Bunge Litii Mahakama; Lisipotii Nani Aitii Basi?

Mzee mwanakijiji mahakama inatakiwa kuzingatia katiba na sheria katika kutoa haki. Lakini pia haki inatakiwa ionekane ikitolewa hata kwa mchakato wake. Haiwezekeni mchakato uonekane unatoa haki kwa upendeleo na bado mahakama iweze kupewa heshima yake. Ikitokea amri ya mahakama imedharauliwa ni kwa matendo ya mahakama yenyewe. Je kuna kesi ngapi zimekaa miaka na miaka zinahitaji maamuzi lakini hazisikilizwi, iweje hii inapelekwa asubuhi na ndani ya masaa matano imetolewa maamuzi? Je hao IPTL wana haki kuliko hawanga wengine waliowekwa benchi kwa miaka? Pili, hii mahakama imeonyesha double standard kwa suala linalofanana na hili hili. Utakumbuka ombi kama hili lilifunguliwa ili kusimamisha mjadala wa katiba mpya, lilitupiliwa mbali na kesi ya msingi pia ilitupiliwa mbali. Sasa kwa mtazamo huu mahakama ndio inataka yenyewe kudharauliwa. Na hapa ndo tunaanza kuona kilio chetu cha mda mrefu cha kwanini majaji wanateuliwa na mkuu wa mhimili mwingine ambaye ni Rais. Hapa tunaiona loyalty ya Judiciary (majaji) kwa serikali hasa rais maana ndio mamlaka yake ya uteuzi. Katika kashfa hii serikali inafanya mbinu zote kupigana isianguke na inawatumia wote walio loyal kwake hii isitokee. Mie nasema Bunge liendelee na mjadala wa report hii na IWE FUNDISHO KWA COMPETENT PEOPLE NDANI YA JUDICIARY KUSIMAMA NA KUWAKEMEA WANAOUDHARAULISHA MHIMILI WAO.
 
Kwamba kuna taarifa kuwa Mahakama Kuu imeweka zuio (injunction) ya kuzuia Bunge kujadili suala la escrow kwa sababu kuna watu wameenda mbele ya mahakama kutafuta 'relief' fulani ni taarifa ambazo zilitarajiwa na zimekuwa zikinong'onwa kwa siku kadhaa sasa wakati taifa linasubiria mjadala huo Bungeni. Tukikubali kuwa Mahakama imetoa zuio hilo basi swali ni je Bunge linatakiwa kutii au lisitii?

Kuna watu ambao wanaamini mjadala huu ni lazima uendelee kwa sababu Bunge linafanya kazi zake "bila kuingiliwa". Lakini pia tunafahamu kwenye masuala ya haki Mahakama nayo inatakiwa kufanya kazi zake "bila kuingiliwa". Je, hili lina maana pande hizi mbili zinaweza kujikuta kwenye stalemate (kukodoleana) hadi mmoja wao apepese macho?

Naomba kupendekeza kuwa katika masuala ya kutafuta haki Mahakama na maamuzi yake yako juu ya mtu yeyote; yako juu ya Bunge na hata juu ya Ikulu. Mahakama inapotoa uamuzi fulani uamuzi huo unatakiwa kutiiwa na wanaohusika. Kwamba sasa Bunge linataka kuendelea na mjadala wakati Mahakama imetoa zuio halali siyo tu ni kutengeneza mwelekeo mbaya (bad precedence) lakini pia utatuletea matatizo huko mbeleni pale ambapo ama Ikulu au watendaji wengine watakapoamua kupuuzia maamuzi ya mahakama kwa sababu hawayapendi au wanaona yanawazuia kupata manufaa fulani ya kisiasa.

