Bunge Litii Mahakama; Lisipotii Nani Aitii Basi?

Mkuu Mzee Mwanakijiji, kwanza asante kwa mada hii, pili naomba kukupa pole kwa sababu this time utashambuliwa sana na watu wa aina mbili, ignorantas wasiojua umuhimu wa utawala wa sheria, "the rule of law", wao wamehamanika na mjadala wa escrow tuu hata kama ni kinyume cha sheria!, hawa wasikuumize kichwa, ni kuwaelimisha tuu wataelimika, ila pia unaweza kupingwa na sisi baadhi yetu, ambao tunauelewa umuhimu wa utawala wa sheria, lakini tutalisupport bunge kuendelea na mjadala huu kwa sababu tunaelewa fika loop holes kwenye sheria zetu, hivyo wenye fedha na mafisadi, kuitumia mahakama kama kichaka cha kufucha maovu yao, dhidi ya Watanzania masikini ambao cannot afford hata their basic rights!.

Kwa muda mrefu sana nchi yetu imekuwa na tatizo kwenye kitu kinachoitwa "The Doctrine of Checks and Balances" and "Separation of Powers" kati ya mihimili hii mitatu ya dola, "The Legislature, The Executive and The Judiciary, ambavyo vyombo hivi vyote vitatu vinapaswa kuwa "huru bila kuingiliwa" "independence of its decisions" ili kila kimoja kiwe na nguvu zake chenyewe " powers" ambazo zimetenganishwa na kingine, "separations" ila pia vimepewa mamlaka ya kitu kinachoitwa "checks and balances" kama a watchdog of one another ili mihimili hii isivuke mamlaka yake, au ikitaka kuleta madhara, izuiliwe na one onother!.

Kwa vile suala hili la miingiliano ya mihimili hii, nimeisha wahi kulizungumzia sana humu, nafanya reference, ili nije na uzi mahsusi, ila uamuzi huu wa mahakama kuzuia escrow kujadiliwa na bunge, umekuja wakati muafaka kabisa, kwa sababu sasa ndio hii "The Doctrine of Checks and Balances" and "Separation of Powers" is put the real test against kitu kinachoitwa "public interest", kwamba maslahi yataifa yatawekwa mbele!, kwenye suala hili, naomba kutofatiana na wewe, kuwa ikibidi sheria kuvunjwa!, "for public interest", sheria na zivunjwe!, mahakama na idharauliwe!, "escrow ijadiliwe!"

Pasco.

Pasco, nadhani hapa umemaliza. The check and balance is a core of Katiba ya Tanzania. Japokuwa is not perfect lakini that is a core thread ya Katiba ya Jamuhuri.

Sasa kama tunataka kusema mahakama ina haki ya kukataza bunge lisifanye majadiliano ya aina yoyote, jee ipo wapi check and balance?
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, kwanza asante kwa mada hii, pili naomba kukupa pole kwa sababu this time utashambuliwa sana na watu wa aina mbili, ignorantas wasiojua umuhimu wa utawala wa sheria, "the rule of law", wao wamehamanika na mjadala wa escrow tuu hata kama ni kinyume cha sheria!, hawa wasikuumize kichwa, ni kuwaelimisha tuu wataelimika, ila pia unaweza kupingwa na sisi baadhi yetu, ambao tunauelewa umuhimu wa utawala wa sheria, lakini tutalisupport bunge kuendelea na mjadala huu kwa sababu tunaelewa fika loop holes kwenye sheria zetu, hivyo wenye fedha na mafisadi, kuitumia mahakama kama kichaka cha kufucha maovu yao, dhidi ya Watanzania masikini ambao cannot afford hata their basic rights!.

