Bunge Litii Mahakama; Lisipotii Nani Aitii Basi?

Bunge Litii Mahakama; Lisipotii Nani Aitii Basi?

Mwanakijiji mimi naomba kuelimishwa kuhusu suala la muda. Je, hakuna muda maalum wa kutoa na kuwasilisha maamuzi ya mahakama kwenye masuala mazito kama hili? Uamuzi umetolewa jioni ya leo na mjadala umepangwa kesho. Ni saa ngapi katibu wa bunge amepewa taarifa na saa ngapi amewasilisha taarifa hizo kwa wabunge? kwa upande wangu huu ni mfano wa amri zisizo halali zinazotolewa na mahakama nikizingatia kipengele cha muda
 
Mwanakijiji umeeleza vema hoja yako.Pamoja na hilo nadhani umeteleza kwa kuzingatia maslahi ya upande mmoja.
Umeeleza kuhusu precedence itakayojengwa kama bunge halitatii amri ya mahakama.
Nikukumbushe kuwa BMK halikusitishwa kusubiri uamuzi wa mahakama juu ya shauri la Kubenea Saidi.
Pili,mbona husemi ubaya wa precedence itakayojengwa kama bunge litatii amri ya mahakama?
Ina maana huoni madhara ya chombo kinachowakilisha wananchi kufifishwa nguvu?
Kwamba precedence itakayojengwa ni "kila uchunguzi wa kibunge" utakuwa unazuiliwa na mahakama kama utahatarisha maslahi ya wazito?
Ushauri wangu.Bunge lilinde heshima na hadhi yake kwa kuijadili kwa mapana ripotii ya IPTL na kutoa maazimio stahiki.
Hizo ni fedha za raia na bunge ndilo lenye mamlaka ya kuzilinda.
Hao majaji kwanza "don't live amongst us" na hatujawachagua kuwa majaji ila tumechagua wabunge.
Then lastly,hata "conflict of interest"muingiliano wa maslahi mkuu Mwanakijiji ume-skip.!
 
Mahakama wameyataka wenyewe na hawaaminiki kwa sasa.
Mahakama zetu zinanuka rushwa na wametumika sana kukandamiza haki za wanyonge.
Bunge liendelee tu na mjadala.
Wakiahirisha wananchi tuingie mtaani kudai kilicho haki yetu.

Nilisikia kuwa CUF wamesikia kilio cha watanzania na kutangaza maandamano Jumamosi, sijui kama ni kweli lakini nitaipa heshima kubwa sana CUF kama kweli tutaandamana. Sitakuwa na option zaidi ya kununua kadi ya uanachama wa CUF kama heshima kwao kwa kutetea fedha za umma kwa vitendo.
 
Hahahaa, hamchomoki hapa.

Bunge halipeleki mtu JELA. Linakuadhibu Kisiasa kama Mwana Siasa.

Mahakama itakuadhibu kama RAIA baada ya kuwa umevuliwa Ubunge/Uwaziri/Urais kama Raia wa kawaida.

Ili Mahakama ifanye kazi, Bunge lazima likushughulikie kwanza na kukuvua hadi ubaki MTUPU.
Leo kwa mara ya kwanza nakubali hoja ya huyu anaejiita Mzee Mwanakijiji na hii pia inanifanya niamini kuwa Mbowe ana mkono katika hilo zuio linalosemekana.
 
kwamba kuna taarifa kuwa mahakama kuu imeweka zuio (injunction) ya kuzuia bunge kujadili suala la escrow kwa sababu kuna watu wameenda mbele ya mahakama kutafuta 'relief' fulani ni taarifa ambazo zilitarajiwa na zimekuwa zikinong'onwa kwa siku kadhaa sasa wakati taifa linasubiria mjadala huo bungeni. Tukikubali kuwa mahakama imetoa zuio hilo basi swali ni je bunge linatakiwa kutii au lisitii?

Kuna watu ambao wanaamini mjadala huu ni lazima uendelee kwa sababu bunge linafanya kazi zake "bila kuingiliwa". Lakini pia tunafahamu kwenye masuala ya haki mahakama nayo inatakiwa kufanya kazi zake "bila kuingiliwa". Je, hili lina maana pande hizi mbili zinaweza kujikuta kwenye stalemate (kukodoleana) hadi mmoja wao apepese macho?