Ni kwa sababu hii naamini Bunge litatambua hatari waliyo nayo kwa kutokutii amri ya mahakama. Mahakama haina majeshi na wala haina polisi lakini kama maamuzi yake hayawezi kutiiwa na watu ambao walitunga sheria nani basi ataweza kuyatii maamuzi ya mahakama? Kinachosikitisha ni kuwa hata baadhi ya watu ambao wanatarajiwa kuwa watetezi wa utawala wa sheria wanaonekana kukubali kutokutii huku kwa Bunge. Hii ni hatari.

Hata mwizi ana haki ya kwenda mbele ya mahakama kutafuta msaada; mafisadi na wezi wa mali za umma nao wana haki hiyo hiyo. Ni jukumu la wanaodai kuthibitisha madai yao. Na kwa vile serikali yetu kwa makusudi au kwa bahati mbaya hadi hivi sasa haijaanzisha uchunguzi wa kihalifu (criminal investigation) kuhusiana na escrow na kwa vile jukumu hilo linamuangukia DPP ambaye ofisi yake amekuwa dhaifu mara zote linapokuja suala la ufisadi basi wezi wetu wanapoenda mbele ya mahakama na kutumia mchakato wa mahakama kujilinda hatuwezi kuwakatalia ati kwa vile hatuwwapendi au tunaamini wanatumia mahakama vibaya. Ndio uzuri wa nchi ya kidemokrasia hata wezi wakikimbilia polisi lazima walindwe!

Hivyo basi, nasihi Bunge litii mahakama kwani kama halitotii hakuna mtu mwingine Tanzania ambaye atatakiwa kutii mahakama hasa kama inachukua uamuzi ambayo mtu huyo haupendi.

Kitu pekee ambacho Bunge linaweza kufanya na ninaamini ndio njia pekee ya kutokugongana na mahakama ni

a. Kuahirisha mjadala huo wa escrow
b. Mara moja kutuma wanasheria wake kutaka wasikilizwe ili kuondoa zuio hilo na hata ikibi kulikatia rufaa chini ya certificate of emergency ili lisikilizwe mara moja na kutolewa uamuzi kwani linahusiana na maslahi makubwa ya taifa.
c. Na kutii uamuzi utakaotolewa.
d. Kama Bunge kweli linataka kujadili mada hizi na kuwa na uwezo wa kuzuia masuala ya ufisadi lingengalia sheria zake ilizotunga ambazo baadhi yetu tunaamini ndio chanzo cha ufisadi. Hadi leo hii hawajafanyia mabadiliko sheria ya usalama wa taifa, bado hawajafanya mabadiliko sheria ya DPP na hata CAG mwenyewe na badala yake tunazunguka kwenye sheria zile zile mbovu. Binafsi ningeona la maana kama wabunge wangekaa kujadili kwa uhuru suala la udhaifu wa usalama wa taifa na haja ya mabadiliko kuliko kujadili kitu ambacho tayari tunajua nini kimetokea ila wapo baadhi ya watu wanaotafuta njia ya kutokea kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu. Usalama wa taifa kwangu ndio tatizo kubwa zaidi la kukabiliana na ufisadi nchini kuliko kitu kingine chochote.

Tusikubali Bunge nalo lijiinue dhidi ya mahakama, maana tukikubali basi mahakama zetu zitakuwa zimedhoofishwa kwa madhara makubwa sana katika suala la haki.

Kwa upande wa serikali tungetarajia hadi hivi sasa tayari uchunguzi wa kihalifu ungekuwa umeanza kufanyika badala ya kuacha uchunguzi wa kibunge (parliamentary inquiry) uliofanywa na Kamati ya PAC chini ya Zitto. Kama uchunguzi huu ungekuwa umeanza hata akaunti zinazodaiwa kugawiwa fedha zingewekwa chini ya ulinzi ili zisitoe fedha na wamiliki wake kuhojiwa. Na hata hili lingeweza kutumika kuzuia mjadala wa kisiasa Bungeni.
Mahakama kuu ilishatoa uamuzi kwamba jengo lile ambalo limejengwa karibu na ikulu livunjwe zibaki ghorofa ambazo zinakubalika pale kisheria. Uamuazi huu wa mahakama umepuuzwa!
 
