Bunge Litii Mahakama; Lisipotii Nani Aitii Basi?

Bunge Litii Mahakama; Lisipotii Nani Aitii Basi?

Ndio uzuri wa nchi ya kidemokrasia
Uzuri wa nchi ya kidemokrasia?

Naomba ututajie nchi moja duniani "ya kidemokrasia" ambapo ukifungua kesi mahakamani basi bunge lao na nchi nzima inatakiwa kufunga mdomo kuongelea suala husika.
 
Nakubaliana na Mwanakijiji.Suala likianzia mahakamani lazima liishie huko.Hata hayo mabishano kwamba mahakama haina mamlaka ya kuzuia mijadala bungeni lazima yafanyikie mahakamani.
Lakini kwa kesho bunge linaweza kufanya "ujanja" wa kuchelewesha kupokea hiyo amri.Kwa sababu inaonekana kuna mtu atakuwa ametumwa kuipeleka mapema kesho.

Ibara ya 100.-(1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika
Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

(2) Bila ya kuathiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema
au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo
 
Baada ya kulielewa hili:

Ibara ya 100.-(1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika
Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

(2) Bila ya kuathiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema
au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo



Nimefuta kuunga mkono hoja hii ya anaejiita Mzee Mwanakijiji, anapoteza watu maboya kwa maslahi yake.

Nimestuka!

Ndio ukweli wenyewe huo. Mahakama ikitaka isubiri Bunge limalize kazi yake.
 
Last edited by a moderator:
Kwamba kuna taarifa kuwa Mahakama Kuu imeweka zuio (injunction) ya kuzuia Bunge kujadili suala la escrow kwa sababu kuna watu wameenda mbele ya mahakama kutafuta 'relief' fulani ni taarifa ambazo zilitarajiwa na zimekuwa zikinong'onwa kwa siku kadhaa sasa wakati taifa linasubiria mjadala huo Bungeni. Tukikubali kuwa Mahakama imetoa zuio hilo basi swali ni je Bunge linatakiwa kutii au lisitii?

Kuna watu ambao wanaamini mjadala huu ni lazima uendelee kwa sababu Bunge linafanya kazi zake "bila kuingiliwa". Lakini pia tunafahamu kwenye masuala ya haki Mahakama nayo inatakiwa kufanya kazi zake "bila kuingiliwa". Je, hili lina maana pande hizi mbili zinaweza kujikuta kwenye stalemate (kukodoleana) hadi mmoja wao apepese macho?

Naomba kupendekeza kuwa katika masuala ya kutafuta haki Mahakama na maamuzi yake yako juu ya mtu yeyote; yako juu ya Bunge na hata juu ya Ikulu. Mahakama inapotoa uamuzi fulani uamuzi huo unatakiwa kutiiwa na wanaohusika. Kwamba sasa Bunge linataka kuendelea na mjadala wakati Mahakama imetoa zuio halali siyo tu ni kutengeneza mwelekeo mbaya (bad precedence) lakini pia utatuletea matatizo huko mbeleni pale ambapo ama Ikulu au watendaji wengine watakapoamua kupuuzia maamuzi ya mahakama kwa sababu hawayapendi au wanaona yanawazuia kupata manufaa fulani ya kisiasa.

Ni kwa sababu hii naamini Bunge litatambua hatari waliyo nayo kwa kutokutii amri ya mahakama. Mahakama haina majeshi na wala haina polisi lakini kama maamuzi yake hayawezi kutiiwa na watu ambao walitunga sheria nani basi ataweza kuyatii maamuzi ya mahakama? Kinachosikitisha ni kuwa hata baadhi ya watu ambao wanatarajiwa kuwa watetezi wa utawala wa sheria wanaonekana kukubali kutokutii huku kwa Bunge. Hii ni hatari.