Naomba kupendekeza kuwa katika masuala ya kutafuta haki mahakama na maamuzi yake yako juu ya mtu yeyote; yako juu ya bunge na hata juu ya ikulu. Mahakama inapotoa uamuzi fulani uamuzi huo unatakiwa kutiiwa na wanaohusika. Kwamba sasa bunge linataka kuendelea na mjadala wakati mahakama imetoa zuio halali siyo tu ni kutengeneza mwelekeo mbaya (bad precedence) lakini pia utatuletea matatizo huko mbeleni pale ambapo ama ikulu au watendaji wengine watakapoamua kupuuzia maamuzi ya mahakama kwa sababu hawayapendi au wanaona yanawazuia kupata manufaa fulani ya kisiasa.

Ni kwa sababu hii naamini bunge litatambua hatari waliyo nayo kwa kutokutii amri ya mahakama. Mahakama haina majeshi na wala haina polisi lakini kama maamuzi yake hayawezi kutiiwa na watu ambao walitunga sheria nani basi ataweza kuyatii maamuzi ya mahakama? Kinachosikitisha ni kuwa hata baadhi ya watu ambao wanatarajiwa kuwa watetezi wa utawala wa sheria wanaonekana kukubali kutokutii huku kwa bunge. Hii ni hatari.

Hata mwizi ana haki ya kwenda mbele ya mahakama kutafuta msaada; mafisadi na wezi wa mali za umma nao wana haki hiyo hiyo. Ni jukumu la wanaodai kuthibitisha madai yao. Na kwa vile serikali yetu kwa makusudi au kwa bahati mbaya hadi hivi sasa haijaanzisha uchunguzi wa kihalifu (criminal investigation) kuhusiana na escrow na kwa vile jukumu hilo linamuangukia dpp ambaye ofisi yake amekuwa dhaifu mara zote linapokuja suala la ufisadi basi wezi wetu wanapoenda mbele ya mahakama na kutumia mchakato wa mahakama kujilinda hatuwezi kuwakatalia ati kwa vile hatuwwapendi au tunaamini wanatumia mahakama vibaya. Ndio uzuri wa nchi ya kidemokrasia hata wezi wakikimbilia polisi lazima walindwe!

Hivyo basi, nasihi bunge litii mahakama kwani kama halitotii hakuna mtu mwingine tanzania ambaye atatakiwa kutii mahakama hasa kama inachukua uamuzi ambayo mtu huyo haupendi.

Kitu pekee ambacho bunge linaweza kufanya na ninaamini ndio njia pekee ya kutokugongana na mahakama ni

a. Kuahirisha mjadala huo wa escrow
b. Mara moja kutuma wanasheria wake kutaka wasikilizwe ili kuondoa zuio hilo na hata ikibi kulikatia rufaa chini ya certificate of emergency ili lisikilizwe mara moja na kutolewa uamuzi kwani linahusiana na maslahi makubwa ya taifa.
C. Na kutii uamuzi utakaotolewa.
D. Kama bunge kweli linataka kujadili mada hizi na kuwa na uwezo wa kuzuia masuala ya ufisadi lingengalia sheria zake ilizotunga ambazo baadhi yetu tunaamini ndio chanzo cha ufisadi. Hadi leo hii hawajafanyia mabadiliko sheria ya usalama wa taifa, bado hawajafanya mabadiliko sheria ya dpp na hata cag mwenyewe na badala yake tunazunguka kwenye sheria zile zile mbovu. Binafsi ningeona la maana kama wabunge wangekaa kujadili kwa uhuru suala la udhaifu wa usalama wa taifa na haja ya mabadiliko kuliko kujadili kitu ambacho tayari tunajua nini kimetokea ila wapo baadhi ya watu wanaotafuta njia ya kutokea kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu. Usalama wa taifa kwangu ndio tatizo kubwa zaidi la kukabiliana na ufisadi nchini kuliko kitu kingine chochote.

Tusikubali bunge nalo lijiinue dhidi ya mahakama, maana tukikubali basi mahakama zetu zitakuwa zimedhoofishwa kwa madhara makubwa sana katika suala la haki.

Kwa upande wa serikali tungetarajia hadi hivi sasa tayari uchunguzi wa kihalifu ungekuwa umeanza kufanyika badala ya kuacha uchunguzi wa kibunge (parliamentary inquiry) uliofanywa na kamati ya pac chini ya zitto. Kama uchunguzi huu ungekuwa umeanza hata akaunti zinazodaiwa kugawiwa fedha zingewekwa chini ya ulinzi ili zisitoe fedha na wamiliki wake kuhojiwa. Na hata hili lingeweza kutumika kuzuia mjadala wa kisiasa bungeni.
hoja ipo kwenye bad precedence
 
Zile bilioni Kadhaa alizolipwa CHENGE na wale majaji zimeanza kufanya kazi. Jamani hawa watu wamejipanga, wana plan hadi Z, so wakiona moja haifanyi kazi wanahamia nyengine.