Leo kwa mara ya kwanza nakubali hoja ya huyu anaejiita Mzee Mwanakijiji na hii pia inanifanya niamini kuwa Mbowe ana mkono katika hilo zuio linalosemekana.

Wewe ni wa kupuuzwa tu,tunataka mjadala ufanyike kesho na si hizi brabra zenu nyie wapambe wa wezi!
 
Last edited by a moderator:
Mzee Mwanakijiji,
Sina maelezo marefu zaidi ya kusema tu kwamba, uhuru wako unaishia kwenye pua ya mwenzako! Uhuru wa Mahakama ni LAZIMA uishie kwenye geti la jengo la bunge kama ambavyo uliishia getini siku waliposema Mahakama haina uwezo wa kuzuia Bunge Maalum la Katiba!

Hatuwezi kuendelea na huu uhuni unaoongezeka hivi sasa Tanzania ambapo wahalifu wamekuwa na silika ya kukimbilia mahakamani kuweka court injuction... huu ni uhuni!
 
Last edited by a moderator:
Kumbe hili jamaa nalo huwa inatokea siku moja moja linaandika uharo? Yaani mahakama iwe juu ya Bunge kwenye maswala yanayogusa maslahi ya Taifa? No way!! Au kwa jile umeona Mjita mwenzio kawekwa kibano ndo unataka yaishe kimya kimya ili apumue? Haiwezekani, kwa ustaarabu mahakama ilipaswa kulitupa hilo pingamizi la hao mafisadi kwa vile tayari kitu kiko kwenye mhimili mwingine!!

Umechemkaaaaaaa!!
 
Wanaoendeshwa na mihemko watampinga MWANAKIJIJI.ila ninaamini yuko sahihi 100%.
kinachonisikitisha, hawa mafisadi wamekuwa very smart to the extent that mihimili yetu inaingia kwenye msigano mkubwa. Ukweli ulio wazi ni kwamba MAHAKAMA NI CHOMBO PEKEE CHA KUTOA HAKI NA KINAFANYA SHUGHULI ZAKE KWA KUTUMIA SHERIA ZINAZOTUNGWA NA BUNGE.... hivyo basi, BUNGE KAMA CHOMBO CHA KUTUNGA SHERIA, KINATAKIWA KUWA MFANO HALISI WA JINSI YA KUTII AMRI ZA MAHAKAMA.
kwa mihemko ya wabunge na wadau, haya yote yanaweza yasionekane kama ni muhimu, lakini yataweka rekodi mbaya sana katika UTII WA HUKUMU ZA MAHAKAMA.
lakini pamoja na huu ukweli mchungu, bado kuna haja ya bunge kuonyesha nguvu zake haswa katika mambo yenye maslahi ya usalama wa taifa.
 
Kwamba kuna taarifa kuwa Mahakama Kuu imeweka zuio (injunction) ya kuzuia Bunge kujadili suala la escrow kwa sababu kuna watu wameenda mbele ya mahakama kutafuta 'relief' fulani ni taarifa ambazo zilitarajiwa na zimekuwa zikinong'onwa kwa siku kadhaa sasa wakati taifa linasubiria mjadala huo Bungeni. Tukikubali kuwa Mahakama imetoa zuio hilo basi swali ni je Bunge linatakiwa kutii au lisitii?

Kuna watu ambao wanaamini mjadala huu ni lazima uendelee kwa sababu Bunge linafanya kazi zake "bila kuingiliwa". Lakini pia tunafahamu kwenye masuala ya haki Mahakama nayo inatakiwa kufanya kazi zake "bila kuingiliwa". Je, hili lina maana pande hizi mbili zinaweza kujikuta kwenye stalemate (kukodoleana) hadi mmoja wao apepese macho?