Kwa muda mrefu sana nchi yetu imekuwa na tatizo kwenye kitu kinachoitwa "The Doctrine of Checks and Balances" and "Separation of Powers" kati ya mihimili hii mitatu ya dola, "The Legislature, The Executive and The Judiciary, ambavyo vyombo hivi vyote vitatu vinapaswa kuwa "huru bila kuingiliwa" "independence of its decisions" ili kila kimoja kiwe na nguvu zake chenyewe " powers" ambazo zimetenganishwa na kingine, "separations" ila pia vimepewa mamlaka ya kitu kinachoitwa "checks and balances" kama a watchdog of one another ili mihimili hii isivuke mamlaka yake, au ikitaka kuleta madhara, izuiliwe na one onother!.

Kwa vile suala hili la miingiliano ya mihimili hii, nimeisha wahi kulizungumzia sana humu, nafanya reference, ili nije na uzi mahsusi, ila uamuzi huu wa mahakama kuzuia escrow kujadiliwa na bunge, umekuja wakati muafaka kabisa, kwa sababu sasa ndio hii "The Doctrine of Checks and Balances" and "Separation of Powers" is put the real test against kitu kinachoitwa "public interest", kwamba maslahi yataifa yatawekwa mbele!, kwenye suala hili, naomba kutofatiana na wewe, kuwa ikibidi sheria kuvunjwa!, "for public interest", sheria na zivunjwe!, mahakama na idharauliwe!, "escrow ijadiliwe!"

Pasco.
I salute you Comrade.
 
Mzee Mwanakijiji Kwa hali ya mahakama zetu, ni bora mjadala ukaendelea Bungeni. Kulikuwa na kesi ya kusimamisha Bunge la katiba majaji wakasema hawana uwezo. Tena majaji ndio hao watuhumiwa wa escrow! Safari hii uwezo wa kusimamisha Bunge la jamhuri wanao!
Mfumo mzima wa mahakama umeoza na kuna majaji wamewekwa kwa maslahi ya mchwa wachache. Moja ya mambo nimejifunza mchakato wa katiba mpya kwa jirani zetu kenya ni kusafisha mahakama tukiwa na katiba mpya. Waliunda tume ya kuwafanyia vetting majaji wala rushwa. Tanzania tunahitaji kitu kama hicho. Baada ya kupata katiba mpya, sio hii pendekezwa ya vijisenti, itabidi majaji na mahakimu wafawidhi wafanyiwe vetting kuleta matumaini mapya kwenye mfumo wa mahakama.

Wengi wa waliopo hawana moral authority ya kusimamisha mijadala Bungeni.
 
Vipi,do you see any trias politica kwenye rasimu ya Warioba?
Hahaaa....very clever. Yes i did see it. But the three tier government structure was never and is still not my favourite! If only the mzee had proposed a one government alongside devolution....!
 
Kuna mawili either hujui sheria ya kikatiba, au umeamua kujikita kwenye kutetea hoja isiyo na mashiko. Hakuna mtu aliyesema kwamba Bunge lipo juu la sheria, tumesema bunge ni sehemu ya mihilimili ya nchi. Mahakama, bunge na Raisi wote wapo chini ya katiba, inchi inaongozwa kwa sheria na katiba. Sasa katiba ya nchi inalipa bunge nyadhifa ya kujadili chochote pasipo kuiruhusu mahakama kuingilia, tafadhali rejea ibara ya 14 ya mwaka 1984.

Kama ujui kazi ya mahakama ni kulinda utawala wa sheria, KATIBA ni sehemu ya sheria, sasa kama mahakama haifuati uwepo wa katiba nani atafuata?