What is most obvious ni kwamba Urefu na upana wa RUSHWA umefahamika kwa wote. Nasubiri kuona wananchi machizi watakaowachagua hao waliolipwa hayo mabilioni 2015.

Halafu wananchi hao hao warudi humu kutupigia kelele dawa zikikosekana hospitali.
 
Mwanakijiji mimi naomba kuelimishwa kuhusu suala la muda. Je, hakuna muda maalum wa kutoa na kuwasilisha maamuzi ya mahakama kwenye masuala mazito kama hili? Uamuzi umetolewa jioni ya leo na mjadala umepangwa kesho. Ni saa ngapi katibu wa bunge amepewa taarifa na saa ngapi amewasilisha taarifa hizo kwa wabunge? kwa upande wangu huu ni mfano wa amri zisizo halali zinazotolewa na mahakama nikizingatia kipengele cha muda


hapa ngoja nimsaidie,

Bunge likikubali hoja ya kwanza ya mahakama, then wanaweka precedence ya kukubali hoja zote zilizobaki, kwani mshika pini anakuwa mahakama, list ya waliolipwa na rugemalila wapo majaji, sasa unategmemea nini kitokee?itapigwa danadana, miaka nenda rudi, by the time kesi inakwisha, wadanganyika wenye attention span ya kuku wameshasahau kila kitu.

Mk.were aliposema ni upepo alimaanisha, plan c sasa ni kutengeneza upepo wa mahakama baada ya kuona upepo hauji. na ESCROW inazidi kuchafua hali ya hewa. ZImebaki dk sifuri watu wamfunike bakuli la mboga, sio kumwaga mboga tu.
 
Kwamba kuna taarifa kuwa Mahakama Kuu imeweka zuio (injunction) ya kuzuia Bunge kujadili suala la escrow kwa sababu kuna watu wameenda mbele ya mahakama kutafuta 'relief' fulani ni taarifa ambazo zilitarajiwa na zimekuwa zikinong'onwa kwa siku kadhaa sasa wakati taifa linasubiria mjadala huo Bungeni. Tukikubali kuwa Mahakama imetoa zuio hilo basi swali ni je Bunge linatakiwa kutii au lisitii?

Kuna watu ambao wanaamini mjadala huu ni lazima uendelee kwa sababu Bunge linafanya kazi zake "bila kuingiliwa". Lakini pia tunafahamu kwenye masuala ya haki Mahakama nayo inatakiwa kufanya kazi zake "bila kuingiliwa". Je, hili lina maana pande hizi mbili zinaweza kujikuta kwenye stalemate (kukodoleana) hadi mmoja wao apepese macho?

Naomba kupendekeza kuwa katika masuala ya kutafuta haki Mahakama na maamuzi yake yako juu ya mtu yeyote; yako juu ya Bunge na hata juu ya Ikulu. Mahakama inapotoa uamuzi fulani uamuzi huo unatakiwa kutiiwa na wanaohusika. Kwamba sasa Bunge linataka kuendelea na mjadala wakati Mahakama imetoa zuio halali siyo tu ni kutengeneza mwelekeo mbaya (bad precedence) lakini pia utatuletea matatizo huko mbeleni pale ambapo ama Ikulu au watendaji wengine watakapoamua kupuuzia maamuzi ya mahakama kwa sababu hawayapendi au wanaona yanawazuia kupata manufaa fulani ya kisiasa.

Ni kwa sababu hii naamini Bunge litatambua hatari waliyo nayo kwa kutokutii amri ya mahakama. Mahakama haina majeshi na wala haina polisi lakini kama maamuzi yake hayawezi kutiiwa na watu ambao walitunga sheria nani basi ataweza kuyatii maamuzi ya mahakama? Kinachosikitisha ni kuwa hata baadhi ya watu ambao wanatarajiwa kuwa watetezi wa utawala wa sheria wanaonekana kukubali kutokutii huku kwa Bunge. Hii ni hatari.

Hata mwizi ana haki ya kwenda mbele ya mahakama kutafuta msaada; mafisadi na wezi wa mali za umma nao wana haki hiyo hiyo. Ni jukumu la wanaodai kuthibitisha madai yao. Na kwa vile serikali yetu kwa makusudi au kwa bahati mbaya hadi hivi sasa haijaanzisha uchunguzi wa kihalifu (criminal investigation) kuhusiana na escrow na kwa vile jukumu hilo linamuangukia DPP ambaye ofisi yake amekuwa dhaifu mara zote linapokuja suala la ufisadi basi wezi wetu wanapoenda mbele ya mahakama na kutumia mchakato wa mahakama kujilinda hatuwezi kuwakatalia ati kwa vile hatuwwapendi au tunaamini wanatumia mahakama vibaya. Ndio uzuri wa nchi ya kidemokrasia hata wezi wakikimbilia polisi lazima walindwe!