Naomba kupendekeza kuwa katika masuala ya kutafuta haki Mahakama na maamuzi yake yako juu ya mtu yeyote; yako juu ya Bunge na hata juu ya Ikulu. Mahakama inapotoa uamuzi fulani uamuzi huo unatakiwa kutiiwa na wanaohusika. Kwamba sasa Bunge linataka kuendelea na mjadala wakati Mahakama imetoa zuio halali siyo tu ni kutengeneza mwelekeo mbaya (bad precedence) lakini pia utatuletea matatizo huko mbeleni pale ambapo ama Ikulu au watendaji wengine watakapoamua kupuuzia maamuzi ya mahakama kwa sababu hawayapendi au wanaona yanawazuia kupata manufaa fulani ya kisiasa.

Ni kwa sababu hii naamini Bunge litatambua hatari waliyo nayo kwa kutokutii amri ya mahakama. Mahakama haina majeshi na wala haina polisi lakini kama maamuzi yake hayawezi kutiiwa na watu ambao walitunga sheria nani basi ataweza kuyatii maamuzi ya mahakama? Kinachosikitisha ni kuwa hata baadhi ya watu ambao wanatarajiwa kuwa watetezi wa utawala wa sheria wanaonekana kukubali kutokutii huku kwa Bunge. Hii ni hatari.

Hata mwizi ana haki ya kwenda mbele ya mahakama kutafuta msaada; mafisadi na wezi wa mali za umma nao wana haki hiyo hiyo. Ni jukumu la wanaodai kuthibitisha madai yao. Na kwa vile serikali yetu kwa makusudi au kwa bahati mbaya hadi hivi sasa haijaanzisha uchunguzi wa kihalifu (criminal investigation) kuhusiana na escrow na kwa vile jukumu hilo linamuangukia DPP ambaye ofisi yake amekuwa dhaifu mara zote linapokuja suala la ufisadi basi wezi wetu wanapoenda mbele ya mahakama na kutumia mchakato wa mahakama kujilinda hatuwezi kuwakatalia ati kwa vile hatuwwapendi au tunaamini wanatumia mahakama vibaya. Ndio uzuri wa nchi ya kidemokrasia hata wezi wakikimbilia polisi lazima walindwe!

Hivyo basi, nasihi Bunge litii mahakama kwani kama halitotii hakuna mtu mwingine Tanzania ambaye atatakiwa kutii mahakama hasa kama inachukua uamuzi ambayo mtu huyo haupendi.

Kitu pekee ambacho Bunge linaweza kufanya na ninaamini ndio njia pekee ya kutokugongana na mahakama ni

a. Kuahirisha mjadala huo wa escrow
b. Mara moja kutuma wanasheria wake kutaka wasikilizwe ili kuondoa zuio hilo na hata ikibi kulikatia rufaa chini ya certificate of emergency ili lisikilizwe mara moja na kutolewa uamuzi kwani linahusiana na maslahi makubwa ya taifa.
c. Na kutii uamuzi utakaotolewa.
d. Kama Bunge kweli linataka kujadili mada hizi na kuwa na uwezo wa kuzuia masuala ya ufisadi lingengalia sheria zake ilizotunga ambazo baadhi yetu tunaamini ndio chanzo cha ufisadi. Hadi leo hii hawajafanyia mabadiliko sheria ya usalama wa taifa, bado hawajafanya mabadiliko sheria ya DPP na hata CAG mwenyewe na badala yake tunazunguka kwenye sheria zile zile mbovu. Binafsi ningeona la maana kama wabunge wangekaa kujadili kwa uhuru suala la udhaifu wa usalama wa taifa na haja ya mabadiliko kuliko kujadili kitu ambacho tayari tunajua nini kimetokea ila wapo baadhi ya watu wanaotafuta njia ya kutokea kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu. Usalama wa taifa kwangu ndio tatizo kubwa zaidi la kukabiliana na ufisadi nchini kuliko kitu kingine chochote.