Unaposema kukaidi agizo la mahakama ni kuiwa mahakama, jee kukubali agizo ambalo lipo nje ya katiba sio kuliuwa Bunge? Kama hujui ibara ya 14 inasemaja tafadhali rejea hapa
"100.-(1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bung"

Mwanakijiji hapa hakufanya due diligence, amekurupuka to say the less. Mahakama haina nguvu hiyo, that doesnt mean kwamba bunge lipo juu ya sheria.
...ni vizuri umetoa hoja kwa kurejea ibara ya 100, lakini tunachozungumzia hapa ni kuwa, hata kama mahakama itakuwa imekosea kutoa hukumu au rulling ya aina yoyote huwezi kaidi agizo lake kienyeji (arbitrarily) ni lazma ufuate utaratibu mfano kukata rufaa na kama ni ya haraka kuna certificate of emergency.

hiyo ndiyo hoja yangu maana ukipitia hoja mbalimbali za wadau wana support maamuzi ya bunge of which it is not good element in law. soma ibara ya 107A na 107B ingawa hizi sheria hasa hii ya pili ni mbaya
 
Ibara ya 100.-(1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika
Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

(2) Bila ya kuathiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema
au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo

Faiza naomba usiwe unabeba kitu jumla jumla, ni kweli ibara ya 100, inatoa immunity kwa bunge, lakini je ni hatua gani huchukuliwa pale mahakama inapokuwa imekosea kutoa maamuzi??, je ni kukaidi yale maamuzi moja kwa moja, hapa ndipo ilipokuwa hoja ya mzee mwanakijiji kuwa watu wasikaidi, bali watumie mwanasheria wa bunge kwenda kukata rufaa kwa sababu ya mahakama kukosa jurisdiction ya kuliamulia bunge.

suala la ibara ya 100, hata mzee mwanakijiji naamini analifahamu, ila huwezi ukakaidi agizo la mahakama in that manner aisee, mahakama haijaanza leo kukosea, we always see in grounds of appeal watu wameandika "the trial magistrate/judge has erred both in law and fact" sasa ni kitu gani hapa kisichoeleweka.

mzee mwanakijiji kasema waende wakakate rufaa kupinga hiyo injuction kwa sababu si halali "period" wala msimuelewe vibaya maana lengo lake ni kuendelea kuijengea mahakama yetu heshima na nguvu yake. ila watu wakikaidi hivyo, ina maana watu watakuwa na nguvu tya kuipinga mahakama kienyeji bila kufuata taratibu za sheria kwa ku refer bad precedent, na ikumbukwe kuwa mahakama ndiyo chombo pekee cha kutoa maamuzi refer Article 107A&B, na siyo mtu au chombo kingine kutoa maamuzi.
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, kwanza asante kwa mada hii, pili naomba kukupa pole kwa sababu this time utashambuliwa sana na watu wa aina mbili, ignorantas wasiojua umuhimu wa utawala wa sheria, "the rule of law", wao wamehamanika na mjadala wa escrow tuu hata kama ni kinyume cha sheria!, hawa wasikuumize kichwa, ni kuwaelimisha tuu wataelimika, ila pia unaweza kupingwa na sisi baadhi yetu, ambao tunauelewa umuhimu wa utawala wa sheria, lakini tutalisupport bunge kuendelea na mjadala huu kwa sababu tunaelewa fika loop holes kwenye sheria zetu, hivyo wenye fedha na mafisadi, kuitumia mahakama kama kichaka cha kufucha maovu yao, dhidi ya Watanzania masikini ambao cannot afford hata their basic rights!.

Kwa muda mrefu sana nchi yetu imekuwa na tatizo kwenye kitu kinachoitwa "The Doctrine of Checks and Balances" and "Separation of Powers" kati ya mihimili hii mitatu ya dola, "The Legislature, The Executive and The Judiciary, ambavyo vyombo hivi vyote vitatu vinapaswa kuwa "huru bila kuingiliwa" "independence of its decisions" ili kila kimoja kiwe na nguvu zake chenyewe " powers" ambazo zimetenganishwa na kingine, "separations" ila pia vimepewa mamlaka ya kitu kinachoitwa "checks and balances" kama a watchdog of one another ili mihimili hii isivuke mamlaka yake, au ikitaka kuleta madhara, izuiliwe na one onother!.