Hivyo basi, nasihi Bunge litii mahakama kwani kama halitotii hakuna mtu mwingine Tanzania ambaye atatakiwa kutii mahakama hasa kama inachukua uamuzi ambayo mtu huyo haupendi.

Kitu pekee ambacho Bunge linaweza kufanya na ninaamini ndio njia pekee ya kutokugongana na mahakama ni

a. Kuahirisha mjadala huo wa escrow
b. Mara moja kutuma wanasheria wake kutaka wasikilizwe ili kuondoa zuio hilo na hata ikibi kulikatia rufaa chini ya certificate of emergency ili lisikilizwe mara moja na kutolewa uamuzi kwani linahusiana na maslahi makubwa ya taifa.
c. Na kutii uamuzi utakaotolewa.
d. Kama Bunge kweli linataka kujadili mada hizi na kuwa na uwezo wa kuzuia masuala ya ufisadi lingengalia sheria zake ilizotunga ambazo baadhi yetu tunaamini ndio chanzo cha ufisadi. Hadi leo hii hawajafanyia mabadiliko sheria ya usalama wa taifa, bado hawajafanya mabadiliko sheria ya DPP na hata CAG mwenyewe na badala yake tunazunguka kwenye sheria zile zile mbovu. Binafsi ningeona la maana kama wabunge wangekaa kujadili kwa uhuru suala la udhaifu wa usalama wa taifa na haja ya mabadiliko kuliko kujadili kitu ambacho tayari tunajua nini kimetokea ila wapo baadhi ya watu wanaotafuta njia ya kutokea kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu. Usalama wa taifa kwangu ndio tatizo kubwa zaidi la kukabiliana na ufisadi nchini kuliko kitu kingine chochote.

Tusikubali Bunge nalo lijiinue dhidi ya mahakama, maana tukikubali basi mahakama zetu zitakuwa zimedhoofishwa kwa madhara makubwa sana katika suala la haki.


Kwa upande wa serikali tungetarajia hadi hivi sasa tayari uchunguzi wa kihalifu ungekuwa umeanza kufanyika badala ya kuacha uchunguzi wa kibunge (parliamentary inquiry) uliofanywa na Kamati ya PAC chini ya Zitto. Kama uchunguzi huu ungekuwa umeanza hata akaunti zinazodaiwa kugawiwa fedha zingewekwa chini ya ulinzi ili zisitoe fedha na wamiliki wake kuhojiwa. Na hata hili lingeweza kutumika kuzuia mjadala wa kisiasa Bungeni.


Umeandika meengi lkn ulichosahau ni Kimoja na ambacho ni Muhimu kuliko vyoote, Ni kwamba watu wetu wana IQ ndogo ya wastani wa 70 Ukilinganisha na Duniani nje ya Afrika ni kuanzia 90 hata Afrika ya Kaskazini wanaanzia 90 pia, na IQ ndio kila kitu hayo mengine yoote tunapoteza muda tu!

U
meongelea kuhusu Bunge kubadili Sheria ulizozitaja lkn wakati wa kufanya hayo ulivyofika (Katiba) Wabunge na Watanzania kwa ujumla wakiongozwa na Mzee wa tukana Nyerere Tundu Lisu walikuwa wanadai Tanganyika irudi, walikuwa wanapigania Haki yao ya kuishi na kupata kiwanja Zanzibar nchi yenye ukubwa wa km² 2000 na Watu kam Milioni Moja hv, hii ndio iliyokuwa hoja kuu kuanzia Bungeni, mitaani mpaka Hapa JF, hilo peke yake linakuonyesha ya kwamba Watu wetu wana IQ ndogo sana kwa maana kwa Mtu mwenye IQ kubwa swala la Zanzibar lingekuwa ishu ndogo sana, angeshughulika na mambo ambayo yanamfanya awe Maskini kwa kuanzia kama Malighafi zetu kuibiwa Bila manufaa yoyote, Wageni kushikilia njia Kuu zetu za Uchumi na kuiba fedha zetu, Kuhakikisha kuna Utenganisho wa kofia mbili yaani Mwenyekiti wa Chama asiwe Raisi, lkn wapi tunataka Zanzibar (km² 2000) na Tanzania Bara (Km² 940 000) tuwe 50-50 ndiyo Kipaumbele kikubwa kuliko vyote!

sasa wazungu wanasema chickens coming home to roost! Hivyo mtulie na msilalamike!
 