Tusikubali Bunge nalo lijiinue dhidi ya mahakama, maana tukikubali basi mahakama zetu zitakuwa zimedhoofishwa kwa madhara makubwa sana katika suala la haki.

Kwa upande wa serikali tungetarajia hadi hivi sasa tayari uchunguzi wa kihalifu ungekuwa umeanza kufanyika badala ya kuacha uchunguzi wa kibunge (parliamentary inquiry) uliofanywa na Kamati ya PAC chini ya Zitto. Kama uchunguzi huu ungekuwa umeanza hata akaunti zinazodaiwa kugawiwa fedha zingewekwa chini ya ulinzi ili zisitoe fedha na wamiliki wake kuhojiwa. Na hata hili lingeweza kutumika kuzuia mjadala wa kisiasa Bungeni.

Mzee Mwanakijiji BUNGE ni Chombo huru cha kutunga na kufuta SHERIA ZA NCHI; MAHAKAMA ni CHOMBO HURU cha kutekeleza SHERIA ZA NCHI -- Hakuna MKUBWA KATI ya hivyo vyombo isipokuwa RAIS wa NCHI kwa KATIBA YA SASA YA TANZANIA

Kwahiyo Vyombo hivyo havishindani au kupeana UONGOZI WA MASUALA YA NCHI....

Kwahiyo ISSUE NI DRAW kama BUNGE PIA IMEIPATA HIYO ISSUE WATAIJADILI Mahakama haiko MBELE YA BUNGE
 
Mwanakijiji unamaanisha una sympathize na Mahakama au ndo kutupa somo pana madhara ya mihimili hii mikuu ya dola kusigana na hatimaye sasa KUDHARAULIANA Kwa masilahii binafsi????

Mtu mzima kalambishwa asali leo anasomeka kiarabu. Huwezi kuamini kama hii imetoka kwa mtu ambae siku zote ana advocate haki na wajibu kwa wananchi. Unacheza na pesa wewe! Mwanakijiji Kwisha habari yake! Ndembendembe mbele ya pesa ya Escrow account
 
Majaji wengi Kanjanja, ni wale ambao Mh. Tundu Lissu alisema hawajui vizuri kingeleza ndio mana tafsiri nyingi wanakosea na wajanja wanawapiga changa la macho. Katika mahamuzi ya kesi hii majaji wanatafuta jinsi ya kujilinda ikibainika kuwa walipindisha sheria ili fungu hili lililokosa mwenye liliwe kirahis huku nyuma wakitegemea mgao. naye Sethi akufanya agizi kwani yeye kawa njanja hakutumia Mkombozi benki bali kuwapakilia kwenye vitauni hiace na kuwapelekea karibu na benki waweke wenyewe. Kwa waliotajwa wote tuanze na account zao waonyeshe mzigo wa ghafla umetoka wapi.

lissu huyu mwenye ugonjwa wa akili
 
Una Hoja.Lakini Bunge Liliagiza Uchunguzi Ambao Lazima Liujadili,huu Ni Mtiririko Wa Kawaida Wa Kazi Za Bunge,kuzuia Mjadala Kwa Namna Yoyote Kutakuwa Na Athari Kwa Wananchi Na Kwa Bunge Kama Mhimili Wa Uwakilishi.Zuio Halitafuti Haki Bali Kuna Nia Ovu Ya Kuzuia Wezi wasiwajibike Na Pesa Walizoiba Zisirudi.UjanjaHuu Ulitazamiwa.Mahakama Isiingilie Kazi Za Bunge.Zuio Ni Batili Kulingana Na Wakati Na Uzito Wa Jambo Lenyewe
 
Kwamba kuna taarifa kuwa Mahakama Kuu imeweka zuio (injunction) ya kuzuia Bunge kujadili suala la escrow kwa sababu kuna watu wameenda mbele ya mahakama kutafuta 'relief' fulani ni taarifa ambazo zilitarajiwa na zimekuwa zikinong'onwa kwa siku kadhaa sasa wakati taifa linasubiria mjadala huo Bungeni. Tukikubali kuwa Mahakama imetoa zuio hilo basi swali ni je Bunge linatakiwa kutii au lisitii?