Hata mwizi ana haki ya kwenda mbele ya mahakama kutafuta msaada; mafisadi na wezi wa mali za umma nao wana haki hiyo hiyo. Ni jukumu la wanaodai kuthibitisha madai yao. Na kwa vile serikali yetu kwa makusudi au kwa bahati mbaya hadi hivi sasa haijaanzisha uchunguzi wa kihalifu (criminal investigation) kuhusiana na escrow na kwa vile jukumu hilo linamuangukia DPP ambaye ofisi yake amekuwa dhaifu mara zote linapokuja suala la ufisadi basi wezi wetu wanapoenda mbele ya mahakama na kutumia mchakato wa mahakama kujilinda hatuwezi kuwakatalia ati kwa vile hatuwwapendi au tunaamini wanatumia mahakama vibaya. Ndio uzuri wa nchi ya kidemokrasia hata wezi wakikimbilia polisi lazima walindwe!

Hivyo basi, nasihi Bunge litii mahakama kwani kama halitotii hakuna mtu mwingine Tanzania ambaye atatakiwa kutii mahakama hasa kama inachukua uamuzi ambayo mtu huyo haupendi.

Kitu pekee ambacho Bunge linaweza kufanya na ninaamini ndio njia pekee ya kutokugongana na mahakama ni

a. Kuahirisha mjadala huo wa escrow
b. Mara moja kutuma wanasheria wake kutaka wasikilizwe ili kuondoa zuio hilo na hata ikibi kulikatia rufaa chini ya certificate of emergency ili lisikilizwe mara moja na kutolewa uamuzi kwani linahusiana na maslahi makubwa ya taifa.
c. Na kutii uamuzi utakaotolewa.
d. Kama Bunge kweli linataka kujadili mada hizi na kuwa na uwezo wa kuzuia masuala ya ufisadi lingengalia sheria zake ilizotunga ambazo baadhi yetu tunaamini ndio chanzo cha ufisadi. Hadi leo hii hawajafanyia mabadiliko sheria ya usalama wa taifa, bado hawajafanya mabadiliko sheria ya DPP na hata CAG mwenyewe na badala yake tunazunguka kwenye sheria zile zile mbovu. Binafsi ningeona la maana kama wabunge wangekaa kujadili kwa uhuru suala la udhaifu wa usalama wa taifa na haja ya mabadiliko kuliko kujadili kitu ambacho tayari tunajua nini kimetokea ila wapo baadhi ya watu wanaotafuta njia ya kutokea kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu. Usalama wa taifa kwangu ndio tatizo kubwa zaidi la kukabiliana na ufisadi nchini kuliko kitu kingine chochote.

Tusikubali Bunge nalo lijiinue dhidi ya mahakama, maana tukikubali basi mahakama zetu zitakuwa zimedhoofishwa kwa madhara makubwa sana katika suala la haki.

Kwa upande wa serikali tungetarajia hadi hivi sasa tayari uchunguzi wa kihalifu ungekuwa umeanza kufanyika badala ya kuacha uchunguzi wa kibunge (parliamentary inquiry) uliofanywa na Kamati ya PAC chini ya Zitto. Kama uchunguzi huu ungekuwa umeanza hata akaunti zinazodaiwa kugawiwa fedha zingewekwa chini ya ulinzi ili zisitoe fedha na wamiliki wake kuhojiwa. Na hata hili lingeweza kutumika kuzuia mjadala wa kisiasa Bungeni.

Ninavyoelewa Mwanakijiji iwapo Bunge linajadili kitu Mahakama haina uwezo wa kustrike down isipokuwa baada ya maamuzi ya bunge basi watu wanaweza kukimbilia mahakamani lakini iwapo kuna process mahakama haina uwezo mfano seneti ya Marekani inataka kumuondoa rais kwa impeachement wanasheria hawawezi kimbilia mahakani kusimamisha process swala la Escrow mahakama haina uwezo mpaka process ya bunge ipite kwanza mahakamani wanaruhusiwa kutafsiri ile out come sio kabla hapa ni uhuni wa CCM
 
Uzuri wa nchi ya kidemokrasia?

