Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 21,755
- 57,215
MAHAKAMA KUU MUSOMA YAMWACHIA GEORGE MAPULI BUKINGI:
Mahakama kuu ya Tanzania, masijala ya Musoma imekubali rufaa ya George Mapuli Bukingi aliyetiwa hatiani na mahakama ya wilaya ya Bunda.
George Bukingi ni miongoni mwa vijana walioshitakiwa kutokana na vurugu za October 29, 2026 na kupewa kesi ya uhaini na baadaye ikabadilishwa na akashitakiwa kwa kosa la kumjeruhi Askari Polisi.
Mahakama ya wilaya ya Bunda ilimhukumu Bukingi kifungo cha miaka 5, ikidai kwamva Mahakama iliridhika na ushahidi uliotolewa wakati wa usikilizwaji wa kesi .
Hata hivyo, mawakili wa CHADEMA hawakuridhika na uamuzi wa Mahakama ya wilaya Bunda na wakaamua kukata rufaa Mahakama kuu - Musoma. Leo Mahakama kuu masijala ya Musoma, Mhe Jaji Kakolaki ametoa uamuzi.
Katika uamuzi wake, Mhe Jaji Kakolaki amekubali hoja za warufani kwamba ushahidi haukijitosheleza kumtia hatiani na hivyo mahakama imemuachia rasmi leo.
Kuachiwa kwa Bukingi, kumefanya watuhumiwa wote 30 walioshitakiwa kwa makosa ya uchaguzi wa october 29, Wilayani Bunda kuwa huru.
Nawashukuru mawakili Alex Massaba na Aloyce Kajitamusi kwa kuwa sehemu ya kutetea haki ya George Mapuli.
Asanteni Bunda kwa ushirikiano kwa kipindi chote cha kushughulika na kesi ya Kaunya nanwenzake 29.