Chagga King
JF-Expert Member
- Jul 6, 2011
- 1,932
- 1,179
Mzee mwenzangu hapa kidogo umefuka. Bunge alifanyi judgement, linafanya majadiliano kuhusu report. Ni sawa tumwambie rahisi huwezi fanya kitu fulani sababu kipo mahakamani. Bunge, Rahisi na Mahakama ni mihili mitatu tofauti isiyoingiliana kazi. Mahakama iendelee na kazi yake na bunge liendelee na kazi yake. Kusema mahakama ipo juu zaidi ya bunge sio sawa.
kumwelewa huyu mzee itawachukua muda sana, kwa sababu wengi wetu hatuna ile basic knowledge of the Law, kwanza siyo sahihi kusema bunge lipo juu ya mahakama kisheria, kwa mtu anayejua sheria hawezi sema hivyo, labda nikupe mfano rahisi kwa mtindo wa swali, jibu utakalotoa ndiyo utakuwa umejifunza kitu. mf. mtu akikata rufaa katika mahakama kubwa kuliko zote Tz i.e. mahakama ya rufani (court of appeal) na mahakama hiyo ikatoa hukumu, je ni chombo gani Tanzania kinaweza tengua?, je ni bunge? maana umesema bunge lipo juu ya mahakama. nafikiri utakuwa umepata jibu.
nimeona watu wengi wamekurupuka kupinga hoja ya mzee mwanankijiji, kwa sababu tu wameisoma juujuu, embu jaribuni kuielewa kwanza. kwa elewa nini maana ya demokrasia, elewa haki ya usawa mbele ya sheria, na pia elewa supremacy ya maamuzi ya mahakama,
kimsingi ni kwamba, mtu yoyote anaweza kwenda kutafuta haki mahakamani, ( hata kama ni fisadi) kwa sababu ya udemokrasia, pili, mahakama ikitoa uamuzi hata kama unam favour huyo fisadi basi hauna budi kuuheahimu, kama haujaridhika nao una haki ya kukata rufaa, kama alivyoeleza mzee mwanakijiji, hivyo hapo anaelekeza rufaa ikatwe siyo kukaidi maamuzi ya mahakama kinyume na utaratibu.
mzee mwanakijiji ameeleza hayo kwa nia nzuri tu, kuwa kukaidi maamuzi ya mahakama ni kuiua nguvu mahakama, kwa sababu siku nyingine watu watakaidi kwa kutumia vigezo hivi.
na wala hana maana ya kuwatetea mafisadi,kesi iko palepale, na mjadala upo pale pale ila ndo utaratibu ufatwe kulinda nguvu ya mahakama isiyokuwa na jeshi.
cc: mzee mwanakijiji