Kuna watu ambao wanaamini mjadala huu ni lazima uendelee kwa sababu Bunge linafanya kazi zake "bila kuingiliwa". Lakini pia tunafahamu kwenye masuala ya haki Mahakama nayo inatakiwa kufanya kazi zake "bila kuingiliwa". Je, hili lina maana pande hizi mbili zinaweza kujikuta kwenye stalemate (kukodoleana) hadi mmoja wao apepese macho?

Naomba kupendekeza kuwa katika masuala ya kutafuta haki Mahakama na maamuzi yake yako juu ya mtu yeyote; yako juu ya Bunge na hata juu ya Ikulu. Mahakama inapotoa uamuzi fulani uamuzi huo unatakiwa kutiiwa na wanaohusika. Kwamba sasa Bunge linataka kuendelea na mjadala wakati Mahakama imetoa zuio halali siyo tu ni kutengeneza mwelekeo mbaya (bad precedence) lakini pia utatuletea matatizo huko mbeleni pale ambapo ama Ikulu au watendaji wengine watakapoamua kupuuzia maamuzi ya mahakama kwa sababu hawayapendi au wanaona yanawazuia kupata manufaa fulani ya kisiasa.

Ni kwa sababu hii naamini Bunge litatambua hatari waliyo nayo kwa kutokutii amri ya mahakama. Mahakama haina majeshi na wala haina polisi lakini kama maamuzi yake hayawezi kutiiwa na watu ambao walitunga sheria nani basi ataweza kuyatii maamuzi ya mahakama? Kinachosikitisha ni kuwa hata baadhi ya watu ambao wanatarajiwa kuwa watetezi wa utawala wa sheria wanaonekana kukubali kutokutii huku kwa Bunge. Hii ni hatari.

Hata mwizi ana haki ya kwenda mbele ya mahakama kutafuta msaada; mafisadi na wezi wa mali za umma nao wana haki hiyo hiyo. Ni jukumu la wanaodai kuthibitisha madai yao. Na kwa vile serikali yetu kwa makusudi au kwa bahati mbaya hadi hivi sasa haijaanzisha uchunguzi wa kihalifu (criminal investigation) kuhusiana na escrow na kwa vile jukumu hilo linamuangukia DPP ambaye ofisi yake amekuwa dhaifu mara zote linapokuja suala la ufisadi basi wezi wetu wanapoenda mbele ya mahakama na kutumia mchakato wa mahakama kujilinda hatuwezi kuwakatalia ati kwa vile hatuwwapendi au tunaamini wanatumia mahakama vibaya. Ndio uzuri wa nchi ya kidemokrasia hata wezi wakikimbilia polisi lazima walindwe!

Hivyo basi, nasihi Bunge litii mahakama kwani kama halitotii hakuna mtu mwingine Tanzania ambaye atatakiwa kutii mahakama hasa kama inachukua uamuzi ambayo mtu huyo haupendi.

Kitu pekee ambacho Bunge linaweza kufanya na ninaamini ndio njia pekee ya kutokugongana na mahakama ni

a. Kuahirisha mjadala huo wa escrow
b. Mara moja kutuma wanasheria wake kutaka wasikilizwe ili kuondoa zuio hilo na hata ikibi kulikatia rufaa chini ya certificate of emergency ili lisikilizwe mara moja na kutolewa uamuzi kwani linahusiana na maslahi makubwa ya taifa.
c. Na kutii uamuzi utakaotolewa.
d. Kama Bunge kweli linataka kujadili mada hizi na kuwa na uwezo wa kuzuia masuala ya ufisadi lingengalia sheria zake ilizotunga ambazo baadhi yetu tunaamini ndio chanzo cha ufisadi. Hadi leo hii hawajafanyia mabadiliko sheria ya usalama wa taifa, bado hawajafanya mabadiliko sheria ya DPP na hata CAG mwenyewe na badala yake tunazunguka kwenye sheria zile zile mbovu. Binafsi ningeona la maana kama wabunge wangekaa kujadili kwa uhuru suala la udhaifu wa usalama wa taifa na haja ya mabadiliko kuliko kujadili kitu ambacho tayari tunajua nini kimetokea ila wapo baadhi ya watu wanaotafuta njia ya kutokea kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu. Usalama wa taifa kwangu ndio tatizo kubwa zaidi la kukabiliana na ufisadi nchini kuliko kitu kingine chochote.