Kwa vile suala hili la miingiliano ya mihimili hii, nimeisha wahi kulizungumzia sana humu, nafanya reference, ili nije na uzi mahsusi, ila uamuzi huu wa mahakama kuzuia escrow kujadiliwa na bunge, umekuja wakati muafaka kabisa, kwa sababu sasa ndio hii "The Doctrine of Checks and Balances" and "Separation of Powers" is put the real test against kitu kinachoitwa "public interest", kwamba maslahi yataifa yatawekwa mbele!, kwenye suala hili, naomba kutofatiana na wewe, kuwa ikibidi sheria kuvunjwa!, "for public interest", sheria na zivunjwe!, mahakama na idharauliwe!, "escrow ijadiliwe!"

Pasco.

Pasco umenena vyema kwa nyongeza kazi ya mahakama ni kutafsiri sheria zilizotungwa na bunge kwahiyo iwapo bunge lina process ya kitu fulani mahakama haina uwezo wa kusimamisha ingekuwa hivyo kungekuwa na injuctions nyingi kupinga kusimamishwa bajeti na kufanya serikali kutorun. Hii ni scandal lazima bunge waiangalie imekaaje ingekuwa ni hivyo tusingeskia Water Gate Scandal.ikifikishwa bungeni maana wanasheria wa Nixon wangekimbilia mahakamani kuzuia
 
ndiyo hayo sasa ambayo tunasema hamsomi nilichoandika. Nimesema wapi kuwa ikifunguliwa kesi mahakamani watu basi hawaruhusiwi kujadili jambo hilo?
Okay, naanza upya, kwa lugha nyingine.

Umesema huu ndio uzuri wa nchi ya kidemokrasia, chombo cha haki kupata utii kinapotoa gag order kwa bunge.

Sasa basi, naomba utaje nchi moja duniani "ya kidemokrasia" ambapo ukifungua kesi basi mahakama hutoa gag order kwa bunge, na amri hiyo hupata utii.
 
Mwanakijiji nakuunga mkono mtazamo wako japo sio kila mtu atakuelewa. Kila mhimili una nafasi yake katika utawala wa sheria. Mahakama ina wajibu wa kutoa haki kwa mwananchi yoyote kama ambavyo Bunge lina wajibu wa kutunga sheria na kusimamia utendaji wa serikali. Mtu yeyote hana hatia mpaka itakapothbitishwa na mahakama kuwa hivyo na yeyote anayehisi kuingiliwa haki yake ana uhuru wa kuitafuta mahakamani,
 
By the way, hao waliokwenda mahakamani wamekwenda kudai haki ipi? Je, wamekwenda kudai haki ya kutojadiliwa bungeni au nini hasa?
 
Mahakama haiwezi kutoa amri dhidi ya Bunge. Kufanya hivyo no uhaini na kuvunja katiba.

Mahakama imepotoka. Haina mamlaka hayo.
 
ts hard to explain and make u understood.

Mzee Mwanakijiji hasemi kuwa suala hili lijadiliwe mahakamani wala mimi si suppprt hivyo pia, ila anachotaka ni kuwa bunge litii agizo la mahakama kwa kukata rufaa ile rulling ambayo mahakama haina jurisdiction kuiamulia bunge, hii ni mahakama sote na mfahamu hakuna nchi isyokuwa na mahakama, huu ni muhimili muhimu sana nchini, kwa hiyo msi support kudharauliwa kwa mahakama yetu maana ipo siku haya yataikosesha nguvu.

na kwa kuongeza pia

naomba usiwe unabeba kitu jumla jumla, ni kweli ibara ya 100, inatoa immunity kwa bunge, lakini je ni hatua gani huchukuliwa pale mahakama inapokuwa imekosea kutoa maamuzi??, je ni kukaidi yale maamuzi moja kwa moja, hapa ndipo ilipokuwa hoja ya mzee mwanakijiji kuwa watu wasikaidi, bali watumie mwanasheria wa bunge kwenda kukata rufaa kwa sababu ya mahakama kukosa jurisdiction ya kuliamulia bunge.