Naomba ututajie nchi moja duniani "ya kidemokrasia" ambapo ukifungua kesi mahakamani basi bunge lao na nchi nzima inatakiwa kufunga mdomo kuongelea suala husika.

ndiyo hayo sasa ambayo tunasema hamsomi nilichoandika. Nimesema wapi kuwa ikifunguliwa kesi mahakamani watu basi hawaruhusiwi kujadili jambo hilo?
 
Ninavyoelewa Mwanakijiji iwapo Bunge linajadili kitu Mahakama haina uwezo wa kustrike down isipokuwa baada ya maamuzi ya bunge basi watu wanaweza kukimbilia mahakamani lakini iwapo kuna process mahakama haina uwezo mfano seneti ya Marekani inataka kumuondoa rais kwa impeachement wanasheria hawawezi kimbilia mahakani kusimamisha process swala la Escrow mahakama haina uwezo mpaka process ya bunge ipite kwanza mahakamani wanaruhusiwa kutafsiri ile out come sio kabla hapa ni uhuni wa CCM

Mwanamutapa si hivyo hasa; ni kwamba kuna amri au agizo la mahakama kuzuia (injunction). Hivi zuio la mahakama mtu ana hiari ya kulitii au kutokulitii kwa sababu hapendi implication yake?
 
Hivi kweli ikitokea bunge likaiamrisha mahakama kuu isihukumu itakuwaje....
 
Mwanamutapa si hivyo hasa; ni kwamba kuna amri au agizo la mahakama kuzuia (injunction). Hivi zuio la mahakama mtu ana hiari ya kulitii au kutokulitii kwa sababu hapendi implication yake?
Zitto Kabwe alikimbilia mahakamani kuzuia kamati kuu CHADEMA isijadili swala la uanachama wake na ikawa hivyo.
 
Kwani hakuna wabunge ambao nao weamedaiwa kupokea mlungula?

Wabunge wanahojika sambamba na majambazi wengine, ila majaji bila kupeleka mahakamani hawawezi kuhojiana na hakuna watu wanafiki kwa kulindana kama majaji zaidi ya wabunge, kungekuwa na majaji kambi pinzani tungesema kunauhuru ila hawa majaji majambazi sina imani hata kidogo
 
kumuelewa Mzee Mwanakijiji inahitaji uwe na uweledi wa sheria, mimi sioni usahihi wa watu humu kumpinga, inaonesha ni jinsi gani hatujui hii mihimili mitatu ya serikali inavyotenda kazi, na hatujui ni upi wenye nguvu kuliko mwingine, kimsingi hakuna chombo chochote kilichopo juu ya sheria katika mfumo wetu wa kidemokrasia, nalazimika kukubali kuwa wengi wetu tunahitaji kurudi darasani kusoma somo la uraia.

kama utahitaji ufafanuzi kwanini bunge linahitaji kutii mahakama uliza, pamoja na kwamba bunve ndicho chombo cha kutunga sheria lakini haimaanishi ndo kipo juu ya hiyo sheria itungayo, huu ni mfumo, hivyo utendaji kazi wake hutegemeana.

binafsi nakiri kuwa uamuzi wa mahakama upo sahihi na bunge kukaidi agizo la mahakama ni kosa ambalo litaigharimu nchi yetu kwa kutengeneza bad precedent.

M nawaelewa sana na huyo Mzee Mwanakijiji ila kitu kimoja mnafeli ww na huyo mzee ni ku~address ni wapi mipaka ya hiyo mihimili inakoma na wapi inaaanza mnaongea jumla jumla na kuwafanya hao mnaowataka kurudi kusoma uraia darasani badala ya kuchukuwa jukumu lenu kutoa hiyo elimu hapa. Si kila mtu hapa ana elewa sheria ki~uweledi kutotambua hilo ninyi mmefeli zaidi ya mnaowabeza kuwa hawajui elimu uraia.
Lakini pia mngetumia wasaa huu kutueleza kuwa bad precedent ni kwa mahakama tu hatuoni tatizo lilianzia pale mahakama ya ilipokataa zuio la kubenea kuhusu BMK mi nadhani PANDOLA BOX lilifunguliwa hapo na mahakama so kama bunge lilitulia kinafiki basi madhara yake ndio hayo. Tusubiri maana ndio mwanzo
 
Last edited by a moderator:
Then you go to court and challenge the order; you just don't arbitrarily choose to disregard it.

