mtu masikini kwa kufuata sheria. Lazima hili liwe na mwisho, tuachane na meneno haya yasiyokuwa na faida kwetu, maneno yanayotufanya tuwe dhalili kila siku. China, Malaysia, Korea kaskazini ziliamua kuachana na mazingaombwe haya na wakasonga mbele. Wakati umefika watanzania wenye kuipenda kuiona nchi yao inabaki waseme basi inatosha.
 
Kwa hiyo ukiangalia kipengele hicho hao majaji hawajakijua? Na kama wamekijua rationale yao ni ipi?

Kuna mtu ana maandishi ya kutoka mahakamani yanayoelezea vizuri mahakama imesemaje?

Isije kuwa kinachosemwa kimesemwa na mahakama ni tofauti na mahakama ilichosema, muandishi mmoja kajanja kapindisha maneno na wote tunaingia mkumbo.

Halafu katiba ya Tanzania nayo haieleweki, haichelewi kutoa kwa mkono mmoja na kuchukua haki ile ile kwa mkono mwingine. Inabidi kuangalia habari za independence of the judiciary zinaingiaje hapo? Mahakama ikisikiliza kesi na kusema habari fulani zisitolewe kwa sababu ni nyeti katika kesi hii, na bunge likasema habari hizi zitolewe kwa sababu zinatakiwa katika mjadala wa bunge, hapo patakuwaje?

Constitutional crisis?

CC EMT

Mkubwa nchi ipo kama vile ndege inayojiendesha bila rubani, tegemea lolote!Kama vifungu ambavyo mimi na wewe ambao sio wanasheria tunavisoma na kuvielewa tena viko wazi namna hii havionwi na wanasheria unategemea kitu gani?
 
Nimefurai sana baada yakusikia kwenye taarifa ya habari SAA 2 ucku kwamba muheshimiwa Anna makinda amesema bunge halitaingiliwa kufanya kazi zake.
Hivyo ripoti itagaiwa kwa wabunge wote ili waisome tayari kwa kuijadili.
 
Back
Top Bottom