suala la ibara ya 100, hata mzee mwanakijiji naamini analifahamu, ila huwezi ukakaidi agizo la mahakama in that manner aisee, mahakama haijaanza leo kukosea, we always see in grounds of appeal watu wameandika "the trial magistrate/judge has erred both in law and fact" sasa ni kitu gani hapa kisichoelewe mwanakijiji kasema waende wakakate rufaa kupinga hiyo injuction kwa sababu si halali "period"

wala msimuelewe vibaya maana lengo lake ni kuendelea kuijengea mahakama yetu heshima na nguvu yake. ila watu wakikaidi hivyo, ina maana watu watakuwa na nguvu ya kuipinga mahakama kienyeji bila kufuata taratibu za sheria kwa ku refer bad precedent, na ikumbukwe kuwa mahakama ndiyo chombo pekee cha kutoa maamuzi refer Article 107A&B, na siyo mtu au chombo kingine kutoa maamuzi.
 
- Kwanza ni nani alipeleka hilo zuio?
- Mihimili mikuu ni
1. Serikali Kuu, Chini ya Rais
2. Mahakama Chini ya Jaji Mkuu
3. Bunge Chini ya Spika​
Hapo kila mhimili una sheria na miongozo yake, siamini kama kuna kutishiana nyau hapo.
 
Wabunge Kafulila, Zitto na Hamad Rashid wako Bungeni kwa court injuction. Hivyo Bunge, na hasa Spika, halina mamlaka ya kupuuzia zuio la sasa la mahakama hata kama hawakubaliani nalo. Kwani hata CUF, CHADEMA na NCCR hawakuridhishwa na mazuio yaliyowawezesha wabunge waliokuwa na ugomvi nao kuendelea na ubunge wao kwa baraka za Spika wa Bunge.
 
Kwamba kuna taarifa kuwa Mahakama Kuu imeweka zuio (injunction) ya kuzuia Bunge kujadili suala la escrow kwa sababu kuna watu wameenda mbele ya mahakama kutafuta 'relief' fulani ni taarifa ambazo zilitarajiwa na zimekuwa zikinong'onwa kwa siku kadhaa sasa wakati taifa linasubiria mjadala huo Bungeni. Tukikubali kuwa Mahakama imetoa zuio hilo basi swali ni je Bunge linatakiwa kutii au lisitii?

Kuna watu ambao wanaamini mjadala huu ni lazima uendelee kwa sababu Bunge linafanya kazi zake "bila kuingiliwa". Lakini pia tunafahamu kwenye masuala ya haki Mahakama nayo inatakiwa kufanya kazi zake "bila kuingiliwa". Je, hili lina maana pande hizi mbili zinaweza kujikuta kwenye stalemate (kukodoleana) hadi mmoja wao apepese macho?

Naomba kupendekeza kuwa katika masuala ya kutafuta haki Mahakama na maamuzi yake yako juu ya mtu yeyote; yako juu ya Bunge na hata juu ya Ikulu. Mahakama inapotoa uamuzi fulani uamuzi huo unatakiwa kutiiwa na wanaohusika. Kwamba sasa Bunge linataka kuendelea na mjadala wakati Mahakama imetoa zuio halali siyo tu ni kutengeneza mwelekeo mbaya (bad precedence) lakini pia utatuletea matatizo huko mbeleni pale ambapo ama Ikulu au watendaji wengine watakapoamua kupuuzia maamuzi ya mahakama kwa sababu hawayapendi au wanaona yanawazuia kupata manufaa fulani ya kisiasa.