Tusikubali Bunge nalo lijiinue dhidi ya mahakama, maana tukikubali basi mahakama zetu zitakuwa zimedhoofishwa kwa madhara makubwa sana katika suala la haki.

Kwa upande wa serikali tungetarajia hadi hivi sasa tayari uchunguzi wa kihalifu ungekuwa umeanza kufanyika badala ya kuacha uchunguzi wa kibunge (parliamentary inquiry) uliofanywa na Kamati ya PAC chini ya Zitto. Kama uchunguzi huu ungekuwa umeanza hata akaunti zinazodaiwa kugawiwa fedha zingewekwa chini ya ulinzi ili zisitoe fedha na wamiliki wake kuhojiwa. Na hata hili lingeweza kutumika kuzuia mjadala wa kisiasa Bungeni.

Bush lawyer!
 
Sijamwelewa kabisa lecture yake; hivi kutakalika kweli mtaani kama escrow ikizimwa? Hivi tukingoja hadi mahakama procedures, si ishu itapoa? Ikipoa kwakweli haitakuwa na kazi (watu watajisafisha kabla ya yote), jamani supu iliwe ikiwa ya moto.......!!!!
 
huu utawala wa kikwete sasa too much mbona mikanganyiko hii ilikuwa haitokei kipindi cha mkapa
 
hiyo ni demokrasia ya marekani...askari anamuua raia aisiye na silaha kwa kumpiga risasi sita kisha anaachiwa huru....halafu Obama oh samahani rais wa marekani anasema raia andamaneni kwa amani kupinga uamuzi wa mahakama lakini msifanye vurugu maana tulikubaliana nchi hii idenshwe kisheria.

Hiyo demokrasia utawala umeijaribu kwa wafanyabiahashara wa madini wa Moro, kwa Ulimboka kwa Mwangosi, Jeet P., Kwa Andrea na EL mara ya kwanza na wengineo safari hii hatuikubali....

mkuu chukua like ya maneno,umeongea sahihi kabisa mkuu. Demokrasia hii/uhuru huu hatuwezi kuukubali kabisa kwa sasa,something extraordinary must be done,Let's take it to the street once & for all
 
Mzee Mwanakijiji wataoelewa ni wale wanaofatilia mijadala ya humu kwa muda mrefu.Nimekuelewa .......mbaya zaidi sina karama ya ualimu ya kuwafanya wengine wakuelewe .........

am sure over 99% ya watu humu wanaelewa vizuri sana anachokisema huyu ndugu bali nadhani hawamwelewi kwa kushindwa kwake kutambua kuwa anachokisema hakiwezi ku-apply kwenye hii serikali na viongozi wake viazi. kupiga buti uwanjani siyo conventional play kwenye football lakini timu ikiona conventional way hai-work zina-apply kibuti.

so, hapa ni kibuti tu hakuna kurudi nyuma. usisahau kusoma signature yangu by the way!!
 
Last edited by a moderator:
Two contradicting doctrines. Parliamentary supremacy and independence of judiciary. Hapa lazima tumfufue Montesquieu atuambie nani ni mbabe
 
Kwa tathmini Yangu kwenywe swala hili Wananchi wanaimani kubwa na Bunge kuliko Mahakama
 
Back
Top Bottom