Bunge Litii Mahakama; Lisipotii Nani Aitii Basi?

Bunge Litii Mahakama; Lisipotii Nani Aitii Basi?

Wabunge wanatakiwa kutoa onyo kwa rais kwamba hawana imani na rais kwisha
 
Ibara ya 100.-(1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika
Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

(2) Bila ya kuathiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema
au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo
 
Nakubaliana na Mwanakijiji.Suala likianzia mahakamani lazima liishie huko.Hata hayo mabishano kwamba mahakama haina mamlaka ya kuzuia mijadala bungeni lazima yafanyikie mahakamani.
Lakini kwa kesho bunge linaweza kufanya "ujanja" wa kuchelewesha kupokea hiyo amri.Kwa sababu inaonekana kuna mtu atakuwa ametumwa kuipeleka mapema kesho.
 
Kauli ya mahakama iko wapi?
 
Bora umewaandikia labda wataelewa
 
Mzee mwenzangu hapa kidogo umefuka. Bunge alifanyi judgement, linafanya majadiliano kuhusu report. Ni sawa tumwambie rahisi huwezi fanya kitu fulani sababu kipo mahakamani. Bunge, Rahisi na Mahakama ni mihili mitatu tofauti isiyoingiliana kazi. Mahakama iendelee na kazi yake na bunge liendelee na kazi yake. Kusema mahakama ipo juu zaidi ya bunge sio sawa.

mwanakijiji ameshakunywa viroba vyake
 
Mahakama ilitoa zuio kwa msanii davido kuperfom kwenye fiesta lakini the nextday tulimuona jukwaani.....sasa kama kwa issue ndogo vile mahakama ilidharaulika sembuse hili sasa??
 
Mkuu

Unchosema kinadharia ni kweli na ndicho kinachotakiwa kifanyike.
Umesema kauli moja muhimu (bad precedence). Nitaijadili

Kwanza, kiuhalisia Tanzania tunaishi kwa kile kinachoitwa ''rule of the jungle''
Si mara moja au mbili, tumeona sheria hii ikitumiwa na Bunge, Mhakama na Serikali.
Hiyo tu ilishajenga bad precence unayosema, na ikatengeneza rule of the jungle. Tunapaswa kuishi katika rule of the jungle.

Utakuwa ni ujinga ukiwa mwituni unahubiri dini, mtu akidhani Simba au Chui watampa nafasi ili hali matumbo yao yanapweta kwa njaa. Ndio maana swala na nyumbu hukimbia na kuacha mwenzao atafunwe ili waione kesho.
Sheria za mwituni ndizo tulizo nazo.

Bad precedence
Hii imeanza siku nyingi. Mfano, bunge lilifanya uchunguzi na kuagiza viongozi wa Ikulu na wizara waliohusika na rushwa ambayo ilitolewa bungeni wachukuliwe hatua. Serikali ikaamua wastaafu na sasa wanakula mafao ya umma na rushwa zao

Tumeona watu wakiuawa au kujeruhiwa katika mazingira tatanishi. Serikali imekimbilia kukamata wahuni ili suala hilo lisizungumzwe na huo unakuwa mwisho. Unakumbuka hadithi ya Mwanamalundi aliyemjeruhi Daktari na vifo vya wataalam kadha katika mazingira ya utatanishi

Unakumbuka kuna viporo vya ufisadi ambavyo siku za nyuma vimejadiliwa, vikakabidhiwa serikali. Hadi leo hatujui nani amechota pesa za rada, meremeta n.k. Serikali imetumia mahakama kuzuia mjadala. bad precedence

Mahamakama nayo imeshindwa kutoa haki. Suala linapochukua miaka 20 na mahakama imekaa kimya si tu ni justice delay, bali pia ni justice denial. Haya yanafanyika ili kuzuia na kupoteza ushahidi ima kwa watuhumiwa au watuhumu.
Mahakama imekuwa chaka la kuficha maovu.