Ni kwa sababu hii naamini Bunge litatambua hatari waliyo nayo kwa kutokutii amri ya mahakama. Mahakama haina majeshi na wala haina polisi lakini kama maamuzi yake hayawezi kutiiwa na watu ambao walitunga sheria nani basi ataweza kuyatii maamuzi ya mahakama? Kinachosikitisha ni kuwa hata baadhi ya watu ambao wanatarajiwa kuwa watetezi wa utawala wa sheria wanaonekana kukubali kutokutii huku kwa Bunge. Hii ni hatari.

Hata mwizi ana haki ya kwenda mbele ya mahakama kutafuta msaada; mafisadi na wezi wa mali za umma nao wana haki hiyo hiyo. Ni jukumu la wanaodai kuthibitisha madai yao. Na kwa vile serikali yetu kwa makusudi au kwa bahati mbaya hadi hivi sasa haijaanzisha uchunguzi wa kihalifu (criminal investigation) kuhusiana na escrow na kwa vile jukumu hilo linamuangukia DPP ambaye ofisi yake amekuwa dhaifu mara zote linapokuja suala la ufisadi basi wezi wetu wanapoenda mbele ya mahakama na kutumia mchakato wa mahakama kujilinda hatuwezi kuwakatalia ati kwa vile hatuwwapendi au tunaamini wanatumia mahakama vibaya. Ndio uzuri wa nchi ya kidemokrasia hata wezi wakikimbilia polisi lazima walindwe!

Hivyo basi, nasihi Bunge litii mahakama kwani kama halitotii hakuna mtu mwingine Tanzania ambaye atatakiwa kutii mahakama hasa kama inachukua uamuzi ambayo mtu huyo haupendi.

Kitu pekee ambacho Bunge linaweza kufanya na ninaamini ndio njia pekee ya kutokugongana na mahakama ni

a. Kuahirisha mjadala huo wa escrow
b. Mara moja kutuma wanasheria wake kutaka wasikilizwe ili kuondoa zuio hilo na hata ikibi kulikatia rufaa chini ya certificate of emergency ili lisikilizwe mara moja na kutolewa uamuzi kwani linahusiana na maslahi makubwa ya taifa.
c. Na kutii uamuzi utakaotolewa.
d. Kama Bunge kweli linataka kujadili mada hizi na kuwa na uwezo wa kuzuia masuala ya ufisadi lingengalia sheria zake ilizotunga ambazo baadhi yetu tunaamini ndio chanzo cha ufisadi. Hadi leo hii hawajafanyia mabadiliko sheria ya usalama wa taifa, bado hawajafanya mabadiliko sheria ya DPP na hata CAG mwenyewe na badala yake tunazunguka kwenye sheria zile zile mbovu. Binafsi ningeona la maana kama wabunge wangekaa kujadili kwa uhuru suala la udhaifu wa usalama wa taifa na haja ya mabadiliko kuliko kujadili kitu ambacho tayari tunajua nini kimetokea ila wapo baadhi ya watu wanaotafuta njia ya kutokea kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu. Usalama wa taifa kwangu ndio tatizo kubwa zaidi la kukabiliana na ufisadi nchini kuliko kitu kingine chochote.

Tusikubali Bunge nalo lijiinue dhidi ya mahakama, maana tukikubali basi mahakama zetu zitakuwa zimedhoofishwa kwa madhara makubwa sana katika suala la haki.

Kwa upande wa serikali tungetarajia hadi hivi sasa tayari uchunguzi wa kihalifu ungekuwa umeanza kufanyika badala ya kuacha uchunguzi wa kibunge (parliamentary inquiry) uliofanywa na Kamati ya PAC chini ya Zitto. Kama uchunguzi huu ungekuwa umeanza hata akaunti zinazodaiwa kugawiwa fedha zingewekwa chini ya ulinzi ili zisitoe fedha na wamiliki wake kuhojiwa. Na hata hili lingeweza kutumika kuzuia mjadala wa kisiasa Bungeni.

Huyu naye lazima amevuta kiasi z escrow
 
Back
Top Bottom