Nasema hivi ili suala kweli likipita bila kujadiliwa na watanzania tukakaa kimya na kuacha hawa wapumbavu wale pesa yetu ss tuendelee kupigwa mtaani tukidaiwa pesa ya maabara,tusubri kuwa announced as saints
 
Madaraka na Haki za Bunge
100.-(1) Kutakuwa na Uhuru wa mawazo,
majadiliano na utaratibu katika Bunge na
Uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na
chombo chochote katika Jamhuri ya
Muungano, au katika Mahakama au
mahali penginepo nje ya Bunge
 
Hizi shenanigans zinachezwa na serikali; mahakama hapa inatumiwa tu kama ngao. Hata hivyo serikali yenyewe imeshagawanyika vipande vipande. Uamzi huu wa mahakama unaweza kuwa unatoa muda kwa serikali kupumua ... lakini ukiangalia ukweli wa mambo tupo kwenye tipping point. Ni kajitu kadogo tu unrelated kanaweza kuzua balaa. Kwanza implications ya kuacha hali hii iendelee ni kuzipa muda romour mills kuendelea na uumbaji. Wabunge inatakiwa walipasue jipu hili kama wanaipenda nchi hii. Tunaweza kujikuta hatuna nchi ikiwa wabunge watakubaliana na mahakama kuendelea kukumbatia uozo huo. Wafadhili hawatatoa fedha and you know what .... serikali itakopa mabenki yake, thamani ya shillingi itaanga kuporomoka, purchasing power ya watanzania kushuka, ... na maumivu yatakayofuatia hakuna atakayeweza kuzuia impact yake. Yanapotokea kwingine siku zote tunasema sisi ni tofauti ..... mhhh, iko siku tutaona kumbe sisi si tofauti. Njia pekee ni hoja ijadiriwe, wa kuwajibika wawajibike, tubaki tunajadiri yatakayofuatia. Vinginevyo ... tusubiri tuone!!!
 
Rushwa aina mipaka. Kweli mafisadi wana mkono mrefu. Pole sana kikogwe, umechelewa.
 
Dhana ya Separation of Powers inaambatana na dhana ya Checks and Balance. Hapo ndipo kuliko na muingiliano wa hizi 3 pillars of state. kuhusu zuio la mahakama, lazima tukubaliane kuwa mahakama haijatumia Hekima inayohitajika, badala yake imetaka kuonesha Superiority over Parliament. Je!haikujua kufanya hivyo ni kuleta mgogoro wa Kimihimili?Bunge nalo lina kinga dhidi ya mihimili mingine, je! nalo bunge likionesha Parliamentary Supremacy, tutarajie nini katika taifa kama si muendelezo wa ubabe wa mihimili?Mahakama ingeweza kutumia HEKIMA na KUJILINDA kutoingilia shughuli za MIHIMILI mingine kama ambavyo nayo haitaki kuingiliwa kwani mchakato huu ulianzishwa na Bunge, umesimamiwa na Bunge, na lazima lihitimishwe na Bunge, hili ni jukumu la kikatiba ambalo bunge linalo katika kuisimamia serikali.
Naomba Bunge Liendelee na mjadala wa ESCROW kwa MASLAHI MAPANA YA TAIFA, lakini pia katika DHANA NZIMA YA PARLIAMENTARY SUPREMACY!!!
CC:Mwanakijiji
 
Zile bilioni Kadhaa alizolipwa CHENGE na wale majaji zimeanza kufanya kazi. Jamani hawa watu wamejipanga, wana plan hadi Z, so wakiona moja haifanyi kazi wanahamia nyengine.

What is most obvious ni kwamba Urefu na upana wa RUSHWA umefahamika kwa wote. Nasubiri kuona wananchi machizi watakaowachagua hao waliolipwa hayo mabilioni 2015.

Halafu wananchi hao hao warudi humu kutupigia kelele dawa zikikosekana hospitali.
Hii amri ina mkono wa Kikwete mwenyewe kutoka US, anajua fika kuwa Mtoto wake Miraj Kikwete ndio mwenye Simba Trust ya Australia, so mwisho wa siku ishu ikijadiliwa na watu kuwajibishwa kuna wengine wataamua kumwaga ugali na kumtaja Miraj Kikwete, hivyo hii amri ya mahakama ina mkono wa tezi dume toka US. Pia ieleweke Kikwete yuko US, Mwanakijiji yuko US, upo uwezekano wa kumtuma kupima upepo hapa....
 
Back
Top Bottom