Katika mazingira ya kawaida, mahakama ina uwezo wa kumwachia mtu kama ushahidi haupo au unacheleweshwa.
Mahakama zetu zimekuwa hazifanyi hivyo kwasababu zinafanya kazi chini ya serikali. Bad precedence

Bunge nalo limeamua kupora haki za wananchi kwa kuandika katiba tena ikitumia watuhumiwa wanaojulikana wazi.
Bunge linaendelea na mchakato huo likijua si halali, na serikali inajua imedhulumu watu, mahakama inatumika kukinga serikali. Hapo ni suala la nifae kwa jua nikufae kwa mvua. Bad precedence.

Katika mazingira hayo, nchi hii haina utawala wa sheria. Ingekuwa nao, leo vipi watu watoke Kenya, wachote mabilioni tena kwa mihuri ya serikali bila kujulikana. Nchi hii ina viongozi au tuna genge la watu wanaoitwa viongozi? Bad precedence

Hapa kinachoendelea ni rule of the jungle, na sasa wananchi wanataka kujua simba amekula nini, chui amepata nini, je kuna mbweha aliyeamulia chochote. Hilo tu!! wajue kuwa mwituni wanakoishi kuna tatizo, na pengine wataamka na kusema pori hili basi tuhamie pori lingine. Vinginevyo bad precedence itajenga mazingira ya wao kutafunwa kwa kutumia sheria halali kabisa za mwituni, rule of the junge.
 
USIROPOKE TU KAMA HUJASOMA KATIBA.

Kasome Ibara ya 100(1) inayoelekeza kuwa Bunge lina haki na madaraka yasiyohojiwa na chombo chochote kingine nje ya Bunge ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Halafu ndo uje utuambie hoja yako umeitoa wapi?

ACHA KUPOTOSHA wasiosoma katiba
 
Unahoja nzuri mzee ila swala hili linajitaji kujadiliwa kwa sababu:-

1. Hali ya hewa kisiasa imechafuka, kila mtu anajumuishwa na kila leo wanaongezeka, hii inahatari siku si nyingi kama haitawekwa sawa mapema ikizingatiwa baada ya bunge hili kikao kingine ni mwakani hivyo kuinyima jamii nafasi ya kuelewa jambo hili vyema

2. Haitakuwa amri ya kwanza ya mahakama kupuuzwa, tumeona nyingi hata ambazo hazina public interest

3. Baadhi ya majaji ni washutumiwa na kwa vile hatuna idadi au majina kamili ya nani kafanya nini yawezekana (labda) na waliotoa order ni baadhi yao au ni marafiki wa washutumiwa...

4. Bunge ni chombo kinachojitegemea na mahakama pia, kila kimoja kinamamlaka katika eneo lake na kila kimoja kinajukumu lake hivyo jukumu la bunge linataiwa kutekelezeka katika kuismamia serikali
 
Kazi kuu ya mahakama ni kusimamia Sheria na kutoa Haki. Sheria zenyewe zinatungwa na Bunge. Inakuwaje leo Bosi amsikilize na kumtii mfanyakazi wake anayempa kuishi? La hasha, haiwezekani hata siku moja. Labda kama hakuna anayejua haki yake ya Msingi
 
Kwanza hilo zuio nadhani halihusu bunge.kwani katiba imetamka wazi kuwa bunge haliwezi kuingiliwa wala kuhojiwa na chombo chochote ikiwemo mahakama. Ila kinachoshangaza zaidi ni kwamba inakuwaje zuio linatolewa bila kupata utetezi wa wanaoshitakiwa? hapa kuna harufu ya mahakama kutumika vibaya kulinda uhalifu.
 
Unahoja nzuri mzee ila swala hili linajitaji kujadiliwa kwa sababu:-

1. Hali ya hewa kisiasa imechafuka, kila mtu anajumuishwa na kila leo wanaongezeka, hii inahatari siku si nyingi kama haitawekwa sawa mapema ikizingatiwa baada ya bunge hili kikao kingine ni mwakani hivyo kuinyima jamii nafasi ya kuelewa jambo hili vyema

2. Haitakuwa amri ya kwanza ya mahakama kupuuzwa, tumeona nyingi hata ambazo hazina public interest

3. Baadhi ya majaji ni washutumiwa na kwa vile hatuna idadi au majina kamili ya nani kafanya nini yawezekana (labda) na waliotoa order ni baadhi yao au ni marafiki wa washutumiwa...