Why do you need to go to court while you have constitution power? Bunge have the power to discuss anything anytime that is a constitution power.
 
Then you go to court and challenge the order; you just don't arbitrarily choose to disregard it.

Don't you think that the same court(in its judicial hrc) will sustain the same, considering that there is conflict of interest to the same as other have contended above
 
Mzee mwanakijiji nimekuelewa vizuri sana tu. Embu nisaidie vipi mihimili inapoingiliana pale mahakana inapofanya maamuzi yanayaingilia haki na kinga ya bunge. To put it in a simple language kama ilivyo bunge haliruhusiwi kuzungumzia mambo yaliopo mahakamani don't u think its about time mahakama isizungumzie jambo ambalo liko bungeni

Yaani umegusa saana, Nilipomsoma mwanakijiji wazo langu la kwanza lilikuwa hili, Kwamba Kunapokuwa na Conflict of Interest kati ya hii mihimili mitatu, na jambo likapelekwa kwenye moja ya hii mihimili kwanza, Muhimili mwingine usiiingiliwa jambo hili mpaka litakapomalizika na kutolewa maamuzi kwenye muhimili mwingine.
Kwanza mahakama na serikali zimetuhumiwa, kwa hiyo nafasi ya kutoa haki imeingiliwa angalau basi muhimili mwingine unaweza kutenda haki, Nani asiyejua uchafu wa mahakama zetu!!! Japo mihimili yote mitatu haina sifa nzuri kumtendia haki Mwananchi inayemuwakilisha. Mahakama ni Corrupt, Bunge limetekwa na serikali ina Kiburi.
 
Una habari kwamba mahakama iliwahi kufanya kazi hadi saa nane usiku ili kuzuia mgomo wa walimu?

Una habari kuwa mahakama ilimtosa Kubenea kuhusu bunge la katiba na pia ilimtosa Mtikira ishu ya mgombea binafsi kwa kuogopa serikali?

Kuna kila dalili kuwa mahakama imeshinikizwa, hata Jaji Agustino Ramadhani aliwahi kusema kuhusu mahakama kushinikizwa na serikali. Hii ya IPTL shinikizo limetoka aliko Baba yake Miraj Kikwete
acha kuendeshwa na mihemko na story za vijiweni.
usiwe kama YERICKO NYERERE ambaye kila habari kwake ni udaku. soma CONTENTS za post ya MWANAKIJIJI then uje upya na hoja za kueleweka. kulalamika kama kigori aliyekosa mume haitakusaidia.
all in all... WOOTE TUNAUNGANA KATIKA KUTAKA HOJA YA KUIJADILI HII KASHFA BUNGENI ISIPUUZWE NA BUNGE LISINYIMWE HADHI NA MAMLAKA YAKE.
 
umemegewa fungu nini,acha kila mhimili ufanye kazi yake ipasavo mbivu na mbichi zijulikane,hakuna kuficha wahalifu kupitia mahakama zetu au sheria,ikishindikana nguvu ya umma ichukue nafas
 
kumwelewa huyu mzee itawachukua muda sana, kwa sababu wengi wetu hatuna ile basic knowledge of the Law, kwanza siyo sahihi kusema bunge lipo juu ya mahakama kisheria, kwa mtu anayejua sheria hawezi sema hivyo, labda nikupe mfano rahisi kwa mtindo wa swali, jibu utakalotoa ndiyo utakuwa umejifunza kitu. mf. mtu akikata rufaa katika mahakama kubwa kuliko zote Tz i.e. mahakama ya rufani (court of appeal) na mahakama hiyo ikatoa hukumu, je ni chombo gani Tanzania kinaweza tengua?, je ni bunge? maana umesema bunge lipo juu ya mahakama. nafikiri utakuwa umepata jibu.