4. Bunge ni chombo kinachojitegemea na mahakama pia, kila kimoja kinamamlaka katika eneo lake na kila kimoja kinajukumu lake hivyo jukumu la bunge linataiwa kutekelezeka katika kuismamia serikali

Naungana na wewe. achana na mwanakijiji ni kigeugeu kama kinyonga.
 
Nakubaliana na Mwanakijiji.Suala likianzia mahakamani lazima liishie huko.Hata hayo mabishano kwamba mahakama haina mamlaka ya kuzuia mijadala bungeni lazima yafanyikie mahakamani.
Lakini kwa kesho bunge linaweza kufanya "ujanja" wa kuchelewesha kupokea hiyo amri.Kwa sababu inaonekana kuna mtu atakuwa ametumwa kuipeleka mapema kesho.
Ilikuwaje Bunge la katiba liliendelea wakati kulikuwa na kesi mahakamani?
 
Mahakama ingeingiliwa kazi yake endapotu jambo hili lingekuwa mahakamani then likajadiliwa bungeni lakini huwezi zuia jambo lilikwisha anza jadiliwa na bunge sheria hiyo haipo.

Hakuna uwezekano huo wa mjadala kuzuia labda kwa sababu nyingine n sio mahakama.

Mfano mzuri ni bunge la katiba lilipoendelea wakati kuna zuio la mahakama.
 
Mzee mwanakijiji mahakama inatakiwa kuzingatia katiba na sheria katika kutoa haki. Lakini pia haki inatakiwa ionekane ikitolewa hata kwa mchakato wake. Haiwezekeni mchakato uonekane unatoa haki kwa upendeleo na bado mahakama iweze kupewa heshima yake. Ikitokea amri ya mahakama imedharauliwa ni kwa matendo ya mahakama yenyewe. Je kuna kesi ngapi zimekaa miaka na miaka zinahitaji maamuzi lakini hazisikilizwi, iweje hii inapelekwa asubuhi na ndani ya masaa matano imetolewa maamuzi? Je hao IPTL wana haki kuliko hawanga wengine waliowekwa benchi kwa miaka? Pili, hii mahakama imeonyesha double standard kwa suala linalofanana na hili hili. Utakumbuka ombi kama hili lilifunguliwa ili kusimamisha mjadala wa katiba mpya, lilitupiliwa mbali na kesi ya msingi pia ilitupiliwa mbali. Sasa kwa mtazamo huu mahakama ndio inataka yenyewe kudharauliwa. Na hapa ndo tunaanza kuona kilio chetu cha mda mrefu cha kwanini majaji wanateuliwa na mkuu wa mhimili mwingine ambaye ni Rais. Hapa tunaiona loyalty ya Judiciary (majaji) kwa serikali hasa rais maana ndio mamlaka yake ya uteuzi. Katika kashfa hii serikali inafanya mbinu zote kupigana isianguke na inawatumia wote walio loyal kwake hii isitokee. Mie nasema Bunge liendelee na mjadala wa report hii na IWE FUNDISHO KWA COMPETENT PEOPLE NDANI YA JUDICIARY KUSIMAMA NA KUWAKEMEA WANAOUDHARAULISHA MHIMILI WAO.

Wasi wasi wangu na maswali yangu yanaanzia hapa katika kesi hii iliyofunguliwa leo na uamuzi ukatolewa leo leo,nina wasi wasi sana kesho hakuna mjadala utakaoendelea kuhusu sakata hili la wizi wa fedha za wananchi.Wakati spika wa bunge Anne Makinda akitoa ufafanuzi kuwa ripoti ya CAG itajadiliwa hapo kesho alisema pia ofisi ya Bunge haijapokea taarifa rasmi juu ya zuio hilo.

Muda ndio utaamua hiyo kesho japo wasi wasi wangu ni mkubwa sana hasa ukizingatia na ukigeugeu wa baadhi ya viongozi wa nchi yetu ,na ukichanganya tena na sakata la wizi huu wa mali ya umma umewahusisha viongozi wengi wazito-wasi wasi unaongezeka zaidi ya hapa.
 
Back
Top Bottom