nimeona watu wengi wamekurupuka kupinga hoja ya mzee mwanankijiji, kwa sababu tu wameisoma juujuu, embu jaribuni kuielewa kwanza. kwa elewa nini maana ya demokrasia, elewa haki ya usawa mbele ya sheria, na pia elewa supremacy ya maamuzi ya mahakama,

kimsingi ni kwamba, mtu yoyote anaweza kwenda kutafuta haki mahakamani, ( hata kama ni fisadi) kwa sababu ya udemokrasia, pili, mahakama ikitoa uamuzi hata kama unam favour huyo fisadi basi hauna budi kuuheahimu, kama haujaridhika nao una haki ya kukata rufaa, kama alivyoeleza mzee mwanakijiji, hivyo hapo anaelekeza rufaa ikatwe siyo kukaidi maamuzi ya mahakama kinyume na utaratibu. Hakuna mahala ambapo nimesema bunge lipo juu ya mahakama nimesema hivi vyote viko parallel kutoa Check and Balance.


mzee mwanakijiji ameeleza hayo kwa nia nzuri tu, kuwa kukaidi maamuzi ya mahakama ni kuiua nguvu mahakama, kwa sababu siku nyingine watu watakaidi kwa kutumia vigezo hivi.

na wala hana maana ya kuwatetea mafisadi,kesi iko palepale, na mjadala upo pale pale ila ndo utaratibu ufatwe kulinda nguvu ya mahakama isiyokuwa na jeshi.

cc: mzee mwanakijiji

Kuna mawili either hujui sheria ya kikatiba, au umeamua kujikita kwenye kutetea hoja isiyo na mashiko. Hakuna mtu aliyesema kwamba Bunge lipo juu la sheria, tumesema bunge ni sehemu ya mihilimili ya nchi. Mahakama, bunge na Raisi wote wapo chini ya katiba, inchi inaongozwa kwa sheria na katiba. Sasa katiba ya nchi inalipa bunge nyadhifa ya kujadili chochote pasipo kuiruhusu mahakama kuingilia, tafadhali rejea ibara ya 14 ya mwaka 1984.

Kama ujui kazi ya mahakama ni kulinda utawala wa sheria, KATIBA ni sehemu ya sheria, sasa kama mahakama haifuati uwepo wa katiba nani atafuata?

Unaposema kukaidi agizo la mahakama ni kuiwa mahakama, jee kukubali agizo ambalo lipo nje ya katiba sio kuliuwa Bunge? Kama hujui ibara ya 14 inasemaja tafadhali rejea hapa
"100.-(1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bung"

Mwanakijiji hapa hakufanya due diligence, amekurupuka to say the less. Mahakama haina nguvu hiyo, that doesnt mean kwamba bunge lipo juu ya sheria.
 
Ukiona chombo kinacho tenda haki nacho kina husika katika uozo fulani. Basi panashida. Mbona richmond ilijadiliwa, kwanini leo escrow iwekewe pingamizi? Double standards zisiwepo na hili sakata ni janga lakitaifa. Nikama kusema nchi imevamiwa, rais ana amulu majeshi ya nchi kupambana, mwingine nyuma anakwenda mahakamani kupinga maamuzi ya rais. Jamani kuna mambo ya maslahi ya taifa tunapashwa kuya weka mbele. Huu ujanjaujanja sio mzuri na nikutumia mahakama vibaya. Bunge lina haki ya kujadili jambo lolote dharura linalo gusa taifa kwa mapana. Kujadili sio kuhukumu, ni kufahamisha wana nchi ni nini kinachoendelea ndani ya taifa lao. Mahakama yenyewe haiamini kwa maswala mengi na nimuhili wa dola ambao umeteteleka sana, na acha bunge wawa amushe.
 
Back
Top Bottom